Mambo ya kawaida ambayo wanandoa huyakwepa

Peter Mwaihola

JF-Expert Member
Jun 23, 2022
227
333
Una mpango wa kuoa hivi karibuni, au wewe ni mwanandoa unaeishi na mwenza wako?

Kuna mambo kadhaa nataka nikujuze ambayo wanandoa wengi wanaonekana kuyakwepa katika ndoa zao ingawaje mambo hayo ni ya kawaida sana kwa kuyatazama.

Wanandoa wengi licha ya kujigamba kuwa wanapendana na wenza wao lakini wamekuwa wagumu kutekeleza mambo fulani kwa wakati fulani katika ndoa zao.

Ingawaje mambo haya yanayokwepwa na baadhi ya wanandoa hayafanywi na kila mwanandoa Ila yameonekana kwa walio wengi kama sio mwanamke basi ni mwanaume.

Jambo la kwanza ni wanandoa wengi kukataa kuwa wameoa au wameolewa pindi wanapoulizwa na mtu ambae hawamfahamu, wengi wao hupata ukakasi wakiulizwa swali je umeoa au umeolewa?.

Kundi hili la wanandoa huwa na walakini kujibu swali hili kwa sababu mbalimbali pengine huhofia kukosa fursa fulani kutoka kwa watu wanaowauliza, mfano mwanamke akikutana na mwanaume ambaye hamfahamu akiulizwa umeolewa, hukaa kimya pasipo kujibu akiulizwa tena atajibu ndio lakini....kisha hunyamaza na kuna wakati fulani hukataa kabisa kujibu sijaolewa.

Na kwa upande wa wanaume jambo hili lipo mwanaume akikutana na mwanamke anaevutiwa nae ni rahisi kuikana ndoa yake wengine hufika mbali kwa kusema wake zao walifariki jambo ambalo ni usaliti wa hali ya juu.

Jambo lingine ambalo wanandoa hulikwepa ni kuongozana na wenza wao kwa kutembea umbali fulani maeneo ya hadharani mfano barabara kuu mpaka sokoni, Viwanja vya starehe na maeneo mengine.

Wengi huhofia kukutana na watu wao wa nje na kusababisha mtafaruku na wengine hufanya hivyo kwa kuhisi kuwa wenza wao hawana hadhi ya kuongozana nao kwani hata ndoa ilitokea tu kama bahati mbaya.

Wakati mwingine muonekano wa kimavazi, au kiasi cha unadhifu wa wenza wao hufanya wanandoa washindwe kuongozana kwa mfano kuna wanawake hawapendi aina fulani ya nguo ivaliwe na wanaume wao ikitokea ubishani nyumbani basi hukataa kuongozana.

Kupiga picha za pamoja pia ni jambo ambalo baadhi ya wanandoa hulikwepa hawapendi kuonekana pamoja na wenza wao kwenye matukio mbalimbali mfano sherehe mara kadhaa utoana mwanamke anataka kupiga picha na mume wake lakini mume anakwepa, kwa sababu anazozijua yeye.

Pia katika maisha ya ulimwengu wa kiutandawazi kuna baadhi ya wanandoa hukwepa kutumia mitandao ambayo wenza wao pia hupendelea kuitumia mfano utakuta mwanaume hataki kutumia mtandao wa WhatsApp kwasababu mke wake anatumia mtandao huo, umewahi kujiuliza ni kwanini baadhi ya wanandoa hawataki kabisa kukaa kwenye kundi moja la Watsap au Facebook pamoja na wenza wao?

Wengi wao huogopa kujulikana tabia zao kwa wenza wao katika mitandao ya kijamii hivyo huona ni vema kuwakwepa katika kutumia mtandao mmoja wa kijamii.

Si hivyo tu wanandoa wengi hukwepa kupakia "Kupost" picha za wenza wao ndani ya mitandao ya kijamii kwa hofu ya kuulizwa huyo ni mkeo au mumeo? na maswali mengine ya ndani.

Jambo lingine ambalo wanandoa wengi hulikwepa ni kushiriki chakula kwa pamoja wawapo nyumbani unaweza kuona mke akimaliza kupika anajifanyisha mambo mengine akiona mume wake amekula Kisha na yeye anaenda kula, pia kuna wanaume nao hivyo hivyo mke akishamaliza kupika anamwita kula kama yupo nje huko ataendelea na mambo yake akiona mke amekula ndio na yeye huingia ndani kula.

Mambo haya ni ya kawaida mno kuyatekeleza lakini yamekuwa magumu kwa baadhi ya wanandoa tena wengine hujigamba kuwa wanawapenda wenza wao lakini ikifika hatua hii uanaona wazi walivyo na mgawanyiko.

Ingawaje kuna wengine husingizia kuwa kila mtu ana hulka yake dunaini kuwa unaweza kuona jambo fulani ni la muhimu na la kawaida kulifanya lakini mwingine akaliona kuwa ni gumu na halina umuhimu wowote katika maisha.

Peter Mwaihola ni Mwandishi, Mhariri wa Habari na Mchambuzi wa Masuala ya Siasa na Jamii.
 
Wanaume hatuna matatizo kuelezea kuwa tuko kwenye ndoa, kuongozana na wenza wetu,kupiga picha pamoja ni mambo ya kawaida, ukibahatika kufika kwenye kurasa zangu za social media utaelewa ninachosema.
Kwa sifa hiyo ya mitandaoni itoshe kusema wewe ni mvulana pyuwa.
 
Kuulizwa kama nimeoa kwangu huwa haina shida sijui kuhusu yeye niliyemuoa....
Kuongoza a nae nadhani ni kwa asilimia kubwa huwa tunaongozana tena mjini kabisa.
Kila pamoja hutolewa hata Sasa tumekula pamoja..
Kupiga picha ya pamoja Mara ya mwisho ilikuwa 2015😀....
Mke hataki kabisa kupiga picha za pamoja pamoja...
Huwa nampost ila yeye hajawahi kunipost kwa siku za hivi karibuni nadhani lastly ilikuwa miaka minne hadi saba iliyopita...


Hapa kitaalamu sijui imekaaje😂
 
Tangu nigundue kuwa wanaume waliooa ni mchongo sana kwa wanawake timamu, siku hizi natembea na pete kidoleni na haijawahi kuniangusha.
Kimsingi pete inaaongeza ulimbo kwa walimbwende.

Wenyewe wanajua wako njia kuu kufanya Mapinduzi matukufu
 

Attachments

  • Screenshot_2022-02-19-12-37-54-95.jpg
    Screenshot_2022-02-19-12-37-54-95.jpg
    13.4 KB · Views: 1
Back
Top Bottom