Importing a car to Tanzania

rchingalo

New Member
Dec 30, 2008
1
0
Kama kuna mtu ana uzoefu hivi mwaka ambao gari linatozwa charge ya uchakavu ni chini ya mwaka 1999 au 2000? Mfano nikiagiza gari ya mwaka 1999 nitatozwa kodi ya uchakavu na TRA?
 
Kama kuna mtu ana uzoefu hivi mwaka ambao gari linatozwa charge ya uchakavu ni chini ya mwaka 1999 au 2000? Mfano nikiagiza gari ya mwaka 1999 nitatozwa kodi ya uchakavu na TRA?
It's almost 95% of CIF price.

That's it.

That means:

If the car is $7,000.00 FOB

Add: Inspection charges (If applicable)

Add: Insurance charges (If applicable)

Add: Transportation charges

Then you've CIF price!

If you're importing to Dar es Salaam port, you'll be charged 95% of the CIF price (including registration of your vehicle).

I faced the same when I was importing my 2001 car and I believe you'll have to face it.
 
bt nowadays kuna unafuu wa kwenye cc, kwa sasa ukiagiza gari ya 1999 utalipa uchakavu kwani inakuwa na zaidi ya 10 years (1999 inclusive)
 
Rchingalo,

Kwa uzoefu wangu mdogo nilio nao kwenye importation ya magari, ukitaka kukwepa kulipa uchakavu hakikisha gari unalo-import lisiwe chini ya mwaka 2000. Mwongozo uliotolewa na kupitishwa na bunge ni kwamba gari likizidi miaka kumi basi linapashwa kulipiwa uchakavu lakini wenzetu wa TRA kwa kuwa wao wanaangalia na kuzingatia kuvuka malengo ya kukusanya ushuru (hawaangalii hizo pesa wanazokusanya zinatumika vipi), basi wameamua kwa makusudi kupindisha rasimu iliyopitishwa na bunge. Katika mazingira ya kawaida, gari la mwaka 1999 ndio kwanza limefikisha miaka kumi hivyo alipashwi kulipiwa uchakavu. Lakini TRA amini usiamini ukilileta mwaka huu watakutoza ushuru wa uchakavu.

Labda mwana JF anayejua atusaidie ni kwa nini TRA wanafanya hivyo? Kwa mtindo huu watu wengi wameshindwa kutoa magari yao bandarini kwa sababu wanapokuwa wanaagiza wanajua gari alijazidi miaka kumi lakini TRA ikifika tu miaka kumi, wako na wewe.

Nafikiri hii itakusaidia kuamau ni gari la mwaka gani unapashwa kununua.
 
Back
Top Bottom