Imevuja sauti inayodaiwa ni Maongezi ya Simu ya Nape Nnauye na Abdulrahman Kinana kuhusu njama za kuichafua CCM

Yaliyoko kwenye clip na uliyoandika ni tofauti kabisa!!!Unakwama wapi?
 
Wapanga mpango wa kutoa tamko makusudi ili JPM aonekane mbaya huku wakijua fika kuwa Magufuli amepata tabu kuiweka Tanzania kwenye ramani ya haki na utawala bora kama ilivyokuwa enzi za Nyerere,
Wao ndo walio hujumu korosho, Sukari na kwe saruji pia kwa kushirikiana na wafanyabiashara wasiokuwa waaminifu.https://www.facebook.com/100034337745756/posts/157134872107770/
Msingi gani ya haki dog wewe
 
How comes Kinana, akaongea mambo makubwa hivyo na yasiyo na mashiko na Nape! ?

Itakuwa nape kavujisha tu
 
Pressure inapanda pressure inashuka... mwaka huu waliokatwa mikia itaota, mabubu wataongea ndani ya CCM.
 
Hahahahahahahahhahahah...........

TCRA!!

Inamaana mpango huu umeasisiwa na kinana na nape.mbona makamba kama amehusishwa tu.au nape yy ndio mjumbe wait!!?.

Vilevile ccm inaonekana kuna utawala kivuli kama upinzani na unafanyakazi chino kwachini.

Kwann nape aendelee kutumwa kama wao ndio wapo madarakani!!!

Duh!!!
 
Hao Wazee si wa kuwarembaremba kisiasa wapewe makavu tu inatosha. Kwanza Wao Wenyewe waliwapa wengine makavu enzi zao, sasa watulie sindano za kristapen ziwaingie vizuri. Hawakutambua ipo siku na wao watapewa makavu walipokuwa wanafanya siasa za majivuno. Mzee mwingine alisema ubatizo wa moto, alitegemea nani apatizwe kwa huo ubatizo? Mwingine alitaka wenzake wavuliwe gamba. Kikombe kichungu utakaponywesha wenzako ipo siku nawe utakinywea, siasa ndiyo zilivyo
 
Duh, ina maana nyumba, ofisi za watu , nguo nk vimetegwa vinasa sauti?
Duh hii sasa ni noma, walioleakisha hii kitu wameharibu sana interms of security, sasa hivi wanaopanga njama au mishe watakuwa extra carefu
 
Wapanga mpango wa kutoa tamko makusudi ili JPM aonekane mbaya huku wakijua fika kuwa Magufuli amepata tabu kuiweka Tanzania kwenye ramani ya haki na utawala bora kama ilivyokuwa enzi za Nyerere,
Wao ndo walio hujumu korosho, Sukari na kwe saruji pia kwa kushirikiana na wafanyabiashara wasiokuwa waaminifu.https://www.facebook.com/100034337745756/posts/157134872107770/
KUMBE WAO NDIYO WALIOPORA KOROSHO ZA WAKULIMA BILA KULIPA?
 
So kwako kumuita rais ni mshamba ni maongezi ya kawaida sio?
Kiufupi audio iko utube,sidhani kama ni halisi,lakini hata tukiassume ni halisi yale ni maongezi ya kawaida kabisa kati ya watu wawili na hakuna kitu cha ajabu,
kama hiyo audio ni ya kweli,yaweza kuwa wamevujisha wao wenyewe,ama ofisi walimokuwa wakiongelea iko bugged,ama simu zao ziko hacked,kwa maana kuwa simu zimekuwa remotely turned into a listening device kiasi kwamba ukiongea kitu na simu iko mezani inanasa maongezi na kutuma file kwa huyo mtu aliekuhack,
ni vyema kama unaongea maongezi ya faragha weka simu mbali au iweke ndani ya friji kwa ushauri wa snowden
 
Back
Top Bottom