Imenikuta katika kutafuta kazi

Vijana kuweni makini na poleni sana kwa mihangaiko. Yaani hawa matapeli, mtu anatafuta kazi hajui ataipata lini, wao wanataka kumtapeli, akatowe wapi hizo pesa jamani nae anatafuta kazi? si ataenda kukopa kwa nia njema kabisa, sasa akishatapeliwa huko alikokopa ataonekana yeye ndio tapeli na hatokuwa na pahala pa msaada tena.

Halafu, naomba vijana wakiwatokea tena watu kama hawa, muwawekee mitego ya kuwakamatisha, kubalini tu kuwa mkutane wapi muwapelekee pesa za polisi. Hawafai kabisa hawa watu.

Nawaonea huruma sana vijana. Poleni sana na msikate tamaa na Mwenyeezi Mungu atawapa kazi za halali na zenye heri kwenu na familia zenu. msirudishwe nyuma na hawa majambazi iwe ndio kichocheo cha kuwafanya mfanye bidii zaidi.
 
Mkuu siku hizi matapeli wapo mpaka mazikoni, majuzi juzi kuna maiti kaibiwa pete. Tujihazarini wakuu. na nashauri mods michango yetu waiwekee password.
 
Vijana kuweni makini na poleni sana kwa mihangaiko. Yaani hawa matapeli, mtu anatafuta kazi hajui ataipata lini, wao wanataka kumtapeli, akatowe wapi hizo pesa jamani nae anatafuta kazi? si ataenda kukopa kwa nia njema kabisa, sasa akishatapeliwa huko alikokopa ataonekana yeye ndio tapeli na hatokuwa na pahala pa msaada tena.

Halafu, naomba vijana wakiwatokea tena watu kama hawa, muwawekee mitego ya kuwakamatisha, kubalini tu kuwa mkutane wapi muwapelekee pesa za polisi. Hawafai kabisa hawa watu.

Nawaonea huruma sana vijana. Poleni sana na msikate tamaa na Mwenyeezi Mungu atawapa kazi za halali na zenye heri kwenu na familia zenu. msirudishwe nyuma na hawa majambazi iwe ndio kichocheo cha kuwafanya mfanye bidii zaidi.

Kweli CCM mmeshindwa kazi! Wakati wa kampeni mnasema mtatengeneza ajira mil.1, wakati wa utekelezaji mnakumbuka Mungu anatoa kazi!
 
Alipotaja mambo ya hela tu nikamwambia usijali nitakutafuta kesho nikukabidhi mzigo wako. Nilishtuka pia aliposema ni project ya miaka mitano ila wataniweka probation kwa miaka miwili! hapo ndio niliona hamna kitu

Bora umeshituka ndugu yangu, hata humu kuna mtu alitumia jina la JENNIFER UYAM alinitaka niwe rafiki yake, baada ya kumpa email yangu FAKE alinitumia maelezo ya utapeli wa kizamani, eti yeye ni mtoto wa waziri wa zamani sudani mara bla bla bla kibao anataka atume pesa zake kwenye acc. yangu halafu tugawane... how dare... SO SILLY!
 
Alikuwa anakugeuza ww uwe ajira yake ni ubunifu tu maisha baada ccm kushindwa kutoa zile ajira milioni moja!
 
Hawa watu ni wabaya sana, wametumia vibaya sana jina langu kutapeli watu ajira nimepiga hizo namba mbili kesho mapema akifika ofisini na security juu...hawa wanaipa ajira a bad name!
Hapa Mbeya walitaka kuwatapeli vigogo wa sekretarieti ya Mkoa wakitumia trick kali sana kwamba wao ni wafanya biashara wa Kimataifa. Mimi pia niliwahi kukutana na hii kitu enzi hizo nimeitwa kwenye interview ya Ofisi nyeti katika nchi walipoona namba zangu kwenye gazeti wakapiga simu na kunitaka nitoe shilingi laki moja ili niajiriwe kabla ya interview. Niliwaambia kazi nataka lakini hela sitatoa
 
kuna tapeli mwingine anajiita Mkurugenzi wa UNHCR Kigoma anatapeli sana watu anatumia namba 0718 171741 anapenda sana kutaja majina ya Dr. au proffesa fulani anapokuwa anasomesha mteja wa kumtapeli. niliponea tundu la sindano kuliwa ingawa na yeye aliponea bahati ya mtende kutiwa mbaroni. naomba sana wanausalama tumieni namba hiyo hapo juu kuwakamata matapeli wa hapa Bongo.
 
Yaan me nashangaa sana. Et cc watafuta ajra sasa hv 2megeuzwa mitaj!! Matapel wote sasa hv wamegeuzia makengeza yao kwa watafuta ajra! Inaumiza sana. Nakerwa mimi aaaagh!!
 
bora wewe wamekuomba hamsini tu, wengine wanaambiwa watoe mwili kwanza.
 
Ni juzi tu nimepigiwa simu na jamaa mmoja ambaye tulivyozidi kuongea na kumsikiliza vizuri sikutaka hata kukumbuka jina lake. Habari ilianza hivi; kanipigia simu akasema ameona namba yangu ya simu sehemu kuwa natafuta kazi, akasema wao wana NGO ya watu wa canada wanadeal na nyumba za watoto yatima, hivyo wanahitaji mtu mwenye ujuzi na elimu kama yangu. Mwisho kabisa anasema atanipa fomu mbili ambazo nitatakiwa kulipa 50,000 ili nipewe hiyo ajira!. Sielewi huu utaratibu na ndio maana sijarudi kwake tena wala sijamtafuta kama nilivyomuahidi kumtafuta baadae. Naomba niwaulize wakongwe katika haya mambo je hizi zimo au ndio kuibiana? maana bora hata angekuwa recruitment agent labda angesema ni utaratibu wao. Anyway kiufupi sijamfatilia tena.

Naombeni mawazo yenu tafadhali
kwanini umepigia picha, ofisini kwa baba yako?
 
mimi nilikutana na mmoja anayejifanya usalama wa taifa na anaweza kunitafutia kazi tra eti wana mkubwa wao wenye influence huko akasema nimtumie vyeti na majina yangu ktk mchakato kila saa anaomba vocha nikasema usalama gani huyu anaomba vocha kila saa mara kachukue barua za kazi tra huku hata jina langu hana.

let's be aware na hawa watu wenye njaa
 
Hata mimi yamenikuta nafikiri ni watu hao hao mmoja anayejiita Mr. Haule anatumia no. 0656 009 696 jana amenipigia kuniomba nimpigie kwani ana deal laku supply mikate anataka kuniunganisha na mtu ambaye ndiye muusika mkuu. Nikamwambia nipo barabarani ila nikifika ofisini nitampigia. Mambo yakawa mengi nikasahau, leo asubuhi huyo Mr. Haule akani beep nikampigia akanipa namba ya Mr. Emannuel 0717 500 036 ambaye ndio muhusika mkuu.

Basi nikampigia Mr. Emmanuel, lakini katika mazungumzo nikamshtukia mara moja kwanza anababaika kama mtu ambaye ameshaongea same issue na watu wengi, anyways akaniambia kuna vituo vya watoto yatima ambavyo anataka niwe na supply mikate na kwamba ni kazi kubwa hivyo inabidi tuonane tena leo. Hapo ndio nikazidi kuwa na mashaka, kwani kazi yenyewe ina uharaka gani mpaka tuonane leo tena Jumapili? Nikamdanganya nipo njiani naelekea Kibaha nitarudi jioni akasisitiza nikirudi toka kibaha hata jioni nimpigie ili tuonane, nikamwambia sitaweza tufanye kesho asubuhi. Nilipokata simu tu Mr. Haule akanibeep, nikampigia akaniuliza kama nimeshaongea naye na mimi nikam brief kila kitu akaniomba sana nikisha sign contract na yeye nisimsahau kumpatia kitu kidogo, nikamwambia haina tatizo asubiri mpaka kila kitu kitakapo mature.

Nimeshaepuka majaribio mengi ya kutapeliwa kwa njia ya simu kwani kama mtu simfahamu halafu ananipigia simu kutaka kunipa deal kwanza huwa najiuliza KWA NINI MIMI? Huyo mtu hana Marafiki au ndugu anaofahamiana nao mpaka anipe mimi deal wakati hata hatujawahi kuonana face to face? Kinachofuatia ili kupata uhakika wa majina yake huwa najaribu kutuma hela kwa Mpesa au tigo pesa au mtandao wowote atakaokuwa anatumia, kawaida kama namba imesajiliwa kabla ya ku confirm transaction lazima itaandika jina la mtu unayetaka kumtumia. Nilipojaribu kufanya hivyo kwenye hili jaribio nimekuta majina yaliyopo kwenye account zao za tigo pesa ni tofauti na walivyojitambulisha kwangu.

Cha pili nilichofanya ni ku google namba zao za simu ndio nimezikuta hapa kwenye JF.
 
Back
Top Bottom