Imenikuta katika kutafuta kazi

Mabagala

JF-Expert Member
Nov 27, 2009
1,477
325
Ni juzi tu nimepigiwa simu na jamaa mmoja ambaye tulivyozidi kuongea na kumsikiliza vizuri sikutaka hata kukumbuka jina lake. Habari ilianza hivi; kanipigia simu akasema ameona namba yangu ya simu sehemu kuwa natafuta kazi, akasema wao wana NGO ya watu wa canada wanadeal na nyumba za watoto yatima, hivyo wanahitaji mtu mwenye ujuzi na elimu kama yangu. Mwisho kabisa anasema atanipa fomu mbili ambazo nitatakiwa kulipa 50,000 ili nipewe hiyo ajira!. Sielewi huu utaratibu na ndio maana sijarudi kwake tena wala sijamtafuta kama nilivyomuahidi kumtafuta baadae. Naomba niwaulize wakongwe katika haya mambo je hizi zimo au ndio kuibiana? maana bora hata angekuwa recruitment agent labda angesema ni utaratibu wao. Anyway kiufupi sijamfatilia tena.

Naombeni mawazo yenu tafadhali
 
Hizo zimo katika aina mpya za utapeli..kwa vile suala la ajira limeonekana ni burning issue kuna watu wameanzisha mitandao ya kitapeli,mi nna ndugu yangu alipelekwa hadi kwenye ofisi ila akastuka.tuwe makini na pia tupeane habari...Information is power!
 
Alipotaja mambo ya hela tu nikamwambia usijali nitakutafuta kesho nikukabidhi mzigo wako. Nilishtuka pia aliposema ni project ya miaka mitano ila wataniweka probation kwa miaka miwili! hapo ndio niliona hamna kitu
 
Mpwa, achana nao hao ni matapeli sijapata ona, walishanipigiaga mara kibao kiasi kwamba wakishasikia sauti yangu wanalata simu,, eti wao ndio wanakazi halafu ana kwambia naomba nipigie!! Ukimpigia ndio anaanza kujieleza ooh mara nitumie vocha nimpigie huyo mtu....sijawahi kuwapa hata senti tano yangu, washenzi wakubwa hawa, mara ya mwisho mmoja nikamwambia ngoja nikituafute nikupatie hio pesa ila tuonane maeneo fulani nikiwa na nia ya kumkamata sijui hata kashtukia nnji, hajawahi kunitafuta tena....ok, take care Mpwa, na asante kwa share infor
 
Kuwa makini sana na matapeli,kwa uzoefu wangu huyo ni msanii,angekuita kwenye usaili,hakuna mashirika ya kimataifa yanayofanya madudu kama hayo ya huyo bwana.
 
Hata mimi huyu jamaa alianza na design za kubeep sana, infact ni mimi nilimpigia sio yeye aliyepiga. Akaomba vocha eti aongee na mkurugenzi wake ili nipange nae appointment tufanye interview. Akadai ngoja ampe huyo administrator wake ili niongee nae. Huyo ndio alifanya machale yanicheze, kwamba natakiwa kujaza fomu mbili ambazo nitalipia 50,000, pia itabidi wanicheki afya ili kama nina ukimwi basi wasiniajiri!. Bahati mbaya hawajapata kitu kwangu, na wala sijawasikia tena. Tuwe makini, kama angekuwa mtu katoka shule ana hamu ya kazi basi angetusumbia kuipata hiyo 50,000 ili akampe jamaa apate ajira. Pole na wewe mpwa kwa kuptezewa muda.
Mpwa, achana nao hao ni matapeli sijapata ona, walishanipigiaga mara kibao kiasi kwamba wakishasikia sauti yangu wanalata simu,, eti wao ndio wanakazi halafu ana kwambia naomba nipigie!! Ukimpigia ndio anaanza kujieleza ooh mara nitumie vocha nimpigie huyo mtu....sijawahi kuwapa hata senti tano yangu, washenzi wakubwa hawa, mara ya mwisho mmoja nikamwambia ngoja nikituafute nikupatie hio pesa ila tuonane maeneo fulani nikiwa na nia ya kumkamata sijui hata kashtukia nnji, hajawahi kunitafuta tena....ok, take care Mpwa, na asante kwa share infor
 
Ati!!! alipoona Mabagala akaona sijawahi ona maghorofa sio! lol. Nasubiri apige tena lakini naona kimya. Watu kama hawa wanatakiwa wakomeshwe. Huwezi jua watu wangapi yanawakuta
 
Naomba namba yake kuna kikosi malum cha kuwanasa hao wala isikupe shida,wanapunguzwa taratibu.
 
Kiongozi hebu nipe uhakika wa kitu ulicho comment, ni kweli kuna uwezekano wa kuwakamatisha hawa wahuni, ili tuokoe vijana, na hata watu wengine wanaoweza kutapeliwa kwa njia nyingine yoyote?
Mimi walikuja kwa style tofauti kidogo, nilikuwa nauza kiwanja changu maeneo flani, na nilikuwa nimetangaza kwa njia ya magazine, wakanipigia, jamaa akaomba vocha nikampatia eti awasiliane na mkuu wake, then tukapanga appointment pale Move n Pick, tukakutana wakanipa zaeti yupo na suveyor wao wanataka ku lease for 5 years na wanalipa $600 kwa mwezi, so kwa kuwa wananipa deal itabidi wao niwape $100 kila mwezi na option ni mimi kuamua nachukua pesa ya miaka yote 5 au kwa installments kadri navyotaka. Eneo walitaka kuweka mitambo ya mawasiliano/Booster. Man nilikwenda na mkulima the so called Surveyor akachuka sample ya udogo, tuakarudi...eti funny enough joini hiyo hiyo naambia results zinaonyesha eneo lipo ok na deal itakuwa fresh.....hapo ndipo nipoanza kuona uzushi, na nikapewa eti taratibu za tender lazima nitoe applicaation fee ya $50 plus other charges zisizoeleweka total ikafika $375 akawa anadai nimpatie hiyo amount kesho yake asubuhi pamoja na docs zangu...from there nilianza ku link dots...nika conclude ni upuuzi mtupu sikutaka kuhangaika nao tena. So these people are out there we need to fight them as we can.

Naomba namba yake kuna kikosi malum cha kuwanasa hao wala isikupe shida,wanapunguzwa taratibu.
 
Mmoja alisema anaitwa Amos, mwengine kama sikosei alisema anaitwa Emanuel, hebu cheki nao kwenye namba 0717500036 na 0714841243
Naomba namba yake kuna kikosi malum cha kuwanasa hao wala isikupe shida,wanapunguzwa taratibu.
 
mimi nilishawai kutana na mtu kama huyo-kwanza nilikuwa sijaapply kwenye ofisi zao,alikuwa anadai yupo barrick,kanda ya ziwa huko,yeye alifikia hatua akanipa namba ya mpesa,sikutuma then akanitsha kuwa deadline inakaribia nimtumie haraka,akanitumia acount number ya nmb,pia sikutuma,
nikaona anaendelea kulalamiak kuwa nachezea bahati-nikamwambia nitachezeaje bahata ambayo hata sijaaply?baada ya muda sijamsikia tena
 
Mm nawataka waje kwa hamu kwangu....then waone cha mtema kuni....ni moja kwa moja nawaandalia chezo la maana......, Pole mkuu
 
Wako wengi sana siku hizi wengine wanakujifanya transport officers kwa wenye daladala kazi kwao!!!
 
Hawa watu ni wabaya sana, wametumia vibaya sana jina langu kutapeli watu ajira nimepiga hizo namba mbili kesho mapema akifika ofisini na security juu...hawa wanaipa ajira a bad name!
 
Ngoja siku wapige kwangu ntawaambia ela ninazo mje kuchukua then nawasurrender police
 
Back
Top Bottom