Imagine ZITTO anahama CHADEMA

Status
Not open for further replies.
...Hata hii barua sioni umuhimu wake kuwa hapa... Je kuna mtu anapinga kuwa Zitto hasomi Ujerumani?....
 
Barua yenyewe mbona haisomeki vizuri...iko too light...

Halafu JF inaanza kuwa obsession na Zitto maana kila siku lazima kuwe na thread mpya inayomhusu Zitto. It's getting old...
Mkuu I do understand, kuna topic kibao zinamhusu Zitto, ukiangalia zinaunganishwa kwenye topic moja mama. Hata hiii baadae itaunganishwa huko huko, na nimeileta hii pekee ili kuonesha utofauti kidogo tu, kuwa yawezekana wakadai watu kuwa yuko financed nao lakini sidhani kama ni kweli, tujadili vitu tukiwa na facts kwenye meza.

Issues za magazeti ili yauze tuwaachie, ni suala la biashara!
 
Mkuu I do understand, kuna topic kibao zinamhusu Zitto, ukiangalia zinaunganishwa kwenye topic moja mama. Hata hiii baadae itaunganishwa huko huko, na nimeileta hii pekee ili kuonesha utofauti kidogo tu, kuwa yawezekana wakadai watu kuwa yuko financed nao lakini sidhani kama ni kweli, tujadili vitu tukiwa na facts kwenye meza.

Issues za magazeti ili yauze tuwaachie, ni suala la biashara!

Mkuu Invisible,

Afadhali umekata mizizi ya fitina. JF imevamiwa na wajinga wengi ambao hawaelewi hata maana ya facts.

Kazi ni kuzua tu kila siku, wanatia kichefu chefu ile mbaya.

Wanazua hata yale ambayo majibu yake yako hapa hapa JF. Kibaya zaidi hata hao wanaojiita waandishi wa habari ndio wamejilegeza ile mbaya kwa faida za mabwana wao ili waje hapa na kwenye magazeti yao kuchafua watu bila hata ya kuwa na chembe ya data.

Lakini njia ya kuumbua waongo na wapika majungu ni kuweka data kama ulivyofanya.
 
kwani zito ndio hawezi kuiama chadema, hivi bila yeye hakuna chadema, tusidanganyane na yeye pia ni binadamu na pia mawazo huwa yanabadilika wakati mwingine, mwacheni afanye anavyotaka bana, nakuunga mkono zito, chadema kuna ubaguzi na upendeleo
 
kwani zito ndio hawezi kuiama chadema, hivi bila yeye hakuna chadema, tusidanganyane na yeye pia ni binadamu na pia mawazo huwa yanabadilika wakati mwingine, mwacheni afanye anavyotaka bana, nakuunga mkono zito, chadema kuna ubaguzi na upendeleo

Sorry kijana hapa hatujadili chadema vs ccm,tunamjadili mwanasiasa Zitto.Sasa kama mnaona hii topic inachosha basi mambo mengi hamtayajadili kwa vile yatawachosha.Ndo maana Rais mstaafu aliwahi kusema "wtz ni wavivu sana wa kufikiri"yaani kila kitu wao wanaona uvivu kujadili na matokeo yake ndo hayo ufisadi kwa kwenda mbele.Anyway
.............ndivyo ilivyo, acha mie niende zangu nikajibebee mabox.
 
si ilitangazwa kuwa anafanya Doctorate na sio hiyo Masters hapo Bucerius?

Kama ulivyosikia Mkuu Epigenetics,Kabla ya kusoma degree ya Uzamivu(PhD),Zitto Kabwe ni chuo gani alisomea degree yake ya Uzamili(Masters)?

Au na yeye kama Adam Malima MB-Mkuranga;ambaye baada ya kumaliza form 4 alikwenda moja kwa moja kuchukua masters yake!Nasisitiza tena,badala ya kuhitimu form 4 na wala sio form 6 aMalima likwenda kuchukua Masters yake"saafi kabisa"kwenye nchi ya kikomunist!
 
Sidhani kama tunapaswa kujadili mambo ya kudhaniwa. Zitto yeye kama ameheshimika ndani ya jamii yetu binafsi anafahamu ni kina nani wanamheshimu na ni kwa lipi wanamheshimia. Basi tunamsubiri yeye mwenyewe kueleza kusudio lake ili tuanzie hapo kwenye hiyo fact kumjadili. Pia mh Zitto afahamu kukaa kimya kwake kwaweza kumaanisha tetesi anazotuhumiwa ni kweli.
 
Kuhama kwa Zitto kwa sasa hakuzuiliki kwa kuwa viongozi wenziwe wanaonekana kumkamia tangu. Mbowe angekuwa kiongozi makini na asiyeendekeza migogoro angeita mkutano wa waandishi wa habari na kumtetea Zitto. Lakini kwa kuwa Mbowe anaogofya na uwepo wa Zitto Chadema, anakaa kimya na anatumia kigazeti chake cha Mtanzania na vikaragosi vyake kumuangusha Zitto. Mbowe anavuruga imani kwa Chadema iliyokua imeanza kujengeka! Leo Zitto, jana Wangwe, Juzi Kaburu kesho ni wewe Mwanyika... Mbowe ni mfanyabiashara na si mwanasiasa
 
Nyerere alipokufa,baadhi ya wananchi walitahayari wasijue mwelekeo wa nchi ungekuwaje.Lakini pamoja na madudu yote yanayoendelea bado Tanzania iko hai.Hapo tunazungumzia kifo cha mtu na sio kuhama.Chadema itaendelea kuwepo hata kama Zitto atahama kesho.

Kwanza credibility yake imeshaingia mushkeli kutokana na baadhi ya matendo yake yasiyoeleweka vema kwa jamii.Anajivunia umaarufu alioupata kupitia kwa Chadema,na anaamini kuwa CCM wanamtamani kwa udi na uvumba.

I wish he would go tomorrow...good riddance
 
Zitto Ahame Chadema, Yes inawezekana lakini iwapo anahama ni kwa maslahi ya nani? Chadema itabaki kuwa Chadema, itatetereka kidogo lakini baadaye wataibuka kina Zitto wengine, pengine zaidi who knows. Mbona Kabouru alihama na sasa yuko wapi, je Chadema imeyumba kutokana na kutokuwapo kwa Kabouru?

Inawezekana pia kinachompa umaarufu mtu ni chama chake mwenyewe kutokana na uhuru anaopewa ndani ya chama. Naamini hakuna empty space. ukitoka mwingine anaijaza ingawa wakati mwingine kwa style tofaouti.

Heshima Mkuu, hayo ndo mawazo ya ukweli.
 
Tumechoka na story za Zitto na kuhama kwake, who is Zitto by the way. mnampandisha chati tu dogo wa watu ajione yupo matawi, mnamdanganya. walikuwepo kina Mrema enzi za NCCR ya ukweli, DR Kabour na chadema ya 1990's kule Kigoma harafu nyie mnaongelea kasisimizi ndani ya Chadema kwamba kanataka kukimbia, wapi na wapi JF.
 
Tumechoka na story za Zitto na kuhama kwake, who is Zitto by the way. mnampandisha chati tu dogo wa watu ajione yupo matawi, mnamdanganya. walikuwepo kina Mrema enzi za NCCR ya ukweli, DR Kabour na chadema ya 1990's kule Kigoma harafu nyie mnaongelea kasisimizi ndani ya Chadema kwamba kanataka kukimbia, wapi na wapi JF.

Nimeuliza kuhusu mchango wa Zitto katika mustakabali wa Tafa letu. Hakuna aliweza kunijibu. Nilitaka nielimishwe mambo matatu ambayo Zitto ameyafanya ambayo yatatufanya sisi wananchi tumkumbuke katika utumishi wake kama mwanasiasa na mbunge.
Haya ya kuhama au kutohama Chadema sioni ni jinsi gani yanaweza kutuletea maendeleo sisi na kuboresha uwajibikaji wa serikali yetu.

Naomba nirudie tena, Who is Zitto Kabwe na nini mchango wake katika Taifa au amelifanyia nini Taifa letu?
Naomba kuelimishwa!
 
kwani alivoingia CHADEMA kilitokea nini?akiondoka CHADEMA itaendelea kuwepo tu...kwani yeye ni nani?
 
nimeuliza kuhusu mchango wa zitto katika mustakabali wa tafa letu. Hakuna aliweza kunijibu. Nilitaka nielimishwe mambo matatu ambayo zitto ameyafanya ambayo yatatufanya sisi wananchi tumkumbuke katika utumishi wake kama mwanasiasa na mbunge.
Haya ya kuhama au kutohama chadema sioni ni jinsi gani yanaweza kutuletea maendeleo sisi na kuboresha uwajibikaji wa serikali yetu.

naomba nirudie tena, who is zitto kabwe na nini machango wake katika taifa au amelifanyia nini taifa letu?
naomba kuelimishwa!
kwanza kukuweka sawa ni kuwa zitto kesha sema hahami (kwa mdomo wake sio magazeti)
kafanya nini? Jibu ni kuwa zitto ni mbunge na tunaangalia michango yake ya mawazo ndani na nje ya bunge. Usiwe mvivu, tembelea tovuti ya bunge usome michango yake utapata jibu la maswali yako.
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom