Imagine ZITTO anahama CHADEMA

Status
Not open for further replies.
kwani alibatizwa chadema mtu anaweza kuhama wakati wowote ule , kama anaona hakuna utendeaji wa haki ,akae tu hapo? Kwanza anaweza kuachana na mambo ya siasa akaenda zake kuajiriwa kazi nzuri tu na akaishi vizuri.

kama anataka kujimaliza ahame!
 
kwani alibatizwa chadema mtu anaweza kuhama wakati wowote ule , kama anaona hakuna utendeaji wa haki ,akae tu hapo? Kwanza anaweza kuachana na mambo ya siasa akaenda zake kuajiriwa kazi nzuri tu na akaishi vizuri.

wewe dogo naona unajifunza politics ukiwa jeiefu!angalia historia za wanaohama hama!wote wamejizika kisiasa.

unapoona sehemu hakuna utendaji WEWE NDO UWE CHACHE YA UTENDAJIZ!anyways wewe naona huna unalolijua.somasignature yangu mdogo wangu!...............
 
Wewe umetokea wapi tena?
Mamaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
Haya MF mnatufanyia mambogani tena, mmekuwa mukiiandama CUF eti chama cha Seif na Lipumba, sasa nyinyi Chadema mmekuwa vp tena, Mbowe na wachagga wenzake siyo ndo wenye haki za kuhodhi ubosi wa chama siyo?
 
Thanks GT for the question!!!

Zitto anaweza hama, lakini dhamira yake itakuwa sawa?? to be honest, hata kama JK au MAndela wangehama vyama vyao winning the majority wouldnt have been the same... most likely, they would be losers!!!

Zitto and Chadema are synonymus! but that doesnt mean Zitto was born for CHADEMA and CHADEMA only...

A careful young person would have done what Zitto did, kachukua fomu knowing he has potentials!!! BUt in real political platforms hasa katika national levels; huwezi chukua fomu ya uenyekiti bila kufanya upembuzi wa kina na kupata feedback ya vetting gurus!!! in less that 12 months we have witnessed a few slip ups typical of a young, smart and ambitious young man!! Probably they expected some drama but what they got was dumb and dumber expose!!

Sadly the biggest loser of all this is CHADEMA!!!

Personnaly i would say prognosis towards the whole CHADEMA election was messed up and i am wondering what would happen if they were a ruling party!!!
 
Haya MF mnatufanyia mambogani tena, mmekuwa mukiiandama CUF eti chama cha Seif na Lipumba, sasa nyinyi Chadema mmekuwa vp tena, Mbowe na wachagga wenzake siyo ndo wenye haki za kuhodhi ubosi wa chama siyo?
Si na mimi ni mchaga?! Wacha wachaga tuile nchi bwana kama wapemba wanavyokula yao.
 
Mimi sioni cha ajabu, maana Mwalimu Nyerere alikuwa maarufu kuliko TANU na hatimaye CCM, Clinton alikuwa maarufu kuliko Democratic party, hivyo Zitto kuwa maarufu kuliko CHADEMA halijaharibika neno!
Itakuwa poa tuu,nisawa na wabongo wengi wanamjua Obama while hawajui chama chake,hii haitakuwa mpya hata kidogo!!!
 
Jamani kuhama au kutokuhama Chama ni uamuzi wa mtu binafsi na sioni kama Zitto akiamua kukihama chama itakuwa tatizo kubwa as ameamua kuufuata moyo wake. Cha muhimu lazima tukubali ukweli kuwa maisha yataendelea aidha Zitto akiwa Chadema, CCM, au chama chochote kile.

CHADEMA itaendelea kuwepo na Zitto ataendelea kuwepo, cha muhimu tuombe Mungu maslahi ya Nchi yapewe kipaumbele kuliko maslahi ya mtu mmoja mmoja.
 
wewe dogo naona unajifunza politics ukiwa jeiefu!angalia historia za wanaohama hama!wote wamejizika kisiasa.

unapoona sehemu hakuna utendaji WEWE NDO UWE CHACHE YA UTENDAJIZ!anyways wewe naona huna unalolijua.somasignature yangu mdogo wangu!...............

Geoff,

Salama ?kwanza nataka nikukumbushe kua si vizuri na hujatumia busara kuniita mimi Dogo !! na hata kama ningekua dogo ninaweza nikawa na fahamu mambo mengi ya siasa kuliko wewe.kwa hiyo naomba tutoe maoni kama vile wewe ni mtu mzima kama ulivyoonyesha kwenye mchango wako wa hii thread.

Jazba weka pembeni.

Haya tukija katika swala la Mh, Zitto.jibu la kwanza ni kwamba mwenye maamuzi ya mwisho ni yeye mwenyewe,kama anaona kuna kuhatarisha maisha yake sio lazima aendelee kukaa kwenye chama.Zitto anaweza akafanya kitu kingine hawezi akaaa tu anashabikia halufa akidhuriwa mtakuwepo kumsaidia ?ama ndio nyie hua mnakaa tu pembeni na kupiga kelele ?Mimi nimeshiriki kwenye mambo ya uchaguzi na kuna wakati nilishafikia kujitoa kwa manufaa ya familia yangu !! sio tu kung'ang'ania kwa sababu ya washabiki hiyo haifai mwacheni MBunge huyu kijana aaamue yeye na familia yake nini cha kufanya.nafikiri Bwana mkubwa umenielewa kidogo.

nasubiri maoni yako mkubwa

Radikali
 
Last edited:
Binafsi nilifikia kumwamini sana huyu bwana mdogo,ila anakoenda anaweza kuvuruga chama japo nae anaweza kuvurugwa baadae.

Kuna tetesi kibao kuwa tayari alisha nunuliwa na ccm na mafisadi ili kudhoofisha nguvu chadema na upinzani kwa ujumla,ndio maana alifikia kutofautiana na msimamo wa chama chake kuhusu mitambo ya dowans kwnai tayari kuna mkono wa akina lowasa na rostam amini usiamini huo ndio ukweli.

Naamini mimi naweza kuwa zito mpya nasubiri tu time. Bora aondoke na hakitaharibika chochote..........
 
Zitto sio Mungu wa CHADEMA wapo vijana wengi wazuri tu wakipata nafasi wataonesha uwezo wao vizuri.

Namkumbuka marehemu Sokoine huyu ndo alikuwa mwanasiasa waukweli anayeamini katika alichokuwa anafanya bila woga kwa maslahi ya taifa hawa wengine manyang'au tu.
 
Hata aondoke dakia hii bado chama Cha Demokrasia na Maendeleo kitaendelea kuwepo. Zitto si Mungu wa Chama.

Kwani akifa leo Zitto chama kitazikwa naye? Chama ni wanachama si mtu mmoja. Kwani Zitto ana umaarufu gani wakati ameshadanganywa akaanza kuchemka?? Tena uongozi na wanachama wa Chadema including Wazee wa chama wawe makini na Zitto, si mtu wao tena.

Ni kigeugeu huyo, hata akiwa mwenyekiti ndiyo kabisa atakipotosha chama kwa ukigeugeu wake. mara hataki kugombea ubunge, mara anabatilisha kauli, mara nataka uenyekiti mara anabatilisha kali kisa eti ni wazee amezingatia ushauri wao, mara vile mara vile. Ni fuata upepo wewe. Ulishaona debe tupu linatikiswa na upepo au miti?? Ndivyo mifano ya ZITTO ZUBERI KABWE!!
 
Mimi ningekuwa mshauri wa Zitto ningemshauri kuhama si sulihisho la matatizo yake na hatapacha chama ambacho ataishi milele bila misukosuko.

Zitto wakati akishutumiwa kununuliwa na mafisadi wakati wa ajenda ya kununua mitambo ya Dowans nilikuwa mmoja ya watu niliyemkingia kifua saaana tukiwa kwenye mijadala mbalimbali kufikia hata wakati wa kuhitilafiana na mume wangu. Na kuanzia pale zto amekuwa haelewi eleweki ila kwa mambo yanavyoendelea sasa naanza kupata wasi wasi.

Kuhama anaweza ila ajue asitegemee kwamba umaarufu utaendelea kama ulivyo. Asipewe kichwa na wapambe wake wachache na wana CCM walio na lengo la kuibomoa chadema akajiona bila yeye CHADEMA itakufa.

Sasa hivi anawalaumu watu ndani ya chadema kwamba wanamtuhumu fisadi, ila ajue hata wananchi wengi wana wasiwasi na hilo kwa namna fulani na ilianza mara aliposimama kidete mitambi ya Dowans inunuliwe. Pale alianza kuharibu. Na ni wapiganaji ndani ya CCM ndio waliosimama kidete kulisimamisha hilo. Je wakati ule ni CHADEMA ilimtuma? Mpaka leo Zitto hajawahi kutoa maelezo ya kuturidhisha kuhusu msimamo wake wa kununua Dowans. Zitto kuwa makini na kila maamuzi unayochukua.

Kwa mtazamo wangu mimi, Ukihama CHADEMA utanidhihirishia kwamba kuna mikono ya mafisadi. Jua kwamba hatukupendi sababu wewe ni zitto tunapenda kazi unayoifanya ndania ya chadema. Ukihama unahama mwenyewe na si rahisi kupata kundi la kuhama nalo kama Mrema.

Utaenda wapi? CCM si shwari wanafukuzana, NCCR ndio wale wale karibu kinakufa, TLP haitaweza kukaa na Mrema, CUF, lWEKATARE KAKIMBIA.
 
good stuff!
 
GT hiki chama kilikuwepo kabla ya Zitto na kitaendelea kuwepo hata baada ya zitto.Umaarufu wa mtu mmoja hauwezi kuua Chama chenye sera zinazokubalika na wanachama wengi!! Leo hii Jakaya akisema anaondoka CCM je unadhani wenye chama asilia watastuka? It will be good riddance ; same applies!!
 
Kuna personalities zinazoweza kukikuza chama na kukipa upeo mkubwa zaidi iwe katika philosophy au kiutawala. Pamoja na ukweli kuwa Zito hajafikia upeo huo lakini ametoa challenge ya kimtazamo na kimsimamo.
Kuongoza chama si maneno tu na maneno yenyewe yawe a one way street.

Kambarage hakuwa mjinga kuwaingiza hata wale watu wa hali ya chini kabisa na waliweza kumuelewa na kuliendeleza debe la siasa za Tanu na hatimaye CCM.

Mimi si mwana Chadema lakini kuondoka kwa Zito will be sill born. Upeo wa kisiasa Chadema bado haujafikia kileleni.
 
Mbona wamemchukua Lwakatare kwa mbewembewe na bado CUF iko juu evidence "uchanguzi wa serikali ya mtaa"..Zitto akihama anajimaliza..dawa ni kubanana huko huko..mimi siwaamini watu wanaokimbia vyama mara nyingi ni"Wabinafsi".
 
I always say that zitto is not "STABLE" at all,He is just popular like JK in 2005, but has nothing to do to Tanzanians,if he wishes to quite from our party, he better do it Now, Zitto is like a burden to the party now, every time we here Zito zito zito, who is ZItto by the way!!!!!!!,if he quite,essentialy he will leave a room for others to grow,lets not waste our time discussing about a person who is merely popular but usesless as we are witnesesing now.

ZITO,PLEASE,DONT SPOIL OUR PARTY,IF YOU WISH TO QUIT, YOU JUST QUITY AND LEAVE US!!! "I hope Zitto you will respond to my post"
 
GT,

Zitto kushindwa kunyakua uenyekiti wa CHADEMA hivi majuzi hakuendani na assertion yako kwamba Zitto ni maarufu kuliko CHADEMA (angalau ndani ya chama). Kinyume chake, jambo hili limeonyesha kwamba Zitto ni mwanachama wa CHADEMA ambaye alikuwa na ambitions za kuwa mwenyekiti akashindwa.

Maoni yako hayaonyeshi kutokana na ukweli wa mambo unavyoendelea.
 
mwache ahame tu kwani ameikuta CHADEMA ipo na itaendelea kuwepo
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom