SoC03 Ili kumuwezesha mhitimu wa chuo kujiajiri, serikali ikate asilimia 25 ya pesa yake ya kujikimu (boom) na kumlipa baada ya kuhitimu kama mtaji

Stories of Change - 2023 Competition

cupvich

JF-Expert Member
Aug 2, 2022
408
246
UTANGULIZI
Ndugu msomaji wa MAKALA hii Utakubaliana nami kwamba neno "KUJIAJIRI" sio geni masikioni mwako, hususa ni pale linapo kugusa moja Kwa moja. Huenda Kwa nyakati fulani umelisikia neno hili likitamkwa na Watu mbalimbali wakiwemo viongozi pamoja na watu maarufu na kulipokea Kwa mtazamo hasi au chanya. Ni ukweli kwamba vijana wengi wa kitanzania hususan wale wanaohitimu masomo yao kutoka vyuoni wanapata ugumu Katika kujiajiri hali inayopelekea kuwa tegemezi pale wanapohitimu, huku wengine wakikata tamaa ya maisha licha ya kuwa na elimu kubwa.

images (46).jpeg

(picha kutoka mtandaoni)

Pamoja na wahitimu wengi wa vyuo kuamini kuwa ni vigumu kujiajiri kutokana na sababu mbalimbali huku Sababu kubwa ikitajwa kuwa ukosefu wa MTAJI, Bado watu mbalimbali wakiwemo Viongozi wa Serikali wameendelea kusisitiza vijana kujiajiri. Makongamano mbalimbali yametumika pia katika kuwahamasisha Vijana kujiajiri. Lakini Kwa upande wa vijana wenyewe bado mwamko umekuwa mdogo.

KWANINI WAHITIMU WENGI WA VYUO WANASHINDWA KUJIAJIRI
Wahitimu wengi wanachukulia neno KUJIAJIRI Katika muktadha hasi, hali inayopelekea hadi kuwachukia viongozi wa serikali wanao waambia wajiajiri, Zipo sababu nyingi zinazosababisha vijana kushindwa kujiajiri baada ya kuhitimu masomo yao kama vile ukosefu wa mtaji, uoga (kukosa udhubutu) na kutokuwa na maarifa ya kutosha kuhusu fursa za kujiajiri. Ili kukabiliana na changamoto hizo,Serikali pamoja na Asasi mbalimbali za kiraia zimekuwa zikiandaa matamasha na makongamano mbalimbali ya kuwaleta pamoja vijana na kuwapatia elimu.

images (47).jpeg

(picha kutoka mtandaoni)

Changamoto kubwa imebaki kuwa ukosefu wa MTAJI ili kuweza kujiajiri. Upo msemo usemao "MANENO MATUPU HAYAVUNJI MFUPA" Ndugu msomaji utakubaliana nami kwamba ili vijana waweze kujiajiri lazima wawezeshwe elimu pamoja na mtaji. Vijana wengi wanapomaliza masomo yao na kurudi nyumbani wanakuwa hawana mtaji wa kuwawezesha kujiajiri licha ya walio wengi Kupata mkopo wa Serikali kama pesa ya kujikimu wawapo vyuoni. Hii ni kwasababu walio wengi wanashindwa kuweka akiba.

NAMNA MAKATO YA ASILIMIA 25 KUTOKA KWENYE PESA YA KUJIKIMU (BOOM) YANAVYOWEZA KUMSAIDIA MHITIMU WA CHUO KUPATA MTAJI WA KUJIAJIRI
Imefika wakati Sasa Serikali imsaidie mhitimu wa chuo Katika kujiajiri Kwa kumuwezesha Kupata mtaji ambao utamsaidia kuanzisha programu au biashara ambayo Itamsaidia Kupata kipato na kuacha fikra potofu kwamba Kila MSOMI ni lazima aajiriwe serikalini. Ni lazima vijana waamini kuwa KUJIAJIRI NI FURSA YA KUWA TAJIRI KULIKO KUAJIRIWA". Kama tunavyojua hali ya uchumi wa nchi yetu haijawa imara sana kiasi cha kuweza Kutoa MITAJI Kwa wahitimu wote wanaotoka Vyuoni, Hivyo kupitia njia ya kukata asilimia 25 kutoka Katika pesa ya kujikimu ya mwanachuo awapo chuoni na kumtunzia, na baada ya kuhitimu kumlipa itamsaidia Kupata mtaji wa Kuanzishia Biashara au programu ndani au nje ya taaluma yake.

Screenshot_20230717-124511_1689602794855_1689602811317.jpg

(picha kutoka mtandaoni)

Serikali yetu chini ya Raisi wetu mheshimiwa Dkt. Samia suluhu Hassan imeongeza kiwango Cha pesa ya kujikimu Kwa mwanachuo hadi kufikia Tsh 10,000 Kwa siku na Kwa mwaka wa fedha 2023/2024 serikali imedhamiria kuanza Kutoa mikopo Kwa wanafunzi wa vyuo vya kati. Mchanganuo Ufuatao unaonesha kiasi anacholipwa mwanafunzi wa chuo kikuu kama pesa ya kujikimu na asilimia 25 ya kiasi cha pesa ambacho ninapendekeza kikatwe na kutunzwa Kwa ajili ya kumsaidia Mhitimu kama mtaji baada ya kuhitimu masomo yake. (Mchanganuo huu ni Kwa wale wanachuo wanaosoma Kwa muda wa miaka mitatu chuoni)
  • Muda wa masomo - miaka 3
  • Idadi ya mihula ya masomo - 6
  • Idadi ya mihula Kwa mwaka- 2
  • Idadi ya miezi Katika muhula - 4
  • Idadi ya Siku Katika muhula- 120
  • Kiwango Cha pesa ya kujikimu Kwa Siku - 10,000/=
  • Kiwango Cha pesa ya kujikimu Kwa muhula mmoja- 120 X 10000= 1,200,000/=
  • Kiwango Cha pesa ya kujikimu (bumu) Kwa mwaka mmoja wa masomo-2X1,200,000= 2,400,000/=
  • Kiwango Cha pesa ya kujikimu Kwa miaka mitatu ya masomo- 3 X 2,400,000= 7,200,000/=
  • Asilimia 25 ya pesa ya kujikimu Inayopendekezwa kukatwa = 1,800,000/=.
Hivyo kutokana na mchanganuo huo hapo juu utagundua kuwa asimilia 25 ya pesa ya kujikimu ni tsh 1,800,000 (millioni Moja na laki nane), Hicho ni kiasi ambacho Mhitimu wa chuo akilipwa Kwa Wakati mmoja mara baada ya kuhitimu masomo yake kinaweza kumsaidia mtaji Katika kujiajiri Kwa kufanya Biashara au kuendesha programu inayoweza kumuingizia kipato. kupitia mtaji huo wa tsh 1,800,000 mhitimu wa chuo kikuu anaweza kujiajiri na kusahau kabisa kuajiriwa Katika taasisi za Umma au Binafsi.

Kuweka akiba ni jambo gumu Kwa wanachuo walio wengi kutokana na changamoto zinazo weza kujitokeza vyuoni, hivyo Serikali kupitia Bodi ya mikopo ya elimu ya juu haina budi kuchukua jukumu la kukata kiasi hicho Cha pesa na kukitunza Kwa ajili ya kuwapatia wahitimu pale wanapohitimu masomo yao. Kupitia mtaji huo wa 1,800,000 (millioni Moja) Mhitimu ataweza kufanya kazi mbalimbali za Ujasiliamali, Biashara, kilimo na hata kazi zilizoendana na taalamu yake kama vile kufungua kituo Cha masomo ya ziada Kwa Walimu, na duka dogo la dawa Kwa wataalamu wa afya.

HITIMISHO
Kijana ndio Nguvu kazi ya taifa, Serikali pamoja na wadau wengine hawana budi kutengeneza mazingira rafiki kwa kijana kujiajiri, Mazingira ambayo yatamfanya kijana kuondoa fikra kwamba baada ya kuhitimu masomo ni lazima aajiriwe, Elimu ya darasani ibakie tu kuwa ufunguo wa maisha Kwa kijana ambaye ni Mhitimu wa chuo kikuu au chuo cha kati. Kwa kufanya hivi vijana wataondoa utegemezi na kukuza uchumi wa taifa.Na hivyo Kupitia njia hii ya Kukata asilimia 25 kutoka katika pesa ya Kujikimu na Mhitimu kulipwa pesa yake baada ya kuhitimu, dhana ya KUJIAJIRI Itatimia.
 
Hii nchi ina fursa nyingi sana za kutengeneza ajira kwa wahitimu tatizo ni aina ya viongozi tulio nawo! Katiba mpya kwanza mengine yafata
 
UTANGULIZI
Ndugu msomaji wa MAKALA hii Utakubaliana nami kwamba neno "KUJIAJIRI" sio geni masikioni mwako, hususa ni pale linapo kugusa moja Kwa moja. Huenda Kwa nyakati fulani umelisikia neno hili likitamkwa na Watu mbalimbali wakiwemo viongozi pamoja na watu maarufu na kulipokea Kwa mtazamo hasi au chanya. Ni ukweli kwamba vijana wengi wa kitanzania hususan wale wanaohitimu masomo yao kutoka vyuoni wanapata ugumu Katika kujiajiri hali inayopelekea kuwa tegemezi pale wanapohitimu, huku wengine wakikata tamaa ya maisha licha ya kuwa na elimu kubwa.

View attachment 2691232

View attachment 2691233

View attachment 2691238

Idea nzuri sana. Hongera mwandishi
 
Itoshe kusema kuwa una mawazo ya kimaskini.
Yaani laki 3 unataka mtu akatwe.
Umaskini mbaya sana.
Watumishi tunakipesheka mpaka sh. 50 milioni lakini bado maisha magumu.
Hivi milioni na laki 8 utafanya biashara gani?
Hiyo hata fremu tu sehemu iliyocganfamka hupati.
 
Unapopinga hoja unatakiwa utoe wazo la kuboresha.

Jambo ambalo unashindwa kuelewa ni kwamba wanafunzi wengi wanatumia BUMU vibaya kiasi cha kumaliza hadi nauli... kama huyu mhitimu anakosa nauli anapohitimu chuo, Vipi kuhusu MTAJI?

Ni vigumu kwa mwanafunzi wa chuo kuweka akiba anaposoma. Hivyo njia hii itamuwezesha Kupata kiasi kikubwa kidogo pindi anapomaliza masomo.

Labda jambo la kuboresha ni kwamba kama mwanachuo atakatwa asilimia 25 basi na serikali imuongezee asilimia hata 25 ili ziwe 50 aweze kufanya jambo kubwa anapohitimu masomo yake. Angalau akipata 3,6000,0000 itamsaidia.
 
Hii nchi ina fursa nyingi sana za kutengeneza ajira kwa wahitimu tatizo ni aina ya viongozi tulio nawo! Katiba mpya kwanza mengine yafata
Fursa zipi hizo... na je fursa bila mtaji kuna uhakika kweli mwana jamii forum?
 
1. Kabla sijachangia hoja yako ningependa kujua ni wahitimu wangapi wanapata hiyo hela ya mkopo yote (100%) ili tuwe na hakika kuna cha kukata
2. Nafikiri ipo haja pia ya kuwafundisha hawa wasomi wetu kujiwekea akiba na sio kuchezea hela wakati mtu anajua kabisa ametoka familia ya kimaskini
3. Ifike mahali wazazi wajue kuwa, baadhi ya kozi za Chuo kikuu gharama zake ni ndogo kulinganisha na ada za shule ya Sekondari za binafsi hivyo wale wanaojiweza wawe na utamaduni wakuwalipia ada za Chuo watoto wao ili wakianza maisha, wasiwe na mzigo wa kudaiwa mkopo
 
3. Ifike wakati pia wazazi wajue kuwa, baadhi ya kozi za Chuo kikuu gharama zake ni ndogo kulinganisha na ada za shule ya Sekondari za binafsi hivyo wale wanaojiweza wawe na utamaduni wakuwalipia ada za Chuo watoto wao ili wakianza maisha, wasiwe na mzigo wa kudaiwa mkopo.
Utashangaa wazazi wanaojiweza wapo tayari hata kutumia njia ya mkato mtoto apate mkopo; bila kujua kuwa wanamtengenea mtoto mazingira magumu ya kuanza maisha na madeni....SHAME!
Na hii hupunguzia uwezo serikali kupata hela za kukopesha masikini au hata kukopesha mitaji kwa vijana...
Asante mwana

Asante mwana jukwaa.
Moja, takwimu mbalimbli zinaonesha kwamba sio wanafunzi wote wanaojiunga na vyuo vikuu wanapata mkopo au wanapata kwa asilimia zote 100. Hivyo bado wapo wanaoshindwa kupata kutokana na sababu mbalimbali.

HIVYO ili pendekezo hilo la kukata asilimia 25 ya bumu lifanikiwe vizuri, serikali haina budi kuhakikisha kila MWANAFUNZI ANAPATAMKOPO ASILIMIA 100.
 
Itoshe kusema kuwa una mawazo ya kimaskini.
Yaani laki 3 unataka mtu akatwe.
Umaskini mbaya sana.
Watumishi tunakipesheka mpaka sh. 50 milioni lakini bado maisha magumu.
Hivi milioni na laki 8 utafanya biashara gani?
Hiyo hata fremu tu sehemu iliyocganfamka hupati.
Bora hiyo mkuu wanamaliza chuo hao hawana akiba hata ya elfu 30.
Tunawaona wahitimu mtaani wanateseka sana,mhitimu hata elfu tano mfukoni hana.
Hili ni wazo zuri kwa kupata kianzio cha maisha,mengine yatajiongeza
 
Bora hiyo mkuu wanamaliza chuo hao hawana akiba hata ya elfu 30.
Tunawaona wahitimu mtaani wanateseka sana,mhitimu hata elfu tano mfukoni hana.
Hili ni wazo zuri kwa kuoata kianzio cha maisha,mengine yatajiongeza
Asante mwana jukwaa kwa kulitambua hili pia.

Haiwezekani mhitimu wa chuo anakosa hadi nauli ya kurudia nyumbani wakati alikuwa akipokea Bumu asilimia 100. Ni ukweli usiopingika kuwa vijana wengi wa chuo HAWAJUI KUWEKA AKIBA
 
1. Kabla sijachangia hoja yako ningependa kujua ni wahitimu wangapi wanapata hiyo hela ya mkopo yote (100%) ili tuwe na hakika kuna cha kukata
2. Nafikiri ipo haja pia ya kuwafundisha hawa wasomi wetu kujiwekea akiba na sio kuchezea hela wakati mtu anajua kabisa ametoka familia ya kimaskini
3. Ifike mahali wazazi wajue kuwa, baadhi ya kozi za Chuo kikuu gharama zake ni ndogo kulinganisha na ada za shule ya Sekondari za binafsi hivyo wale wanaojiweza wawe na utamaduni wakuwalipia ada za Chuo watoto wao ili wakianza maisha, wasiwe na mzigo wa kudaiwa mkopo
Umewaza vyema
 
UTANGULIZI
Ndugu msomaji wa MAKALA hii Utakubaliana nami kwamba neno "KUJIAJIRI" sio geni masikioni mwako, hususa ni pale linapo kugusa moja Kwa moja. Huenda Kwa nyakati fulani umelisikia neno hili likitamkwa na Watu mbalimbali wakiwemo viongozi pamoja na watu maarufu na kulipokea Kwa mtazamo hasi au chanya. Ni ukweli kwamba vijana wengi wa kitanzania hususan wale wanaohitimu masomo yao kutoka vyuoni wanapata ugumu Katika kujiajiri hali inayopelekea kuwa tegemezi pale wanapohitimu, huku wengine wakikata tamaa ya maisha licha ya kuwa na elimu kubwa.

View attachment 2691232
(picha kutoka mtandaoni)

Pamoja na wahitimu wengi wa vyuo kuamini kuwa ni vigumu kujiajiri kutokana na sababu mbalimbali huku Sababu kubwa ikitajwa kuwa ukosefu wa MTAJI, Bado watu mbalimbali wakiwemo Viongozi wa Serikali wameendelea kusisitiza vijana kujiajiri. Makongamano mbalimbali yametumika pia katika kuwahamasisha Vijana kujiajiri. Lakini Kwa upande wa vijana wenyewe bado mwamko umekuwa mdogo.

KWANINI WAHITIMU WENGI WA VYUO WANASHINDWA KUJIAJIRI
Wahitimu wengi wanachukulia neno KUJIAJIRI Katika muktadha hasi, hali inayopelekea hadi kuwachukia viongozi wa serikali wanao waambia wajiajiri, Zipo sababu nyingi zinazosababisha vijana kushindwa kujiajiri baada ya kuhitimu masomo yao kama vile ukosefu wa mtaji, uoga (kukosa udhubutu) na kutokuwa na maarifa ya kutosha kuhusu fursa za kujiajiri. Ili kukabiliana na changamoto hizo,Serikali pamoja na Asasi mbalimbali za kiraia zimekuwa zikiandaa matamasha na makongamano mbalimbali ya kuwaleta pamoja vijana na kuwapatia elimu.

View attachment 2691233
(picha kutoka mtandaoni)

Changamoto kubwa imebaki kuwa ukosefu wa MTAJI ili kuweza kujiajiri. Upo msemo usemao "MANENO MATUPU HAYAVUNJI MFUPA" Ndugu msomaji utakubaliana nami kwamba ili vijana waweze kujiajiri lazima wawezeshwe elimu pamoja na mtaji. Vijana wengi wanapomaliza masomo yao na kurudi nyumbani wanakuwa hawana mtaji wa kuwawezesha kujiajiri licha ya walio wengi Kupata mkopo wa Serikali kama pesa ya kujikimu wawapo vyuoni. Hii ni kwasababu walio wengi wanashindwa kuweka akiba.

NAMNA MAKATO YA ASILIMIA 25 KUTOKA KWENYE PESA YA KUJIKIMU (BOOM) YANAVYOWEZA KUMSAIDIA MHITIMU WA CHUO KUPATA MTAJI WA KUJIAJIRI
Imefika wakati Sasa Serikali imsaidie mhitimu wa chuo Katika kujiajiri Kwa kumuwezesha Kupata mtaji ambao utamsaidia kuanzisha programu au biashara ambayo Itamsaidia Kupata kipato na kuacha fikra potofu kwamba Kila MSOMI ni lazima aajiriwe serikalini. Ni lazima vijana waamini kuwa KUJIAJIRI NI FURSA YA KUWA TAJIRI KULIKO KUAJIRIWA". Kama tunavyojua hali ya uchumi wa nchi yetu haijawa imara sana kiasi cha kuweza Kutoa MITAJI Kwa wahitimu wote wanaotoka Vyuoni, Hivyo kupitia njia ya kukata asilimia 25 kutoka Katika pesa ya kujikimu ya mwanachuo awapo chuoni na kumtunzia, na baada ya kuhitimu kumlipa itamsaidia Kupata mtaji wa Kuanzishia Biashara au programu ndani au nje ya taaluma yake.

View attachment 2691238
(picha kutoka mtandaoni)

Serikali yetu chini ya Raisi wetu mheshimiwa Dkt. Samia suluhu Hassan imeongeza kiwango Cha pesa ya kujikimu Kwa mwanachuo hadi kufikia Tsh 10,000 Kwa siku na Kwa mwaka wa fedha 2023/2024 serikali imedhamiria kuanza Kutoa mikopo Kwa wanafunzi wa vyuo vya kati. Mchanganuo Ufuatao unaonesha kiasi anacholipwa mwanafunzi wa chuo kikuu kama pesa ya kujikimu na asilimia 25 ya kiasi cha pesa ambacho ninapendekeza kikatwe na kutunzwa Kwa ajili ya kumsaidia Mhitimu kama mtaji baada ya kuhitimu masomo yake. (Mchanganuo huu ni Kwa wale wanachuo wanaosoma Kwa muda wa miaka mitatu chuoni)
  • Muda wa masomo - miaka 3
  • Idadi ya mihula ya masomo - 6
  • Idadi ya mihula Kwa mwaka- 2
  • Idadi ya miezi Katika muhula - 4
  • Idadi ya Siku Katika muhula- 120
  • Kiwango Cha pesa ya kujikimu Kwa Siku - 10,000/=
  • Kiwango Cha pesa ya kujikimu Kwa muhula mmoja- 120 X 10000= 1,200,000/=
  • Kiwango Cha pesa ya kujikimu (bumu) Kwa mwaka mmoja wa masomo-2X1,200,000= 2,400,000/=
  • Kiwango Cha pesa ya kujikimu Kwa miaka mitatu ya masomo- 3 X 2,400,000= 7,200,000/=
  • Asilimia 25 ya pesa ya kujikimu Inayopendekezwa kukatwa = 1,800,000/=.
Hivyo kutokana na mchanganuo huo hapo juu utagundua kuwa asimilia 25 ya pesa ya kujikimu ni tsh 1,800,000 (millioni Moja na laki nane), Hicho ni kiasi ambacho Mhitimu wa chuo akilipwa Kwa Wakati mmoja mara baada ya kuhitimu masomo yake kinaweza kumsaidia mtaji Katika kujiajiri Kwa kufanya Biashara au kuendesha programu inayoweza kumuingizia kipato. kupitia mtaji huo wa tsh 1,800,000 mhitimu wa chuo kikuu anaweza kujiajiri na kusahau kabisa kuajiriwa Katika taasisi za Umma au Binafsi.

Kuweka akiba ni jambo gumu Kwa wanachuo walio wengi kutokana na changamoto zinazo weza kujitokeza vyuoni, hivyo Serikali kupitia Bodi ya mikopo ya elimu ya juu haina budi kuchukua jukumu la kukata kiasi hicho Cha pesa na kukitunza Kwa ajili ya kuwapatia wahitimu pale wanapohitimu masomo yao. Kupitia mtaji huo wa 1,800,000 (millioni Moja) Mhitimu ataweza kufanya kazi mbalimbali za Ujasiliamali, Biashara, kilimo na hata kazi zilizoendana na taalamu yake kama vile kufungua kituo Cha masomo ya ziada Kwa Walimu, na duka dogo la dawa Kwa wataalamu wa afya.

HITIMISHO
Kijana ndio Nguvu kazi ya taifa, Serikali pamoja na wadau wengine hawana budi kutengeneza mazingira rafiki kwa kijana kujiajiri, Mazingira ambayo yatamfanya kijana kuondoa fikra kwamba baada ya kuhitimu masomo ni lazima aajiriwe, Elimu ya darasani ibakie tu kuwa ufunguo wa maisha Kwa kijana ambaye ni Mhitimu wa chuo kikuu au chuo cha kati. Kwa kufanya hivi vijana wataondoa utegemezi na kukuza uchumi wa taifa.Na hivyo Kupitia njia hii ya Kukata asilimia 25 kutoka katika pesa ya Kujikimu na Mhitimu kulipwa pesa yake baada ya kuhitimu, dhana ya KUJIAJIRI Itatimia.
Tuendelee kupitia andiko hili wana jf
 
Back
Top Bottom