Uchaguzi 2020 Ilani ya uchaguzi ya CHADEMA kuathiri ndoa na ajira

RMC

JF-Expert Member
Nov 16, 2013
1,338
1,757
Nimeisoma ilani ya uchaguzi ya CHADEMA kurasa zote. Nimeona kasoro nyingi sana lakini kwa leo nitazungumzia kaosro mbili ambazo zina athari kwa jamii ya watanzania nazo ni ndoa na pia kwa watakaokuwa wanamaliza masomo na kutafuta kazi. Pia nitazungumzia na ushoga jao haupo katika ilani lakini Lissu amekuwa akiutetea.

NDOA
Ilani ya CHADEMA inakusudia kuweka sheria ya kutambua kitu wanachoita ubakaji ndani ya ndoa. Wanasema kuwa wakiingia madarakani watafanya kuwa ni kosa la jinai ubakaji ndani ya ndoa. Tuangalie athari ya hii sheria. Sheria hii itamuamini mke kwa anachokisema kuliko mume hata kama mume atakuwa anasingiziwa. Fikiria ndani ya nyumba mpo wawili tu mke na mume, mnaweza mkafanya mapenzi kwa ridhaa kabisa lakini mke akaamua kumkomoa mume kwa sababu ya ugomvi wao mwingine mathalani mume amezaa nje ya ndoa au ana nyumba ndogo au mke anataka kuondoka katika ndoa lakini mume anamng;ang;ania. Hivyo anaweza akafanya mapenzi kwa ridhaa yake na kisha asubuhi akaenda polisi kushtaki kuwa amebakwa na mumewe. Uwepo wa mbegu za mume katika uke wa mkewe unaweza ukawa ndio ushahidi ambao mke anautumia lakini kumbuka kuwa katika mazingira yao ya ndani si rahisi kutofautisha ni lini mbegu katika uke zimeingia kwa ridhaa au kwa kubakwa. Sheria hii ikipitishwa waume wengi watafungwa tena kwa kuonewa. Athari ya pili mume akishafungwa atapoteza kazi, pensheni ya jumla na ile mwezi kwa sababu kwa wale wanaofanya serikalini wanapopatikana na hatia katika jinai yeyote hufukuzwa kazi. Jambo hili litaleta mvurugano mkubwa katika jamii ya watanzania. Lissu na CHADEMA hawalizungumzii hili na kwa kuwa wanajua watanzania wengi ni wavivu wa kusoma basi wanajua si rahisi kulielewa jambo hili ambalo lipo ndani ya ilani yao.

Ninanukuu hicho kipengele katika ilani ya CHADEMA: “Kufanyia mabadiliko sheria ya Ndoa ili kuhakikisha kuwa ubakaji ndani ya ndoa unatambulika kuwa ni kosa la jinai” {f (a) ukurasa wa 46}.

USHOGA
Hivi karibuni Lissu alipozungumza na waandishi wa habari kabla ya kurudisha fomu alithibitisha kutetea ushoga kwa kisingizio kuwa katiba ya Tanzania inatambua haki ya faragha hivyo kinachofanyika ndani ya vyumba sio jukumu la serikali kujua. Hapa Lissu anapotosha makusudi na anajua kuwa anapotosha. Suala linaloleta mgogoro mpaka watu wengine tunapinga ni kuwa hawa mashoga wanataka watambulike rasmi. Maana yake sheria za nchi zitambue ushoga hivyo waweze kufunga ndoa, maana yake wapenzi wawili wa jinsia moja wakienda bomani basi wafungishwe ndoa ya kiserikali na hata ndoa za kidini. Pili waweze kupata stahiki ambazo wanandoa wa kawaida (mwanaume na mwanamke) wanazopata makazini. Tatu miundombinu mbalimbali iwe rafiki kwa watu wanaofanya ushoga kama vile vyooni kuwekewa huduma za kutupa uchafu wao kama unaotokana na kuvuja kinyesi katika pampasi pamoja na kupewa vilainishi. Nne waweze kuwa na haki ya kulea watoto; nchi ambazo ushoga ni halali wanaruhusiwa kukodisha matumbo kwa wamama hata nje ya nchi zao ili kuzalishiwa watoto na kuja kuishi nao kama familia moja ndani ya nchi zao. Kwa mfano nchini Israel wamefanikiwa kudai walipiwe baadhi ya gharama na serikali katika utafutaji huo wa watoto nje ya nchi. Hivyo mwisho wa siku jambo hilo la ushoga linakuwa sio lao peke yao wahusika bali linatuhisisha wote kwa maana ya kutumia kodi zetu bila kujali wengine ni wakristu, waislamu, dini za asili na imani zingine ambazo hazitaki kabisa jambo hilo.

Ukichukulia hilo jambo linaloitwa ubakaji ndani ya ndoa na ukaongeza na lile la ushoga basi kutakuwa na athari kubwa sana ya kijamii na kifamilia

AJIRA
Ilani ya CHADEMA inaeleza kuwa katika Halmashauri wataanzisha kanzidata ya kuwasajili vijana ili kuandikisha taaluma zao, Kifungu hicho kinaeleza kuwa yule ambaye alitangulia kujiandikisha ikitokea kazi ya taaluma yake ataajiriwa yeye kwanza ili kuondoa hicho CHADEMA wnachoita upendeleo katika ajira.

Athari kubwa ya jambo hili ni kuwa kutakuwa hakuna ushindani wa kupata ajira katika taaluma ya aina moja bali itategemea kigezo kimoja tu cha nani alitangulia kujiandikisha. Jambo hili litawa condemn baadhi ya wahitimu hasa wale ambao ni competent zaidi wasiweze kuajiriwa pengine maisha yao yote hivyo itaua morali wa mwanafunzi kusoma kwa bidii. Pia waajiri watanyimwa haki ya kuchagua mfanyakazi bora anayeweza kutoa tija kubwa. Ushindani siku zote ndio njia bora ya kupata kilicho bora ndio maana hata kwenye siasa kuna uchaguzi ili wananchi wachague kilicho bora zaidi sasa kwani nini waajiri wanyimwe haki hii? Tuliosoma tunaelewa kuwa mtu anaweza kusoma na kumaliza chuo kuijanjaujanja kama vile kujaziwa maksi nzuri na wahadhiri kwa kutoa rushwa ya ngono, pesa, undugu na mambo mengine ya kibnafsi lakini kiutendaji akawa haelewi kitu.

Kwanza ieleweke kuwa sio kweli kuwa kila anapoajiriwa mtu basi amepata kazi hiyo kiupendeleo. Pili utaratibu huo sio njia sahihi ya kumaliza hicho wanachoita upendeleo.

Ninanukuu hicho kipengele katika ilani ya CHADEMA: “Chadema itaweka utaratibu kwa kila Halimashauri nchini kuwa na kanzi data ya vijana kuweza kujiandikisha juu ya taaluma zao na hivyo kuwa na senta moja ya utambuzi wa vijana ambao hawana ajira na pindi fursa itakapopatikana kulingana na uwezo na au taaluma ya kijana husika wataweza kujulikana na kuajiriwa, na hii itaondoa upendeleo na kujuana katika kutoa ajira kwani wataajiriwa kulingana na sifa na yupi alitangulia kujiandikisha” {g ukurasa wa 48}.

Waandishi wa habari msaidie kuzisoma ilani hasa za vyama hivi vitatu CCM, CHADEMA na ACT Wazalendo na kuwaelezea wananchi kupitia vyombo vyenu vya habari ili wanapofanya uamuzi tarehe 28/10/2020 wasije wakajutia kwa maamuzi yao. Naamini hata wengi wa wale mashabiki kindakindaki wa Lissu na Zitto hawajaisoma ilani ya vyama vyao na kuzielewa.
 
Back
Top Bottom