Precious Diamond
JF-Expert Member
- Jun 9, 2023
- 397
- 993
Katika sherehe za kukabidhiwa kazi leo, Askofu Malasusa amesema;
"Kumekuwa na majadiliano mengi kuhusu suala la ndoa za jinsia moja na kwamba jambo la ndoa za jinsia moja tuachieni viongozi wa dini kwasababu ni letu, sisi tunajua vitabu vimesema ndoa ni mume na mke full stop. Tunahitaji kuheshimu uumbaji wa Mungu aliyeumba mwanaume na mwanamke
"Na ndani ya neno la Mungu mwanadamu hapaswi kupewa uhuru tu lakini pia heshima ya neno la Mungu ndio linalotuongoza."
Rais Samia ameongeza kuwa, "kuna changamoto sana kwenye taasisi ya familia linapokuja suala la malezi, akisema Ripoti ya Utafiti ya Ufatiliaji wa Kaya mwaka 2022 ya Ofisi yaTaifa ya Takwimu inaonesha kwamba zaidi ya nusu wa watanzania walio katika umri wa kuoa au kuolewa hajaingia kwenye ndoa.
"Kwa wakazi wa mijini ni wastani wa 61.5 na vijijini ni asilimia 55.5, lakini wanaofanikiwa kuingia kwenye ndoa kuna changamoto mbalimbali zinazosabisha migorogoro kwenye ndoa, ukatili kwa watoto, matukio ya ukatili kuongeza huku wanawake wakiwa ni hawanga wakubwa na hivyo kutaka taasisi ya dini pamoja na wananchi kuhakikisha wanafanya kwa nafasi zao ili kupeleka kujenga taifa bora."