Ilani ya CHADEMA 2010-2015

:mad2: MUHIMU!!! NIKIWA MWANANCHI MPENDA MAENDELEO, NAJUA UMUHIMU WA UPINZANI. NASHAURI CHADEMA WAIWEKE RASIMU HII KATIKA PDF PROTECTED MODE ILI MTU AKIIFUNGUA ASIWEZE KUIBADILI. KUNA HATARI MAFISADI WA CCM WAKAIFUNGUA NA KUONGEZA VIPENGELE VYAO NA KUI UPLOAD UPYA KISHA CHADEMA WAKAONEKANA HAWAFAI KABISA. HUO NI USHAURI WA BURE. NAWAPONGEZA SANA CHADEMA
 
Mwanakijiji was right, INATISHA!!!

Daaaaym! Haki ya nani tena naanza kutamani CHADEMA !!!:A S 8:
 
Nimependa sana kuhusu Elimu maana mfumo uliopo Tanzania kwa sasa ni mbovu kabisa, ila kuwa na community colleges kama hapa Marekani ni vizuri sana
 
Kaka nimesoma hata mimi na pia kweli CHADEMA wamefanya mambo mengi sana CCM sio warudi Darasani bali wajifunze kufanya au kuona mengi toka CHADEMA. Hongera CHADEMA
 
Hii ndio Ilani, inachanganua vipaumbele na jinsi ya kuvitekeleza. Sio CCM wanasema Ilani kumbe ni ahadi bila ya kuwa na maelezo ya ufanikishaji wake....mtu mkubwa anasimama na kusema nitawaletea Meli! hahahah! ni sehemu gani ya ilani hiyo?

Tunaomba ilani ya CCM, CUF na wengine hapa ukumbini tuchambue pumba......
 
Ni Ilani Nzuri sana... Tatizo ni namna ya kuisambaza na kuhakikisha ujumbe uliomo unawafikia walengwa wapiga Kura wote kabla ya 30/10/2010.
na watanzania tulivyo wavivu kusoma sijui...ili kusaidia kuisambazaunaweza kui-attach na kuwatumia watu wote unao wafahamu nafikiri itasaidia wewe ukituma kwa watu 50 nao wakatuma angalau kwa watu 10 itasaidia...
 
"Katika kuinua ubora wa elimu CHADEMA inaamini kuwa Elimu bora ni walimu bora. Hivyo basi, CHADEMA itaweka mkazo katika kuwapatia walimu mafunzo bora na ujira stahiki ili waweze kuwa na maarifa ya kutosha na kutulia mashuleni"

Naam ili ndilo tatizo halisi!!! CHADEMA NITAKUNYWA SUMU JUU YAKO!!
 
Hii sehemu ya ilani imenikuna

Katika kupanua wigo na kuboresha elimu ya juu, Serikali ya CHADEMA itachukua hatua zifuatazo:
• Kulipiwa gharama kamili ya masomo ya Chuo Kikuu (Full Scholarship). Serikali ya CHADEMA itaanzisha mfuko wa elimu uitwao "Uhuru Scholarship Fund
 
:mad2: MUHIMU!!! NIKIWA MWANANCHI MPENDA MAENDELEO, NAJUA UMUHIMU WA UPINZANI. NASHAURI CHADEMA WAIWEKE RASIMU HII KATIKA PDF PROTECTED MODE ILI MTU AKIIFUNGUA ASIWEZE KUIBADILI. KUNA HATARI MAFISADI WA CCM WAKAIFUNGUA NA KUONGEZA VIPENGELE VYAO NA KUI UPLOAD UPYA KISHA CHADEMA WAKAONEKANA HAWAFAI KABISA. HUO NI USHAURI WA BURE. NAWAPONGEZA SANA CHADEMA
Hili nalo neno...
 
Hakika imetulia na ninaamini inatekelezeka. Kila kitu kiko wazi. Malengo na namna ya kutekeleza na ni measurable! Safi sana hii ilani. Aliyeiandika naye kichwa
 
Ilani ya Chadema imeandaliwa na Wazalendo wenye utaalamu na wenye uchungu na nchi yao: hasa jinsi licha ya kurundikana kwa maliasili Tz. watu wetu wameendelea kuwa maskini wa kutupwa.

Jambo ambalo linanitatiza ni kwamba labda Chadema hawajajiandaa vya kutosha kulinda kura zitakazopigwa kuwaunga mkono, hasa kutokana na Mgombea u-Rais wao kuwa shoulder higher than J.K.

Labda hii ni siri yao. Lakini jinsi CCM walivyojikita ktk kukwapua fedha za umma ku-finance kampeni zao za 2005 na 2010, ndivyo hivyo wanavyo-specialize katika kuiba kura au kununua vitambulisho vya wapiga kura ambao wanaonekana watawapinga. Chadema jihadharini.
 
Mwanakijiji was right, INATISHA!!!

Daaaaym! Haki ya nani tena naanza kutamani CHADEMA !!!:A S 8:

umenichekesha ngosha.. miaka karibu mitano ya harakati za mapambano ya fikra kweli una mashaka bado...?

La maana ni kuwa kama watu kweli wanaona hii ilani inauzika na ni nzuri wasibakie kuitafuna mbele ya kompyuta yao.. wanatakiwa kuizungumza, kuishawishi, kuijadili hata kama katika vikundi n.k?
 
Ndugu mnaweza kudownload Ilani ya CHADEMA hapa. Kwa kweli kama watanzania wangekuwa wanachagua sera basi nafikiri hii ilani imekamilika na ipo makini kwa maendeleo ya nchi.
View attachment 12998
 
Wadau, nimesikia na kuambiwa mengi kuhusu ilani hii kwamba ni ya kumwokoa Mtanzania kutoka katika hali duni kwenda katika hali bora. Naomba kama kuna mdau anayo atuwekee hapa kama yawezekana tuisome wenyewe. Kura yangu nitaitoa kwa chama chenye ilani bora, maana wakati umefika tuchague sera na sio sura.....
 
Ahsante sana mwanakijiji kwa kutuwekea Ilani ya Chadema nibofya nakuisoma,Hongera Chadema kazeni buti
 
Source:Sera ya Elimu ya CHADEMA

Sera ya Elimu na Elimu ya Uraia
Hali ya Elimu yetu Tanzania ikoje?
  1. Elimu bado ni ya kikoloni inayozalisha watwana.
  2. Mitaala haiendani na hali halisi ya kidunia.
  3. Wanafunzi wanalazimishwa kusoma kila somo kupata vyeti wakati vipaji haviendelezwi.
  4. Mpango wa Elimu ya Msingi wa kudandia uliyogubikwa na rushwa – Maandalizi ya walimu ni duni na rasilimali hazifikii walengwa.
  5. Bajeti ya elimu finyu sana – asilimia 9 tu!
  6. Tanzania ni nchi ya tatu kutoka mwisho duniani ambayo kiuwiano na idadi yake ya watu, ina idadi ndogo ya wasomi wa sekondari na vyuo.
  7. Elimu inawezeshwa kwa fedha za mikopo na misaada ya wahisani wakati fedha itokanayo na kodi atozwayo mwananchi inafanyiwa anasa tu.
  8. Gharama za elimu bado ni mzigo mkubwa kwa familia masikini.
  9. Mazingira ya elimu ni duni – madarasa, nyumba za walimu, maabara na vitabu.
  10. Mfumo wa Elimu hauna mtazamo wa Kijinsia hivyo hauweki mazingira mazuri ya kupata maarifa kwa wanafunzi wa kike na pia wanafunzi wenye ulemavu.
  11. Mazingira ya shule haya kidhi haja na sio rafiki kwa watoto wenye ulemavu wa viungo,wasioona na viziwi.
  12. Elimu ya teknohama hususan sayansi ya kompyuta haijaanzishwa.
  13. Mfumo wa elimu unaochelewesha kuhitimu – kuchelewa kuanza (miaka 7+) na kuchelewa kumaliza (2,7,6,3+)
  14. Elimu ya Uraia ni finyu na potofu.
  15. Michezo mashuleni imefutwa na hivyo kuziba vipaji vya watoto mfano UMITASHUMTA na UMISETA.


Serikali ya CHADEMA itafanyaje ili kuboresha Elimu ya Tanzania?

  1. Itabadili mitaala ya elimu – Italenga mahitaji na maslahi ya Taifa, mitaala itakayochochea fikra, udadisi, ugunduzi na kuendeleza vipaji.
  2. Itatenga kwa sekta ya Elimu na Elimu ya Uraia asilimia 35% ya bajeti yote ya Serikali – italenga kuboresha mazingira ya elimu, ya ufundishaji na uboreshaji wa maslahi ya Waalimu na kuweka mazingira mazuri kwa wanafunzi wenye ulemavu kupata elimu bila vikwazo
  3. Kamwe elimu haitategemea misaada ya wafadhili na hatutakopa ili kusomesha Watanzania. Elimu italipiwa na fedha za ndani kutokana na makusanyo ya mapato ya kodi na pia mkakati utawekwa ili mapato yote yanayotokana na uchimbaji wa madini yalipie elimu ya watoto wa Tanzania.
  4. Tutajali walimu kwa kuboresha kipato, makazi na mafunzo yao.
  5. Mfumo wa elimu utarekebishwa kwa kiasi kikubwa na utakuwa na mtazamo wa kijinsia ili tuoe fursa sawa kwa wananfunzi wa kike na wenye ulemavu katika kujifunza.
  6. Elimu itatolewa bure kutoka CHEKECHEA mpaka SEKONDARI.
  7. Tutashirikisha wadau wote muhimu kuweka mfumo wa elimu unaowahisha kuhitimu – kuwahi kuanza (miaka 5) na kuwahi kumaliza (2,6,4,3+)
  8. Elimu ya msingi itakuwa mpaka darasa na tisa (Kidato cha Pili) na itakuwa ni lazima kwa kila mtoto anaeishi Tanzania.
  9. Ushirikishwaji wa jamii na wanafunzi katika uendeshaji wa shule utaimarika ili kuboresha ufundishaji na uwazi katika matumizi ya pato la shule.
  10. Elimu sahihi ya Uraia inayochochea kujitambua na uzalendo itafundishwa katika ngazi zote.
  11. Kila mwanafunzi wa sekondari atafundishwa somo la sayansi ya kompyuta na utumiaji wa kompyuta.
  12. Tutageuza majengo yote ya Serikali Dodoma kuwa vyuo vikuu na vyuo vya ufundi kwa kuendelea na azma yetu ya kuachilia mbali mpango wa kuhamishia makao makuu kwenda Dodoma. Dodoma itakuwa ni jiji la vyuo na kitovu cha elimu cha nchi.
  13. Uendeshaji wa shule za msingi na sekondari itakuwa ni jukumu la Serikali za Mitaa na Serikali kuu itatunga sera, kusimamia utekelezajiwa sera na kugawa rasilimali kama fedha.
  14. Tutaelekeza kila halmashauri kwa kutumia rasilimali zao kuanzisha vyuo vya ufundi katika kila wilaya.
  15. Tutatoa kipaumbele katika elimu ya ujasiriamali ili Watanzania waweze kujiajiri baada ya masomo.
  16. Tutarejesha masomo ya biashara katika shule za sekondari ili kuwajenga vijana wa Kitanzania waweze kujiajiri.
  17. Tutao ruzuku kwa shule za sekondari na vyuo vya elimu ya juu. Tutabadili shule za serikali kuwa ni vituo vya ubora wa elimu ili kuondoa matabaka.
 
Source: Sera ya Ajira ya CHADEMA

Sera ya Ajira
Hakuna Ajira, Watanzania tukale wapi?

  1. Watanzania wengi wanaishi kwa kubahatisha – Asilimia 28 ya vijana wanaoishi mjini hawana ajira.
  2. Wafanyakazi wanakandamizwa – mifumo ya ajira ya soko holela inawaminya.
  3. Wafanyakazi wanazidi kupunguzwa bila maslahi yao kuzingatiwa.
  4. Wafanyakazi wa Kitanzania wanalipwa mishahara midogo kuliko wa kigeni kwa kazi ileile.
  5. Mishahara na mazingira ya kazi bado ni duni.
  6. Hakuna juhudi mahususi za kutengeneza ajira kwa Watanzania.
  7. Hakuna takwimu sahihi za masuala ya ajira.
  8. Wawekezaji wanaajiri wageni hata kwa kazi ambazo kuna Watanzania wengi wanaweza kuzifanya.


Serikali ya CHADEMA itatengezena ajiri nyingi na hasa kwa vijana, kivipi?
  1. Tutaweka kipaumbele kuweka mazingira ya kuongezeka fursa za ajira
  2. Tutatengeneza ajira milioni moja ndani ya mwaka mmoja wa utawala wa CHADEMA kwa kuimarisha sekta za ujenzi, madini, kilimo, utalii na huduma za jamii (walimu, madaktari na manesi)
  3. Tutakomesha ubaguzi wa ajira kwa watu wenye ulemavu na tutatoa motisha kwa mashirika yatakayoajiri watu wenye ulemavu na kuwaendeleza kitaaluma.
  4. Tutaweka sheria kali kulinda haki za ajira kwa wanawake na mashirika na makampuni yatakayo ajiri wanawake zaidi yatapewa motisha katika kodi na hata zabuni za serikali.
  5. Tutaweka mifumo yenye kulinda haki na maslahi ya wafanyakazi.
  6. Vyama vya wafanyakazi vitalindwa kisheria na kupewa nafasi kubwa katika kulinda maslahi ya wafanyakazi.
  7. Vyama vya wafanyakazi vitakuwa huru kweli kweli na itakuwa ni marufuku kwa serikali kuingilia utendaji wa vyama vya wafanya kazi.
  8. Tutasimamia wazawa na wageni wenye ujuzi unaolingana kulipwa sawasawa.
  9. Tutatunga sheria itakayohakikisha kuwa Wageni wataajiriwa pale tu hakuna mtanzania anayemudu kazi husika na kwamba Wawekezaji watafanya juhudi kufundisha Watanzania kumudu kazi hizo siku za mbeleni.
  10. Tutatoa msamaha wa kodi wa kiasi kwa kila atakaye ajiri mhitimu wa chuo mara baada ya masomo.
  11. Tutaweka kipaumbele umuhimu wa kurekebisha ajira na maslahi ya wafanyakazi.
 
Source: Sera ya Afya ya CHADEMA


Sera ya Afya
Hali ya afya Tanzania ikoje?
  1. Serikali imekwepa jukumu lake la kutoa huduma za afya kwa wananchi, imelifanya kuwa la kibiashara kuliko huduma.
  2. Huduma za afya nchini zimezidi kupororoka siku hadi siku.
  3. Bajeti ya Wizara ya Afya haina mtazamo wa kijinsia kwani madawa mengi yanayoagizwa nchini ni ya magonjwa ya jumla.
  4. Mpango wa afya ya msingi umeshindikana – wananchi wenye uwezo wanatibiwa na wasio na uwezo wanakufa kwa magonjwa yanayotibika kama malaria na kipindupindu.
  5. Wanawake wajawazito hawana uhakika wa maisha yao wakati wa kujifungua kwani katika kila wanawake elfu moja wanaojifungua sita hupoteza maisha yao kwa sababu ya mfumo mbaya wa afya usiojali kazi muhimu ya kuzaa.
  6. Ni wanawake 47 tu kati ya wanawake mia moja wanajifungulia hospitalini. Mafunzo kwa wakunga wa jadi hayatoshi na hakuna juhudi za kutatua tatizo hili.
  7. Maslahi ya wafanyakazi wa sekta ya afya ni finyu.
  8. Pesa za vita dhidi ya ukimwi zinaishia mifukoni mwa wajanja wachache.
  9. Upanuzi wa sekta ya afya haulingani na ongezeko la watu – Daktari mmoja anahudumia wagonjwa.
  10. Wagonjwa wachache sana wa Ukimwi wanapata madawa ya kurefusha maisha – madawa mengi yaliyotolewa kwa msaada yanaporwa na vigogo.
  11. Gharama za afya bado ni mzigo mkubwa kwa wananchi wa kawaida kiasi cha kupelekea kujitibu kwa matabibu wasiyofuzu ilhali viongozi wakitibiwa nje kwa kodi ya wananchi.
  12. Mzigo wa kulea wagonjwa wa Ukimwi limeachwa kwa akina mama majumbani peke yao bila msaada wowote wa serikali (serikali kuu na serikali za mitaa).


Serikali ya CHADEMA itafanya nini ili kuboresha huduma za Afya?
  1. Kupanua mpango wa bima ya afya kumshirikisha kila Mtanzania. Mkazo utawekwa katika kusisitiza ‘lishe bora’ na siyo ‘bora lishe’ – miongoni mwa wananchi Mamlaka za serikali za Mitaa zitaunda mfuko wa Hifadhi ya jamii kwa wananchi ili kuweka bima ya Afya kwa wananchi wengi vijijini.
  2. Mfumo wa Afya utajengwa kuanzia ngazi ya kijiji ili kupata mahitaji halisi ya madawa kutoka na historia ya magonjwa katika maeneo husika.
  3. Tutahakikisha bajeti ya wizara ya afya inakuwa na mtazamo wa kijinsia kwa kujali sana madawa muhimu kwa akina mama kufuatia masuala ya kimaumbile.
  4. Nguo za watoto wachanga kama nepi n.k hazitatozwa kodi VAT.
  5. Madawa yote muhimu kwa akina mama wajawazito na watoto hayatakuwa na kodi ya forodha na pia VAT.
  6. Ushuru wa forodha na VAT kwa vifaa vya hedhi utakuwa sifuri.
  7. Hamasa itatolewa kwenye utafiti, utumiaji na uboreshaji wa tiba zetu za asili.
  8. Elimu ya afya itatolewa ikiwemo kuhusu lishe ili kurekebisha mila na desturi ambazo zinaathiri afya ya jamii.
  9. Huduma zitakazolipiwa na serikali nje ya nchi ni zile tu zisizopatikana nchini na kwamba wananchi wote watapewa haki sawa ya kupata nafasi hizo.
  10. Vituo vya afya vitaanzishwa vijijini kuwapunguzia wananchi umbali wa kutembea kutafuta huduma za msingi.
  11. Itawajali na kuwahudumia Watanzania wenye kuishi na virusi vya ukimwi kwa kuweka mfumo bora utakaosimamiwa na serikali za Mitaa ili kuondoa mzigo wa kuhudumia wagonjwa kwa akina mama peke yao.
  12. Watanzania wote wenye kuishi na virusi vya ukimwi watapatiwa madawa {bure} na jamii kupitia serikali za vijiji na Mitaa na pia kupitia Asasi zisizo za kiserikali zitabeba jukumu la kuhudumia wagonjwa bila ubaguzi wa kijinsia.
  13. Tutatangaza malaria kuwa janga la kitaifa na tutoa huduma za afya kwa malaria bure.
  14. Huduma za afya zitatolewa bure kwa makundi maalum – waja wazito, vikongwe, wanafunzi, wenye kuishi na virusi vya ukimwi, watoto wachanga na walemavu
 
Back
Top Bottom