Ilani ya CHADEMA 2010-2015

Sera ya Kilimo​
Kilimo chetu kidemorora, kwa nini?

  1. Watanzania wengi bado wanalima kwa kutumia jembe la mkono.
  2. Kilimo bado kinategemea huruma ya mwenyezi Mungu kupata mvua.
  3. Soko finyu la mazao ya kilimo – Mengi yanaozea shambani, au kuuzwa kwa bei ya kutupa.
  4. Mifumo mibovu ya kuhifadhi na kusindika mazao ya kilimo.
  5. Sera potofu za soko holela zimeua kabisa motisha ya wakulima wa mazao ya chakula na yale ya biashara.
  6. Bado tunategemea mazao ya biashara tuliyorithi kutoka kwa wakoloni.
  7. Barabara hazifiki vijijini na hivyo mazao ya wakulima kuoza kabla ya kufika sokoni.

Serikali ya CHADEMA itafanya nini kurejesha hadhi ya kilimo na Wakulima?

  1. Kodi zote za pembejeo za kilimo zitafutwa ikiwemo VAT.
  2. Itatilia mkazo wa kipekee barabara zingiazo vijijini.
  3. Tutatumia mabonde yote, mito na maziwa katika kilimo cha umwagiliaji maji.
  4. Tutarejesha vyama huru vya ushirika na mali zake.
  5. Serikali itadhibiti ya soko holela ya mazao ya kilimo.
  6. Tutatoa ruzuku kwa wakulima wetu ili wazalishe chakula cha kutosha na pia kupambana na ushindani wa bidhaa hafifu kutoka nje.
  7. Tutatoa motisha kwa wakulima kuzalisha mazao mbadala ya biashara km maua, viungo, mboga.
  8. Tutatoa motisha katika sekta ya usindikaji ya mazao ya kilimo – maelekezo kwa halmashauri ya wilaya kuweka mazingira ya uwekezaji katika usindikaji wa mazao yapatikanayo ndani ya wilaya.
  9. Serikali itashirikiana na nchi zingine zinazoendelea kushinikiza nchi zilizoendelea kulegeza masharti ya kuuza bidha zetu za kilimo katika masoko yao.
  10. Tutalinda soko la ndani la bidha zetu.
  11. Tutatafsiri kilimo sio tu kuishia katika kulima na kuvuna bali kwenye kuzindika na kuongeza thamani ya bidhaa.
SOURCE-chadema.or.tz

Naombeni ufafanuzi kwa wanaofahamu data zaidi kuhusu sera hii,,mfano ni jinsi gani ulinzi wa soko letu la ndani utafanyika.
 
  1. Kodi zote za pembejeo za kilimo zitafutwa ikiwemo VAT. OK
  2. Itatilia mkazo wa kipekee barabara zingiazo vijijini. OK
  3. Tutatumia mabonde yote, mito na maziwa katika kilimo cha umwagiliaji maji. OK
  4. Tutarejesha vyama huru vya ushirika na mali zake. OK
  5. Serikali itadhibiti ya soko holela ya mazao ya kilimo. CHADEMA FAFANUA TAFADHALI
  6. Tutatoa ruzuku kwa wakulima wetu ili wazalishe chakula cha kutosha na pia kupambana na ushindani wa bidhaa hafifu kutoka nje. OK
  7. Tutatoa motisha kwa wakulima kuzalisha mazao mbadala ya biashara km maua, viungo, mboga. OK
  8. Tutatoa motisha katika sekta ya usindikaji ya mazao ya kilimo – maelekezo kwa halmashauri ya wilaya kuweka mazingira ya uwekezaji katika usindikaji wa mazao yapatikanayo ndani ya wilaya. OK
  9. Serikali itashirikiana na nchi zingine zinazoendelea kushinikiza nchi zilizoendelea kulegeza masharti ya kuuza bidha zetu za kilimo katika masoko yao. OK
  10. Tutalinda soko la ndani la bidha zetu. CHADEMA FAFANUA TAFADHALI
  11. Tutatafsiri kilimo sio tu kuishia katika kulima na kuvuna bali kwenye kuzindika na kuongeza thamani ya bidhaa. OK
SOURCE-chadema.or.tz

Naombeni ufafanuzi kwa wanaofahamu data zaidi kuhusu sera hii,,mfano ni jinsi gani ulinzi wa soko letu la ndani utafanyika.

Hiyo namba 9 na 10 zinahitaji ufafanuzi zaidi.................wana-Chadema mliopo hapa toeni ufafanuzi...............huyu bwana aliyeuliza atawafaa sana kuelimisha wale ambao watajiuliza kama yeye na mimi..............
 
Ni rahisi tu, watatoza kodi zaidi kwa bidhaa za nje ambazo tuna uwezo wa kutosha kuzizalisha hapa hapa nchini.
 
Kulinda soko la ndani maana yake ni kuweka Policy ambazo zitapunguza au kuzuia bidhaa kutoka nje ya nchi kushindana na za ndani. Njia mojawapo ni kuwawezesha wazalishaji wa ndani kutengeneza bidhaa BORA na zenye hadhi ya Kimataifa, Kuwapa uwezo wa kuzalisha kwa bei ya chini kulinganisha na zile za kutoka nje, kwa mfano kutoa ruzuku, au unafuu wa Kodi.

Ukifuatilia budget za Serekali ya CCM utaona hiki kipengele hakipo japo wanasema KILIMO KWANZA. Hivi karibuni walitoa unafuu kwa mafuta ya kupikia kutoka nje (Sijui kwa manufaa ya nani), wakati wakulima wa Alizeti, Ufuta na mazo mengine ya kuzalisha mafuta wakikosa soko mana viwanda vinakimbilia kuingiza mafuta kutoka nje. Hii ndio maana CHADEMA wameweka kuwa kuna haja sana ya kulinda mazao ya ndani kama kweli unataka kuondoa umasikini. Hili linafanyika kila mahali ISIPOKUWA TANZANIA!
 
Sera ya Kilimo​
Kilimo chetu kidemorora, kwa nini?

  1. Watanzania wengi bado wanalima kwa kutumia jembe la mkono.
  2. Kilimo bado kinategemea huruma ya mwenyezi Mungu kupata mvua.
  3. Soko finyu la mazao ya kilimo – Mengi yanaozea shambani, au kuuzwa kwa bei ya kutupa.
  4. Mifumo mibovu ya kuhifadhi na kusindika mazao ya kilimo.
  5. Sera potofu za soko holela zimeua kabisa motisha ya wakulima wa mazao ya chakula na yale ya biashara.
  6. Bado tunategemea mazao ya biashara tuliyorithi kutoka kwa wakoloni.
  7. Barabara hazifiki vijijini na hivyo mazao ya wakulima kuoza kabla ya kufika sokoni.

Serikali ya CHADEMA itafanya nini kurejesha hadhi ya kilimo na Wakulima?

  1. Kodi zote za pembejeo za kilimo zitafutwa ikiwemo VAT.
  2. Itatilia mkazo wa kipekee barabara zingiazo vijijini.
  3. Tutatumia mabonde yote, mito na maziwa katika kilimo cha umwagiliaji maji.
  4. Tutarejesha vyama huru vya ushirika na mali zake.
  5. Serikali itadhibiti ya soko holela ya mazao ya kilimo.
  6. Tutatoa ruzuku kwa wakulima wetu ili wazalishe chakula cha kutosha na pia kupambana na ushindani wa bidhaa hafifu kutoka nje.
  7. Tutatoa motisha kwa wakulima kuzalisha mazao mbadala ya biashara km maua, viungo, mboga.
  8. Tutatoa motisha katika sekta ya usindikaji ya mazao ya kilimo – maelekezo kwa halmashauri ya wilaya kuweka mazingira ya uwekezaji katika usindikaji wa mazao yapatikanayo ndani ya wilaya.
  9. Serikali itashirikiana na nchi zingine zinazoendelea kushinikiza nchi zilizoendelea kulegeza masharti ya kuuza bidha zetu za kilimo katika masoko yao.
  10. Tutalinda soko la ndani la bidha zetu.
  11. Tutatafsiri kilimo sio tu kuishia katika kulima na kuvuna bali kwenye kuzindika na kuongeza thamani ya bidhaa.
SOURCE-chadema.or.tz

Naombeni ufafanuzi kwa wanaofahamu data zaidi kuhusu sera hii,,mfano ni jinsi gani ulinzi wa soko letu la ndani utafanyika.

Ni rahisi tu, watatoza kodi zaidi kwa bidhaa za nje ambazo tuna uwezo wa kutosha kuzizalisha hapa hapa nchini.

Kulinda soko la ndani maana yake ni kuweka Policy ambazo zitapunguza au kuzuia bidhaa kutoka nje ya nchi kushindana na za ndani. Njia mojawapo ni kuwawezesha wazalishaji wa ndani kutengeneza bidhaa BORA na zenye hadhi ya Kimataifa, Kuwapa uwezo wa kuzalisha kwa bei ya chini kulinganisha na zile za kutoka nje, kwa mfano kutoa ruzuku, au unafuu wa Kodi.

Ukifuatilia budget za Serekali ya CCM utaona hiki kipengele hakipo japo wanasema KILIMO KWANZA. Hivi karibuni walitoa unafuu kwa mafuta ya kupikia kutoka nje (Sijui kwa manufaa ya nani), wakati wakulima wa Alizeti, Ufuta na mazo mengine ya kuzalisha mafuta wakikosa soko mana viwanda vinakimbilia kuingiza mafuta kutoka nje. Hii ndio maana CHADEMA wameweka kuwa kuna haja sana ya kulinda mazao ya ndani kama kweli unataka kuondoa umasikini. Hili linafanyika kila mahali ISIPOKUWA TANZANIA!

Thanks guys

Mkuu Simple,

umeshapata majibu................kama unalo la nyongeza uliza otherwise wafikishie ujumbe Wakulima na Watanzania kwa ujumla wake..........wale utakaoweza kuwafikishia ujumbe huu...............

Bandugu tuendelee na kuelimisha umma juu ya umuhimu wa kupiga kura kwenye uchaguzi huu.............watu wajifunze kuwa kura yao ina uwezo wa kumletea mabadiliko............yenye faida kama hizo hapo juu.........walizofafanua Wakuu Prof. Kichuguu na Mozze
 
Hiyo namba 9 na 10 zinahitaji ufafanuzi zaidi.................wana-Chadema mliopo hapa toeni ufafanuzi...............huyu bwana aliyeuliza atawafaa sana kuelimisha wale ambao watajiuliza kama yeye na mimi..............
Kulimit/kupunguza extremely importation ya bidhaa ambazo tuna uwezo wa kuzi zalisha sisi wenyewe kwa malighafi ambazo zinapatikana hapa nnchini. kwa mfano Juice za mabox kutoka uarabun, pamoja na maziwa ikiwa hapa nchini yanazalishwa kwa wingi tu. kuingiza tekinologia mpya ya uzalishaji na usindikaji wa mazao ya kilmo badala ya kuingiza V8 mpya kila mwaka. kutoa elimu ya micro-finance kwa wakulima, kuanzisha kiwanda madhubuti cha kutengeneza Vipakio (containers) au vyombo vya kuhifadhia mazao yetu. kwa kufanya yote hayo sidhani kama kutakua na haja ya kuanzisha vyama huru vya ushirika kwani kitu kama hicho kitazidisha makato kwa mkulima huku tukijua hakitakua fair.
yangu ni hayo tu mwenye marekebisho anakaribishwa.
 
Ilani ya Chadema imesema hivi:

muhimu kwa taifa kama msusuru wa magari ya maafisa, warsha, makongamano na safari zisizo za lazima na kuunda serikali ndogo inayozingatia tija ya matumizi ya fedha,ufanisi na utendaji. Katika kupunguza matumizi ya serikali, CHADEMA itafanya yafuatayo:
o Itapunguza mishahara na posho za viongozi wote wa juu wa kisiasa kuanzia Rais, hadi wakuu wa mikoa kwa asilimia 20. Mishahara na posho za wabunge zitapunguzwa kwa asilimia 15 huku mishara na posho ya watendaji wote na wakuu wa mashirika na taasisi za umma itapunguzwa kwa asilimia 15.
o Rais Slaa hatofanya safari ndefu za nje katika mwaka wa kwanza wa Urais wake. Ukiondoa safari za Baraza la Umoja wa Mataifa ambapo ni nafasi ya kukutana na kufahamiana na viongozi wengine duniani na za nchi majirani zetu, safari nyingine zote zitafanywa na viongozi wengine na kwa utaratibu utakaozingatia maslahi ya nchi, gharama, na faida inayopatikana kwa safari husika.
o Misafara yote ya viongozi wa juu wa serikali na taasisi zake zitawekewa utaratibu ili kuhakikisha kuwa ni watu wale tu wanaotakiwa kuwepo kwenye ziara hizo wanashiriki. Lengo ni kuhakikisha kuwa ziara za kiserikali hazitumiki kama mitaji ya posho.
o Kutokana na ukweli kuwa serikali imekuwa ikitenga kiwango kikubwa sana cha fedha katika posho ni muhimu serikali mpya kubadilisha utaratibu huo ili hatimaye kuinua mishahara ya watumishi wa umma. Kwa mfano, serikali ya CCM katika mwaka 2008/2009 ilitenga zaidi ya shilingi bilioni 509 (zaidi ya nusu Trilioni) kwa ajili ya posho mbalimbali. Hii ni sawa na malipo ya mwaka mzima ya walimu zaidi ya 109,000! Taarifa zinaonesha kuwa Ofisi ya Rais
49
ndiyo inaongoza kwa posho hizo ikijigawia zaidi ya shilingi bilioni 148 kwa mwaka wa 2009/2010 na Bunge ikijigawia zaidi ya shilingi bilioni 36 katika kipindi hicho hicho.
o Serikali ya CHADEMA itaweka utaratibu ili semina, warsha na mafunzo katika taasisi mbalimbali za umma yanafanyika ndani na katika wakati wa kazi na bila uwepo wa posho maalum za “vikao za siku”. Mafunzo au mikutano yoyote itakayofanyika nje ya vituo vya kazi itahesabiwa ni sehemu ya kazi na serikali italipia na kurudisha gharama za safari, hoteli na posho ya kujikimu. Utaratibu mkali wa kisheria utawekwa ili kuzuia ulaghai wa aina yoyote na kuhakikisha wale wote (wafanyakazi na watoa huduma) watakaoshiriki kuiibia serikali kwa nyaraka au risiti za uongo wanachukuliwa hatua mara moja ikiwemo kuachishwa ajira. Lengo ni kupunguza posho hizi kwa zaidi ya asilimia 80 zikiendana na nyongeza ya mishahara kwa watumishi wa umma kuendana na ujuzi, nafasi, na vyeo vyao kazini. Tunataka wafanyakazi wetu walipwe kwa haki kwa kile wanachofanya kwa haki.

Hatua ya Mbowe leo ni utekelezaji tu wa sehemu ya ilani yao. They did the talk; now they are doing the walking.
 
Kimtazamo na kimanti kwa jicho huru la siasa inatanabaisha wazi ccm itatumikia mlengo wa Chadema, baadhi wanayoyatekeleza ni ya Ilani ya Chadema, kuwa wakanushaji kila uchao ni dalili za kushindwa kusimamish
 
Mwanakijiji unaenda mbali saana kwa kuwaza Ilani.

Kamwe nchi hii, ilani haitaiangusha CCM. Leo hii tuulizane hapa hata kabla yakufika kule vijijini, ni nani aliisoma Ilani ya CCM ya 2005 na nani anaweza kuizungumzia utekelezaji wake! Jibu ni kuwa utashangaa saana. Wengi kati yetu tunapenda kusoma mistari miwili na kufunika na hao ndio tunajiita wasomi. Sasa, vipi kuhusu wanakijiji?

Matatizo ni makubwa saana katika kujisomea kwa Taifa letu na ndio maana hata umakini hakuna. Tena basi si kusoma tu hata kuandika. Jipe fursa upitie hata magazeti yetu utashangaa.

Kwahiyo binafsi naona CCM itaondoka madarakani kwa njia za kupayuka tu na kuzungumza na wananchi zaidi juu ya haki zao bila hata ya kuwaeleza ilani inasema nini!

Uko sawa maana idadi kubwa ya wapiga kura wanasubiri na kushabikia Upayukaji.
Lakini kwa wale wa aina ya Mzee Mwanakiji bado kuna haja ya Chama kuwa na Sera inayoieleweka(Muhimu sana).Lakini ikikufanikisha Ushindi upyukaji na kulipua mabomu ya Ufisadi na namna ya Umma na mtu mmoja mmoja kudai haki na uhuru ni hatua moja kuelekea kujitambua .

Mpiga Kura akishajitambua hatua inayofuata ni kudai kuona Mpango wa Mtaka nafasi ya Uongozi. Mifano iko mingi kwa sasa toka Uchaguzi wa 2005 na wa 2010 unaweza kuona Tofauti

Sera hii ya CDM natumai watakuwa wamekaa chini na kufanya tathimni kwa kufanya maboresho muhimu sana-65% inaleta matumaini .
Kwa sasa ukiongeza na hii hatua ya UKAWA ni vizuri Vyama hivi vikaanza kuwa na Memorundum of Understanding Mapema in writting kwa kuoanisha hizi Sera ilikuja na Kapu Mmoja mapema Kabla hata ya kuja na Mgombea mmoja-sidhani hii nalo kunakutegeana.

Kwa Upande wa CDM kuna haja 35% iliyobaki ifanyiwe kazi mapema.

Kwangu Mimi pamoja na maeneo mingine-bila kuona hesabu inayohusiana na namna ya kufikia Mipango tajwa bado nitaamini na kubaki kuwa ni hadidhi ile ile ya Serikali ya CCM bajeti trilioni 10 za ndani trilioni 4 hizo 6 usipopewa utafikiaje malengo?

Kwa hiyo hizi ndoto zakutuletea matumaini ziwe na hesabu (mapato ya Ndani kufikia malengo) na ibandikeni Vipengele Maaalumu.

SURA YA KUMI NA MOJA
VIPENGELE MAALUM
Mpango wa miaka kumi wa kuinua Tanzania

CC Kurugenzi ya Habari Tumaini Makene Ben Saanane

Hii ni bila kusahau Wimbo wa Ufisadi.

Ufisadi umetu cost kiasi .................... 2010 -2015
Misahama ya Kodi kiasi...................... 2010-2015
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom