Ikulu yalijibu Gazeti la Dira ya Mtanzania: Yataka watoe majibu au wachukuliwe hatua...

Mbona pia inaonekana ikulu inaisemea familia ya HSC kwani wanasema gazeti lina nia ya kuchafua jina la kampuni.je ikulu imejiridhisha vipi kwa muda mfupi namna hii wa leoleo.je wamewahoji saa ngapi wakazi wa eneo husika waliosema wanavyonyanyaswa ?

Pia kurugenzi ya ikulu itasema nini kama DIRA watakuja na ushahidi wa Tape wa matamshio ya yule secretary wa HSC kuhusu kauli za bosi wake akiwaonya wasimfuatefuate kwani watapata matatizo na pia kwa nini mtoto wea rais alikataa kwa muda wa wiki nzima kuongea na DIRA kuihusu hili?. Lazima kuna jambo zitop hapa na kwa mtindo huu Tatizo la nchi hii si mawaziri bali ni Tabia ya Rais wetu.

Ujue hiyo habari ya Ikulu kuisemea HSC ndiyo inaonyesha kuna kitu hapa.

Inakuwaje Ikulu ikurupuke tu, kwanza kujibu suala leoleo, pili kuitetea HSC?

Hapo utaona Ikulu inatuma message kimafia "shughuli za wakubwa hizi, msiwasumbue hawa".
 
kwa nini hawa jamaa wasishtakiwe?

Mwanzo tuliambiwa ohh home shopping centre wana genge lao TRA na Bandari kupitisha makontena bandarini bila ushuri kwa sababu wanalindwa na wakubwa.

Sasa wanazuliwa kuwa wanafanya biashara na familia ya JK jambo ambalo kwa maelezo ya Ikulu halina chembe ya ukweli...soma hapa:

MICHUZI: MADAI YA GAZETI LA DIRA YA MTANZANIA

Nashauri Home shopping centre na familia ya JK wawafungulie mashtaka haya magazeti ambayo yanawachafulia majina.

Inaudhi sana kusoma habari kama hizi ambazo zimejaa chuki na kuharibiana bila sababu zozote zile

Gazeti hili kwa nini liko kimya juu ya ufisadi unaofanywa na Kitilya na genge lake pale TRA?
 
Kwanini Rweyemamu amekimbilia kukanusha kama hakuna ukweli? Hivi Rweyemamu ni msemaji wa familia ya rais au rais? Uvumi ni chanzo kizuri cha habari. Nijuavyo, kwa staili iliyotumika kukanusha kuna jambo linaepukwa. Maana watawala wetu walivyo, hali ingekuwa vinginevyo gazeti la Dira lisingeliona jua. Nendeni mahakamani badala ya kukimbilia kuhemkwa.
 
Amekanusha hata ku overdo! Amepitiliza but luckily letter head haikuwa na nafasi zaidi. Ni ajabu, haifanani anaweza kuwa sahihi lakini directorate ndio kazi pekee inayotakiwa kufanya? Kukanusha!
 
MADAI YA GAZETI LA DIRA YA MTANZANIA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.

Gazeti la kila wiki la Dira ya Mtanzania toleo la leo, Jumatatu, Mei 7, mwaka huu, 2012,* limechapisha habari yenye kichwa cha habari, “Familia ya JK yachafuliwa”.

Katika habari hiyo, Gazeti hili linadai kuwa familia ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete inafanya biashara na kampuni ya Home Shopping Centre (HSC) ya Dar es Salaam.

Aidha, Gazeti hili linadai kuwa Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Bwana Said Saad ndiye msimamizi wa biashara za familia hiyo ya Mheshimiwa Rais.

Tunapenda kuujulisha umma habari hizo si za kweli. Ni uongo unaolenga kuupotosha umma na kuchafua jina la Mheshimiwa Rais Kikwete na familia yake. Na, au vinginevyo unalenga kuchafua jina la Kampuni ya Home Shopping Centre. Kama nia ni kufanya hivyo tafadhali msilitumie jina la familia ya Rais.

Mheshimiwa Rais Kikwete haendeshi, hajawahi kuendesha, na wala hana mpango wa kuendesha biashara iwe ni yeye binafsi au na familia yake. Shughuli azipendazo na ambazo anajishughulisha nazo ni kilimo na ufugaji. Kwa ajili hiyo ana mashamba Sanzale, Kiwanga na Msoga. Hata shughuli hizo hazijafikia kiwango cha kibiashara kwani hutumia pesa yake ya mfukoni kugharamia shughuli hizo.

Badala ya kutoa tuhuma za jumla jumla zisizokuwa na ushahidi wowote ni vema muwe wawazi. Ni vema gazeti likaeleza namna gani au likamtaja ni nani ndani ya familia ya Mhe. Rais Kikwete anaendesha biashara kwa kushirikiana na Kampuni ya Home Shopping Centre.

Kwa kufanya hivyo , Gazeti la Dira ya Mtanzania litawathibitishia Watanzania kuhusu ukweli wa habari hizo. Aidha, litaondoa doa baya na chafu linalotaka kuelekezwa kwa Rais na Familia yake. Kitendo hicho hakimtendei haki Rais na Familia yake.

Ni imani yetu kuwa Gazeti hili litatoa majibu ya masuala haya muhimu katika toleo lake lijalo, vinginevyo Familia ya Mheshimiwa Rais itakuwa na haki ya kuchukua hatua stahiki za kisheria.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
 
kwa nini hawa jamaa wasishtakiwe?

Mwanzo tuliambiwa ohh home shopping centre wana genge lao TRA na Bandari kupitisha makontena bandarini bila ushuri kwa sababu wanalindwa na wakubwa.

Sasa wanazuliwa kuwa wanafanya biashara na familia ya JK jambo ambalo kwa maelezo ya Ikulu halina chembe ya ukweli...soma hapa:

MICHUZI: MADAI YA GAZETI LA DIRA YA MTANZANIA

Nashauri Home shopping centre na familia ya JK wawafungulie mashtaka haya magazeti ambayo yanawachafulia majina.

Inaudhi sana kusoma habari kama hizi ambazo zimejaa chuki na kuharibiana bila sababu zozote zile

Gazeti hili kwa nini liko kimya juu ya ufisadi unaofanywa na Kitilya na genge lake pale TRA?

Washitakiwe?
Kwaninini? Au wewe Ni moja Kati ya wafaidio? Tukueleweje? Ingekuwaje Kama ungekuwa hakimu Wa kesi hii?
Acha hizo, kuna vile unaweza kuwa smart zaidi!
 
kwa nini hawa jamaa wasishtakiwe?

Mwanzo tuliambiwa ohh home shopping centre wana genge lao TRA na Bandari kupitisha makontena bandarini bila ushuri kwa sababu wanalindwa na wakubwa.

Sasa wanazuliwa kuwa wanafanya biashara na familia ya JK jambo ambalo kwa maelezo ya Ikulu halina chembe ya ukweli...soma hapa:

MICHUZI: MADAI YA GAZETI LA DIRA YA MTANZANIA

Nashauri Home shopping centre na familia ya JK wawafungulie mashtaka haya magazeti ambayo yanawachafulia majina.

Inaudhi sana kusoma habari kama hizi ambazo zimejaa chuki na kuharibiana bila sababu zozote zile

Gazeti hili kwa nini liko kimya juu ya ufisadi unaofanywa na Kitilya na genge lake pale TRA?
Amka wewe! huyo muhidin issa michuzi ana maslahi binafsi na famikia ya kikwete.

Kwa taarifa yako pamoja na rais kuwa na mpiga picha wa ikulu lakini michuzi ndie mpigapicha rasmi wa matukio yote ya rais kikwete pamoja na familia yake na ndie anasafiri mara kwa mara na mheshimiwa hukui aki update picha na matukio toote kwwenye blog yake pia.

Sasa kwa mtindo huo unatarajia aseme nini? Au na wewe umo?
 
Ni wasemaji wa familia ya JK na Riz
dosama hii ishu imenichekesha sana hivi kulikuwa kuna umuhimu wa Ikulu kukanusha kwa niaba ya familia na mwishoni wanasema Dira wasipothibitisha familia itakuwa na haki kisheria ya kuchukua hatua, kwanini wasiseme Ikulu itakuwa na haki ya kuchukua hatua? Nahisi ipo siku Ikulu itakanusha hata masuala ya ndoa ya Rais yakizagaa mitaani. Kwa heading kama hii "IKULU INAKANUSHA VIKALI TUHUMA ZA KWAMBA MUHESHIMIWA ANATOKA NJE YA NDOA"
 
Last edited by a moderator:
Mheshimiwa Rais Kikwete haendeshi, hajawahi kuendesha, na wala hana mpango wa kuendesha biashara iwe ni yeye binafsi au na familia yake.

watu wanajua kuwa mkuu wetu na familia yake wanafanya biashara
tena za mapesa mengi.

kwanini kutudanganya jamani. Zama hizi hazina siri tena,
si mngekaa kimya tu, au mnataka kutufanya watz ni mbumbumbu.
 
na pia dk slaa ashitakiwe au atoe ufafanuzi haraka ile issue ya R1. Hatuwezi tukawa tunachafua majina namna hii.

Ushahidi unatolewa mahakamani...Riz aliambiwa kama amesingiziwa akamshtaki Dr. Silaa ili apeleke ushahidi. Ila kwa kuwa ni kweli, Riz hadi keshokutwa hajamshtaki Dr Silaa kwa sababu ni ukweli alichoambiwa.

Na kama Familia ya JK inaone imeonewa, iende mahakamani watu waje na document za ushahidi.....!!!!!
 
Mheshimiwa Rais Kikwete haendeshi, hajawahi kuendesha, na wala hana mpango wa kuendesha biashara
iwe ni yeye binafsi au na familia yake. Shughuli azipendazo na ambazo anajishughulisha nazo ni kilimo na ufugaji. Kwa ajili hiyo ana mashamba Sanzale, Kiwanga na Msoga. Hata shughuli hizo hazijafikia kiwango cha kibiashara kwani hutumia pesa yake ya mfukoni kugharamia shughuli hizo.

Aisee........Salva ni muongo kweli........Sasa Ridhiwani anaishije?
 
Kweli hatuna ikulu,biashara za miraji na ridhiwani anakanusha salva rweyemamu mchumia tumbo!!!!!!!!!!!!!!
 
Ryeyemamu! Tehee!
Ja Kaya? Tihiii!
Ikulu, mmhu!
Gazeti likidhibitisha Ryeyemamu nae ataleta vidhibitisho vyake, vya ikulu, vya JK au vya R1
 
Back
Top Bottom