Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Even the speculative part? Ikulu itasemaje kwamba gazeti lina nia ya kumchafua mfanyabiashara kama haina biashara yoyote na huyu mfanyabiashara? Itajuaje habari hii?
Vipi kama mfanyabiashara mwenyewe ka brag bila ukweli kwamba anafanya biashara na familia ya rais, ile kibongobongo kuwatisha watu?
Na, au vinginevyo unalenga kuchafua jina la Kampuni ya Home Shopping Centre. Kama nia ni kufanya hivyo tafadhali msilitumie jina la familia ya Rais.
Much ado about nothing. The response is spot on.
NN matamko ya ikulu yanatakiwa kujikita ktk hoja and in this case they misfired.
Ila kama ni kimipasho kama huku uswahilini wako kwenye mstari!
Ukiisoma hii Press Release utadhani imeandikwa na bibi yangu ambaye alijifunza kusoma kwenye miembe na ambaye hana muda wa kutosha kutafakari kabla ya kuandika kwa hadhara kubwa na namna hii kutoka na shuguli nyingi za shamba.
Pathetic! Jamani ina maana Ikulu imeshindwa kuwapata watànzania wenye weledi kutuepusha na aibu hizi?
Nadhani unazungumzia kipande hiki, sio?
Kama ni hicho basi mimi sioni ubaya wowote hapo kwani ni kuna mawili, mosi, Ikulu imekanusha na kusema habari si za kweli na zenye lengo la kumchafua Kikwete na familia yake, pili, kama lengo si hilo basi litakuwa ni kuchafua jina la Home Shopping Centre kwa kulihusisha na jina la rais.
Hakuna ubaya wowote hapo. Ikulu wameshakanusha and now the ball is in the weekly's court to back up its allegations with supporting evidence.
Sasa watu sijui mlitaka Ikulu waandikeje....
Yaani siku hizi mdosimdosi akijitapa tu "ninafanya biashara na familia ya rais", gazeti likiandika "Mdosi kajitapa anafanya biashara na familia ya rais" Ikulu inakuja juu siku hiyo hiyo na communique kukanusha?
Methinks the lady protests too much!
Kwanza Ikulu wamejuaje kwamba gazeti linaipaka matope hiyo biashara?
I mean hata kama Ikulu haihusiki, imejuaje kwamba mdosi hajajitapa na kusema hivyo hata kwa uongo?
Much ado about nothing. The response is spot on.
Ikulu ishajiingiza katika speculations, na inaonekana kuanza kumtetea mfanyabiashara kabla hata ya kuwa na habari kamili.
Hili linaweza kuwafanya wengine waanze kujiuliza, kuna jambo hapa?
Mbona ikulu imejibu siku hiyo hiyo habari hii wakati kuna habari kemkem zinaandikwa kuhusu Kikwete kila siku hazijibiwi?
Mbona Ikulu inamtetea sana huyu mfanyabiashara kwamba anachafuliwa kabla hata ya kupata habari kamili na bila hata kutuonyesha kwamba mfanyabiashara mwenyewe ndiye aliyejitapa?
Au maneno haya yana ukweli na Ikulu inaona ni bora iyazime mapema yasije kulipuka baadaye?
mkuu tunaogopa kujadili maana barua za kurugenzi ya ikulu huwa zina saini hii imekuweje
Mimi ndio nimejua leo kuwa kumbe rais wetu ni mkulima na mfugaji
Wewe ndiyo una speculate like you are on steroids!
Ikulu wameshafanya walichokuwa wanatakiwa kufanya: kukanusha au kuthibitisha. Wao wamekanusha.
Watu kuongea na kujiuliza na kuja na tafsiri zao ni jambo la kawaida sana.
Mengi mno yamesemwa na bado yatasemwa. Na wao hawawezi kujibu kila lisemwalo au kuandikwa la sivyo hawatafanya kazi zingine zozote zaidi ya kujibu yasemwayo na watu.
Ikulu wameshafanya walichopaswa kufanya na kibao kimerudi kwa Dira ya Mtanzania. Tuone kama watathubutu kuthibitisha waliyoyachapisha.
Ikulu ime speculate kwa kujiingiza kwenye habari na kusema gazeti linamchafua mfanyabiashara wakati gazeti linasema mfanyabiashara ndiye anayejitapa kwamba ana biashara na familia ya rais.
Kama Ikulu/ familia ya rais haina biashara na mfanyabiashara huyu, kurugenzi inachotakiwa inachotakiwa kusema ni kwamba familia ya rais haina biashara na huyu mtu. Hizi habari nyingine za kwa nini gazeti limeandika ni tofauti. Ikulu / familia ya rais inaweza isiwe na biashara na mfanyabiashara lakini ikakosea vile vile kusema gazeti linamchafua mfanyabiashara kwa sababu mfanyabiashara anaweza kuwa anajigamba openly kwamba ana biashara na familia ya rais, hata kama si ukweli.
Hizi habari za kujichomeka chomeka kumkingia kifua mfanyabiashara si kazi yao Ikulu, sanasana zitatupa maswali tu. Kwa nini Ikulu inamkingia mfanyabiashara kifua?
Ni kwa sababu waandishi wa Ikulu ni bongokamasi na hawakupata legal counsel kabla ya kufyatua huo utumbo wa speculations bila kujua ukweli?
Au ni kwa sababu habari ina ukweli fulani ndani yake wanataka kuizima mapema?
Na, au vinginevyo unalenga kuchafua jina la Kampuni ya Home Shopping Centre. Kama nia ni kufanya hivyo tafadhali msilitumie jina la familia ya Rais.