Ikulu yalijibu Gazeti la Dira ya Mtanzania: Yataka watoe majibu au wachukuliwe hatua...

Hii taasisi imeharibika kupindukia. Sijui ni makusudi, au ni hujuma, au ni uhuni, au ni ujinga.

Rais ajaye kweli atakuwa na kazi kubwa sana kusafisha haya madudu. Yaani taasisi ya umma imefanywa kuwaa kamradi cha wanafamilia wachache. Kweli ni aibu tosha. Ikulu imekuwa trade mall!
 
Ikulu imetoa taarifa kukanusha kuhusika kwao kwenye biashara na Home shopping centre.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Gazeti la kila wiki la Dira ya Mtanzania toleo la leo, Jumatatu, Mei 7, mwaka huu, 2012, limechapisha habari yenye kichwa cha habari, "Familia ya JK yachafuliwa".

Katika habari hiyo, Gazeti hili linadai kuwa familia ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete inafanya biashara na kampuni ya Home Shopping Centre (HSC) ya Dar es Salaam.

Aidha, Gazeti hili linadai kuwa Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Bwana Said Saad ndiye msimamizi wa biashara za familia hiyo ya Mheshimiwa Rais.Tunapenda kuujulisha umma habari hizo si za kweli. Ni uongo unaolenga kuupotosha umma na kuchafua jina la Mheshimiwa Rais Kikwete na familia yake.

Na, au vinginevyo unalenga kuchafua jina la Kampuni ya Home Shopping Centre. Kama nia ni kufanya hivyo tafadhali msilitumie jina la familia ya Rais.

Mheshimiwa Rais Kikwete haendeshi, hajawahi kuendesha, na wala hana mpango wa kuendesha biashara iwe ni yeye binafsi au na familia yake. Shughuli azipendazo na ambazo
anajishughulisha nazo ni kilimo na ufugaji. Kwa ajili hiyo ana mashamba Sanzale, Kiwanga na Msoga. Hata shughuli hizo hazijafikia kiwango cha kibiashara kwani hutumia pesa yake ya mfukoni kugharamia shughuli hizo.

Badala ya kutoa tuhuma za jumla jumla zisizokuwa na ushahidi wowote ni vema muwe wawazi. Ni vema gazeti likaeleza namna gani au likamtaja ni nani ndani ya familia ya Mhe. Rais Kikwete anaendesha biashara kwa kushirikiana na Kampuni ya Home Shopping Centre.

Kwa kufanya hivyo , Gazeti la Dira ya Mtanzania litawathibitishia Watanzania kuhusu ukweli wa habari hizo. Aidha, litaondoa doa baya na chafu linalotaka kuelekezwa kwa Rais na Familia yake. Kitendo hicho hakimtendei haki Rais na Familia yake.

Ni imani yetu kuwa Gazeti hili litatoa majibu ya masuala haya muhimu katika toleo lake lijalo, vinginevyo Familia ya Mheshimiwa Rais itakuwa na haki ya kuchukua hatua stahiki za kisheria. ……..Mwisho…..

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.Dar es Salaam.

7 Mei, 2012

MY TAKE: Hivi Kurugenzi ya mawasiliano ni msemaji wa IKULU am
a msemaji wa Familia ya JK?

JK anaihughulisha na kilimo na ufugaji!! mmh!!!
 
Ikulu imetoa taarifa kukanusha kuhusika kwao kwenye biashara na Home shopping centre.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Gazeti la kila wiki la Dira ya Mtanzania toleo la leo, Jumatatu, Mei 7, mwaka huu, 2012, limechapisha habari yenye kichwa cha habari, "Familia ya JK yachafuliwa".

Katika habari hiyo, Gazeti hili linadai kuwa familia ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete inafanya biashara na kampuni ya Home Shopping Centre (HSC) ya Dar es Salaam.

Aidha, Gazeti hili linadai kuwa Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Bwana Said Saad ndiye msimamizi wa biashara za familia hiyo ya Mheshimiwa Rais.Tunapenda kuujulisha umma habari hizo si za kweli. Ni uongo unaolenga kuupotosha umma na kuchafua jina la Mheshimiwa Rais Kikwete na familia yake.

Na, au vinginevyo unalenga kuchafua jina la Kampuni ya Home Shopping Centre. Kama nia ni kufanya hivyo tafadhali msilitumie jina la familia ya Rais.

Mheshimiwa Rais Kikwete haendeshi, hajawahi kuendesha, na wala hana mpango wa kuendesha biashara iwe ni yeye binafsi au na familia yake. Shughuli azipendazo na ambazo anajishughulisha nazo ni kilimo na ufugaji. Kwa ajili hiyo ana mashamba Sanzale, Kiwanga na Msoga. Hata shughuli hizo hazijafikia kiwango cha kibiashara kwani hutumia pesa yake ya mfukoni kugharamia shughuli hizo.

Badala ya kutoa tuhuma za jumla jumla zisizokuwa na ushahidi wowote ni vema muwe wawazi. Ni vema gazeti likaeleza namna gani au likamtaja ni nani ndani ya familia ya Mhe. Rais Kikwete anaendesha biashara kwa kushirikiana na Kampuni ya Home Shopping Centre.

Kwa kufanya hivyo , Gazeti la Dira ya Mtanzania litawathibitishia Watanzania kuhusu ukweli wa habari hizo. Aidha, litaondoa doa baya na chafu linalotaka kuelekezwa kwa Rais na Familia yake. Kitendo hicho hakimtendei haki Rais na Familia yake.

Ni imani yetu kuwa Gazeti hili litatoa majibu ya masuala haya muhimu katika toleo lake lijalo, vinginevyo Familia ya Mheshimiwa Rais itakuwa na haki ya kuchukua hatua stahiki za kisheria. ……..Mwisho…..

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.Dar es Salaam.

7 Mei, 2012

MY TAKE: Hivi Kurugenzi ya mawasiliano ni msemaji wa IKULU am
a msemaji wa Familia ya JK?

mkuu tunaogopa kujadili maana barua za kurugenzi ya ikulu huwa zina saini hii imekuweje
 
Km kweli hamna mwanafamilia wa mhe rais anaefanya biashara itakua ni maajabu kwelkwel,na hii itafanya tumuhoji Dr Slaa yale mabilioni ya riz1 alyoyasemea yanatokana na nin?hawa jamaa kazi yao ni kukanusha kila ki2 mpk vile vyenye ukwel unaodhihirika kabsa mf ile ishu ya jk kupelekwa london na kufanyiwa shopping ya suti.
 
OK, rais hajawahi, wala hana mpango wa kuendesha biashara yeye na familia yake. Hayo mananasi anayovuna kila siku shambani kwake yanaliwa yote Ikulu, au anatoa msaada kwa baadhi ya taasisi? Miraji ni sehemu ya familia ya Kikwete, hafanyi biashara?
 
Nafikiri gazeti lilikuwa straight to the point kuwa ni biashara gani analink nayo. Si kazi tena ya gazeti kutoa utetezi bali ni hizo link kujitetea kwamba hazipo.
 
Hivi Salva anajua anachokifanya? Hivi mkuu akituhumiwa ni kazi ya kurugenzi ya mawasiliano kumjibia? Kama yeye ni mtuhumiwa na hakubaliani na tuhuma ni vema akajibu mwenyewe sio kutuingiza kwenye gharama zisizo na msingi kupitia vyombo vya umma, pia kama kuna haja yakwenda mahakamani si kwa kutumia rasilimali zetu bali anapaswa kufanya kwa taratibu zake binafsi.
 
Hawa mbona wanakuwa haraka kujibu,duuh kweli Bongo ni noma yaani vitu ambavyo wana maslahi navyo wako so fast kuvijibu mbona hawajakuwa fasta kuwakamata wale jamaa wa Downs au wezi wa EPA.Moja kwa moja hapo hii biashara ni ya kwao na huyu msimamizi ni chambo tu.
 
Back
Top Bottom