IKULU: Kamati ya Pili ya Mchanga wa Madini kuwasilisha ripoti yake kwa Rais Magufuli Juni 12

Alianza kukimbilia mambo ya sheria wakati mda wa sheria ulikuwa bado.
Kwahyo ulitaka akae kimya tu??? Ssa si walifuata kuuliza maoni yake!!! Mbona spika alichangia na wengi tu walitoa mawazo ya kisheria iweje kwa lisu iwe kesi????

Yaani nchi nzima mnasubiri habari za mchanga ambao hata tukiuzuia tutaambulia kontena 4 kati ya kontena 100 kma mrahaba!!!!! alafu tunaacha kujadili iweje matofali ya dhahabu wanayonufaika nayo wazungu kwenye hyo 96%

Ni sawa na kuacha chakula mezani ukaenda gombea ukoko na mbwa jikoni!!!!
 
Weka utabiri wako hapa tuone kama utakuwa sawa na mheshiwa prezidaa juu ya nini atachukua dhidi ya kampuni ya ACACIA
 
mambo haya hayajawahi kumwacha mtu salama.

kuna mtu kesho ataondoshwa
 
Kuna mtu lazima apokee barua yake kesho! Hizi tume za JPM hazijawai kumuacha mtu salama
 
Hayawi hayawi..sasa yamekuwa.

Leo jumatatu ya tarehe 12 June 2017 itabaki kuwa miongoni mwa siku za kipekee za kukumbukwa na watanzania Wote Hasa wale wazalendo wakati Ripoti ya Pili ya tume iliyoundwa na mh.Rais John Pombe Joseph Magufuli alias JPM.

Baada ya muheshimiwa Rais JPM kutokea Ripoti ya kwanza (watanzania,prof Muhongo, TMAA, Tundu Lissu,Acacia na wenzake na dunia nzima kwa ujumla wanajua kilichowasilishwa).

Mbivu na mbichi kuhusu mchanga Wa makanikia kujulikana.

Kamati hii ya pili iliapishwa na kuanza kazi zake mnano 11 April 2017 chini ya uenyekiti Wa profesa Nehemiah Eliachim Ossoro.

Huku ikisaidiwa kwa ukaribu na wajumbe wake , ambao ni, Prof. Longinus Kyaruzi Lutasitara, Dr.Osward Joseph Mashindano, Bw. kasmir Sumba Kyuki, Bw. Andrew Wilson Masawe, Bw. Gabriel Paschal Malata, Bw. Usaje Bernard Usubisye na Bi. Butamo Kasuka Philip.

Hadidu rejea za Kazi kuu waliyopewa:
  • Kubaini aina ya madini yaliyomo katika mchanga unaosafirishwa nje ya nchi.

  • Tamani ya madini yaliyomo katika mchanga unaosafirishwa nje ya nchi.

  • Kiwango cha kila aina ya madini yanayopatikana katika mchanga unaosafirishwa nje ya nchi.

  • Uzito Wa mchanga unaowekwa kwa kila kontena la mchanga wa dhahabu unaosafirishwa nje ya nchi.

  • Kujua kiwango /idadi ya makontena yaliyosafirishwa nje ya nchi kwa kila mwezi kuanzia mwana 1998.

  • Kufafanua juu ya sheria zinavyosema na Kutoa kushauri Wa kisheria kwa serikali na mamlaka zake kuhusu hatua za kuchukua.

  • Kuchunguza na kujiridhisha kama mchakato wa kusafirisha mchanga huo ulikuwa unafata sheria zilizopo au la.
Karibu tuwe pamoja (kuanzia saa 3 kamili asubuhi) katika kufatilia undani Wa Ripoti hii inayosubiliwa kwa hamu na gamu na mamilioni ya watanzania ndani na nje ya nchi.

Saa ya ukombozi Wa maliasili za nchi ya Tanzania kwaajilo ya mtanzania mwenyewe imewadia..go....go...go..baba Magufuli.
 
hii ni vita ya khaki dhidi ya mende wa kijani
utaifa dhidi ya kujifanya utaifa
kwanini walipata dhidi ya kwanini sipati
maamuzi yako utawala wangu dhidi ya haya ni maamuzi ya utawala uliopita
wenye msimamo dhidi ya hiena hiena (kila kitu ndioooo)
mwisho kabisa hii ni vita ya;
KUTEKENYWA DHIDI YA KUJITEKENYA
[HASHTAG]#ImedhaminiwaNaMashobo[/HASHTAG]
[HASHTAG]#IsidingoHalisiBongoBahatiMbaya[/HASHTAG]
 
Dah tukimalize hili twende kufanya marekebisho ya Sheria ambazo ndiyo kiini cha matatizo yote Haya na mikataba iwekwe waz iliyo sainiwa na itakayokuja kusainiwa ili tupate faida

Iwe ni 50% mwekezaji na sisi 50% ya mapato faida ya madini

Tofaut na hapo ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu tu
 
Back
Top Bottom