Ikulu, Chamwino: Rais Magufuli aapisha Baraza la Mawaziri. Awapunguzia adhabu wafungwa waliohukumiwa kunyongwa

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,814
11,991
Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli leo anaapisha jumla wa Mawaziri 21 baada ya kuwa tayari ameshawaapisha Mawaziri Mawili ambao ni Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philipo Mpango na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi. Pia anawaapisha jumla ya Manaibu Waziri 23.


Mawaziri walioapishwa ni;

1. Wizara ya Maji - Juma Aweso

2. Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo - Innocent Bashungwa

3. Wizara ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Vijana na wenye ulemavu - Jenister Mhagama

4. Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto - Dkt. Doroth Gwajima

5. Wizara ya Uwekezaji ofisi ya Rais - Profesa Mkumbo Kitila

6. Wizara ya Katiba na Sheria - Dkt. Mwigulu Nchemba

7. Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia - Profesa Joyce Ndalichako

8. Wizara ya Mifugo na Uvuvi -Mashimba Mashauri Ndaki

9. Wizara ya Maliasili na Utalii - Dkt. Ndumbalo Damas

10. Ofisi ya Rais TAMISEMI -Suleiman Jaffo

11. Wizara ya Madini - Dotto Biteko

12. Wizara ya Nishati - Dkt. Medard Kalemani

13. Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi - Mhandisi Dkt Leonard Chamuliho

14. Wizara ya Kilimo - Profesa Adolph Mkenda.

15. Wizara Viwanda na Biashara - Mwambie Geofrey Idelphonce

16.Wizara ya Mambo ya Ndani - George Simbachawene

17. Wizara ya Muungano na Mazingira - Ummy Mwalimu

18. Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya habari - Dkt Faustine Ndugulile

19. Wizara ya Ardhi na Makazi -William Lukuvi

20. Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa - Elias John Kwandikwa

21. Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora - Capt Mstaafu George Mkuchika

---
Manaibu Waziri walioapishwa ni...

1. Kigahe Exaud Silaoneka kuwa Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara

2. Dkt. Angelina Sylvester Lubala Mabula kuwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

3. Patrobas Paschal Katambi kuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira).

4. Khamis Hamza Khamis kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.

5. Mwanaidi Ali Khamis kuwa Naibu Waziri wa Fedha na Mipango.

6. Kipanga Juma Omary kuwa Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia.

7. Dkt. Festo Stephen Dugange kuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa – TAMISEMI).

8. Byabato Stephen Lujwahuka kuwa Naibu Waziri wa Nishati.

9. John Deogratius Ndejembi kuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora).

10. Mhandisi Kundo Andrea Mathew kuwa Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.

11. Pauline Philipo Gekul kuwa Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi.

12. Ndulane Francis Kumba kuwa Naibu Waziri wa Madini. - Ameshindwa kuapa

13. Msongwe Godfrey Kasekenya kuwa Naibu Waziri wa Ujenzi.

14. Ummy Hamis Nderinanga kuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Wenye Ulemavu).

15. Mhandisi Marryprisca Winfred Mahundi kuwa Naibu Waziri wa Maji.

16. Abdallah Hamis Ulega kuwa Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

17. Mwita Mwikwabe Waitara kuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira).

18. William Tate Ole Nasha kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

19. Marry Francis Masanja kuwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii.

20. David Ernest Silinde kuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa – TAMISEMI).

21. Hussein Mohamed Bashe kuwa Naibu Waziri wa Kilimo.

22. Dkt. Godwin Oloyce Mollel kuwa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.

23. Geophrey Mizengo Pinda kuwa Naibu Waziri wa Katiba na Sheria.


Hotuba za viongozi mbalimbali

Salamu za Jaji Mkuu, Prof. Ibrahim Juma
Ningependa kuwapongeza viongozi walioapishwa leo.

Nina mambo mawili ya kusema. Kwanza kuwakumbusha kuwa mna ni mzigo mzito sana wa matumaini. Mzigo wa kwanza unatokana na mandate kubwa ambayo mmepata kutoka kwa wananchi ambao wana matumaini makubwa toka kwenu. Na wao wanachotaka ni ustawi wao tu, na haki na maendeleo yao.

Mzigo wa pili ni kuwakumbusha tu ile ahadi aliyotoa Mh. Benjamin William Mkapa, Rais wa Awamu ya Tatu, alipokuwa akizindua Dira ya Taifa ya Maendeleo aliwaahidi Watanzania kwamba Karne ya 21 imeanza na kuna mambo ya kutekeleza katika robo ya kwanza ya Karne ya 21.

Ninyi mna bahati kwamba robo ya kwanza ya Karne ya 21 itaisha mwisho wa muda wenu. Kwahiyo kuna mambo mengi sana yaliahidiwa na mtakuwa na mzigo wa kutekeleza mambo hayo yaliyoahidiwa kwa muda wa miaka 25

Mimi napenda kuahidi kuwa Mahakama itawapa ushirikiano.


Spika wa Bunge, Job Ndugai
Ndugu zangu, mmepewa madaraka. Mukajitahidi sana siku yoyote mkitoka kwenye madaraka hayo muache kumbukumbu za kudumu katika mioyo ya Watanzania – kwamba mliwahi kupata heshima hii.

Wengine mlikuwa na madaraka hayohayo na sasa Mh. Rais amewaendelezea. Kabla ya kuanza upya, ukagegeuke nyuma kutathmini, uangalie ulipopata nafasi hii ulifanya nini na kwa hiyo unadhani mbele kuna nini cha kufanya.

Ninyi ndiyo wasaidizi wa Rais wa karibu kabisa, kwahiyo nendeni mkamsaidie Mh. Rais kwa uaminifu kama mulivyoapa. Lakini kubwa zaidi, mkawasaidie Watanzania.

Msiende mkalewa na madaraka. Mkumbuke nafasi mliyopewa ni ya utumishi kwa Watanzania. Hili la Utumishi litangulie zaidi.

Tusaidiane kwa pamoja ili inapofika 2025 Mwenyezi Mungu akijalia tukiwa hai sote, basi tuione Tanzania yenye mabadiliko makubwa zaidi na zaidi.

Kwa sisi upande wa Bunge, ninyi ni Wabunge wenzetu, tutawapa kila aina ya ushirikiano.

Ni muhimu sana kuhudhuria vikao vya Kamati na Bunge. Isiwe kazi ya Spika kuwataka mawaziri kuhudhuria vikao.


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
Lazima tujue tuna jukumu la kuwatumikia Watanzania. Serikali ya Awamu ya Tano ni serikali ya kutenda.

Serikali yetu imejenga msingi wa hayo tunayokwenda kutenda. Tumefanya kazi kubwa sana katika kipindi cha miaka 5 iliyopita ikiwa ni pamoja na kurekebisha nidhamu ya utendaji wa kazi.

Timu tuliyonayo sasa ambayo inaingia awamu ya pili—kutoka kwa Watendaji wa Vujiji mpaka huku juu—ni watu ambao tayari wamejipanga kufanya kazi.

Tuna majukumu makubwa na tutapata muda wa kukumbushana yaliyo mengi. Tanahitaji kuona matokeo ya kazi hizo ambazo tutazitenda. Miongozo tunayo, jukumu sasa ni kufanya kazi.

Mimi na nyie tutakuwa na kikao saa 10 nikijua labda baada ya tukio hili wengine mtaenda kuripoti ofisini. Lakini tunayo mambo ya kupeana – msingi wa kufanya kazi vizuri.


Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan
Kupata safu hii kuna mambo mengi yameangaliwa

Ya kitaaluma, ya uwajibikaji katika maeneo mbalimbali mliyotoka, uwajibikaji katika eneo la kisiasa,Maisha yenu ndani ya jamii. Tumeangalia tukapata ‘cream’ hii pamoja na wengine wa reseverve.

Katika mawaziri mulioapa leo, wapo ambao tulinyooshwa pamoja katika kipindi cha awamu iliyopita. Hivyo ni Imani yangu kwamba sisi tuliyonyooka katika kipindi kilichopita tutanyoosha wenzetu wapya walioingia ili tuweze kwenda nao pamoja.

Nilitoa aghadi kwa Mh. Rais kuwa yeye aendelee kufikiria makubwa kwa taifa hili na sisi tutakuwa tayari kukimbia nalo.

Wengi tulikuwa field katika kipindi cha uchaguzi na tumeona mengi na changamoto nyingi ambazo tunatakiwa kuzitatua. Hivyo tunategemea tukawatumikie Wananchi.


Hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli
Mara nyingine huwa naingiaga kwenye magroup (makundi) nashangaa. Sio kila kitu kinafaa kwenye magroup. Najua mna magroup ya Mawaziri, Ma-DAS nk. Government goes on paper! Zingatieni kiapo cha maadili

Tumeangalia walau kila Mkoa uwe na mtu. Tunajua tuna Mikoa 26, tusingeweza kuwa na Mawaziri 26

Lakini pia, safari hii tumepata hata mtu kutoka Mafia ili aweze kuisemea Serikali

Somo la Historia liwe compulsory kama Kiswahili, na iwe Historia ya Tanzania tumeshasoma sana Historia za nje. Historia itajenga uzalendo. Vijana wengie hawajui Historia

Namuambia Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) amsimamishe kazi Mkurugenzi wa Geita. Amesema alinunua gari la Milioni 400 wakati wanafunzi hawana madawati

‘’Tamisemi kuna challenge nyingi, hasa katika matumizi mabaya ya fedha. Kuzunguka, Jafo umefanya vizuri sana lakini kwenye kudhibiti fedha, bado.

Na nilifikiria sana kukurudisha ama kutokukurudisha hapo. Nataka niseme ukweli tuelewane. Kwahiyo hili la matumizi ni baya.

Unamkuta Mkurugenzi ananunua gari la milioni 400 na kitu. Fedha tumehangaika nazo kuzipata, za CSR. Wananchi, Watoto wanachangishwa. Unakuta madawati hayajatosha.

Nataka kazi yako ya kwanza kwenda kumsimamisha huyo Mkurugenzi leo, wa Geita. Ndiyo kazi ya kwanza ukaanze nayo. Na utume watu wafanye uchunguzi wa matumizi ya hovyo ya namna hiyo.

Hamuwezi kupata fedha, badala ya kununa madawati, unaenda kununua gari la kutembelea, lenye thamani kubwa.

Kwenye taratibu za utumishi zinazungumza kila level na magari gani. RC wa Geita hana gari hana gari hilo alilo nalo Mkurugenzi.

Mambo kama hayo ni vyema yakashughulikiwe vizuri”

Profesa Mkumbo, haukufanya vizuri kwenye maji (Wizara ya Maji) lakini kwa kuwa unajua kuandika na kuzungumza, tunataka ukazungumze ili tupate wawekezaji. Na umekuwa Waziri ili utoe maamuzi kweli


RAIS MAGUFULI: AWAPUNGUZIA ADHABU WALIOHUKUMIWA KUNYONGWA
Rais wa Tanzania, Dkt. John Magufuli amesema alitakiwa kuwa amenyonga watu 256 ambao walihukumiwa kunyongwa kwa makosa mbalimbali

Katika hotuba yake aliyoitoa leo baada ya kuwaapisha mawaziri amesema amewapunguzia adhabu watu hao na sasa watatumia vifungo vya maisha badala ya kunyongwa

Amesema inawezekana kati yao wapo walioua mtu mmoja au wawili, lakini yeye akiruhusu wanyongwe watu 256 atakuwa ameua watu wengi zaidi na atakuwa mwenye dhambi zaidi kuliko wao

Hivyo ametaka watu hao waanze kufanyakazi za jela
 
Rais wetu jembe JPM,leo tutegemee hotuba nzuri kabisa. Mungu ibariki Tanzania.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli leo anaapisha jumla wa Mawaziri 21 baada ya kuwa tayari ameshawaapisha Mawaziri Mawili ambao ni Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philipo Mpango na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi...
Kwa hiyo manaibu mawaziri na hawaapishi leo hapo Ikulu ya Chamwino ?!

Mhe. Kigahe Exaud Silaoneka kuwa Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara

Mhe. Dkt. Angelina Sylvester Lubala Mabula kuwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

Mhe. Patrobas Paschal Katambi kuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira).

Mhe. Khamis Hamza Khamis kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.

Mhe. Mwanaidi Ali Khamis kuwa Naibu Waziri wa Fedha na Mipango.

Mhe. Kipanga Juma Omary kuwa Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia.

Mhe. Dkt. Festo Stephen Dugange kuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa – TAMISEMI).

Mhe. Byabato Stephen Lujwahuka kuwa Naibu Waziri wa Nishati.

Mhe. John Deogratius Ndejembi kuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora).

Mhe. Mhandisi Kundo Andrea Mathew kuwa Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.

Mhe. Pauline Philipo Gekul kuwa Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi.

Mhe. Ndulane Francis Kumba kuwa Naibu Waziri wa Madini.

Mhe. Msongwe Godfrey Kasekenya kuwa Naibu Waziri wa Ujenzi.

Mhe. Ummy Hamis Nderinanga kuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Wenye Ulemavu).

Mhe. Mhandisi Marryprisca Winfred Mahundi kuwa Naibu Waziri wa Maji.

Mhe. Abdallah Hamis Ulega kuwa Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Mhe. Mwita Mwikwabe Waitara kuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira).

Mhe. William Tate Ole Nasha kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Mhe. Marry Francis Masanja kuwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii.

Mhe. David Ernest Silinde kuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa – TAMISEMI).

Mhe. Hussein Mohamed Bashe kuwa Naibu Waziri wa Kilimo.

Mhe. Dkt. Godwin Oloyce Mollel kuwa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.

Mhe. Geophrey Mizengo Pinda kuwa Naibu Waziri wa Katiba na Sheria.
 
Kwakweli tunacho taka mara baada ya kuapishwa wafanye kazi kwelikweli, bado kuna kero nyingi sana ktk jamii.

Waziri Jumaa Awesu kabebeshwa zigo zito sana! kero ya maji ndio iliyo tikisa ktk kampeni karibu kila mahala ktk nchi yetu kuna changamoto kubwa ya upatikanaji wa maji, kilio kikubwa ni maji maji! Mungu amsaidie apambane.

Malimbikizo ya bili za wanchi yaangaliwe vizuri mengi yamekosewa.

lkn pia wananchi walio fungiwa maji kisha kulipia gharama kidogo dogo waongezewe muda wa kuendelea kulipia kidogo dogo

wasikatiwe huduma (mradi uliopita maeneo ya chalinze, kibaha, kibamba,kiluvya hadi mbezi maarufu kama mradi wa wahindi)...lengo ni kutoa huduma na kukusanya mapato, kama mteja analipia kwa mwezi japo kidogo kupunguza deni asikatiwe huduma

tunaomba watendaji wa chini wanao fuatilia bili za wanabchi wafundishwe jinsi ya kuwahudumia wateja.
 
Wakuu muda mfupi ujao rais magufuri atakuwa anawaapisha mawaziri na manaibu mawaziri 46 aliowateuwa .

Ni kuanzia saa nne asubuhi ya leo viwanja vya ikulu ya Tanzania jijini dodoma ,vyombo vyote vya habari vitakuwa live.

Wageni mbalimbali wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama ,marais waftafu ,mawaziri wakuu wastafu na makamu wa marais wastafu pia rais wa Zanzibar wako hapa kwa zoezi hili adhim

Kikubwa ni hotuba ya kikazi ya mh rais na wongozo wa kazi

Pia kutakuwa na ujazaji form za maadili na mali zinazo milikiwa na wateule hawa

Update
 
Ukweli mchungu ni kwamba hao mawaziri ni geresha tu,mtu mmoja ndiye Rais na ndiye waziri wa wizara zote!
1178909.jpg
 
Back
Top Bottom