Jembe Ulaya
JF-Expert Member
- Oct 27, 2008
- 456
- 104
Mojawapo wa viongozi wakuu wa kampeni za CCM amefumaniwa na mke wa mtu gesti wakijivinjari. Mwanamke mwenye uhusiano na mratibu wa kampeni za ccm kapata kipigo cha uhakika imebidi alazwe hospitali. Mumewe aliyempa kipigo vilvile ni kada maarufu wa chama cha mapinduzi. Hata hivyo viongozi wa CCM walijazana polisi na kuweza kuipotezea hiyo issue kuzuia aibu.
Kutoka Tanzania Daima
TIMU ya kampeni ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) imeingia katika msukosuko mkubwa wa chini kwa chini baada ya kiongozi mmoja mwandamizi anayeongoza kampeni hizo (jina tunalihifadhi) kudaiwa kufumaniwa na mke wa mtu, Tanzania Daima limebaini.
Habari za uhakika ambazo gazeti hili limezipata kutoka vyanzo vya kuaminika katika Ofisi Ndogo za CCM Makao Makuu jijini Dar es Salaam na kutoka Igunga zinaeleza kuwa tukio hilo limesababisha kujeruhiwa vibaya kwa mwanamke huyo.
Ofisa mmoja wa juu wa CCM aliyezungumza na Tanzania Daima kwa sharti la jina lake kutoandikwa gazetini alisema sakata hilo lilianza baada ya mume wa mwanamke anayedaiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na kigogo huyo anayeongoza kampeni za chama hicho kuvamia chumba ambacho watuhumiwa hao walikuwamo na kuanza kumwadhibu mkewe kwa kipigo.
Kwa mujibu wa ofisa huyo, wakati vuta nikuvute kati ya mke na mume ikiendelea chumbani, kigogo huyo wa CCM alifanikiwa kutoroka na kuwaacha wanandoa hao ambao wote wawili ni makada wa CCM wakiendelea kupambana.
Habari zinaeleza kwamba mtafaruku huo ulimsababishia mwanamke huyo aliyekuwa miongoni mwa kundi la mabinti wapatao 10 wanaotumika kuhamasisha kwenye kampeni hizo majeraha makubwa yaliyomlazimisha apelekwe hospitalini kwa ajili ya matibabu.
Chanzo kingine cha kuaminika cha habari kililieleza gazeti hili kwamba kabla ya kwenda hospitalini, mwanamke huyo alilazimika kupita katika kituo cha polisi cha Igunga ili akapatiwe fomu maalum ya idhini ya matibabu (PF3).
Inaelezwa kwamba mara baada ya kufikishwa kituoni hapo na wasamaria wema, mwanamke huyo (jina tunalo) alitakiwa kwanza kulitaja jina la mtu aliyemsababishia majeraha hayo na akajikuta akipata wakati mgumu kumtaja mumewe.
Habari zinaeleza kwamba taarifa za tukio hilo zilipofika katika ofisi za CCM wilaya ya Igunga, maofisa wa chama hicho waliingilia kati na kuamua kulizima jambo hilo chini kwa chini ili kuepukana na hatari ya kuvuruga kampeni nzima za ubunge cha chama hicho.
"Ni kweli tumepokea habari za kusikitisha kuhusu kiongozi wetu mmoja wa juu katika kampeni kukumbwa na kashfa ya kufumaniwa na kusababisha mwanamke aliyadaiwa kuwa na uhusiano naye kupata kipigo kikali kutoka kwa mumewe ambaye pia ni kada maarufu wa chama chetu Igunga," alisema ofisa mmoja wa juu wa CCM aliyezungumza na gazeti hili.
Hata hivyo, ofisa huyo alisema uchunguzi walioufanya awali kuhusu tukio hilo umebaini taarifa za kigogo huyo wa CCM kuwa na uhusiano usiofaa na mke wa mtu zilivujishwa na kundi la vijana wengine wa kiume walio katika timu hiyohiyo ya kampeni ya CCM ambao ndiyo waliopenyeza taarifa hizo kwa mume wa mwanamke anayetuhumiwa.
Wakati chama hicho kikihaha kulifunika sakata hilo ili lisivuje, viongozi wake waandamizi walipata wakati mgumu kumnadi mgombea wao, Dk. Peter Kafumu, kwenye ngome ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), katika Kata ya Nyandekwa, katika jimbo la Igunga.