Ifike mahali TUCTA muachane na sherehe za Mei Mosi, masilahi bora Kwa wafanyakazi ni mpaka serikali iamue.

Retina

JF-Expert Member
Mar 6, 2015
1,038
1,154
1.Mlilalamikia kikokotoo kisiwepo,serikali ikaweka
2.Mkalalamikia nyongeza ya mishahara Kwa miaka nenda rudi,nyongeza ni mpaka serikali iamue na iongeze ionavyo
3.Mmelalamikia annual increments,hakuna ushawishi wa kuishawishi serikali kurudisha,mpaka serikali iamue
4.Mnalalamikia Kwa miaka nenda rudi,wastaafu kulipwa pension zao Kwa wakati,mpaka Leo wanacheleweshewa ni mpaka serikali iamue.
Malalamiko ni mengi mno,TUCTA na vyama vyake haijawahi fanikiwa,ni mpaka serikali iamue.Kuna haja gani ya kuwa na vyama vya wafanyakazi au shirikisho linalolalamika Kila kukicha,tangu nasoma msingi Hadi chuo kikuu na hatimaye ni mtu mzima sasa vilio vilevile tu ,huku vikijichukulia michango na matumizi mabaya ya fedha za wanachama.
Kwa upande wa vyama vinavyounda shirikisho mfano Cwt,wamewekeza Kila mahali Hadi benki,hawajawahi kusitisha makato au kupunguza % za makato Kwa wanachama wake,pesa zinatafunwa tu.
Njia nzuri za kuishinikiza serikali kutekeleza matakwa Yao ni migomo tu,tumeona Ujerumani, Kenya,Uingereza n.k migomo ya wafanyakazi ndio suluhu.
Mnaona kuendelea na sherehe za Mei Mosi ni kuendelea kupiga hela za wanachama na ndio msimu wa kula pesa,au shirikisho lina makada wa ccm?
 
Ile iweje sasa na sherehe ni zao

USSR
 
Back
Top Bottom