Angalau roho yangu imetulia sasa !
kweli watanzania wote sasa hivi wanafananishwa na mwanaasha ..baada ya miaka 4 ndio kesi eti inaanza ...na watarudishwa tena mahakani mwaka 2014..na hukumu itasomwa 2020. my hair hii ndio ccm na viongozi wake
Nakumbuka faili la uraia wake wa Burundi lilipotea kiana kimya kimya. Ndiyo Tanzania kama usivyoijua.
aliyekuwa diwani wa sinza salum mwakinginda pamoja na aliyekuwa mbunge wa ilala idd simba wamefikishwa mahakama ya kisutu hivi sasa kwa makosa ya ufisadi wa uda.
Ujeuri umeisha anatetemeka sana
Tanzania ingekuwa China kwa makashifa yote ya rushwa aliowahi kuhusishwa nayo mzee simba angekuwa tayari alishasaulika. Hapa Tanzania watampeleka mahakamani lakini muda si mrefu utakuta anakunywa kahawa pale Ilala na rafiki zake.
Huyo ni mtabiri; yaani anatabiri baada ya miaka minne ya kuendesha kesi, Simba atatamkwa kuwa ameshinda....Sasa mbona mnatuchanganya,
Amefikishwa leo na leo leo ameshinda tayari?
Hebu wekeni sawa hii habari
Gharama ya kesi ni milioni 800 ambazo kisheria anatakiwa alipwe Idd Simba, na Serikali imetakiwa kumuomba radhi.
Wakifikishwa mahakamani kosa, wasipofikishwa mahakamani kosa!
Damned if you do damned if you don't!
Hiyo ndio raha ya upinzani. Mbona siwasikii kuongelea kesi ya Mbowe na fedha za NSSF? iliisha?
Magumashi mengine. Baada ya CCM kuona kinachungulia kaburi kimeanzisha Tamthiria nyingine ya Kuwashtaki akina Idd Simba! Kama walimshindwa Zombe aliyeua watu walioonekana, itakuwa Simba aliyeiba hela ambazo hazionekani! Lakini all in all hii Episode nyie anzisheni tu, Si mmetufanya sisi wote "Mwanaasha"! lakini kwa Watanzania wa leo, mmeula wa chuya. HATUDANGANYIKI!