Idd Simba, Salum Mwakinginda wafikishwa mahakamani

Mwaking'inda alikuwa diwani wangu sinza; likimalizika hili inabidi swala la viwanja vya wazi nalo lifuate; siku hizi watoto wetu hawana mahala pa kucheza sinza. aliuza vyote
 
kweli watanzania wote sasa hivi wanafananishwa na mwanaasha ..baada ya miaka 4 ndio kesi eti inaanza ...na watarudishwa tena mahakani mwaka 2014..na hukumu itasomwa 2020. my hair hii ndio ccm na viongozi wake

My learned friends have a saying, justice delayed is justice denied.
 
Nakumbuka faili la uraia wake wa Burundi lilipotea kiana kimya kimya. Ndiyo Tanzania kama usivyoijua.

Huyu mzee anatuhumiwa pia kuitapeli tz jengo lake la ubalozi pale Bujumbura. Wakati Burundi ikiwa vitani na diplomats wamerejeshwa home, ali-take advantage ya Urundi wake kuliuza na wakati ubalozi unarejea ukakuta mnunuzi ana nyaraka zote halali - ikawa imekula kwa tz.
 
[h=2]Idd Simba apanda kizimbani leo kwa tuhuma za kuitia hasara UDA[/h] 29/05/2012
0 Comments


Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Usafirishaji Dar es Salaam (UDA) Iddi Simba amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam kwa tuhuma za kulitia hasara ya zaidi ya Shilingi Milioni 300 shirika hilo.

Simba alitinga Mahakamani hapo leo mwenyewe na tuhuma hizo zinamkabili yeye na wenzake wengine wawili wanaotuhumiwa pamoja.

Simba aliyewahi kuwa Waziri katika awamu ya pili na yatatu anakuwa niWaziri wa tatu mstaafu kufikishwa Mahakamani hapo kwa tuhuma za kuitia Hasara Serikali na Mashirika.

Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC) ilisema hivi karibuni kuwa, mkataba wa uuzwaji wa hisa za Serikali ndani ya Shirila la Usafiri Dar es Salaam (UDA) ni batili na kwamba fedha zote zipo kwenye akaunti ya kada wa Chama Cha Mapinduzi na mwanasiasa wa siku nyingi Idi Simba, ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Bodi ya shirika hilo na kwa sasa bwana Simba ni mwenyekiti wa baraza la wazee wa mkoa wa Dar es Salaam.

Akizungumza muda mfupi na waandishi wa habari leo mjini Dodoma, baada ya kampuni iliyodai kununua shirika hilo kutoa taarifa kwa vyombo vya habari mjini hapa kuhusu ununuzi wa UDA, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mashirika ya Umma, Kabwe Zitto alisema ununuzi huo ni batili.

“Niwape tu ufafanuzi wa jambo hili, Kamati ya Bunge ya Mashirika ya Umma ndiyo yenye jukumu la kusimamia sera ya ubinafsishaji, na kwa ufuatiliaji wetu, tumebaini kuna taratibu za kisheria zimekiukwa, na huyu mtu anayedai amenunua UDA, afahamu tu kwamba ametapeliwa, UDA bado ni shirika la umma”, alisema Zitto.

Aliongeza kuwa kammpuni ya Simon Group inayodai imenunua hisa asilimia 52 ya shirika hilo, imetapeliwa na kwamba fedha shilingi milioni 300 kati ya fedha shilingi milioni 760 wanazodai wamesha wekeza kwenye shirika hili, ziliwekwa kwenye akaunti ya mtu binafsi.

Alisema fedha hizo zimewekwa kwenye akaunti tofauti ya Idd Simba. Alizitaja akaunti hizo na tarehe ambazo fedha hizo ziliwekwa, ambapo katika benk M tawi la Sea View jijini Dar es Salaam, Septemba 2 mwaka 2009, fedha shilingi milioni 250 ziliwekwa kwenye akaunti binafsi ya Idd Simba .

Aidha, katika benki ya NMB tawi la Makambako, Novemba 26, mwaka 2009 fedha shilingi milioni 30 ziliwekwa kwenye akaunti binafsi ya Idd Simba, na Desemba 9,mwaka 2009 katika benki ya NMB tawi la Mlimani City shilingi milioni 20 ziliwekwa benki na kuingia kwenye akaunti ya Idd Simba tawi la Pride Songea Desemba 18, mwaka huo.

Zitto alisema kwa uchunguzi wa kamati hiyo kuhusu mwenendo mzima wa ubadhirifu wa shirika hilo, wamemwagiza CHC kufuatilia shirika la UDA na kuhakikisha hakuna mali yoyote ya shirika hilo itabadilishwa jina au kumilikiwa na mtu yoyote bila utaratibu wa sheria za ubinafshishaji.


Source: wavuti - wavuti
 
Wakifikishwa mahakamani kosa, wasipofikishwa mahakamani kosa!

Damned if you do damned if you don't!

Hiyo ndio raha ya upinzani. Mbona siwasikii kuongelea kesi ya Mbowe na fedha za NSSF? iliisha?
 
  • Thanks
Reactions: tk
aliyekuwa diwani wa sinza salum mwakinginda pamoja na aliyekuwa mbunge wa ilala idd simba wamefikishwa mahakama ya kisutu hivi sasa kwa makosa ya ufisadi wa uda.


Tanzania ingekuwa China kwa makashifa yote ya rushwa aliowahi kuhusishwa nayo mzee simba angekuwa tayari alishasaulika. Hapa Tanzania watampeleka mahakamani lakini muda si mrefu utakuta anakunywa kahawa pale Ilala na rafiki zake.
 
Ujeuri umeisha anatetemeka sana

aaa wapi utamuona mahakamani anacheka tu kwa sababu hio haimsumbui labda sio utawala huu ....kwani yule wa bank kuu mbona anaendelea kutafuna mahela yake kumbuka alipo kuwa magereza aliweza kumpigia simu rais mpaka leo hakuna hatua yeyote

 
kufikishwa mahakami swala moja na kukutwa na hatia ni swala lingine-kwa mchezo wa hii nchi-kama kwa kuwa bado mambo ni yaleyale-hata hii kesi ichukue miaka mingapi-hakuna la maana litakalofanyika-maana hawa jamaa watashinda TU-
NDIO SUMAYE AMESEMA KAMA WATANZANIA BADO WANAITEGEMEA TAKUKURU KWENYE KUPAMABANA NA UFISADI HALI ITAKUWA NGUMU-NI TOOTHLESS KWA WATU KAMA HAWA-MAY BE UKIIBA KUKU NDO WATAKUMUDU

mtanzania.jpg
 
Hii inafurahisha kuona Hawa mafisadi wanapelekwa mahakamani, Ingawa Mahakama zetu nazo haziaminiki coz hazijashutumiwa sana coz watu nahisi wanaogopa kuilalamikia mahakama ambako nako kuna ufisadi wa haki kutokutendeka hasa kwa kesi za watu wenye fedha
 
Tanzania ingekuwa China kwa makashifa yote ya rushwa aliowahi kuhusishwa nayo mzee simba angekuwa tayari alishasaulika. Hapa Tanzania watampeleka mahakamani lakini muda si mrefu utakuta anakunywa kahawa pale Ilala na rafiki zake.


Ndg China watu wanakula rushwa TZ haioni ndani, ufisadi kule ni mwisho pamoja na sheria zao kali

China wanasiasa ni balaa kwa kula rushwa sema pato lao ni kubwa ndo maana hata wakila zinabaki.
 
Sasa mbona mnatuchanganya,

Amefikishwa leo na leo leo ameshinda tayari?

Hebu wekeni sawa hii habari
Huyo ni mtabiri; yaani anatabiri baada ya miaka minne ya kuendesha kesi, Simba atatamkwa kuwa ameshinda....
 
Wakifikishwa mahakamani kosa, wasipofikishwa mahakamani kosa!

Damned if you do damned if you don't!

Hiyo ndio raha ya upinzani. Mbona siwasikii kuongelea kesi ya Mbowe na fedha za NSSF? iliisha?

Kama huna la kujadili bora usichangie
NSSF wana wanasheria wao na wana utaratibu wao wa kurecover madeni yao so utaratibu utaendelea
na huu wa huyo unayemsema sio ufisadi kama wa huyu aliyetafuna
Jitahidi kuchangia kwa kuona shida za watanzania na sio usukumwe na hisia
 
Magumashi mengine. Baada ya CCM kuona kinachungulia kaburi kimeanzisha Tamthiria nyingine ya Kuwashtaki akina Idd Simba! Kama walimshindwa Zombe aliyeua watu walioonekana, itakuwa Simba aliyeiba hela ambazo hazionekani! Lakini all in all hii Episode nyie anzisheni tu, Si mmetufanya sisi wote "Mwanaasha"! lakini kwa Watanzania wa leo, mmeula wa chuya. HATUDANGANYIKI!


Upuuzi huu!
 
Mbona sijasikia aliyetoa hizo pesa na yeye atafikishwa lini mahakamani,kweli hii yaweza kuwa danganya toto lets wait
 
Wasiofikishwa Kortini mnashinikiza wafikishwe,wakifikishwa mnadai danganya toto,Basi nanyi nanyi ni danganya toto pengine mna agenda ya MALIWATONI,
 
Back
Top Bottom