Idara ya Usalama wa Taifa yakanusha tuhuma

Status
Not open for further replies.
Labda wangekuja na vigezo vinavyowanasua uhusika wao pia wangetuambia nani anahusika,pia wangeshauri iundwe tume huru.
 
Wangekubali hata mimi ningeshangaa maana hata wanyama walijua kuwa watalipinga hili........ Hii ndio bongo akili kichwani
 
tunataka kova atuambie huyu rama mng'oa meno na plaizi ni nani la si hivyo hatutakaa tuwaelewe,damu hii ya dokta haitawaacha kamwe!!!
 
Kwani kuna mtu amewaambia wakubali? Tungewashangaa zaidi kama wangekubali wamefanya sahihi kukataa ukweli cause wote tulitegemea hivyo.Ipo siku tutapata uhuru na wataacha kututesa
 
Wee kila ukicha unaambiwa mchawi! Dawa kama sio mchawi nenda Mahakamani ukashitaki haki ipatikane! Hilo hamlijui au mnakula cover? daa! mnakanusha kisha mnanyuti! endeleeni kutuona mabozi!
 
Kanusho la TISS limetolewa na Ikulu! Hilo moja. Lakini kubwa idara hii (TISS) na wakubwa serikalini wanatakiwa wakae chini na watumie busara ili kurekebisha mambo. Watu wanishi kwa watu wasiwasi na imani kwa idara hii nyeti imeshuka sana kama sio kutoweka. Idadi ya matukio tata yanayogusa hii idara yanazidi kuongezeka siku hadi siku. Dunia haitakaa kimya milele.

Tanzania inaishi kwa kibakuli na kama tulivyoona kwenye saga ya bendera na meli za Iran hawa watu wa magharibi wanaweza kugeuka nyuzi 360 within seconds. Kagame pamoja na kuwa kipenzi cha nchi za magharibi, sasa hivi yuko kwenye misukusuko toka huko huko magharibi. Tanzania tukiendelea na hizi comedy tusishange kuona watu wanakwenda the Hague.

Badala ya kujitetea kwa maneno matupu kwanini serikali isiunde tume huru? Ni kitu gani kinachowafanya wakatae tume huru kuangalia mkasa wa Dr Ulimboka?
 
mi nafikiri hii idara tungeikodisha nafikiri ingekuwa jambo la busara.... kama tutaendelea na hawa vilaza ni maigizo tu kwakwenda mbele, wao wanatakiwa watuambie hao wanaotajwa kwamba ni wana usalama wambao wameshiriki hilo tukio watuambie wametoka wapi na ni kina nani?
 
Just a matter of time, the truth will reveal itselft! We are eagly waiting, watesaji watateswa nao tuu, mark my words!
 
Kama ni uzushi.watuambie ukweli wanaoujua.Ni vigumu kumfanya anayejua kuwa mjinga kama ilivyo rahisi kumwelimisha mjinga.Mtatumia gharama sana kutufanya tunaojua kurudia kwenye ujinga.
Haiwezekani profesa ukamwambia "A" ni "H" akasema yes.ukiona amesema yes ujue kapima upeo wako wa kufikiria.
Ndiyo maana jana walijitahidi sana kudiscard link ya mwanahalisi kwenye jf.
Sms na mazungumuzo watu wanayo hata kama ni miaka 80 italipwa haki iliyopotea
Mpo kazini kwa maslahi ya kikundi chenu.
Wengine wanafanya kwa maslahi ya watanzania hakuna umilele ila Mungu tu.
Nilitegemea polisi watumie mbinu zilizoandikwa na mwanahalisi mapema hata kabla mwanahalisi hawajandika uchunguzi wao.
Binafsi ni siku mbili tu zinatosha kuwatia mbaroni wahuni wote waliouhusika.
usalama wa taifa uko wapi kama mkenya ameingia na kufanya uhalifu.wasomali wanafia Dodoma.
Endeleeni kulinda watawala lakini wanakikomo
 
ukienda kununua kitu dukani muuzaji lazima atakwambia kuwa kitu hicho ni kizuri nunua tu ili yeye apate faida hata kama kitu hicho si kizuri,hawezi kukwa mbi ausikinunue.sitegemei kama wangekubali
 
Hivi nchi zote usalama wa taifa ni kuua watu kistaili km hapa kwetu. Hawawezi kujitoa ktk hili kwani utatu wao wa uovu kati ya serikali polisi na uhasama wa taifa tunaujua vilivyo.
 
Tamko hili hapa;

AMKO RASMI KUHUSU TUHUMADHIDI YA IDARA YA USALAMA WATAIFA

Katikasiku za hivi karibuni, kumejitokeza taarifa zenye tuhuma kadhaa dhidi ya Idaraya Usalama wa Taifa. Taarifa hizo zimekuwa zikitolewa kwenye vyombo vya habarizikiihusisha Idara hii na matukio ambayo yanaidhalilisha na kuzua maswali mengikwa wananchi. Kati ya tuhuma hizo ni tukio la kutekwa kwa Dr. STEPHEN ULIMBOKA,Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari na madai ya kufanywa kwa mipango yakuwadhuru baadhi ya Viongozi wa Vyama vya Upinzani. Gazeti moja la kila wikilimekuwa likurudia tuhuma hizo mara kwa mara kwa madai kwamba ni habari zauchunguzi na kuihusisha Idara.

Idarainataka kuwahakikishia wananchi kwamba taarifa hizo ni zaUZUSHI NA UONGO ambazo zina nia ya kuharibujina na sifa ya Idara. Taarifa hizo zimekuwa zikiunganishaunganisha vipande vyataarifa mbalimbali ili kukidhi malengo yaliyokusudiwa na wanaolitumiagazetihilo. Idara haikuhusika wala haihusiki na matukio yoyote yaliyotajwa katikatuhuma hizo. Hivyo tunawaomba wananchi wazipuuze taarifa hizo.

Matukio yaliyotajwa katikatuhuma hizo yanachunguzwa na Jeshi la Polisi ambacho ndicho Chombo ChenyeDhamana, na kwa Maslahi ya Taifa si vizuri kuachia upotoshaji huo uendelee.

Aidha,tunapenda kuwahakikishia Watanzania kuwa uzushi na tuhuma zinazotolewa dhidi yaIdara hazitatuvunja moyo bali zitatuunganisha na hivyo kutuimarisha katika azmayetu ya kuhakikisha nchi yetu inaendelea kubaki salama kwa kushirikiana nawanachi na Vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama.

Imetolewa na Idara ya Usalama wa Taifa,

Makao Makuu,

DAR ES SALAAM

26 Julai, 2012.

 
Ningeshangaa sana kama wangekuja na kauli ya kukiri kosa,ila tatizo ni kuwa inamaana siku hizi taasisi ndogo kama mwanahalisi wanaweza kuja na investigation za maana but hawa usalama na kova wanatuletea vichaa na kutegemea watu waende kutubu makanisani ndio wawakamate?umakini wao una walakini.Kamwe hamtajisafisha katika ili;bora mkae kimya tu manake huyo Rama namba ya simu yake imeishajulikana na anafanya kazi ikulu,so kama kubenea kaongopa mkamateni kwa kuwachafua taasisi nyeti kama hiyo.
 
hapo serikali hamtoki, moja kwa moja serikali ni mhusika mkuu pamoja na "liwalo na liwe" a.k.a pinda
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom