idadi ya watoto vs maisha bora

Kuzaa inategemea uwezo wa kuzaa na uwezo wa kutunza. Unaweza kusema unataka 2, kumbe hata ukishapata huyo 1 ndiyo huwezi tena, kiafya (nimeshaona mfano). Na pia unaweza kutaka wengi na ukawapata wakakushinda kutunza. Lakini wapo pia waliopata watoto wengi (8, 10 au zaidi) na wamewatunza wote vizuri, inategemea na walivyojizatiti kiuchumi na kijamii, na uimara wa uhusiano wao kama familia.

Kama ni suala la utafiti, ni vigumu kupata idadi ya wastani ya watoto ambao unaweza kupendekeza wanandoa wazae, maana hayo masuala ya social and economic stability yanatofautiana sana baina ya watu.

Mimi nitazaa wangapi? Nitaangalia hali itakavyokuwa wakati huo ninapozaa, na kama yapo matumaini ya improvement. Nilishaona mtu fulani alizaa watoto 2 tu kwa sababu eti hali yake ya uchumi ilikuwa mbaya. Lakini wale 2 walipomaliza sekondari, biashara zake zikamkubali akapata pesa nyingi sana. Akaanza kubwabwaja kuwa angejua angezaa wengi zaidi. Sasa ya nini kujilaumu baadae?

Tunaishi kwa matumaini kuwa hali itakuwa bora huko baadae kutokana na bidii tunazofanya. Hivi kama mimi sasa hivi naishi chumba cha kupanga, niogope kuzaa ati kisa sina nyumba? Sasa nikifika miaka 50 nikapata nyumba yangu mwenyewe, nikizaa muda huo nitatunzaje hao watoto.

Namalizia hivi: Kama unaweza mahitaji ya kawaida ya mtoto kwa wakati huu, zaa. Kama una wawili na hushindwi kumlisha wa 3, na huna shida za kiafya, zaa. Endelea hivyo, hata wakifika 5, 6, 7 nk, idadi ya mwisho ya watoto itajileta yenyewe kulingana na hali ya wakati huo unapofikiria kuzaa mwingine.
 
mie nataka weeeeeeeeeeengi mpaka kizazi kitakapochoka chenyewe

Heeeee! umekaa sana uhindini ndo umeiga mpaka tabia zao .... maana mwanamke anazalishwa mpaka kizazi kinachoka na kuzaa taahira ambaye ndo wa mwisho kazi ipo..........................
 
Watatu me wananitosha, lakini mtarajiwa akihitaji zaidi ya hao poa tu hata kumi.
 
Heeeee! umekaa sana uhindini ndo umeiga mpaka tabia zao .... maana mwanamke anazalishwa mpaka kizazi kinachoka na kuzaa taahira ambaye ndo wa mwisho kazi ipo..........................

mungu alisema enendeni duniani mkaijaze dunia sasa kama mie nitaza kamoja au tuwili dunia itajaa lini??
 
siku nikikutembelea nitakumbana na vitoto vimefatana bila mpangilio haya mi thimo

Kama hawa??? teh teh teh! Mh Inahitaji mgongo!

duggar-family-19th-child.jpg
 
Watu bwana!!! tuko selfish sana!! Yaani tunapenda tu kutanua na hatutaki watoto wengi!! yaani sielewi..msomi unakuwa na mtoto 1 au wawili??

Minimum kwa wasomi iwe ni 5 na wamachinga iwe 3!

Wasomi you are not doing Justice to the future welfare of Tz!

Eti unakuta Professor mzima ana watoto wawili ..na mmachinga ana watoto 6! If this fair kwa future ya hili taifa kweli?
 
Dah wakuu mie wawili tuu, haya maisha ya kusomesha watoto st Maries Academy haya kindergatten tu mtoto analipiwa 1M na zaidi noma mtupu
 
Ningependa kujua hapahapa janvini, wewe uwe mwanaume au mwanamke, ungependa kuwa na watoto wangapi katika familia yako kama hujaanza kuzaa au kama unaeye mmoja tayari. Jibu baada ya kuangalia factors zote za gharama za maisha especially kama unataka mwanao aishi maisha mazuri, elimu bora ili in one day aweze kufanya mambo ya maana na sio kuishi kwa wasiwasi bila kujua kesho itakuwaje. Pia zingatia kipato cha kawaida kwa mtanzania na gharama za elimu zilivyo. Ni kama reseach na ninaamini itatusaidia wengi ambao tuko kwenye dillema ya suala hili.

Kuhusu suala la idadi ya watoto unaotakiwa kuwa nao,kuna factos kadhaa unazotakiwa kuzizingatia kabla hujafanya maamuzi,ila yote juu ya yote kigezo cha uchumi au hali yako ya kipato usikikiuke mana kufanya hivyo ni majuto makubwa baadae,japo kuna wanao egemea upande wa dini kuwa imewaelekeza waje ulimwenguni kuujaza,I don't know!.....kama utakua ni kiwanda (an industry) cha kufyetulia watoto wakati hujawaandalia maandalizi yoyote ki roho na ki mwili huo utakua ni uzembe ambao hao watoto wako watakuja kua ni wa kwanza kukulaani kwa akili zako hizo.
 
Back
Top Bottom