Opaque
JF-Expert Member
- Oct 24, 2008
- 1,359
- 719
Title ya thread inasema IQ ya mtu mlevi, maelezo yanasema IQ ya mtoto wa mlevi, confusion!!! Labda ungeweka sawa, utafiti wako umewafanyia watoto wa walevi au walevi wenyewe? Maana si lazima mtoto wa mlevi awe mlevi. Kigezo kipi ulitumia kumcategorize mtu katika kundi la walevi, idadi ya bia, muda anaospend bar, or just mnywaji yeyote? Sample ilikuwaje? Kwa mujibu wa wesite ya Wiki Answer, IQ ya mtu haibadiliki with age, ila inalinganishwa na mtu mwingine wa the same age. Sasa iwapo mtu aliwahi kuwa mlevi katika umri fulani, miaka kadhaa baadaye akaacha kabisa kulewa, then miaka kadhaa baadaye akaja akapata mtoto katika hali ya kutokuwa mlevi, huyu unamcategorize wapi, kwa walevi au wasio walevi? (Hapa ukumbuke IQ ni ratio, tena a function of age !!!) Kuna doubt nyingi katika utafiti wako. Umeshasubmit somewhere? Au ndo unakusanya data hapa kimtindo?