I don’t wanna marry him, what should I do?

Uvelia

JF-Expert Member
Sep 23, 2018
640
1,191
Nilianzisha mahusiano na huyu mwanaume miaka miwili na nusu ilopita. Baada ya miezi 6 ya mahusiano nilishtuka kajihamishia kwangu. Sikuweza kumfukuza i just decided to play along though sikupendezwa. Akachukua majukumu ya kulipia rent na matumizi mengine ya ndani.

Kuhusu mambo ya matumizi yuko vizuri tu, japo nafanya kazi na nina biashara zangu pia ila bado hunipa pesa za matumizi. Amenitambulisha nafikiri karibia kwa ndugu zake wote na wanajua tunaishi pamoja, lakini mimi anawafahamu marafiki zangu wawili tu.

Sikuwa tayari kumtambulisha sana kwa upande wangu maana i was having second thoughts. Amekuwa akihitaji mtoto tangu tunaanza mahusiano hivyo nikawa na mtihani wa kujitahidi nisishike mimba kwa kipindi chote hicho.

Amekazania sana issue ya kutaka tufunge ndoa, nimeshalikwepa sana ili ajiongeze lakini naona haelewi somo. Naogopa kumwambia direct kuwa siko tayari kuolewa na yeye, i never fell in love with him. We rushed into this, didnt give me time to digest this. Now i feel like am suffocating. Nimejaribu sana kumpenda nimeshindwa.

Nitumie njia gani ambayo haitomuumiza sana, au itakayomfanya yeye aniache? Nisaidieni maana am tired living a lie.
 
Nilitaka kumuoa alinikataa akitarajiwa kuolewa na mwingine, ikashindikana akanirudia eti nimuoe na kipindi hichi sipo tayari.

Haipo faida yako wewe kutaka asiumie kisa tu huitaji kumweleza ukweli kuwa humtaki wakati huo ndiyo ukweli, ataumia tu sababu anamatarajio nawewe hali ya kuwa kwako ipo tofauti.

Mwambie ukweli aumie ili apone haraka, kuliko kuchelewesha ukweli ambao atakapojuwa ataumia kwa muda mwingi zaidi.
 
"...Baada ya miezi 6 ya mahusiano nilishtuka kajihamishia kwangu..."...

Hapo umedanganya. Kuna vitu vilivyokufanya umpende mpaka ukakubali ahamie kwako. Pengine vitu hivyo kwa sasa havipo au vimebadilika. Au pengine ulitaka tu akusaidie katika hayo mambo ya rent na mengineyo na sasa umefikia melengo yako unamwona hafai. Kizungumkuti cha dunia: wenzio wanahaha kutafuta waume wa kuwaoa.

Ili kuzuia mikanganyiko jikaze tu umwambie ukweli. Toa sababu zako. Hata kama umepata mwanaume mwingine unayedhani anakufaa zaidi we mwambie tu. Hii ni bora kuliko kuanza kumfanyia visa na mambo mengine ya kitoto. Kama anakupenda kikweli atakuelewa na hatakulazimisha lakini lifanye hili kwa heshima, utashi mwema, uwazi na unyenyekevu. Kama unaona ni vyema unaweza kumwambia mbele ya mchungaji wenu au mtu mwingine mwenye mamlaka kama mama yako...Ukifanya vinginevyo si ajabu tutakuja kukusoma ukiwa kama mwathirika wa hawa wanaocharangwa mapanga na kuchomwa visu na wapenzi wao baada ya wapenzi wao kuwekeza sana tena kwa muda mrefu halafu wanakuja kuwafanyia visa vya kijinga mwishoni mwishoni huku...

Mungu Akuhekimishe katika hili
 
..Baada ya miezi 6 ya mahusiano nilishtuka kajihamishia kwangu......

Umemaliza mkuu......point Sana
 
Back
Top Bottom