Huyu rais wetu vipi?

JK akikaa kimya mnachonga ooh, Rais mpole jana kawatolea uvivu mawaziri na makatibu wakuu mnasema anatumia hela vibaya. Tz isigeuzwe jamhuri ya walalamishi, tukosoe na kutoa mbadala wa kutatua tatizo si kubwabwaja.
Wapashe walugaluga hawa
 
Wakuu wanaJF,
Salaamz,
Najua tumeshasema sana kuhusiana na utendaji kazi mbaya wa rais wetu, lakini kwa mambo anayoendelea kufanya (pamoja na kusemwa sana) naanza kuhisi ana matatizo makubwa zaidi kuliko kupenda mali, kuongozwa na marafiki mafisadi wenza, poor analytical skills, lack of concentration, na yote ambayo watu wengi tumekuwa tunayahusisha na kuchemsha kwake. Nahisi ana maradhi makubwa zaidi ya kiakili na kisaikolojia (Mtanisamehe kama lugha ni kali sana).
Wakati serikali inahangaika kukopa fedha kwa ajili ya matumizi ya kawaida kama malipo ya mishahara, JK kafanya mapumziko ya siku nne wakati wa sherehe za Muungano, huko Kempiski Zanzibar ambako naamini ikulu imelipa fedha kibao. Pia yeye pamoja na waziri mkuu wamekwenda msibani Njombe kuhudhuria mazishi ya Mama yake Mh. Bi Makinda na bado Mkulu huyo kaibuka na semina elekezi ya viongozi wa juu wa serikali kwa siku nne huko Dom.
Mtazamo wangu ni kwamba mambo haya hayana uzito wa kupoteza fedha za walipa kodi kiasi hicho hasa katika hali ya ukata tulilyonayo. Matatizo ya utendaji wa Mawaziri, Katibu wakuu na wakurugenzi mbalimbali si kwa kuwa hawajui majukumu yao bali ni kwa sababu hakuna sauti ya kuwasisitiza na kuwaonesha njia inayotakiwa. TRA kama wanashindwa kukusanya mapato vizuri ni kwa sababu hata yeye JK haijulikani anafurahia uzembe wao au haupendi.
Anayehitaji tiba au semina ni JK peke yake na anaweza kufanyiwa huduma hiyo akiwa nyumbani au ofisini kwake na si katika mahoteli.
Kama nchi haina fedha za kutosha jambo jema ni kuepuka matumizi yasiyokuwa ya lazima ya kifahari na si kukopa na kuongeza matumizi yasiyokuwa na maana kama semina. Sijui hata JK huwa anatumia nini kufanya maamuzi!

Haswaa, Semina elekezi, anawaelekeza nini sasa wakati Serikali haina hela na wala haiweza kuendesha miradi yake ya maendeleo, hela ya mishahara tu wanakopa.
 
Back
Top Bottom