Huyu ni shujaa au shetani?

dawa yenu

JF-Expert Member
Jan 7, 2014
2,822
3,651
Hii nimeipata huko facebook na nimeona ina hadhi ya kuwekwa hata hapa jamii forums.

dieing child.jpg




picha hii ilipigwa na mwandishi wa habari za picha (Photo journalist) kutoka nchini Afrika ya kusini aliyeitwa Kevin Carter mnamo mwaka 1993 huko Ayod nchini Sudan jirani na kambi ya umoja wa mataifa ya kugawa chakula.

Pichani anaonekana mtoto aliyedhohofu kwa njaa na kunyong'onyea kiasi cha kushindwa hata kusimama kutembea na pembeni yake kukiwa na ndege tai, ambaye chakula chake ni mizoga ya nyama akiwinda kula nyama ya mtoto pale tu, atakapo shindwa kujiburuza chini.

Ilimchukua dakika takribani ishirini Kevin Carter kuipata picha hii, pale ambapo ilimbidi kukaa kwenye angle nzuri kuisubiri. Anapoonekana tai huyo ni makadirio ya mita kumi kumfikia mtoto huyu, aliyekuwa akitambaa chini kutafuta kuokoa maisha yake na njaa.

Ndege tai huyo alitua umbali kidogo na mtoto huyu na kuanza kusogea pole pole kumfuata mtoto mpaka pale alipofika mita 10 karibu nae, ndipo Kelvin Carter akapiga picha hiyo japo awali alipiga nyingine wakati tai anasogea kwa mtoto, kabla ya kuipata hiyo moja iliyoleta utata mkubwa sana Duniani.

Baada ya kupiga picha hii kesho yake Carter aliiuza kwenye gazeti la kila siku la The New York times la huko Marekani na iliuza sana gazeti kwa hiyo siku. Huu ndio Ulikuwa mwanzo wa mjadala mkubwa uliopelekea mpaka wasomaji wa gazeti lile kupiga simu kuulizia kama mtoto huyu alipona ama alikufa na tai kumla nyama.

Kwa mujibu wa Carter mwenyewe anasema baada ya kupiga picha ile alimfukuza tai yule na kuondoka maeneo hayo maana alizuiliwa kabisa kumgusa mtoto na waliokuwa wakimuongoza, kwa kuhofia kuambukizwa magonjwa ambayo pengine angekua nayo mtoto aliyedhoofu kwa njaa kali.

Kevin Carter aliongeza kuwa wazazi wa mtoto huyo walikuwa kwenye kambi ya umoja wa mataifa wakigombea chakula kilichoshushwa na ndege muda huo ambayo haikuwa mbali (mita chache) kutoka alipokuwa mtoto huyo.

Mwaka mmoja baadae yaani 1994 picha hii ilimpelekea Kevin Carter kushinda tuzo ya Pulitzer (Pulitzer prize), kama picha bora iliyofanikiwa kuonyesha hali halisi ya njaa iliyoikumba nchi ya sudan.

Baada ya kushinda tuzo hiyo Carter hakuwa na amani ya moyo kutokana na misukumo aliyokuwa akiipata kutoka kwa jamii, amabayo ilihusiana na mazingira ya upigaji picha ile.

Baadhi walimwona kama mtu mwenye roho mbaya sana pale alipokaa dakika 20 kusubiri kupiga picha ile badala ya kumsaidia mtoto huyo aliyekuwa anateseka kwa njaa.

Licha ya yeye mwenyewe kujitetea kuwa hakutakiwa kumgusa wala kumsogelea mtoto yule bado msukumo ulikuja kuwa asingepiga picha ile yenye kusikitisha na kutoa machozi na angechochea msaada utolewe kwa mtoto kwa kuwa hakuwa mbali na kituo cha msaada.

Kevin Carter alikaa kwa muda kadhaa nchini Sudan akiongozwa na wanajeshi wa nchi hiyo kila alipokwenda kutekeleza majukumu yake.

Miezi kadhaa baada ya Kevin Carter kushinda tuzo ile akiwa nchini kwao Afrika ya Kusini aliendesha gari lake mpaka uwanja aliokuwa akicheza enzi za utoto wake na *kujiua*.

Kabla ya kujiua Aliandika maneno yenye uchungu na masikitiko makubwa akionyesha ni kwa jinsi gani anakosa amani ya moyo mpaka Anajitoa uhai wake mwenyewe.

Kwa miaka kadhaa sasa baada ya kuondoka Carter ameacha picha hii ikibaki kufundishia waandishi wa habari juu ya dilema (ethical dilema) watakazokutana nazo pale watakapo kuwa wanatekeleza majukumu yao.

Swali kubwa linalotatiza kila siku ni je Kelvin Carter alipaswa kupiga picha hii ama hakustahili kuipiga kabisa? je Kelvin Carter ni shujaa au shetani?


SWALI KWAKO MWANA JAMIIFORUMS.

kwa upande wako wewe unamtafsiri vipi huyu mwandishi aliyepiga hii picha? Je ni shujaa au ni wakala tu wa shetani?
 
Limeishajadiliwa humu kitambo sana kabla hata halijaenda huko ulipolikuta, fanya "kufukunyua" baadhi ya uzi humu utakutananalo.
 
Kila siku wanajiunga member wapya, haikosi kuna watu hawajawahi ona hii, na mimi kwangu hiyo stori ni mpya na imenifikirisha!

Na niseme tu, kwamba "mtu hufia mahala alipo" ukikata roho ukiwa safarini utatajwa hivo, huyo Bwana "aliifia kazi yake"

Ni shujaa wakazi, wala hakuwa na makosa kupiga hiyo picha,

hata kama hakuwa na mpango wowote na mtoto huyo, kwa sababu, kutompa mtu kile anachokitaka kutoka kwako siyo lazima iwe dhambi, kuna vingine ukitoa ndiyo inakuwa dhambi!

Ikiwa jamii iliyomzunguka haijachukua hatua, ujasili wasiwasi au hatua yoyote inaweza kujitokeza kwa mtu mwingine haiwezi kuhesabika makosa
 
Hii stor ya kitambo sana arifu. Karibu JF.
Ila kama unataka maoni yetu ni kwamba huyo mwandishi ni mpuuzi no 1.
 
Back
Top Bottom