Magurudumu
JF-Expert Member
- Oct 13, 2012
- 1,747
- 486
Hujui kama nchi hii inaongozwa kwa kupokezana vijiti? Alianza namba 2, akaja namba 3. Kuna ubaya gani namba 4 akifuata nyao za kaka zake?
the same old shit contribution, just from the different old shit 'kamanda'.
Kitu kimoja kimesumbua akili yangu tangia juzi japo wengu kimazoea tunaona ni sawa tu!mmh, kwa maana hiyo, hii nchi wameona ni shamba la Bibi yao, wanachukua wanachotaka wanagawana wao kwa wao, wanampa zawadi ya vitu, mngeni waliyefurahishwa naye, hawafikirii kuwa hii ni nchi, sote tunatakiwa tufaidike, tuijenge, tujijenge, kwa kutumia rasilimali zilizomo, na sio kunufaisha kikundi fulani kidogo cha watu, huku wengi waliobaki wanataabika
Sometimes ukiwa na kitu kichwani, ni vyema basi ukatumia kitu hicho kichwani kuvaa viatu vya Rais aliyeko madarakani.Je wakati anachukua Nchi hali ya Taifa na hasa mfumo alikuwaje?Tusiangalie Mali za Taifa tu,Tuangalie pia Tabia na Matendo ya Wanataifa ,kuanzia ngazi ya familia mpaka Taifa.Naungana na wanajamii wengi kuwa,hata kama issue zako ulizopresent zina ukwel kidogo,i dont think JK is bogus as you think ana washauri hata mambo binafsi,he cannot be that full.Tuachen majungu.Hawa jamaa ni wezi tu wala msimpake matope JK hana sababu yoyote ya kumtumia waziri kuiba tena wizi mdogo mdogo wa mil 600.
Jamaa akiamua kuiba ana uwezo wa kupiga hata 50bil at once na mtu yoyote asielewe.Uongozi ni mgumu hasa kwa misingi iliyoachwa na akina mwinyi na mkapa hawa ndo walioiharibu nchi.
mmh, kwa maana hiyo, hii nchi wameona ni shamba la Bibi yao, wanachukua wanachotaka wanagawana wao kwa wao, wanampa zawadi ya vitu, mngeni waliyefurahishwa naye, hawafikirii kuwa hii ni nchi, sote tunatakiwa tufaidike, tuijenge, tujijenge, kwa kutumia rasilimali zilizomo, na sio kunufaisha kikundi fulani kidogo cha watu, huku wengi waliobaki wanataabika
Sometimes ukiwa na kitu kichwani, ni vyema basi ukatumia kitu hicho kichwani kuvaa viatu vya Rais aliyeko madarakani.Je wakati anachukua Nchi hali ya Taifa na hasa mfumo alikuwaje?Tusiangalie Mali za Taifa tu,Tuangalie pia Tabia na Matendo ya Wanataifa ,kuanzia ngazi ya familia mpaka Taifa.
Kwa ujumla tabia zetu watanzania zimekua hatarishi kwa TAIFA na huku kwa ujumla wetu tabia hizi tunaziona kama UJANJA na MAALIFA.Leo hii mtu akipewa madaraka au nafasi kinachotekea akilini kote tunawaza kupiga.Kama normal citizen wanashabikia matendo ya kialifu na ujanja ujanja sembuse matajiri wenye fedha za kumnunua yoyote yule ikibidi kichwa chake.
Mtaani mtu ambae haeleweki katoka wapi ila anamilki mjengo wa ajabu na magari ya kifhari lukuki tunamsifia kwa manen kedekede mara fogo, zungu, don, msure, na kumwalika kwenye shughuri mbalimbali za kijamii na akione namna gani vipi anaomba madaraka na kwa ufinyu wa akili zetu tunampa kesho na kesho kutwa yuko kwenye kiti cha maamuzi, Je hiyo imekaaje katika sura ya kuunda Taifa katika ngazi yoyote ile ya kijamii au kiuchumi au kiutamduni.
Leo utamaduni wetu uwezi kufanyiwa jambo la kijamii kama huduma bila kutoa chochote,tumefika hapo kwa safari baada ya Mwalimu kuona aliyoyafikilia yanawezekana kuwa neema kwa watanzania wote yaliitaji moyo wa mwendawazimu kuyatekeleza, na yeye kwa kuwa conscious akaona hawezi kuwa Mwendawazimu kukabiliana na ujio huo mpya wa siasa na uchumi wa karne ya ishirini na moja akakubali kung'atuka na kupisha wengine.
Kwa kuwa bado hatujajua jinsi ya kugrom viongozi kulingana na nyakati,yani tulipaswa kuwa na mfumo wenye kutizama NYAKATI na kuwa kwa dhama fulani panaitajika viongozi wenye tabia na matendo ya aina fulani ili kukabiliana na hali halisia na kufanya yaliyo bora kwa mujibu wa nyakati husika.
Hivi kweli wakati mwingine ukivalishwa viatu vya Urais unapambanaje na wabaka uchumi waliokomaa, wauza unga wakubwa, matapeli na wasanii wanaoweza kuforge muhuri na signature ya kiongozi wa juu ambae akionyeshwa sign yake iyo iliyopigwa anakili kuwa ni yake kumbe fake.Anapambanaje na watu wenye itikadi za uafrika ilikufanikisha lao na kama uamini kwa ilo bishana na biblia, anapambanaje na watu wenye nguvu za kifedha wenye tabia na matendo ya kihalamia ambao usiku na mchana wanatafuta kila mbinu kuhakikisha sheria na sera zinawafavour wao na biashara zao na familia zao na washirika wao.Rais anapambanaje na watendaji wa umma na jamii kwa ujumla wake ili kuleta TAIFa lenye mafanikio kwa wote.
Binafsi nakili kuna mbinu ambazo hata ningelikuwa mimi ningezifanya kuwa binafsi lakini ndani yake ni kutengeneza kile ambacho kitazaa jema kwa Taifa, lakini mbinu hizo binafsi ni hatarishi pia kwa tafsiri ya umma,manake jsutification zake ni waerevu tu wanaoweza kuzikubali na si normal people,ila kutekeleza hayo lndipo hapo intelligence na smartness vinapopaswa kulala.Kwa kuwa katika level ya Taifa ilipofika ni nadra sana kukuta kiongozi hana gharama,waswahili wanasema tunatofautina gharama na sio kweli hakuna binadamu asiye na gharama za kunulika.
Marehemu JF Kennedy alipotaka kuingia kwenye songo mbingo ya Russia kuhusu visiwa vya CUBA, alitumia juhusi binafsi kuepusha vita ya tatu ya Dunia.Wakati Naional Security committe inamlazimisha kusign tamko la vita yeye anakula chenga na kuplay delay tactic ili aweze kuepusha vita hiyo kubwa ambayo ingeandika historia ya dunia.Na Kwa kushrikiana na Mdogo wake Bobby walifanikiwa kuepusha vita ile na kuithibitishia Dunia ukweli wa sakata zima kwenye kumbi za UN.J magerali wale walifurahi kwa ilo?
Mikakati na mbinu za kudeal na maswala kadha wa kadha ya kitaifa yenye sura za kubadilisha mwenendo, sura, tabia, mazoea, uwajibikaji, utamaduni, yanaitaji akili nyingi sana na busara za hali ya juu sana kwa kuwa gharama zake wakati mwingine uwa ni vifo na maafa.Kwa kuwa kubadili jambo ambalo vichwani mwa watu lina hesabika kuwa ndio utamaduni na kawaida basi uwa ni KUFA NA KUPONA ili kulifanya liwepo.
Ukitaka kujua linaugumu swala la kugeuza jamii toka kwenye kitu ambacho jamii inaona ni sahihi kwenda kwenye utamaduni mpya nna mgeni kwao ebu nenda kwenye makabila ya wakurya, wamasai, wanyaturu na wasomali zungumza kuhusu tohara ya watoto wa kike kuwa unaipiga vita na kuanzia leo mwisho kisha tegemea majibu ya ndiyo tumesikia Mheshimiwa, kesho tu unasikia RILANDI na LITUNGU linasambaa hewani ukiuliza nini hicho wtakwambia ni SARO.
Naamini Werevu, Elimu, haiba, Malezi na kabila ya Kiongozi pia uongeza ushawishi wa mapambano, wakurya akisema NITAKUTEMA MURA anamaanisha hivyo na hata mpewa ujumbe ataupokea hivyo hivyo kuwa hapa kimesanuka.Hivyo jinsi ya kiongozi mkuu kudeal na issue hizo sensitive inategemea pia wenye washauri werevu hao wamemwada kuwa Rais wa Haiba gani kulingana na jinsi walivyompokea.
wewe naona akili zako ni kibogoyo, hutaelewa au kupevuka hadi ufeumeamua kumaliza chuki zako za kukosa ukuu wa wilaya na uwaziri hapa jf.tuache tufikirie mambo ya nchi sio hasira zako
wewe unaye pinga hili bado hujapevuka mentallyYa nini kumtaka mtu akafuatilie wakati unafahamu fika kwamba inaweza kuwa ngumu kwake kufanya hivyo?! Kama wewe una uhakika na unachokisema, weka hapa huo ukweli unaoufahamu ili wote tuujue! Kumtaka mtu akafuatilie inaonesha basi hata wewe huna uhakika na unachokisema au hauna dhamira ya kweli ya kufichua madudu yanayofanyika nchi hii! Weka hapa huo uozo unaofanyika HSC kwa msaada wa JK!