Huyu ndiye tatizo katika nchi ya Tanzania na sio Ngeleja, Mkulo wala Maige

Taarifa nzuri ambayo imenihakikishia kwamba niliyokuwa naamini all along kumbe ni sahihi.Good analysis and conclusion.Sina cha kuongeza.
Nimeona thread ya invisible

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/266433-mkulo-maige-ngeleja-kikaangoni-takukuru.html

inayozungumzia waliokuwa mawaziri 3 kuwa wanachunguzwa na TAKUKURU na kuwa wameamliwa kuwa wanaripot kila siku saa 3 asubuhi...

Hawa jamaa(ngereja,mkulo na maige) hata wakichunguzwa na hata wakiamliwa kuwa wanaripori TAKUKURU kila baada ya dakika 5 hawawezi kuchukulwa hatua yoyote.

Nasema hawawez kuchukuliwa hatua yoyote maana mali niyngi walizopata kwa njia ya udanganyifu zina Baraka toka kwa rais kikwete.. na pengine niseme kwamba kuondoka kwa hawa mawaizri ni pigo kwa kikwete mwenyewe maana sasa mtiririko wa deal alizokuwa akifanya kupitia kwa hawa jamaa zimeingia doa na inabidi aanze upya.

Mali haramu walizochuma hawa mawaziri zina baraka ya mkuu wa nchi kwa sababu nae anashiriki katika kuiibia nchi kupitia baadhi ya mawaziri anaowaweka hasa kati wizara nyeti..
Ngoja nitoe mfano juu ya maige

Mwaka jana kuna taarifa zilipatikana juu ya maige kuwa ameuza vitalu bila kufata taratibu..taarifa zile zililazimu uchanguzi wa kina nawa kiinteligensia kufanyika..mwaka jana hiyo hiyo mwezi wa 8 huko arusha katka hotel ya Kibo palace maige alikabidhiwa pesa taslimu mil 600(TSH) kama malipo ya vitalu alivyogawa kwa kampuni hiyo. Ndani ya hoteli kulikuwa na vjana wa TISS maana taarifa walikuwa nazo juu ya deal hilo na mara baada ya malipo hayo kufanyika; vijana waliingia chumban na kumuweka maige chini ya ulinzi...maige alijawa na uoga sana baada ya hapo alihojiwa kwa zaidi ya saa mbili..maelezo ya maige yalitoa picha kuwa mkuu wa nchi anahusika maana maige alisema kwa mdomo wake kuwa ni kweli amegawa vitalu lakin hata yeye amekuwa akipokea maagizo toka kwa mkuu wa nchi ..alieleza jinsi mkuu wanchi anavyohusika na kusafirisha pembe za ndovu hasa katika mbuga ya ruaha kazi inayosimamiwa na ISSA ASSASI..

Maige pia alieleza jinsi mkuu wa nchi pamoja na viongozi wengine wa nchi kama lukuvi,luhanjo(aliyekuwa katibu mkuu kiongozi)yeye mwenyewe maige na katibu wake, jinsi wanavyofanya biashara ya kupasua mbao na kusafirisha kutoka msitu wa Sao Hill huko Iringa pasipo kulipia garama zozote za msitu...alieleza mengi lakini mwisho wa siku taarifa hiyo ilipofikishwa makao makuu ilileta mtafaruku mkubwa hali ambayo ilipelekea mmoja wa wakuu wa idara kuondolewa kweye idara na kupelekwa nje ya nchi katika moja ya balozi zetu huko kwa kile kilichodaiwa kuwa kwa nini amefatilia na kutuma vijana kwenda kumkamata maige..

Ngereja nae vivyo hivyo,ngereja amefanikiwa kwa kias kikubwa kwa mkuuwa nchi kupata migodi au kuwa mmoja wa wamiliki wa migodi..ngereja amefanikiwa pia kuhakikisha mkuu wan nchi anapata dhahabu toka kwa kila mgodi uliopo hapa nchi unaomilikwa na kampuni za kigeni...sasa ni katika deal hizo na wao wanapiga cha juu ..

Mkulo amefanikisha kwa kiasi kikubwa kununua na kusafirisha na kuyaingiza nchini magari ya mizigo na mafuta amabayo yote ni mali ya mkuu wanchi...leo mnapoona hizo vogue na vx zimepak ni sehemu ndogo sana ya kile alichoiba .....

Leo ninapoona TAKUKURU wanafatilia swala hili ni kiini macho maana najua hakuna lolote watakalofanywa na TAASISI KIBOGOYO hiyo...

Mwiba mkali na mbaya uliomo katika nchi ni huyo Rais wa nchi..huyu ndiye anapowachagua hawa mawaziri huwachagua akiwa na maslahi binafsi kwa kuwambia ‘’ HAKIKISHA Napata hiki au kile..hili neno HAKIKISHA ndilo huwapa kiburi mawaziri na wanaposhika nyazifa hzo huanza kuiba na kufanya ubadhirifu mkubwa maana wanatii lile neno ‘’HAKIKISHA’’ na wakati huo huo na wao wakinufaika na hilo neon HAKIKISHA na ndio maana mnaona wananunua majumba, wanatoa mil 500 majimboni kwao, na wengine wananunua apartments na mengine mengi. Lakini anayebaka nchi hii kinyume na maumbile bila huruma ni mkuu wa nchi..anzeni na huyu ambaye ndiyo tatizo maana hata juzi kashauriwa kutowangiza katika baraza la mawaziri baadhi ya wabunge lakini alikataa mmoja wa wabunge hao ni steven masele....

Bado kuna giza nene katika uongozi wa nchi
 
Ni fact gani aliyoitoa mleta mada?! Labda tu mie nitumie akili ya kawaida isiyohitaji shahada yoyote! Sh. 600M, kama zote zitakuwa ni denomination ya Sh. 10,000/= then TZS 600M ni sawa na Bundles 60 zenye TZS 10M kila moja! Kama atatembea na briefcase kubwa kubwa, angehitaji si chini ya brief kubwa kubwa 5! haiingii akilini kuona waziri akiingia hotelini na mabegi ya kawaida au viroba kisha vitu hivyo vinatoka vikiwa vimetuna! Ina maana alifuatana na watu wake?! Sizani kwamba MAige anaweza kuwa foolish kiasi hicho....unaenda kuchukua mzigo haramu halafu unafuatana na watu!!! Angesema alipewa cheki au STG or Euros, at least ingeleta sense!

Ngoja nami nitumie elimu yangu ya STD VII: brifcase 5 inawezekana tu hapa tanzania, mbona twiga waliingizwa kwenye ndege? Inanikumbusa animation ya 'MADAGASCAR'
 
Hongera mwanangu kwa taarifa hii, sasa tatizo letu ni KATIBA ndugu, tukomae wananchi waweze kutoa mapendekezo ya namna gani katiba iwe ili ata kipengele cha kumfukuza Rais kazi ata kama muda wake haujaisha kiwekwe pale atakapogundulika ni FISADI au mnaonaje wajemeni.

unachosema nikweli jamani watu tumechoka na haya maisha au mpaka siku mtu ajilipue ndo itaeleweka
 
Nimeona thread ya invisible

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/266433-mkulo-maige-ngeleja-kikaangoni-takukuru.html

inayozungumzia waliokuwa mawaziri 3 kuwa wanachunguzwa na TAKUKURU na kuwa wameamliwa kuwa wanaripot kila siku saa 3 asubuhi...

Hawa jamaa(ngereja,mkulo na maige) hata wakichunguzwa na hata wakiamliwa kuwa wanaripori TAKUKURU kila baada ya dakika 5 hawawezi kuchukulwa hatua yoyote.

Nasema hawawez kuchukuliwa hatua yo.. Eeh kwel kaz ipo..
 
Nishasema sana tatizo kubwa na baya kwenye nchi hii ni rais mwenyewe wala hakuna kingine,matukio yote yanayotokea wewe unganisha dots tu utakuta kila kitu tatizo ni yeye,hata kuitwa dhaifu ni lugha ya kistaarabu imetumika ili kumsitiri huyu jamaa ni hatari kupita maelezo.
 
Jamani mbona makubwa, tunaomba Ikulu itoe ufafanuzi juu ya tuhuma hizi na ikiwezekana aliyezitoa afikishwe mahakama... siyo kushughulikiwa, akajibu mahakamani ili dunia imjue uzushi wake
 
JK anaweza kuwa fisadi lakini hawezi kuwa -------- kiasi hicho cha kuamini watu aliokutana nao ukubwani na kuwapa deal hatari kama hizo!
wewe ndivyo unavyo amini? huyo ni fisadi tena wakati mwingine unashangaa kwanini afanye hivyo? kinacho mponza ni wale wanao mwambia sasa ni zamu yetu!! kuna wakati amewahi kusafiri na jamaa mmoja kwa kisingizio ni mfanya biashara wakati hata kijiko hajawahi kuuza. kwakuwa ni swahiba wake wa siku nyingi basi akapata safari,fedha za walipa kodi wengine wanakula kiulainiiii. NCHI INA SHIDA HII!!
 
Acha ubwege zamani ungetumia media gani kutoa maoni? Leo hii hakuna jinsi ya kudhibiti ndo maana hata yeye anaamua kukaa kimya. Alafu anashindwa kufuatilia maana watu wanafact watamuumbua sana akijitia kuwa mkali. Shangaa jinsi watu wanavyokula nchi kana kwamba hatuna rais
Mungu akubariki Ndugu Jakaya kwa kustawisha uhuru wa kutoa maoni,zamani mawazo kama haya unaweza kuyatoa ukiwa Tunduma au Namanga wakat unatokomeya,leo mtu anaongea haya yupo mita mia kutoka ofis za usalama wa Taifa bila ya waswas
 
Ni fact gani aliyoitoa mleta mada?! Labda tu mie nitumie akili ya kawaida isiyohitaji shahada yoyote! Sh. 600M, kama zote zitakuwa ni denomination ya Sh. 10,000/= then TZS 600M ni sawa na Bundles 60 zenye TZS 10M kila moja! Kama atatembea na briefcase kubwa kubwa, angehitaji si chini ya brief kubwa kubwa 5! haiingii akilini kuona waziri akiingia hotelini na mabegi ya kawaida au viroba kisha vitu hivyo vinatoka vikiwa vimetuna! Ina maana alifuatana na watu wake?! Sizani kwamba MAige anaweza kuwa foolish kiasi hicho....unaenda kuchukua mzigo haramu halafu unafuatana na watu!!! Angesema alipewa cheki au STG or Euros, at least ingeleta sense!

usiwe mbishi sana,unajua ukubwa na uwingi wa pesa ya EPA wewe?just imagine malori ya tani 10 yalikuwa saba yalichukua CRDB na yakaondoka mchana pale AZIKIWE ITAKUWA HIZO 600M.CHEZEA WEZI WEWE
 
"Tumefika hapa kwa sababu ya Wabunge dhaifu wa CCM,serikali dhaifu ya CCM na rais dhaifu wa CCM"

J.J. Mnyika!
 
Mkuu naona ulikuwa unaandika huku ukichungulia nje mara kwa mara kupitia dirishani kwa kuhofia utakutwa. Hata hivyo naweza kuyaamini maneno yako kuwa yana ukweli fulani, sababu kuu ya kuamini hii ni kutokana na uzito wa JK katika kuwachukulia hatu wahusika hasa walipotia nta masikioni na kugoma kujiuzuru. Hilo ndilo taifa lenye watu masikini huku utajiri na rasilimali za nchi wakifaidi watu wachache. Lakini nadhani tunaelekea katika kipindi cha mabadiliko makubwa, nina imani mali yote ya watanzania iliyoibwa na wajanja wachache itarudi mikononi mwa wananchi. Ukomo wa CCM unakaribia kwa sababu hakiwezi kushindana na upepo wa mabadiliko ujao, upepo ambao unakwenda sambamba na kuundwa kwa katiba mpya, katiba ambayo bila shaka itatoa kibano kwa hawa majizi wanaotufirisi sasa.
Hiyo ni ndoto tu mzee wala hakirudi kitu hapo tumeshapitisha uraia wa nchi mbili tukimaliza ngwe tunasepa zetu tehe, tehe, tehe, tehe, teheeeeee
 
Back
Top Bottom