Huyu kuku aingizwe kwenye maajabu ya Dunia

Maboso

JF-Expert Member
Feb 18, 2013
5,164
5,761

0.1kuku+at+sengerema.jpg

Ni kuku asiyekuwa na manyoya amefumwa na kamera ya mtandao huu katika kijiji cha Busisi wilayani Sengerema mkoani Mwanza.

0.1kuku+at+sengerema1.jpg

Manyoya au magoya kama wengine wanavyoyaita humsitiri kuku katika mvua, kujikinga na baridi kwa kumpa joto, hutumika kama kinga ya kuchomwa na vitu vyenye ncha kali kwani ngozi ya ndege ni laini, hivyo anapoingia kwenye purukushani hususani vichaka vyenye miiba hawezi kudhulika. Sasa anapokuwa katika hali hii ya kukosa magoya ni shida.

0.1kuku+at+sengerema2.jpg


Ndege huyu yuko tayari tayari, ni kisu chako tu, haitaji kunyonyolewa!! Cha ajabu si mwewe wala ndege mwarabu (sijui ndiyo ndege aina ya Tai) wala wanyama wakali kama mbwa wote hawajawahi kumdhuru kuku huyu zaidi ya kumpita tu. Duh na uroho wote walionao ..Maajabu..!


 
Duh! Una picha inayomuonyesha huyo 'kuku' na mazingira zaidi y ardhi? Mfano nyumba, vichaka, etc
 
Wa hivi ni mara yangu ya kwanza kumuona.

Ninaowajua mimi ni wale kuku wanoitwa vishingo(akiwa mmoja kishingo)
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom