Huwapendi Freemason ila unapenda vitu vyao

Mhaya

JF-Expert Member
Aug 20, 2023
1,658
4,866
Kitu cha kwanza kitakachokupa nguvu katika dunia hii ni elimu. Utake usitake elimu ina nguvu kuliko kitu chochote kwenye hii dunia. Kwa nini Mafreemason na Illuminat wanaitawala hii dunia? Ni kwa sababu wamesoma sana. Wanajua mambo mengi mno.

Ukikutana na Freemason mwenye digrii 33 na akaanza kukupa elimu ya dunia hii, utashangaa sana, itakufanya ugundue kumbe wewe ni mjinga unayetembea na kuvuta pumzi ya dunia hii.

Sasa dunia hii imejaza wajinga. Maarifa makubwa na mazito yamefichwa kwenye makaratasi. Waroma kitu walichokifanya cha kwanza ni kuondoa ujinga vichwani mwao, na wakafanikiwa.

Ukija kwa viongozi, wanasema hakuna kitu kizuri kama kumuongoza mjinga. Utasoma masomo ya dini, ila kama hujasoma masomo ya duniani, bado kuna ujinga mwingi sana upo kichwani.

Nigeria ni moja ya nchi ngumu sana kutawalika, kwa nini? Ni kwa sababu wamesoma, mtu mwenye elimu huwezi kumuongoza kimagumashi, ni ngumu kumuongoza mtu huyo kwa sababu kila wakati atakuwa anakuuliza maswali, je, utaweza kuyajibu maswali yake?

Unapojiunga na Freemason, kitu cha kwanza wanakupa elimu. Wanakuletea Biblia na uanze kuisoma kwanza, uisome yote, ukimaliza, wanakupa Korani napo uisome yote. Wanataka kwanza ujue kila kitu kuhusu hizi dini mbili halafu sasa nao wakupe elimu yao.

Unapokutana na Freemason na kuzungumza naye, unagundua kabisa huyu jamaa ni tofauti sana. Niliwahi kukutana na marehemu mzee Chande (Mkuu wa Freemason Tanzania) miaka ya nyuma, kwa namna alivyokuwa anaongea, nikasema kama Tanzania tungepata viongozi hata 10 wenye akili ya huyu mzee, aisee tungekuwa mbali sana.

Kitu cha kwanza unapandikizwa elimu. Wanajua kabisa kwamba dunia imejaza watu wengi wasiokuwa na elimu, na wanaziongoza serikali nyingi hasa Afrika kuhakikisha elimu inayopatikana inakuwa duni, ili watu wasije kufunguka na kujua mengi. Na wanashinikiza sana watu wajikite zaidi kwenye dini zao kwa kuwa wanaamini hazitokuja kukusaidia kwa chochote kile.

Mimi napenda sana kuzungumza na mtu mwenye elimu ya darasani lakini si elimu ya kanisa ama msikiti, kwa nini? Kwa sababu kila nitakachokwambia, utanitajia mstari, yaani utanipa andiko ambalo nikikuuliza ameandika nani, stori ilikuwaje, utanipa ileile ambayo Freemason walitaka uwe nayo miaka nenda rudi.

Huwa ninawaambia mara nyingi sana, hii dunia ipo chini ya Freemason, wao ndiyo wametupangia mambo mengi, wao ndiyo walituchagulia siku za kuabudu, wakatuchagulia na muda. Leo kuna makanisa mengi yanadhaminiwa na Freemason, kuna watoto wengi wa wachungaji na mashehe wanasoma katika shule za Freemason.

Ninapokwambia Freemason ninamaanisha dude moja kubwa sana. Siku omba Mungu upate kuwafahamu hawa watu vizuri. Wao wanaimiliki dunia, wao wanamiliki michezo, wanawekeza pesa nyingi sana. Wao wametengeneza pesa za Marekani, ukiangalia dola, wameweka alama zao za Kifreemason na Illuminat.

Leo kila mtu anatamani kwenda Marekani, ile nchi inaongozwa na Freemason. Kwa siku lazima uwatumie na kuwaabudu wao. Unakuja Facebook, unakwenda Youtube kuangalia miziki, ukitoka hapo unakwenda kuangalia muvi, hizo industries zote zipo chini yao. Wanamiliki mitandao yote ya kijamii.

Hivyo ukitaka kwanza kupingana na watu hawa, toka Facebook, toka WhatsApp, toka Instagram, usiangalie muvi na mambo mengine, halafu simama na sema mimi napingana na hawa jamaa. Huwezi kupingana nao huku ukiwa unatumia vitu vyao.

Leo ni sawa na kusema nipambane na serikali yangu tukufu halafu hapohapo natumia ardhi yao, natumia vitu vyao, itakuwa ni kujidanganya tu kwa kuwa wakisema hapana, basi nitakuwa nimekwisha.

Freemason ni dude kubwa, ila kuna dude kubwa zaidi ya Freemason, na hili linaitwa Illuminat. Tatizo huwa ni moja tu, watu hawataki kusoma na kuwajua watu hawa vizuri, wanaamini kuwajua Freemason kwa undani ni dhambi, ila si dhambi kutumia mitandao yao. Ni upuuzi.

Freemason wanamiliki benki ya dunia, wanamiliki benki ndogo ndogo, wao ndiyo wanauendesha uchumi huu na walifanikiwa zamani mpaka kukupangia siku zao za kwenda kuabudu. Wakakuletea tarehe zao, siku na kila kitu.

Mungu alimpa shetani nguvu ya kuutawala huu ulimwengu, yaani upo chini yake na ndiyo maana anaonekana kuwa na nguvu sana. Kumshinda shetani ni kumtumia Mungu, vinginevyo huwezi kushindana naye hata kidogo. Na ndiyo maana tunarudi palepale kwamba Freemason wanamjua Mungu wa kweli ni yupi, inawezekana si huyo unayemuabudu.

Wana siri kubwa mno! Wana elimu nzito sana ya uongozi. Wakati Michael Jackson amechoka kuendeshwa nao, alitoka hadharani na kusema SONY ni mashetani. Hii SONY ipo chini yao, na ni kampuni kubwa ya muziki na filamu, wao wanaendesha mambo mengi kwenye industry ya muziki na muvi. Wakati amekorofishana nao, hakuchukua muda mwingi akafariki dunia.

Unapoanza kufanya kazi nao na baadaye kuwasaliti, jambo la kwanza wanakumaliza. Huwa ipo hivyo. Hawawataki wasaliti, wanakupa kila kitu unachokitaka, mwisho wa siku wanakumaliza kama tu utakwenda kinyume nao.

Kitu cha kwanza nenda kasome. Hata vitabu vya dini vimeandika tupate elimu ya dunia kwanza. Tuijue dunia na mambo yake, tuwajue wamiliki wa hii dunia na tujifunze namna ya kupambana nao.

Lengo kubwa la Freemason ni kuteketeza kila kitu kinachohusiana na Mungu. Ukiangalia hata kwenye simu, wamekuweka Biblia, Korani, wameweka hivi kwa mikakati yao mikubwa. Unapokuwa na Biblia kwenye simu yako ama Kurani, automatic huwezi kununua vitabu hivyo.

Mpango wao mkubwa wanataka uwe bize kuvisoma kwenye simu yako, ukiacha kununua, wanaanza kuzipoteza mitaani, mwisho wa siku Biblia na Korani hazitopatikana mitaani, hutoweza kujua kwa sababu si unazo kwenye simu yako. Wakati zikiwa zimepotea duniani, halafu wanaziondoa kwenye simu yako. Nini kinafuata? Biblia na Korani zinaanza kuwa dili lakini kwa bahati mbaya hazotoweza kupatikana.

Kila kitu hawa jamaa wamekisuka. Wanakuendesha hii dunia kwenye mikakati yao mikubwa sana. Sasa mambo haya huwezi kuambiwa msikitini wala kanisani, wao watakwambia tu changia ujenzi wa msikiti ama kanisa. Haya mambo wachungaji na mashehe wanatakiwa kuwaambia watumishi wao kwamba ni lazima kununua Biblia ama Korani nyumbani lakini si kuwa nazo kwenye simu yako tu.

Freemason hufanya vikao viwili kwa mwaka, ila hufanya ibada mara kwa mara. Kwenye vikao hivyo ajenda kubwa ni kuzungumza ni kwa namna gani waendelee kuimarisha utawala wao ndani ya dunia hii. Wanasuka mipango mikubwa mno. Huwezi kuwashtukia hata kidogo.

Mtu leo ukimwambia niambie kuhusu Freemason, atakwambia majamaa wanamuabudu shetani. Oya! Hakuna chochote utakachosema zaidi ya hicho, wewe bado hujawajua hawa majamaa, unadhani Freemason ni wale unawaona kwenye mabango wakijitangaza wanatoa utajiri.

Freemason wanafanya maugunduzi makubwa duniani, lengo la kufanya maugunduzi hayo ni kuhakikisha dunia inaendelea, vitu vingi vya kupoteza muda vinapatikana, yaani wewe uwe bize na simu yako, games, laptop ili usahau kwenda kusali kanisani ama kuswali msikitini.

Ukisimama kanisani unachoka, ila kusimama kibandani kuangalia mpira huchoki. Unachoka kukaa msikitini kusikiliza mawahidha na kanisani kusikiliza mahubiri, ila huchoki kumsikiliza msanii fulani akiongea.

Mimi kwenye kitu ambacho siwezi kufanya maisha yangu yote ni kuinstall Bible kwenye simu yangu, hata iweje. Napenda sana kusoma Bible halisi mkononi nikiwa nimeishika na si kwenye simu yangu.

Kuna mambo najaribu sana kuyaepuka, najua siwezi kuepuka kila kitu ila najitahidi sana yale ninayoweza kuyaepuka basi niyaepuka.

Ukianza kusoma digrii ya kwanza ya Freemason, kwenye Biblia yao kuna mungu wao, pia kuna Yesu wao. Ukianza kusoma vitabu vyao, kuna mungu wao na kuna mtume Muhammad wao.

Oya! Hawa watu wamejipanga ila wana elimu kubwa mno. Yaani wanaijua dunia kwa undani kuliko mchungaji ama imamu wako. Na ndiyo maana ni rahisi sana kwao kukushawishi hata wewe kutumia vitu vyao kuliko nguvu ya mchungaji kukushawishi uende kanisani kila inapofika leo.

Kabla ya kuanza kupambana na hawa Freemason, kwanza wajue kwa undani. Huwezi kupambana na adui na wakati hujui anatumia silaha gani.

Aya watumishi wa Mungu mnaotumia mitandao ya Freemason, Facebook na WhatsApp njooni mseme neno.
 
Ni ukristo ndio unaweza kudhaminiwa na hicho chama cha siri

Na iko wazi tu kua ukristo ni dini ya LUCIFER

Lucifer yuko smart sana na anajua mambo mengi,na akiwalisha maneno huko na nyie ndio mnakuja huku Kwa mwamvuli wa elimu kubwa na kujifanya mnajua kila kitu na kujiona mna elimu kubwa/pana

Angalia kijana,muda unakutupa huo
 
Kitu cha kwanza kitakachokupa nguvu katika dunia hii ni elimu. Utake usitake elimu ina nguvu kuliko kitu chochote kwenye hii dunia. Kwa nini Mafreemason na Illuminat wanaitawala hii dunia? ...

Ukisoma kwa umakini utaona mleta uzi hajui chochote kuhusu freemason na hao illuminat bali kajazwa hofu na puuzi.

Eti wanatupangia tuabudu nini na tusali siku gani yet unasema tusali sana,tusali nini wakati umesema wao ndio walioshikilia taratibu za dini ulimwenguni

Mara wanamipango ya kuondoa vitabu vya dini kupitia matumizi ya apps,acha ujinga kama una fanya biashara ya kuuza biblia na kurwan hardcopies sema tu wadau waje kununua na sio kuleta illusions zako za kidini.

Kimsingi mleta mada dini zinapoteza mvuto kila siku kwa sababu dini ni nadharia tu hakuna uhalisia.

Acha kupotosha watu mana na wewe umepotoshwa.
 
Ukisoma kwa umakini utaona mleta uzi hajui chochote kuhusu freemason na hao illuminat bali kajazwa hofu na puuzi.

Eti wanatupangia tuabudu nini na tusali siku gani yet unasema tusali sana,tusali nini wakati umesema wao ndio walioshikilia taratibu...
Mkuu ishambulie hoja ya mleta hoja achana na mleta hoja.
 
Hawa jamaa wapo very brief ila maelezo tunayoyatoa huwa ni mengi mno mfano 33 Degrees in Mason deals with space travel with a speed 33 times that of light.
..............................
Ila akija mfafanuzi hapa lazima ukae
 
Hawa jamaa wapo very brief ila maelezo tunayoyatoa huwa ni mengi mno mfano 33 Degrees mason deals with space travel with a speed 33 times that of light.
..............................
Ila akina mfafanuzi hapa lazima ukae
Uchaw na technolojia
 
Ukweli ni kwamba tunaishi kwenye ulimwengu wa ndoto...kuna mengi hatuyafahamu na tunayodhani tunayafaham sivyo yalivyo ila ni janga tulilokutana nalo la kufichwa.
.................................
Infact wengi mpaka muda huu hatujifahamu sisi ni akina nani ukiachilia ambali majina tuliyopewa na wazazi wetu, kazi n.k...
 
Umesema Freemason ndo Wameleta Hizi Dini Alafu tena unakuja kusema Wanatengeneza Laptop, simu na Games ili watu wawe Bize Wasiende makanisani na Mskitini,

Sasa mtoa mada Heb nieleweshe maan ni kam umeung'ata mkia wako mwenyew maan sas kam wameunda Dini ili kupumbaza watu,

Inakuwaje tena waanze kutengeneza simu, laptops, na mitandao ya kijamii ili kuwafanya watu wasiende Ibadani ? Wakt dhumun lao ni kuunda Dini ili ziwapumbaze watu, We huon kwa mantik hiyo hapo ni wanajipinga wenyew ?

Au na wew umeicopy tu sehem umeileta humu hujaipitia, em muwe hat mnaedit vitu kabla hamjavileta hum.
 
Kitu cha kwanza kitakachokupa nguvu katika dunia hii ni elimu. Utake usitake elimu ina nguvu kuliko kitu chochote kwenye hii dunia. Kwa nini Mafreemason na Illuminat wanaitawala hii dunia? Ni kwa sababu wamesoma sana. Wanajua mambo mengi mno.

Ukikutana na Freemason mwenye digrii 33 na akaanza kukupa elimu ya dunia hii, utashangaa sana, itakufanya ugundue kumbe wewe ni mjinga unayetembea na kuvuta pumzi ya dunia hii.

Sasa dunia hii imejaza wajinga. Maarifa makubwa na mazito yamefichwa kwenye makaratasi. Waroma kitu walichokifanya cha kwanza ni kuondoa ujinga vichwani mwao, na wakafanikiwa.

Ukija kwa viongozi, wanasema hakuna kitu kizuri kama kumuongoza mjinga. Utasoma masomo ya dini, ila kama hujasoma masomo ya duniani, bado kuna ujinga mwingi sana upo kichwani.

Nigeria ni moja ya nchi ngumu sana kutawalika, kwa nini? Ni kwa sababu wamesoma, mtu mwenye elimu huwezi kumuongoza kimagumashi, ni ngumu kumuongoza mtu huyo kwa sababu kila wakati atakuwa anakuuliza maswali, je, utaweza kuyajibu maswali yake?

Unapojiunga na Freemason, kitu cha kwanza wanakupa elimu. Wanakuletea Biblia na uanze kuisoma kwanza, uisome yote, ukimaliza, wanakupa Korani napo uisome yote. Wanataka kwanza ujue kila kitu kuhusu hizi dini mbili halafu sasa nao wakupe elimu yao.

Unapokutana na Freemason na kuzungumza naye, unagundua kabisa huyu jamaa ni tofauti sana. Niliwahi kukutana na marehemu mzee Chande (Mkuu wa Freemason Tanzania) miaka ya nyuma, kwa namna alivyokuwa anaongea, nikasema kama Tanzania tungepata viongozi hata 10 wenye akili ya huyu mzee, aisee tungekuwa mbali sana.

Kitu cha kwanza unapandikizwa elimu. Wanajua kabisa kwamba dunia imejaza watu wengi wasiokuwa na elimu, na wanaziongoza serikali nyingi hasa Afrika kuhakikisha elimu inayopatikana inakuwa duni, ili watu wasije kufunguka na kujua mengi. Na wanashinikiza sana watu wajikite zaidi kwenye dini zao kwa kuwa wanaamini hazitokuja kukusaidia kwa chochote kile.

Mimi napenda sana kuzungumza na mtu mwenye elimu ya darasani lakini si elimu ya kanisa ama msikiti, kwa nini? Kwa sababu kila nitakachokwambia, utanitajia mstari, yaani utanipa andiko ambalo nikikuuliza ameandika nani, stori ilikuwaje, utanipa ileile ambayo Freemason walitaka uwe nayo miaka nenda rudi.

Huwa ninawaambia mara nyingi sana, hii dunia ipo chini ya Freemason, wao ndiyo wametupangia mambo mengi, wao ndiyo walituchagulia siku za kuabudu, wakatuchagulia na muda. Leo kuna makanisa mengi yanadhaminiwa na Freemason, kuna watoto wengi wa wachungaji na mashehe wanasoma katika shule za Freemason.

Ninapokwambia Freemason ninamaanisha dude moja kubwa sana. Siku omba Mungu upate kuwafahamu hawa watu vizuri. Wao wanaimiliki dunia, wao wanamiliki michezo, wanawekeza pesa nyingi sana. Wao wametengeneza pesa za Marekani, ukiangalia dola, wameweka alama zao za Kifreemason na Illuminat.

Leo kila mtu anatamani kwenda Marekani, ile nchi inaongozwa na Freemason. Kwa siku lazima uwatumie na kuwaabudu wao. Unakuja Facebook, unakwenda Youtube kuangalia miziki, ukitoka hapo unakwenda kuangalia muvi, hizo industries zote zipo chini yao. Wanamiliki mitandao yote ya kijamii.

Hivyo ukitaka kwanza kupingana na watu hawa, toka Facebook, toka WhatsApp, toka Instagram, usiangalie muvi na mambo mengine, halafu simama na sema mimi napingana na hawa jamaa. Huwezi kupingana nao huku ukiwa unatumia vitu vyao.

Leo ni sawa na kusema nipambane na serikali yangu tukufu halafu hapohapo natumia ardhi yao, natumia vitu vyao, itakuwa ni kujidanganya tu kwa kuwa wakisema hapana, basi nitakuwa nimekwisha.

Freemason ni dude kubwa, ila kuna dude kubwa zaidi ya Freemason, na hili linaitwa Illuminat. Tatizo huwa ni moja tu, watu hawataki kusoma na kuwajua watu hawa vizuri, wanaamini kuwajua Freemason kwa undani ni dhambi, ila si dhambi kutumia mitandao yao. Ni upuuzi.

Freemason wanamiliki benki ya dunia, wanamiliki benki ndogo ndogo, wao ndiyo wanauendesha uchumi huu na walifanikiwa zamani mpaka kukupangia siku zao za kwenda kuabudu. Wakakuletea tarehe zao, siku na kila kitu.

Mungu alimpa shetani nguvu ya kuutawala huu ulimwengu, yaani upo chini yake na ndiyo maana anaonekana kuwa na nguvu sana. Kumshinda shetani ni kumtumia Mungu, vinginevyo huwezi kushindana naye hata kidogo. Na ndiyo maana tunarudi palepale kwamba Freemason wanamjua Mungu wa kweli ni yupi, inawezekana si huyo unayemuabudu.

Wana siri kubwa mno! Wana elimu nzito sana ya uongozi. Wakati Michael Jackson amechoka kuendeshwa nao, alitoka hadharani na kusema SONY ni mashetani. Hii SONY ipo chini yao, na ni kampuni kubwa ya muziki na filamu, wao wanaendesha mambo mengi kwenye industry ya muziki na muvi. Wakati amekorofishana nao, hakuchukua muda mwingi akafariki dunia.

Unapoanza kufanya kazi nao na baadaye kuwasaliti, jambo la kwanza wanakumaliza. Huwa ipo hivyo. Hawawataki wasaliti, wanakupa kila kitu unachokitaka, mwisho wa siku wanakumaliza kama tu utakwenda kinyume nao.

Kitu cha kwanza nenda kasome. Hata vitabu vya dini vimeandika tupate elimu ya dunia kwanza. Tuijue dunia na mambo yake, tuwajue wamiliki wa hii dunia na tujifunze namna ya kupambana nao.

Lengo kubwa la Freemason ni kuteketeza kila kitu kinachohusiana na Mungu. Ukiangalia hata kwenye simu, wamekuweka Biblia, Korani, wameweka hivi kwa mikakati yao mikubwa. Unapokuwa na Biblia kwenye simu yako ama Kurani, automatic huwezi kununua vitabu hivyo.

Mpango wao mkubwa wanataka uwe bize kuvisoma kwenye simu yako, ukiacha kununua, wanaanza kuzipoteza mitaani, mwisho wa siku Biblia na Korani hazitopatikana mitaani, hutoweza kujua kwa sababu si unazo kwenye simu yako. Wakati zikiwa zimepotea duniani, halafu wanaziondoa kwenye simu yako. Nini kinafuata? Biblia na Korani zinaanza kuwa dili lakini kwa bahati mbaya hazotoweza kupatikana.

Kila kitu hawa jamaa wamekisuka. Wanakuendesha hii dunia kwenye mikakati yao mikubwa sana. Sasa mambo haya huwezi kuambiwa msikitini wala kanisani, wao watakwambia tu changia ujenzi wa msikiti ama kanisa. Haya mambo wachungaji na mashehe wanatakiwa kuwaambia watumishi wao kwamba ni lazima kununua Biblia ama Korani nyumbani lakini si kuwa nazo kwenye simu yako tu.

Freemason hufanya vikao viwili kwa mwaka, ila hufanya ibada mara kwa mara. Kwenye vikao hivyo ajenda kubwa ni kuzungumza ni kwa namna gani waendelee kuimarisha utawala wao ndani ya dunia hii. Wanasuka mipango mikubwa mno. Huwezi kuwashtukia hata kidogo.

Mtu leo ukimwambia niambie kuhusu Freemason, atakwambia majamaa wanamuabudu shetani. Oya! Hakuna chochote utakachosema zaidi ya hicho, wewe bado hujawajua hawa majamaa, unadhani Freemason ni wale unawaona kwenye mabango wakijitangaza wanatoa utajiri.

Freemason wanafanya maugunduzi makubwa duniani, lengo la kufanya maugunduzi hayo ni kuhakikisha dunia inaendelea, vitu vingi vya kupoteza muda vinapatikana, yaani wewe uwe bize na simu yako, games, laptop ili usahau kwenda kusali kanisani ama kuswali msikitini.

Ukisimama kanisani unachoka, ila kusimama kibandani kuangalia mpira huchoki. Unachoka kukaa msikitini kusikiliza mawahidha na kanisani kusikiliza mahubiri, ila huchoki kumsikiliza msanii fulani akiongea.

Mimi kwenye kitu ambacho siwezi kufanya maisha yangu yote ni kuinstall Bible kwenye simu yangu, hata iweje. Napenda sana kusoma Bible halisi mkononi nikiwa nimeishika na si kwenye simu yangu.

Kuna mambo najaribu sana kuyaepuka, najua siwezi kuepuka kila kitu ila najitahidi sana yale ninayoweza kuyaepuka basi niyaepuka.

Ukianza kusoma digrii ya kwanza ya Freemason, kwenye Biblia yao kuna mungu wao, pia kuna Yesu wao. Ukianza kusoma vitabu vyao, kuna mungu wao na kuna mtume Muhammad wao.

Oya! Hawa watu wamejipanga ila wana elimu kubwa mno. Yaani wanaijua dunia kwa undani kuliko mchungaji ama imamu wako. Na ndiyo maana ni rahisi sana kwao kukushawishi hata wewe kutumia vitu vyao kuliko nguvu ya mchungaji kukushawishi uende kanisani kila inapofika leo.

Kabla ya kuanza kupambana na hawa Freemason, kwanza wajue kwa undani. Huwezi kupambana na adui na wakati hujui anatumia silaha gani.

Aya watumishi wa Mungu mnaotumia mitandao ya Freemason, Facebook na WhatsApp njooni mseme neno.
Uongo
 
Kiukweli kuhusu freemasons bado huwajui wao ni kina nani. Uwe unajaribu kusoma vitabu vya mysticism vitakuongezea maarifa kuhusu hao jamaaa..
 
Ni ukristo ndio unaweza kudhaminiwa na hicho chama cha siri

Na iko wazi tu kua ukristo ni dini ya LUCIFER

Lucifer yuko smart sana na anajua mambo mengi,na akiwalisha maneno huko na nyie ndio mnakuja huku Kwa mwamvuli wa elimu kubwa na kujifanya mnajua kila kitu na kujiona mna elimu kubwa/pana

Angalia kijana,muda unakutupa huo
Kweli kabisa, LUCIFER yuko smart sana. Siyo kama yule mtume wa mchongo aliyeliwa na nguruwe.

Sent from my Infinix X688B using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom