Huu uzushi kuwa vidonda vya tumbo vinasababishwa na njaa ulitokea wapi?

ubarinolutu

JF-Expert Member
Oct 22, 2012
1,964
3,895
Kwanza Niseme kabisa Mimi sio Daktari, lakini nimeongea na madaktari. Lengo la Uzi huu ni kujaribu kuzungumzia juu ya ugonjwa wa vidonda vya tumbo ambao Kwa kizungu unaitwa ulcers, nimeamua hasa kujikita kwenye mada hiyo.

Kuna uzushi mkubwa Tanzania kuwa vidonda vya tumbo vinasababishwa na kukaa njaa, jambo ambalo kitaalamu sio kweli, ugonjwa wa vidonda vya tumbo unasababishwa na bakteria anaitwa H-pylori ambapo unaweza kumpata Kwa njia mbalimbali kama unavyopata taiphod, Sasa ni jinsi Gani hao h-pailori wanasababisha vidonda Mimi sijui.

Namalizia Kwa SENTENSI KUBWA KUWA UGONJWA WA VIDONDA VYA TUMBO HAUSABABISHWI NA KUKAA NJAA AU KUWA NA MSONGO WA MAWAZO ACHANE KUPOTOKA
 
Madaktari ni waongo sana. 😀😀

Vidonda vya tumbo vinasababishwa na:
. Kunywa maji machafu
. Vyakula vichafu
. Kwa njia ya denda(mate)
. Kushirikiana matumizi ya vijiko,

Nashauri hii nakala, iende kule jamii cheki.
 
1. Ni kweli bakteria aina ya H-pylori wanasababisha vidonda vya tumbo.

2. H-pylori sio sababu pekee ya kupata vidonda vya tumbo.

3. Hydrochloric acid ambayo inazalishwa tumboni inaweza kusababisha kuta za tumbo kuchumbuka, na vidonda vikaanza.

4. Kuta za tumbo zinazalisha ute (mucus) kwa ajili ya kujikinga na hydrochloric acid, kukiwa na tatizo lolote linalozuia au kupunguza kuzalishwa kwa ute michubuko inaweza kutokea.

5. Tumbo huzalisha enzyme pepsin kwa ajili ya kusaidia digestion, kwa bahati nzuri pepsin pia husaidia kupunguza makali ya hydrochloric acid, ikitokezea kuna imbalance kati ya pepsin/hydrochloric acid production utumbo unakua katika risk ya kuchubuka.

6. Histamine nayo inahusika katika kuzalisha acid tumboni, kukiwa na hypersensitivity ya histamine kwenye kuta za tumbo, acid huzalishwa kwa wingi, au kukiwa na overproduction ya histamine pia acid huzalishwa kwa wingi.

7. Ute huzalishwa kukinga kuta za utumbo -kama tulivyotangulia kusema hapo juu- kukiwa na ute mchache vidonda vinaweza kuanza, uzalishaji wa ute tumboni unaathiriwa na factors kadhaa kama vile viwango vya prostaglandins, secretagogues, bicarbonate ions, na mzunguruko wa damu katika kuta za utumbo. Kukiwa na tatizo katika factors hizi, ute hupungua, na kuta za utumbo zinaweza kuchubuka kwa urahisi.

8. Chakula kinapunguza ukali wa hydrochloric acid, kutokua na chakula tumboni kunaziacha kuta katika high risk ya kuwa contact na hydrochloric acid na kuweza kuathirika na kuanza vidonda.

Kwa ufupi stress, kukaa na njaa muda mrefu, baadhi ya cancer za tumbo, baadhi ya vyakula kama jamii ya kunde, alcoholism, H-pylori infection, na mambo mengine yanaweza kusababisha vidonda vya tumbo.
 
8. Chakula kinapunguza ukali wa hydrochloric acid, kutokua na chakula tumboni kunaziacha kuta katika high risk ya kuwa intact na hydrochloric acid na kuweza kuathirika na kuanza vidonda.

Kwa ufupi stress, kukaa na njaa muda mrefu, baadhi ya cancer za tumbo, baadhi ya vyakula kama jamii ya kunde, alcoholism, H-pylori infection, na mambo mengine yanaweza kusababisha vidonda vya tumbo.
Mtoa mada ishi na hii hapa.

Asilimia takribani 80 ya ulcers anayesababisha ni H pylori, the rest 20 ndo other causatives!

Ukibaki na tumbo wazi HCl may damage inner linning of the stomach au utumbo na kusababisha ulcers too!
 
Kwanza Niseme kabisa Mimi sio Daktari, lakini nimeongea na madaktari. Lengo la Uzi huu ni kujaribu kuzungumzia juu ya ugonjwa wa vidonda vya tumbo ambao Kwa kizungu unaitwa ulcers, nimeamua hasa kujikita kwenye mada hiyo.

Kuna uzushi mkubwa Tanzania kuwa vidonda vya tumbo vinasababishwa na kukaa njaa, jambo ambalo kitaalamu sio kweli, ugonjwa wa vidonda vya tumbo unasababishwa na bakteria anaitwa H-pylori ambapo unaweza kumpata Kwa njia mbalimbali kama unavyopata taiphod, Sasa ni jinsi Gani hao h-pailori wanasababisha vidonda Mimi sijui.

Namalizia Kwa SENTENSI KUBWA KUWA UGONJWA WA VIDONDA VYA TUMBO HAUSABABISHWI NA KUKAA NJAA AU KUWA NA MSONGO WA MAWAZO ACHANE KUPOTOKA

Aliyekueleza, ameeleza kama moja ya sababu hapo juu.

Visababishi husika vyaweza kuwa:
1: H. pylori bacteria: kwa kuzalisha kimeng'enya kinacholainisha ukuta wa tumbo.

2: Stress mfano: kuungua eneo kubwa la mwili, ajali yenye madhira makubwa, operation kubwa, shock nk. Husababisha mzunguko wa damu kutokuwa wa kutosha kwenye tumbo na hivyo kusababisha michubuko kirahisi kutokana na ngozi ya tumbo kukosa chakula na oksijeni.

3: Genetic: mfano: kuna watu wamezaliwa wanazalisha hydrochloric asidi kwa wingi.

4: Uvutaji sigara: kwa nikotini kupunguza uzaliahaji wa prostaglandins na kusababisja michubuko kirahisi.

5: Grupu O, kutokana na high binding capacity ya H. Pylori kwa grupu husika.

6: Kutokupata chakula kwa muda mrefu. Kutokuwepo kwa chakula hufanya acidi
kutembea kwenye ukuta wa njia ya chakula moja kwa moja. Baada ya muda mrefu asidi huleta madhara ya kuiharibu ngozi husika au seli za ukuta wa chakula.

7: Matumizi ya dawa za kutuliza.maumivu kwa muda mrefu.
 
Najifunza mengi sana hapa, hii nchi Ina wataalamu sana, SEMA tu CCM ndo inafeli, asanteni wanajamvini
 
Aliyekueleza, ameeleza kama moja ya sababu hapo juu.

Visababishi husika vyaweza kuwa:
1: H. pylori bacteria: kwa kuzalisha kimeng'enya kinacholainisha ukuta wa tumbo.

2: Stress mfano: kuungua eneo kubwa la mwili, ajali yenye madhira makubwa, operation kubwa, shock nk. Husababisha mzunguko wa damu kutokuwa wa kutosha kwenye tumbo na hivyo kusababisha michubuko kirahisi kutokana na ngozi ya tumbo kukosa chakula na oksijeni.

3: Genetic: mfano: kuna watu wamezaliwa wanazalisha hydrochloric asidi kwa wingi.

4: Uvutaji sigara: kwa nikotini kupunguza uzaliahaji wa prostaglandins na kusababisja michubuko kirahisi.

5: Grupu O, kutokana na high binding capacity ya H. Pylori kwa grupu husika.

6: Kutokupata chakula kwa muda mrefu. Kutokuwepo kwa chakula hufanya acidi
kutembea kwenye ukuta wa njia ya chakula moja kwa moja. Baada ya muda mrefu asidi huleta madhara ya kuiharibu ngozi husika au seli za ukuta wa chakula.

7: Matumizi ya dawa za kutuliza.maumivu kwa muda mrefu.
Umeeleza kitaalamu sana na kwa lugha rahisi inayoeleweka. Binafsi natamani kufahamu kwa lugha rahisi kama hii mambo matatu:-

1. Vyakula vinavyomfaa mtu ambaye tayari ameshagundulika na tatizo hili

2. Kwanini ni vigumu sana tatizo hili kupona kirahisi hasa kwa dawa za hospitali? Je, ni kweli halitibiki au waathirika ndio wavivu kuzingatia matumizi sahihi ya dawa?

3. Je, kwa mtu aliyeathirika na H.Parori kwenye njia ya chakula (anayepata maumivu kifuani na kwenye koo) na mtu aliyaathirika tumboni (maumimvu yake yapo tumboni) wote wanatakiwa kuepuka aina sawa ya vyakula?
 
A: Vyakula visivyomfaa mtu mwenye tatizo hili ni vile vinavyoleta muwashawasha kwenye njia ua chakula kama:
1: Vyenye asili ya pilipili

2: Tangawizi

3: Uchachu: kama ndimu, limao, matunda yasiyoiva vizuri

4: Acid: Juisi za madukani, kajawa, majani ya chaink.

5: Vyenye gesi kwa wingi kama soda nk.

6: Vyakula vyenye misuli migumu kama nyama ya kukausha

7: NK.

B: Suala la uponaji linahusisha mambi mengi:

1: Kiasi cha tatizo gastritis/kututumka vs ulcer/kidonda.

2: Kutambua chanzo ili kuzuia

3: Kuzingatia masharti

4: Kutambua tatizo la msingi kama ndilo linalotibiwa. Kuna matatizo mengine yenye dalili sawa na hayo hapo juu na hutibiwa kama gastritis/Ulcer.

5: Tumbo kuhitaji muda wa kutengeneza utando ulioathiriwa. Hivyo kuhitaji muda wakati huo nguvu ya kuharibu nayo ikipita palepale.

6: Tumbo lenyewe kuendelea kutoa vimeng'enyo vyenye asili ya asidi ambavyo huendelea kuathiri tumbo.

7: Tumbo kutoa vimeng'enyo ambavyo husaidi kujeruhi asili ya nyama.

8: Nk.

C: Uepukaji unakuwa ni wa aina ileile kwa kiasi kikubwa, ila unaweza kupunguza au kuongeza kulingana na asili ya tatizo na sehemu tatizo lilipo.
 
A: Vyakula vinavyomfaa mtu mwenye tatizo hili ni vile vinavyoleta muwashawasha kwenye njia ua chakula kama:
1: Vyenye asili ya pilipili

2: Tangawizi

3: Uchachu: kama ndimu, limao, matunda yasiyoiva vizuri

4: Acid: Juisi za madukani

5: Vyenye gesi kwa wingi kama soda nk.

6: Vyakula vyenye misuli migumu kama nyama ya kukausha

7: NK.

B: Suala la uponaji linahusisha mambi mengi:

1: Kiasi cha tatizo gastritis/kututumka vs ulcer/kidonda.

2: Kutambua chanzo ili kuzuia

3: Kuzingatia masharti

4: Kutambua tatizo la msingi kama ndilo linalotibiwa. Kuna matatizo mengine yenye dalili sawa na hayo hapo juu na hutibiwa kama gastritis/Ulcer.

5: Tumbo kuhitaji muda wa kutengeneza utando ulioathiriwa. Hivyo kuhitaji muda wakati huo nguvu ya kuharibu nayo ikipita palepale.

6: Tumbo lenyewe kuendelea kutoa vimeng'enyo vyenye asili ya asidi ambavyo huendelea kuathiri tumbo.

7: Tumbo kutoa vimeng'enyo ambavyo husaidi kujeruhi asili ya nyama.

8: Nk.

C: Uepukaji unakuwa ni wa aina ileile kwa kiasi kikubwa, ila unaweza kupunguza au kuongeza kulingana na asili ya tatizo na sehemu tatizo lilipo.
Hapo kwenye "A" unamaanisha vyakula vinavyofaa au visivyofaa?
 
1. Ni kweli bakteria aina ya H-pylori wanasababisha vidonda vya tumbo.

2. H-pylori sio sababu pekee ya kupata vidonda vya tumbo.

3. Hydrochloric acid ambayo inazalishwa tumboni inaweza kusababisha kuta za tumbo kuchumbuka, na vidonda vikaanza.

4. Kuta za tumbo zinazalisha ute (mucus) kwa ajili ya kujikinga na hydrochloric acid, kukiwa na tatizo lolote linalozuia au kupunguza kuzalishwa kwa ute michubuko inaweza kutokea.

5. Tumbo huzalisha enzyme pepsin kwa ajili ya kusaidia digestion, kwa bahati nzuri pepsin pia husaidia kupunguza makali ya hydrochloric acid, ikitokezea kuna imbalance kati ya pepsin/hydrochloric acid production utumbo unakua katika risk ya kuchubuka.

6. Histamine nayo inahusika katika kuzalisha acid tumboni, kukiwa na hypersensitivity ya histamine kwenye kuta za tumbo, acid huzalishwa kwa wingi, au kukiwa na overproduction ya histamine pia acid huzalishwa kwa wingi.

7. Ute huzalishwa kukinga kuta za utumbo -kama tulivyotangulia kusema hapo juu- kukiwa na ute mchache vidonda vinaweza kuanza, uzalishaji wa ute tumboni unaathiriwa na factors kadhaa kama vile viwango vya prostaglandins, secretagogues, bicarbonate ions, na mzunguruko wa damu katika kuta za utumbo. Kukiwa na tatizo katika factors hizi, ute hupungua, na kuta za utumbo zinaweza kuchubuka kwa urahisi.

8. Chakula kinapunguza ukali wa hydrochloric acid, kutokua na chakula tumboni kunaziacha kuta katika high risk ya kuwa contact na hydrochloric acid na kuweza kuathirika na kuanza vidonda.

Kwa ufupi stress, kukaa na njaa muda mrefu, baadhi ya cancer za tumbo, baadhi ya vyakula kama jamii ya kunde, alcoholism, H-pylori infection, na mambo mengine yanaweza kusababisha vidonda vya tumbo.
Nilitaka kueleza hii kitu, kama mtoa mada asipoelewa hapa bc ameamua kutokuelewa.

Hii kitu iliwahi kunitokea ndani ya siku moja.
Zamani nilikuwa nikisafiri safari ndefu hua natapika hvy nilikuwa sili chcht ili kujizuia kutapika.
Nilipata safari kutoka Arusha kwenda Mbeya na sikula chcht na hali ya kutapika ilinikuta na nilitapika mate yaliyojaa damu, damu hy ndo ilisababishwa na acid inayozalishwa tumboni ili kusaidia digestion mana ilikutana tumbo likiwa halina kitu chcht.
kwahy ukiwa kwenya hali ya mazoea ya kukaa muda mrefu bila kula hapo ndipo tatizo linajijenga na kuwa sugu na kusababisha kuwa na vidonda vya tumbo.
 
2: Stress mfano: kuungua eneo kubwa la mwili, ajali yenye madhira makubwa, operation kubwa, shock nk. Husababisha mzunguko wa damu kutokuwa wa kutosha kwenye tumbo na hivyo kusababisha michubuko kirahisi kutokana na ngozi ya tumbo kukosa chakula na oksijeni.
Sijakuelewa hapa mana umezungumzia mambo mengi kwa pamoja halafu haviendani.
Kila kitu hapo hakuna ht kimoja kinachosababisha vidonda vya tumbo, em fikiria mtu ameungua mgongo mzima hy inasababisha Vp damu kutokufika tumboni.?
Au tangu lini msongo wa mawazo ikasababisha vidonda vya tumbo.?
Operesheni kubwa ipi hy inazuia damu kufika tumboni.?
 
Back
Top Bottom