Huu utaratibu wa kuwakatia viuno wageni kwenye viwanja vya ndege nani aliuanzisha?

TUKANA UONE

JF-Expert Member
Jan 3, 2018
1,816
5,151
Ukihitaji salamu njoo unikatie mauno kwanza kama Yondo, tofauti na hapo utaambulia chuya!

Huu utaratibu ulianza kama mzaha lakini kadiri siku zinavyozidi ndivyo hali inakuwa mbaya,kitu kibaya zaidi hadi wanaume watu wazima utawakuta nao wamejifunga kibwebwe wanakata mauno bila aibu wala soni!.

Viongozi wetu wakienda nchi za watu walioendelea huwezi kuona huu uwendawazimu wa kina mama na kina baba wa huko kukata mauno kama wendawazimu!.

Zamani viongozi walipokuwa wakija hapa nchini kulikuwa na vikundi vya ngoma za asili vilivyocheza kwa staha,madoido na mbwembwe bila kukata mauno ovyo!, Sijajua siku hizi hivi vikundi vimepatwa na nini maana siyo kwa miuno hiyo inayokatwa!.

Kuna mtu nilikuwa najadiliana nae akaniambia kwamba huo ndiyo utamaduni wetu na wageni wanapokuja wanapaswa wakatiwe viuno ili wafurahie utamaduni wa mtanzania!.

Kama ndivyo aisee hii ni hatari sana!.

Nimeshangaa sana kuona mijibaba yenye ndevu ikiwa inakata mauno mbele ya Rais wa Germany!,Rais kazi yake ilikuwa ni kupiga makofi tu na kushangaa!, bila shaka nadhani akirudi Germany ataenda kuwasimulia wenzie, hivyo tutegemee ugeni mzito kutoka Germany kuja kushangaa wakata miuno pale JKNIA!
 
Brass band za vikosi vya majeshi, tena brass band ya jeshi moja inatosha. Hizi ngoma zetu mgeni atazikuta mikoani kama atatembelea huko. Mbona rais wetu akienda nje hatuoni ngoma ngoma tunaona kigwaride cha brass band tu? Tuwe standard kimataifa
 
Walianzisha wazungu wenyewe hasa waingereza wakati wa ukoloni kwamba mwafrika kazi yake kupiga ngoma ku entertain mzungu wanafanya wote hata kenya, uganda au ghana, kenya hata huita wamasai na kuanza kuruka juu ku entertain mzungu.

Bottom line kila kitu ambacho serikali inafanya imekirithi ktk kwa mzungu wakati wa ukoloni usisahau kwamba serikali ni mkoloni kasoro rangi ndo maana jeshi wanapiga watu weusi kama wakati wa ukoloni, jeshi la tanzagiza haliwezi gusa muhindi au mwarabu kwa maana wamekuwa trained kuwalinda wahindi na waarabu na ku adhibu mweusi, kwa serikali ya tanzagiza mtu mweusi ni adui na mwovu wamerithi hiyo system …
 
walianzisha wazungu wenyewe hasa waingereza wakati wa ukoloni kwamba mwafrika kazi yake kupiga ngoma ku entertain mzungu wanafanya wote hata kenya, uganda au ghana, kenya hata huita wamasai na kuanza kuruka juu ku entertain mzungu.

Bottom line kila kitu ambacho serikali inafanya imekirithi ktk kwa mzungu wakati wa ukoloni usisahau kwamba serikali ni mkoloni kasoro rangi ndo maana jeshi wanapiga watu weusi kama wakati wa ukoloni, jeshi la tanzagiza haliwezi gusa muhindi au mwarabu kwa maana wamekuwa trained kuwalinda wahindi na waarabu na ku adhibu mweusi, kwa serikali ya tanzagiza mtu mweusi ni adui na mwovu wamerithi hiyo system …
COLONIAL LEGACY
 
Nchi inqpoongozwa na vilaza, wezi, waongo,watu wenye IQ ndogo, matokeo yake ndio haya,
CCM wanatafuta katibu mwenezi wa chama, chama chenye wanachama milioni 8!, Ila wakaona mwenye uwezo ni Makonda, jitu lenye kashfa za uharifu, ipo siku utasikia Rostam ndio Waziri mkuu!
 
Ukihitaji salamu njoo unikatie mauno kwanza, tofauti na hapo utaambulia chuya!

Huu utaratibu ulianza kama mzaha lakini kadiri siku zinavyozidi ndivyo hali inakuwa mbaya,kitu kibaya zaidi hadi wanaume watu wazima utawakuta nao wamejifunga kibwebwe wanakata mauno bila aibu wala soni!.

Viongozi wetu wakienda nchi za watu walioendelea huwezi kuona huu uwendawazimu wa kina mama na kina baba wa huko kukata mauno kama wendawazimu!.

Zamani viongozi walipokuwa wakija hapa nchini kulikuwa na vikundi vya ngoma za asili vilivyocheza kwa staha,madoido na mbwembwe bila kukata mauno ovyo!, Sijajua siku hizi hivi vikundi vimepatwa na nini maana siyo kwa miuno hiyo inayokatwa!.

Kuna mtu nilikuwa najadiliana nae akaniambia kwamba huo ndiyo utamaduni wetu na wageni wanapokuja wanapaswa wakatiwe viuno ili wafurahie utamaduni wa mtanzania!.

Kama ndivyo aisee hii ni hatari sana!.

Nimeshangaa sana kuona mijibaba yenye ndevu ikiwa inakata mauno mbele ya Rais wa Germany!,Rais kazi yake ilikuwa ni kupiga makofi tu na kushangaa!, bila shaka nadhani akirudi Germany ataenda kuwasimulia wenzie, hivyo tutegemee ugeni mzito kutoka Germany kuja kushangaa wakata miuno pale JKNIA!

Sijui nani alikuja na hili wazi la mauno.
 
Back
Top Bottom