mbingunikwetu
JF-Expert Member
- Feb 17, 2015
- 13,664
- 18,038
Ukiweka sharti la kujitolea ili mtu apewe ajira maana yake ni kwamba kila mwajiriwa mtarajiwa atataka kujitolea! SWALI: Je waajiriwa wote wanaweza kupata fursa ya kujitolea? Jibu la dhati ni HAPANA. Sasa hivi kuna vijana takriban 600,000 wanasaka ajira. Je tuna uwezo wa kuwapa wote hawa fursa ya kujitolea? Jibu ni hapana. SWALI: Kwa nini umbague mtu kwenye ajira wakati hukuwa na uwezo wa kumpa fursa ya kujitolea? Yawezekana huyu ambaye hakupata fursa ya kujitolea ndio ana uwezo zaidi.
Haya mambo ya kujitolea yatafungua mlango wa upendeleo na rushwa!! Kiongozi wa taasisi fulani atakuwa na uwezo wa kuwapa ndugu zake fursa ya kujitolea na hivyo kuwaandalia mazingira ya kuajiriwa!! Huu utaratibu wa sasa umewabana sana wakubwa, hata kama kuna wanaopenyeza lakini si kama zamani!
Anayejitolea mwache ajitolee lakini atapambanishwa kwenye usaili na wale ambao nao wangependa kujitolea lakini hawakupata fursa hiyo. Uwanja wa kupambania ajira tunaomba ubaki sawa kwa wote. Msiturudishe kwenye "testimonial" ambazo nyingi ni za mchongo!! Unategemea kijana anayetoka kijijini apate fursa ya kufanya kazi BOT kama yataingizwa mambo ya kujitolea? Nani atakayempa mtu nafasi ya kujitolea BOT?
Mameneja wa BOT wataleta watu wao, Wahasibu wa BOT wataleta watu wao, na vimemo vya wakubwa vitapigana kikumbo kupenyeza watu wao, na wote hawa watataka waajiriwe kwa kuwa waqmejitolea hata kama uwezo wao ni mdogo!! HAPANA!! Wakubwa wanapigania mlango wa nyuma wa kupenyezea watu wao!! Si vizuri kuweka kigezo ambacho kuna watu watalazimika kukikosa kwa sababu mazingira yao hayawaruhusu!!
Kuna mwingine japo hana ajira rasmi lakini ana mzigo wa kulea familia! Hufanya vibarua ili wadogo zake wasome!! Sasa huyu ukimtaka ajitolee hataweza. Ila watoto wa matajiri wana uwezo wa kujitolea maana wataendelea kuhudumiwa bila shida. Lakini mtoto wa mlala hoi kwa vyovyote vile hawezi kumudu kujitolea maana kila siku analazimika kutafuta riziki ya kutwa!!