Hismastersvoice
JF-Expert Member
- Jan 26, 2013
- 18,673
- 22,264
Kwanza serikali haina mkoa kwanza siasa baadae, pili uonvozi huu umejikita kuijenga nchi peke yake na chama chake na kitendo chako cha kuwalegeza wanambeya hakikubaliki kwani wapinzani bado wanazuiwa kufanya siasa huku yule mama anaruhusiwa kufanya kazi za ubunge wa Mbeya wakati yeye si mbunge wa Mbeya.Imemchukua Rais Magufuli miaka zaidi ya Mitatu na nusu Kukubali kukanyaga Mbeya.Kumbukumbu ya mwaka 2015 ni ngumu yeye kumtoka.
Nawafaham watani zangu hawa Wanyakyusa. Ni wajeuri,wajivuni na wenye maamuzi ya Umoja sana.Ni watu wasioyumba na wasio wanafiki.
Kikwete anawakumbuka vizuri alipotaka wapelekea uswahili likatokea jambo baya sana ktik historia yetu la kupiga mawe msafara wa Rais.na ni hawa waliomwambia Urais tutakupa mwaka 2005/ 2010 ila Mbunge wako ondoka naye.na kweli hawakumpa.
Siasa za mbeya huwa zinahitaji utulivu wake sababu kubwa ni kuwa kuna aina ya watu wanaojiamini na wanaojivuna sana.hawa wamekuwa wakimchagua sugu kama adhabu kwa ccm.nakumbuka 2015 magufuli mwenyewe alisalimu amri.ikabidi atumie akili ya ziada kuwatuliza.
Walishachoka na CCM na maovu waliyohisi,ona wanatendewa.madhara yake wameyaona...jinsi ambavyo walitengwa kwa kipindi kirefu sana.na kudumaza shughuli za kiserikali za maendeleo kwa jiji.
Sasa warud nyuma.huwezi shindana na serikali.wamwombe msamaha raisi aondoke kinyongo afanye nao kazi.jiji liendelee kwa miradi lukuki ya maendeleo.
Wakiendelea kushupaza shingo zitavunjika.mpaka mwaka 2025 watakuwa na wakati mgumu. Kuanza upya si ujinga.waache kwa muda siasa za upinzani.wafanye wanayopaswa kufanya. Maana hata wanaweza wasipate waziri kwenye Serikali ikiwa wataendelea hivi.au ndo watapewa mawaziri wizara kama za mwakyembe.
Wanyakyusa,wasafwa,wandali,wakinga n.k Mkoa Kwanza Siasa baadaye.
Umesahau moja au tulikuwa bado enzi hizo Waziri mkuu Kawawa alipopolewa mawe huko Kyela.