ABEL MAGEMBE LUGIMBA
Member
- May 22, 2016
- 63
- 59
Haya ni maoni yangu binafsi kuhusu mpango mpya wa serikali wa kukabiliana na tatizo la uhaba wa walimu wa sayansi uliotangazwa na Suleiman Jaffo Naibu Waziri wa TAMISEMI.
Kwanza ninaomba watu waelewe ya kwamba Ualimu ni taaluma kama zilivyo taaluma zingine, hivyo basi ninawaomba sana wanasiasa kuheshimu taaluma hii. Kitendo cha serikali kutangaza kuchukua wahitimu wa shahada ya sayansi ambao hawana taaluma ya ualimu nakuwapa shortcourses kuhusu ualimu kwa lengo la kuwaajiri kuwa walimu wa masomo ya sayansi, kwa mtizamo wangu naona hii ni dharau kubwa ya wanasiasa katika kada ya ualimu.
Hatuwezi kuboresha elimu yetu kwa kuajiri watu ambao sio qualified teachers.Kama tunataka kuboresha elimu yetu ni lazima serikali iwekeze ziada katika elimu yetu nasio vinginevyo. Kitu kinachonishangaza ni kuona Walimu wa sayansi wapo mitaani tu, wengine wamehitimu mwaka jana na wengine mwaka huu lakini serikali haitaki kuwapatia ajira,
Halafu bungeni Mheshimiwa Naibu Waziri wa ofisi ya rais TAMISEMI Suleiman Jaffo anatoa tamko kwamba serikali imeandaa mpango wa kuwaajiri wahitimu wa shahada ya sayansi ambao hawajasomea taaluma ya ualimu kufundisha masomo ya sayansi,najiuliza ni kwanini hii inafanyika katika kada ya ualimu tu mbona hata katika sekta ya afya kunaupungufu wa wahudumu wa afya kwani nini serikali isiseme na huko iwachukue wahitimu wa shahada ya sayansi nakuwapatia shortcourses ili wakawe wahudumu wa afya katika zahanati, vituo vya afya na hospitali?.
Binafsi nilipoisikia kauli hii ya serikali kuhusu jambo hili la kutatua uhaba wa walimu wa sayansi nimeshindwa kupata picha au mwelekeo wa serikali yetu kuhusu suala la elimu kwani majuzijuzi tena waziri wa elimu Prof Joyce Ndalichako alitoa tamko lingine na kudai kwa kuanzia sasa masomo ya sayansi kwa sekondari ni ya lazima
Wakati anatoa tamko hilo anajua kabsa kunashule za sekondari zingine hazina kabsa maabara za masomo ya sayansi, lakini pia walimu wa masomo ya sayansi hawatoshi kabsa.Unapomlazimisha mwanafunzi kusoma masomo ya sayansi wakati walimu hawapo wakumfundisha, maabara na nyenzo za kufundishia sayansi hazipo hapo ni kumuonea tu mwanafunzi huyo.
Kama serikali inataka kupunguza au kuondoa kabsa tatizo la uhaba wa walimu wa masomo ya sayansi na hisabati.Inatakiwa kufanya mambo yafuatayo kwa sasa.
1.Kuboresha maslahi ya walimu wa sayansi waliopo, kwani haingii akilini mwalimu wa Sayansi ambaye anaingia darasani kufundisha halafu huyohuyo ndiye anaingia maabara kuandaa practical na kufundisha pia, halafu maslahi yake yakawa sawa na mwalimu wa sanaa.Kiuharisia kama mshahara wa daktari na muuguzi ni tofauti kwa maana daktari anapokea mshahara mkubwa ukilinganisha na nurse.
Kwanini Mwalimu wa Sayansi mshahara wake ulingane sawa na mwalimu wa art wakati Walimu wa Sayansi wamekuwa wanafanya kazi mara mbili ya kufundisha halafu kama lab technician katika mashule ya sekondari lakini pamoja na yote mishahara wanapewa sawa na walimu wa arts.
Walimu wa sayansi wanafanya kazi nzito sana huwezi kulinganisha na walimu wa arts. Kama kweli serikali inadhamira ya kutatua tatizo la walimu wa masomo ya sayansi hainabudi kuongeza mishahara pamoja na kuwapatia posho maalum walimu wa masomo ya sayansi.
Serikali itakapoboresha maslahi ya walimu wa sayansi zaidi automatically hii field itakuwa ni kimbilio la watu wengi sana lakini walimu watafundisha kwa kujituma zaidi nakupelekea ufaulu wa wanafunzi kuwa mkubwa.Endapo serikali ikitekeleza jambo hili, Haitahitajika serikali kuanza kufikiria kuajiri walimu wa sayansi magumashi/mwendokasi ili kumaliza tatizo la upungufu wa walimu wa sayansi.
2.Serikali itoe ajira kwa walimu wote wa Sayansi waliohitimu mwaka jana na mwaka huu.Serikali itoe ajira kwa wakati kwani ucheleweshaji wa makusudi wa ajira za ualimu hususan wa masomo ya sayansi ni hasara kubwa kwa wanafunzi ambao wengi wao ni watoto wa maskini.Shule za serikali ndio zinazokabiliwa na upungufu huu na waathirika wakubwa katika jambo hili ni watoto wa maskini . Viongozi wakubwa wengi wao watoto wao wanasoma katika shule za binafsi ambazo kimsingi hakuna uhaba wa walimu ndio maana jambo wamekuwa wakiliona kama sio kipaumbele cha serikali.
Kitendo cha serikali kuzuia ajira kwa walimu wa sayansi waliohitimu vyuoni na kutangaza mpango wa kuajiri watu ambao kimsingi hawajasomea ualimu lakini kwa sababu wamesomea shahada ya sayansi tu tafsiri yake ni kama serikali imekusudia kuua ubora wa elimu ya watoto wetu.
Huu mpango wa serikali ukifikiria juujuu unaweza ukaona kama ni mwarobaini wa tatizo la walimu wa masomo ya sayansi lakini ndivyo sivyo kabsa.Naishauri serikali huu mpango iweke pembeni kwanza ifanye research upya kuhusu Negative impacts za mpango huu kabla ya kufanya implementation.
Wako,
Abel Magembe Lugimba.
Kada wa CCM, Kalambo-Rukwa.