Huu ndiyo wakati wa majibu uliyokuwa unajiuliza ukiwa mtoto

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,405
52,046
Anaandika, Robert Heriel

Maisha ni mchezo wa maswali na majibu.
Kikawaida swali ndio linatangulia ndipo jibu lifuate. Lakini kwenye maisha majibu huweza kutangulia alafu maswali ndio yafuate. Hayo ni maisha. Yapo majibu yasiyo na maswali. Lakini hakuna swali lisilo na jibu.

Vijana bado hawaamini kwamba haya ndio maisha waliyokuwa wanayachukulia walivyokuwa watoto wadogo au kuna maisha mengine.
Hawaamini haya ndio Yale maisha ambayo walikuwa wakisema; Nikiwa Mkubwa au subiri niwe Mkubwa" au kuna maisha mengine.

Vijana maisha ndio hayahaya, yalikuwepo kabla haujakuwepo na yataendelea kuwa hivihivi siku ukiondoka.
Maisha hayajawahi kuwa rahisi wala hajawahi kuwa magumu.

Akili yako ndio inaweza kuya-categorize vile uonavyo.

Huu ndio wakati wa maswali yote uliyokuwa unajiuliza ukiwa mdogo kujibiwa;

i. Kwanini baba na mama hawalali chumba kimoja? (Kwa baadhi ya Familia)
ii. Kwanini maba alikuwa Mkali?
iii. Kwanini mama anapenda kumtuhumu baba na kumpaka matope ya ubaya? (Hili Vijana wa kiume wakishaoa ndio wataelewa kuwa 90% Mama Hakuwa sahihi)

iv. Kwa nini Baba au Mama alikuwa anavaa nguo moja kama sanda?

v. Kwa nini kila siku tulikuwa tunakula chakula kilekile, chakula kizuri mpaka sikukuu?

Vi. Kwa nini Baba Hakuwa mtu wa Kanisani?๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚ Wakati mama angalau alikuwa anaendaenda.
Yote hayo kijana majibu yake Kwa sasa ushayapata.

Vii. Kwa nini wazazi hawakuweza kujenga makazi mazuri na hawakuwa na mali nyingi?
Jibu la swali hili kama bado hujalipata vita subra, mpaka miaka 40+ utakutana na majibu.

VIII. Kwa nini ulikatazwa kula Kwa watu?
ix. Kwa nini Mama alikuwa anagomba mkitupa chakula, na lazima mle kiporo?
X. Kwa nini Baba yako hajafanikiwa/amefanikiwa kuliko ndugu zake?
xi. Kwa nini kulikuwa na anko au babu yenu aliyekuwa anapenda kuja muda wa kula? Lakini hakuwahi kufukuzwa licha ya kuwa baadhi ya wanafamilia yenu kuwa wanamsengenya.
Naamini sasa umejua ni kwa nini?

Kuna Ile fikra mtoto huwa nayo, Imani kuwa akiwa mkubwa atakuwa na maisha mazuri. Imani ndio kitu pekee ambacho kinaweza kufanya Jambo kubwa kuonekana ni dogo.
Fikra na Imani hizo zilipelekea watoto wengi kuwalaumu kimoyomoyo wazazi wao kuwa hawawajibiki Kwa kuwapa vitu vizuri,
Hawajajenga nyumba nzuri wakati wewe Kwa muda ule uliona kujenga nyumba nzuri ni Jambo dogo.
Sasa umekua nadhani umepata majibu ya maswali yako.

i. Ulikuwa unachukia kusikia malalamiko ya Mama yako kuwa Baba yako anavimada au ikiwezekana ananyumba ndogo.
Sasa umejua sababu ya mwanaume kuwa na Nyumba ndogo bila Shaka. Na Kama hujajua basi bado hujakua, endelea kuishi majibu utayapata mbeleni huko.

ii. Kwa nini Baba yako alikuwa akimdhibiti na kumuwekea vikwazo vingi Mama yako?
Labda ulikuwa unachukia na kumuona Mzee wako ni Mtesaji. Ulikuwa ukitamani kumuona Mama yako akiwa huru na kufurahia Uhuru wake. Lakini Baba yako ni kana kwamba alikuwa akiuingilia mara Kwa mara. Najua sasa ushapata majibu ni Kwa nini ilikuwa vile.

iii. Kwa nini Baba yako alikuwa hakusifii hata kama umefanya vizuri wakati Mama alikuwa anakusifia hata Kwa Jambo dogo lisilo na maana? Baba Labda Kwa nadra sana.
Sasa umejua majibu yake.
Dunia hii haihitaji kusifiwa ukiwa mchezo, mtu husifiwa mwishoni akimaliza mbio.

iv. Kwa nini Mama yako au Mama mdogo/mkubwa alikuwa hampendi mtoto wa nje wa baba yako/baba mkubwa/mdogo.?
Sasa umejua.
Kama hujui subiri Ukue kidogo utaelewa.

v. Kwa nini Baba alitelekeza Familia?
Hilo jibu lake Kama hujalipata basi endelea Kula mtori nyama zipo chini Kabisa.

Huu ndio wakati wa majibu kwa maswali tuliyokuwa tunajiuliza tungali watoto

Hata hivyo majibu mengine huzaa maswali. Na maswali mengine ndio majibu yenyewe.

Ni Yule Mtibeli

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Back
Top Bottom