Huu kama sio ufisadi University of Dar es salaam itakua nini

Lawkeys

JF-Expert Member
Nov 16, 2009
1,118
287
CAUTION MONEY CHUO KIKUU UDSM MNAPELEKA WAPI?

Ni kawaida katika academic institutions mbalimbali kutoa fedha kiasi fulani unapojiunga kwajili ya tahadhari kwa uharibifu wa mali etc. unapokuwa katika nstitution hiyo. Utaratibu huu ni kwamba kama uharibifu haukutokea unatakiwa kurudishiwa pesa yako.

Utaratibu katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kila mwanafunzi anaekuwa admitted analipa Tsh. 10,000/= kama caution money. Lakini cha kushangaza ni kwamba kwa takribani miaka miwili hivi ambayo ndio nina uhakika nayo pesa hizo hawzirudishwi kwa wahitimu. Cha kusikitisha zaidi mwaka jana wahitimu waliandikwa majina yao na wakaahidiwa kurudishiwa pesa hizo lakini mpaka sasa kimya.

Inaonekan pesa ndogo lakini kwa hesabu rahisi UDSM ina admitt wanafunzi takribani 17,000 kwa mwaka ambao ukizidisha kwa 10,000/= unapata 170,000,000/= (Milioni mia moja sabini). Kama kuna wakubwa wawili watatu wakagawana au wakaweka kwenye fixed account...wanaweza kujipatia pesa nyingi kila mwaka isivyokuwa halali at the expense of watoto wa wakulima.

"Wito ufisadi ni kama Cancer tusipokubali kuikata chuchu tutatakiwa kukata ziwa zima, na ikishindikana tunakaribisha kifo". Wahusika shughulikieni hilo na wasomi fanyeni mambo proffessional basi, au ndo PHD feck (siwatusi). Najua kama wahusika wanafanya kusudi itakuwa wanaona hakuna immediate reaction kwasababu wahitimu wapo nje ya chuo hawawezi kuipigania haki yao kirahisi. Hivi vifisadi chipukizi vishughulikiwe jamani.
 
Nakubaliana na wewe kaka. ufisadi huu upo kila mahali. Mifano mingine michache:
1 Application fee ya Masters Muhimbili ni 50,000 for citizens wa Tz, lakini unakuta MSc Public Health wanataka 45 applicants lakini mnaoomba ni 3000 hadi 5000!
2 Shule za secondary St marian Bagamoyo application fee ya F1 inakua 5000 (Kama sijakosea), lakini fomu ni unlimited number. Tanzania nzima wakiomba watoto 10000+ ilhali wanahitajika watoto 45 tuu??
Bado kuna mtu aklikua ananiambia hii biashara ya kutuma SMS ujishindie chance ya kwebda kushuhudia kombe la dunia. Ati inakuwa mjanja kanunua tiketi zake 2, anaingia mkataba na kampuni ya simu, anazichangisha za kutosha.
Inabidi tuwe macho,tusiingizwe mjini kirahisi.
 
Loyola high school kabla mwanafunzi kidato cha tano hajaanza hutakiwa kulipa laki mbili hizo hazipo kwenye ada na application form ni sh elfu ishirini,hivi sasa ada ni milioni moja laki nne kwa mwaka,na hapo tunaambiwa ni shule zilizo chini ya taasisi za dini,fikiria hiyo form ni elfu ishirini wanafunzi wangapi wanaomba,ukikubaliwa kiingilio ni hizo laki mbili hizo haziingiliani kabisa na ada,hizi shule nazo ni fisadi hakuna cha shule za dini wala nini na Loyola si shule ya bweni,nenda Shabaan Robert,mambo ni hayohayo,huko Mzizima ndo usipime
 
Loyola high school kabla mwanafunzi kidato cha tano hajaanza hutakiwa kulipa laki mbili hizo hazipo kwenye ada na application form ni sh elfu ishirini,hivi sasa ada ni milioni moja laki nne kwa mwaka,na hapo tunaambiwa ni shule zilizo chini ya taasisi za dini,fikiria hiyo form ni elfu ishirini wanafunzi wangapi wanaomba,ukikubaliwa kiingilio ni hizo laki mbili hizo haziingiliani kabisa na ada,hizi shule nazo ni fisadi hakuna cha shule za dini wala nini na Loyola si shule ya bweni,nenda Shabaan Robert,mambo ni hayohayo,huko Mzizima ndo usipime


kwani umetumwa huko, nenda shule zinazoendana na kipato chako ukishindwa jaribu shule za kata........kama elimu ni garama jaribu UJINGA
 
Having watch dogs kwenye maswala ya price hiking is very necessary. A lot of services and goods that are of necessity or partly public goods are left un observed.
Kama swala la charges za simu ya mkononi!!! Duh, yani the difference between mtoni na hapa ni amazing!
Umeme na maji pia, bei ya maji namibia ambayo ni arid ni cheaper kuliko hapa kwetu.
Haya Udaiji wa hela kama hapo above. Watu wanadiriki kuandika na kufanya chochote kwasababu eti ni free market kwaio tuache the laws of supply and demand play their part as if ni divine instructions. Hata sheria za Mungu zinakuaga challenged.
 
Back
Top Bottom