mbingunikwetu
JF-Expert Member
- Feb 17, 2015
- 13,664
- 18,041
Wasaidizi wa Rais Samia Suluhu Hassan wametenda kosa kubwa sana kwa kutokumshauri Rais kuwa huu haukuwa muda muafaka wa yeye kutembelea Marekani.
Marekani Ina hasira na Nchi nyingi duniani kwa kutokuiunga mkono katika harakati zake za kuitenga Urusi katika jamii ya kimataifa. Tanzania tumeamua kuwa neutral/kutokuwa na upande katika mzozo wa Urusi na Ukraine.
Kwa Marekani ukiamua kutokuwa na upande unahesabika kuwa uko upande wa Urusi, na inafanya Kila jitihada kuyatisha mataifa yenye msimamo huo Ili yailaani Urusi! Kwa hiyo ukiandaa mazingira ya kukutana na Marekani kwa Sasa lazima ikushinikize kuilaani Urusi.
Sidhani Kama mama atakuwa na ubavu wa kuhimili shinikizo la Marekani katika jambo hili. Anaweza kujikuta amesema jambo ambalo hakutegemea akiwa chini ya shinikizo. Sidhani kama ataweza kuhimili Kama India na Afrika ya kusini zilivyoweza kuhimili.
Afrika hatuwezi kulaani Nchi ya Urusi iliyokuwa mstari wa mbele Sana kwenye harakati za upatikanaji wa uhuru kusini mwa afrika-(Zimbambwe, Msumbiji, Botswana, Angola, Namibia na Afrika ya kusini).
Wakati huo wapigania uhuru akiwemo Mandera walikuwa wanaitwa magaidi na Marekani!! Chonde chonde Samia Mungu akutie nguvu uwatolee nje mabeberu huko Marekani!