Hussein Bashe: Kati ya Ajira 10 ajira 7 ni za sekta ya Kilimo

kalacha mateo

Senior Member
Sep 27, 2021
118
237
Wakati wa uwasilishwaji wa bajeti ya Kilimo leo Bungeni, Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe alielezea maendeleo ya sekta ya kilimo nchini na kusema sekta ya kilimo imetoa wastani wa asilimia 65 za ajira kwa vijana ambayo ni takribani sawa na watu saba kwenye kila watu kumi wanaoajiriwa.

“Sekta ya kilimo imechangia asilimia 26.1, imetoa ajira kwa wananchi wastani wa asilimia 65, na kuchangia asilimia 65 ya malighafi ya viwandani, na asilimia 100 ya chakula.” – Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe

Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu inaendelea kuboresha sekta ya kilimo ili iweze kuongeza ajira zaidi kwa vijana, Lengo la Serikali ni sekta ya kilimo kutoa ajira milioni tatu kwenye kilimo ifikapo mwaka 2025. Mkakati wa kuzalisha ajira hizo umeanza kutekelezwa kupitia utoaji wa mafunzo ya kilimo cha kisasa kwa vijana kupitia Program ya BBT (Build Better Tommorow).

Kupitia program hiyo vijana wanapewa mafunzo na kupewa mtaji wa mashamba kwa ajili ya kilimo, aidha pia uwezeshwaji unafanywa kwenye ufugaji wa mifugo na samaki.

271183503_489982635829946_338260027209042889_n.jpg
 
Back
Top Bottom