Hukumu ya Lema Tar 29/10/2012

Ulimbo

JF-Expert Member
Aug 14, 2009
3,767
4,035
Taarifa nilizozipata kutoka kwa mtu aliye karibu na vyanzo vya mahakama ni kwamba ile hukumu ya rufaa ya lema itatolewa tar 29/10/2012.

Nazidi kufuatilia na nitazidi kuwapa taarifa kadri nitakavyo zipata.
 
Naamini haki itakuwa ni kubwa sana. Kwa hiyo inatakiwa kukubali matokeo ya aina yoyote.
 
Lazima kamanda LEMA arudishiwe ubunge wake maana mpaka sasa hivi yule mwenye nywele nyeupe na yule aliyoko kule mombasa hawako tayari kupanda kizimbani kuthibitisha madai ya wale waliofungua kesi mahakamani,hii kesi inaendana na ile ya igunga ambapo yule mkuu wa ujenzi TZ alishindwa kupanda kizimbani kuthibitisha au kukataa madai yaliyopelekwa na Prof.Safari kuhusu ujenzi wa daraja hautofanikiwa endapo chichiem haitachaguliwa!
 
Kinachotolewa si hukumu(Judgement)bali uamuzi(ruling).


Sawa tu, maana sisi wengine hatujui tofauti ya hukumu(Judgement) na maamuzi(Ruling) kama ulivyo sema. sisi tunajua vyote ni sawa tu.
 
Kwa namna wale wasomi ndugu walivyohenyeshana pale mahakamani wakisaidiwa na wasomi wetu wenye kuvaa majoho mekundu, niko tayari kwa uamuzi wa aina yeyote ile, ingawa karoho kataniuma kama hio rulling itakuwa in favour ya mshindani wangu..
 
itakuwa J3 nzuri kama Lema atashinda

Nadhani kitakachotolewa maamuzi ni kuhusu ile pingamizi iliyo wekwa na wakili msomi Alute kwamba rufaa ya lema ina mapungufu kisheria.For that case tunachotegemea ni mh.chande kuueleza umma wa watanzania na dunia kwa ujumla kama ile rufaa ni batili au halali,ikiwa ni halali itasikilizwa ikiwa ni batili kisheria itatupiliwa mbali kama ile ya Sumbawanga.
 
Viva lema, viva chadema tutashinda kwani MUNGU yu nasi..A-town history, hapa LISU+KIMONGORO+CHANDE=GODBLES LEMA NDANI YA BUNGE
 
Back
Top Bottom