Elections 2010 Hujuma Zingine kwa Serikali Dhidi ya Wanavyuo hizi hapa

Sielewi ni kwa nini huwa wanachukuwa anuani za wananfunzi wnapokuwa wanajaza fomu za kujiunga. Sasa shirika la posta liko kwa kazi gani?

Huu ni ukandamizaji mwingine wa demokrasia.
 
Litakuwa wazo la Ridhiwani tu maana Baba mtu anaanguka sana:dance:

Mkuu umenena vyema, yeye kwa Sababu ya Utajiri wa Baba yake anaweza hata kwenda Ijumaa Havard kuchukua Form halafu akarudi Jumatatu Basi anafikiri kila mtu ana uwezo huo

Yaani Mtoto umtoe Mwanza aje Dar kuchukua form na wakati hizi form zingeweza kutumwa kwenye e-mail au kwa njia ya posta na bado watu wakazipata

Huu ni Uharamia tu
 
Kama waliomba admission kwa internet au simu kwa nini wasipewe hiyo admission kwa njia hiyo hiyo? Dawa ni kuchelewa na barua zao watazikuta baada ya uchaguzi. Viongozi wa wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu kama kweli ni wazalendo kama wakati wetu watangaze wanafunzi hao kufika vyuoni baada ya uchaguzi na barua zao za admission watazikuta kwenye vyuo vyao bila shida.
 
Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam Kimetoa Ratiba za wanafunzi wanaotarajia kujiunga na masomo kwa mwaka wa masomo 2010/2011 kuchukua Admission letter. Ratiba hiyo inaoonesha kwamba Wanafunzi hao wanatakiwa kufika UDSM kati ya tarehe 18/10/2010 mpaka 25/10/2010 kwa ajili ya kuchukua barua za kujiunga Chuo

Jamani hili Jambo halijafanywa kwa Bahati Mbaya, kuna mambo ambayo hii Serikali inayafanya ni ya Hatari na ni ya kipuuzi sana

Nadhani Serikali inatambua kwamba hawa wanafunzi watarajiwa wengi wamemaliza form six mwaka huu na wengi walijiandikisha kupiga kura katika maeneo wanayotoka

Sasa kuwalazimisha watoto hawa wasafiri kutoka kigoma kuja dar kuchukua Admission letter ni kuwaweka katika hatari ya kukosa haki yao ya Msingi kabisa ya Kupiga Kura.

Wengi wao ni watoto wa Maskini ambao wakishafika dar kuchukua Admission letter hawana uwezo tena wa kurudi makwao kupiga kura, hili ni pigo kubwa sana kwa Demokrasia linalofanywa na Serikali dhidi ya kundi lolote linaloonekana kuwa kinyume na Serikali

Jamani naomba wanaharakati waliangalie hili Jambo na ikiwezekana walitolee ufafanuzi mapema

Huu ni Unyongwaji wa Demokrasia unaofanywa na seriklai Dhalimu ya CCM


Naomba kuwakilisha

Wameogopa matokeo ya TCIB!
 
Back
Top Bottom