Huenda kwa DP World, bandari kwao ni mahali pa kuanzia, lengo ni Pwani yote ya Bahari

Bams

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
16,555
41,066
Kuna Watanzania ni laana kwa nchi hii. Wengine ni kutokana na ujinga na uwezo duni wa kuona mbali. Wengine ni mawakala wa maadui wa Taifa letu. Wengine ni sababu ya ubinafsi na tamaa.

Ulimwengu huu tangu uumbwe, vita vilivyopiganwa mara nyingi zaidi, ni vya kugombania maeneo/ardhi. Urusi inapigana na Ukraine kwa nia ya kuyachukua maeneo yote ya mashariki mwa Ukraine. Ukraine nayo inapambana kurudisha maeneo yaliyoporwa. Waisrael na wapalestina wanapigana kugombania maeneo. Kadhalika Spain na Morocco, Tanzania na Uganda, n.k.

Hivyo mtu yeyote mwenye kichwa kinachofanya kazi, anakuwa makini sana kwenye suala la wageni kuwapa rasilimali msingi ambazo siku moja zinaweza kumpa mgeni nafasi rahisi ya ushindi.

WAARABU
Mfalme wa Oman, miaka ya karibuni ametamka kwa uwazi kuwa lazima siku moja makao makuu ya sultani wa Oman yarudi Zanzibar.

Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar amewahi kutamka kuwa maeneo yote ya pwani ya bahari kutoka pwani ya bahari kuingia bara kilometa 20, ukanda wote toka Pangani mpaka Mtwara, ni maeneo ya Zanzibar kwa sababu maeneo hayo yalikuwa chini ya utawala wa sultani.

IGA inasema DP wanatakiwa kumilikishwa ardhi ya maeneo yote watakayowekeza. IGA ni mkataba mama, na haujabadilishwa hata nukta moja hata leo. IGA, kila mmoja mwenye uelewa aliiona, lakini HGA iliyosainiwa hakuna aliyeiona, na wanayoyanena hawa watu wasioaminika, hakuna mwenye uhakika kama yapo kwenye mkataba huo wa bandari ya Dar au ni mwendelezo ule ule wa uwongo na ulaghai wa watawala. Lakini hata kama maneno wanayoyasema ni kweli, bila mabadiliko ya IGA, siku yoyote DP wanaweza kuibuka na kudai kilichopo kwenye IGA.

LENGO LA MUDA MREFU
DP watachukua maeneo ya bandari, na maeneo mengine ya pwani ya bahari watayanunua toka kwa wananchi, ambao wengi wao ni maskini, na hawatakuwa na uwezo wa kukataa donge nono la mnunuzi mwarabu. Baada ya miaka mingi mbeleni, pwani yote ya bahari, toka Pangani mpaka Mtwara, itakaliwa na kumilikiwa na waarabu. Na kutokana na nguvu ya pesa, watajiunga CCM, (na kwa CCM ukiwa na pesa utapewa cheo chochote utakachotaka) na hivyo kuwafanya wageni hawa wawe na nguvu za kisiasa na uchumi.

Yumkini, huko mbeleni pwani yote ya bahari ya hindi itachukuliwa na waarabu, na kisha kuifanya ni sehemu ya Zanzibar. Hilo likitokea, Tanganyika itakuwa landlocked, ikibakiwa na vibandari vya kwenye maziwa, na hivyo kuzitegemea bandari za mataifa mengine. Ukamilifu wa haya unaweza usitokee miaka ya karibuni, lakini ni mpango wa muda mrefu. Baada ya migogoro mingi, Zanzibar itajitenga, na kuridhia kuwa sehemu ya Oman, na hapo ndipo makao makuu ya sultani yatahamia mji mkongwe.
 
Kuna Watanzania ni laana kwa nchi hii. Wengine ni kutokana na ujinga na uwezo duni wa kuona mbali. Wengine ni mawakala wa maadui wa Taifa letu. Wengine ni sababu ya ubinafsi na tamaa...
Hebu fikiri kama mpango wenyewe ulianzia kupoka loliondo miaka 30 imepita. Njama za kuongeza eneo zinawaletea shida wenyewe wamasai.

Huko kuna jiwanja midege mikubwa inashuka lami tu hakuna. Mpango wa loliondo ni siri hatujulishwi kile kinaendelea pale.
 
Nadharia yako ni kama umeichota mbali; lakini ukiona yanayotendeka hapa sasa hivi inakuwa vigumu sana kuikataa nadharia yenyewe.

Labda kusahihisha au kuongezea kidogo. Ukanda wa pwani chini ya himaya ya Sultan ni kuanzia pwani ya Kenya, tena huko ndiko hadi miaka ya 1960's mwanzoni, pwani hiyo ilikuwa inadaiwa kwa nguvu.

Lakini nirudie tena, kama nilivyomweleza mkuu tpaul na mada yake humu.
Hii Tanzania siyo nchi ya kulialia. Hili ni taifa lenye heshima. Lenye historia ya ukombozi.

Usitishike na huu ujinga unaofanyika sasa hivi.
Samia katupa fursa nzuri sana ya kuona jinsi taifa zima tulivyojisahau. Subiri ngoma inayofuata.
 
Kuna Watanzania ni laana kwa nchi hii. Wengine ni kutokana na ujinga na uwezo duni wa kuona mbali. Wengine ni mawakala wa maadui wa Taifa letu. Wengine ni sababu ya ubinafsi na tamaa...
Kwa hiyo hapa unajaribu kututhibitishia kwamba Waarabu wanataka watimize ule msemo wa "historia hujirudia" kwa vitendo?

Form two kwenye somo la history kuna historia inahusu "shift of Sultan Seyyid Said from Oman to Zanzibar in 1840"...halafu zinaendelea mbwe mbwe nyingi lakini kuna maelezo yanasema...."The Sultan decided to shift his capital city from Oman to Zanzibar in order to have full control of the economy of coastal city states"
 
Kuna Watanzania ni laana kwa nchi hii. Wengine ni kutokana na ujinga na uwezo duni wa kuona mbali. Wengine ni mawakala wa maadui wa Taifa letu. Wengine ni sababu ya ubinafsi na tamaa.

Ulimwengu huu tangu uumbwe, vita vilivyopiganwa mara nyingi zaidi, ni vya kugombania maeneo/ardhi. Urusi inapigana na Ukraine kwa nia ya kuyachukua maeneo yote ya mashariki mwa Ukraine. Ukraine nayo inapambana kurudisha maeneo yaliyoporwa. Waisrael na wapalestina wanapigana kugombania maeneo. Kadhalika Spain na Morocco, Tanzania na Uganda, n.k.

Hivyo mtu yeyote mwenye kichwa kinachofanya kazi, anakuwa makini sana kwenye suala la wageni kuwapa rasilimali msingi ambazo siku moja zinaweza kumpa mgeni nafasi rahisi ya ushindi.

WAARABU
Mfalme wa Oman, miaka ya karibuni ametamka kwa uwazi kuwa lazima siku moja makao makuu ya sultani wa Oman yarudi Zanzibar.

Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar amewahi kutamka kuwa maeneo yote ya pwani ya bahari kutoka pwani ya bahari kuingia bara kilometa 20, ukanda wote toka Pangani mpaka Mtwara, ni maeneo ya Zanzibar kwa sababu maeneo hayo yalikuwa chini ya utawala wa sultani.

IGA inasema DP wanatakiwa kumilikishwa ardhi ya maeneo yote watakayowekeza. IGA ni mkataba mama, na haujabadilishwa hata nukta moja hata leo. IGA, kila mmoja mwenye uelewa aliiona, lakini HGA iliyosainiwa hakuna aliyeiona, na wanayoyanena hawa watu wasioaminika, hakuna mwenye uhakika kama yapo kwenye mkataba huo wa bandari ya Dar au ni mwendelezo ule ule wa uwongo na ulaghai wa watawala. Lakini hata kama maneno wanayoyasema ni kweli, bila mabadiliko ya IGA, siku yoyote DP wanaweza kuibuka na kudai kilichopo kwenye IGA.

LENGO LA MUDA MREFU
DP watachukua maeneo ya bandari, na maeneo mengine ya pwani ya bahari watayanunua toka kwa wananchi, ambao wengi wao ni maskini, na hawatakuwa na uwezo wa kukataa donge nono la mnunuzi mwarabu. Baada ya miaka mingi mbeleni, pwani yote ya bahari, toka Pangani mpaka Mtwara, itakaliwa na kumilikiwa na waarabu. Na kutokana na nguvu ya pesa, watajiunga CCM, (na kwa CCM ukiwa na pesa utapewa cheo chochote utakachotaka) na hivyo kuwafanya wageni hawa wawe na nguvu za kisiasa na uchumi.

Yumkini, huko mbeleni pwani yote ya bahari ya hindi itachukuliwa na waarabu, na kisha kuifanya ni sehemu ya Zanzibar. Hilo likitokea, Tanganyika itakuwa landlocked, ikibakiwa na vibandari vya kwenye maziwa, na hivyo kuzitegemea bandari za mataifa mengine. Ukamilifu wa haya unaweza usitokee miaka ya karibuni, lakini ni mpango wa muda mrefu. Baada ya migogoro mingi, Zanzibar itajitenga, na kuridhia kuwa sehemu ya Oman, na hapo ndipo makao makuu ya sultani yatahamia mji mkongwe.
Umeandika fikirisho tosha kabisa, kuna watakao kebei kwakuwa yawezekana wao watakuwa wakisha kufa, na kuna ambao pesa za wakati huo zitakuwa tamu na kusukuma siku za kuishi, hawa ndio hao wasiojali nchi yao bali ccm itawale, hao ndio wale wafia madarakani, hao ndio wale wanaojioma nchi hii ni yao peke yao na familia zao, hao ndio wale wajiitao machawa ili mradj wakati wote wako karibu na viomgozi
Hii ndio Tanzania ya kinafiki wenye busara ni wachache na wengine walikwisha tangulia mbele za haki
Watanzania wanaojitolea kuipigania nchi hii wanafanywa. Maadui wa taifa, masikini wasiojielewa na wao wanaingia kwenye mkumbo wasio uelewa
Kuna neno ni baya lakini ni jema, unaweza kuwa na mzazi saababu ni baba yako ukadhan ni mtu wa busara sababu kakuzaa wewe
Lakini akawa mi mtu wa ovyo dhidi ya matendo yako yasiyo na busara
Kumbe nk mbakaji, kumbe ni jambazi, kumbe ni muuaji
Lakini kwako ni baba bora
Ccm. Si kila kitu katika maisha yetu
Ccm ni kama vyama vingine tu na sio sababu imeleta uhuru basi ni chama chema
Ni chama kilichokwisha poteza wisdom yake ni chama kilichokwisha vunja misingi yake
Ni chama kilichobakiza rangi tu pamoja na picha ya nyundo na jembe
Yani ni chama kilichopitwa na wakati , wao bado anawaza jembe mlaka sasa wakati hivi sasa kuna teknoloji mpya za maendeleo
Sio kila kitu mfundishwe
Nina mengi ila cha muhimu wcha nirudi kwenye point
Parestna inasemekana ilichukuliwa kwa mfano wa andiko hili, mamaanisha post hii tunayoichangia
Wakati wa Israel wanarudi walirudi kwa kununua maeneo yao makubwa ikiwa ni mkakati wa kurudi katika ardhi yao
Ma mpaka kufikia kujikusnya na kuwa na nguvu na kurudisha taifa lao
Hawa ni waraabu hawashindwi kufikia maamuzi kama ya ndugu zao
Tuunganeni kuikomboa nchi yetu sote
Tuwe Islamic, au Kristian au Pagani
Hii nchi ni ya vizazk vijavyo tuache ubinafsi
Samahanini kwa error zozote zilizojitokeza, nina matatizo kidogo ya macho
 
Kuna mtu kaniambia hiyo mbinu ya watu weupe kuja kutawala Africa tena watatumia uwekezaji,,kuzaa watoto na wanawake wakiafrica watoto watalelewa hapa kujua culture baadae watatumiwa kuja kusaidia wazazi,mababu etc kutawala Africa mf.wachina hawa wanaongoza kuwapa mimba wasichana wa Africa,waarabu sitaki hata kugusia mnaona vitukuu vya sultan vinavyosema kwamba bora waungane na waarab,wazungu hawa ndio wanashirikiana na wazawa kununua lands,na kuoa huko Arusha miaka 50 ijayo sijui kama kutakua na ngozi nyeusi anyway Mungu ibarik Africa!
 
Kuna Watanzania ni laana kwa nchi hii. Wengine ni kutokana na ujinga na uwezo duni wa kuona mbali. Wengine ni mawakala wa maadui wa Taifa letu. Wengine ni sababu ya ubinafsi na tamaa.

Kumbe ni hivyo? Basi safi sana.

Tena wewe umechelewa, siyo bahari tu, jana watu walikuwa Njombe huko wanatazama namna ya kuwekeza huko na kupata ardhi za kulima huko, BBT ya Bashe inapata bonge la booster.

Wewe umelala kweli kweli, bado upo baharini tu?

Msikilize Rais wa Zambia leo kasema nini, anasema njooni mchukuwe ardhi mlime, mfunguwe viwanda, fanyeni biashara bila vikwazo.

Mama kawapa Zambia eneo la mizigo yao pale Kwala dry port, ili kusiwe na usumbufu na wanaongelea sasa hivi DP World wajenge dry port kubwa mpakani Tunduma na wanataka mzigo pale upite tuhakuna kuhangaishana, amewataka DP World waweke mifumo, mzigo toka unapokiwa Dar wauone Zambia, wewe umelala doro.
 
Nadharia yako ni kama umeichota mbali; lakini ukiona yanayotendeka hapa sasa hivi inakuwa vigumu sana kuikataa nadharia yenyewe.

Labda kusahihisha au kuongezea kidogo. Ukanda wa pwani chini ya himaya ya Sultan ni kuanzia pwani ya Kenya, tena huko ndiko hadi miaka ya 1960's mwanzoni, pwani hiyo ilikuwa inadaiwa kwa nguvu.

Lakini nirudie tena, kama nilivyomweleza mkuu tpaul na mada yake humu.
Hii Tanzania siyo nchi ya kulialia. Hili ni taifa lenye heshima. Lenye historia ya ukombozi.

Usitishike na huu ujinga unaofanyika sasa hivi.
Samia katupa fursa nzuri sana ya kuona jinsi taifa zima tulivyojisahau. Subiri ngoma inayofuata.
Wenye chuki za dini mna kazi sana. Mtazusha na kuja na kila aina ya assumption hasi lakini Mungu atawafutilia mbali na michuki yenu. Taifa la Tanzania litaendelea kushamiri sawa na misingi yake chini ya mama Samia, The Mother of Modern Tanzania, na wengine watakaofuata.

Wakati mmekomaa huku na hoja hasi za kufikirika, wazungu wanamaliza almasi na dhahabu huko. Wao wala sio suala la kufikirika, wapo live migodini.
 
Back
Top Bottom