How ccm gets to fool itself with Employment Data!!

English Learner

JF-Expert Member
Jan 1, 2012
355
355
Read and analyze for yourself! This is a self cheating like once sung by prof. Jay; two (2) step foward, 8 steps backward and you vigorously celebrate.....crazy .....first class craziest!

Zitto Kabwe,

Mheshimiwa Spika,
Serikali imesema kwamba ilichukua hatua mbalimbali kukabiliana na tatizo la Ajira kwa kuongeza fursa za ajira……… mwaka wa Fedha wa 2012/13 ambapo pia Serikali imetangaza kuajiri watumishi 71,756.

Mheshimiwa Spika,
Duniani kote Serikali haizalishi ajira bali ajira huzalishwa na Uchumi mzima ambapo Serikali ni sehemu tu ya Uchumi(Jobs are created by the economy). Takwimu zinaonyesha kwamba kila mwaka Tanzania inaingiza kwenye soko la Ajira watu takribani 700,000 (laki saba). Shughuli za Uchumi zikiongezeka ndio Ajira zinatengenezwa. Serikali inafikiria nini kuhusu vijana takribani milioni nane walio shule za Msingi hivi sasa, Vijana milioni 1.7 walio katika Shule za Sekondari hivi sasa, Vijana 200,000 waliopo vyuo vya Ufundi na Wanachuo 180,000 walio katika Vyuo vya Elimu ya Juu (takwimu kutoka kitabu cha hali ya uchumi, 2012 sura ya 19).

Serikali ambayo bado inategemea takwimu za Ajira za Mwaka 2006 inajitamba kwa kuajiri watu 70,000.
 
Back
Top Bottom