Lizy, we women arent their servants they also have to cook and wash as well if i can do it why not him ... its another way of expresing love and care for your spouse kwanini usubiri mpaka I do it ... kama they cant .. sawa bedroom we take care but others house girl can manage ... Hey Girl! you are giving them breathing space here wazidi kutukandamiza
naimaomaro,
Ni kweli kabisa unavyosema 'we are not their servant'. Sikuweka wazi zaidi, ila mwenye kuelewa na ataelewa kwamba if they can work and do bussiness, we also can. Hivyo ile lugha kwamba wao watafutaji na sisi tupo nyumbani hivyo majukumu ama shughuli za nyumbani ni zetu haina nafasi tena. The so called "Team work" shouldn't be at the work place only, hata nyumbani iwepo. Kusaidiana kama enzi zileeeeee, za urafiki na uchumba, ndoa isitubadilishe.
interesting stuff!!
tukiacha mambo ya kitandani, je ladies mnapenda mfanyiwe nini na wenzi na mnadhani wao wanapenda muwafanyie nini?
Na gents mnapenda kuwafanyiwa nini na nyie mnadhani wao wanapenda kufanyiwa nini na nyie?
Mimi kwa kuanzia
Napenda nisaidiwe kazi, huwa najisikia raha sana pale baba nanihii anaponisaidia labda kubeba japo glasi yake maji akaipeleka jikoni akaisuuza, au kama napasi akabeba ile nguo ilio tayari akaipeleka mahali pake. yani nampenda mnoo saa hiyo, ni kama vile ananiapproach tena.
Na mimi nadhani anafurahi pale anaponikuta napika (sio kila siku) au nahangaika na nguo zake, kama kushona kifungo nk.
Haika,
Really interesting.
Napenda once in a while nikiwa jikoni napika, basi aje akae akinipigisha stori. I mean nitafeel kama ananisaidia vile, kulikoni yeye yuko huko sijui anaangalia TV huku akiburudika na glasi ya Gongo, hiyo glasi yake aje nayo jikoni, avute kiti na mimi mapishi yanaendelea, story kwa mbali.
Siku moja moja basi na yeye basi anisuprise nikitoka kibaruani nikute kapika lol. (Hapa shughuli, lkn ndio ukweli). Au hata week end hivi, wakati mimi nitakuwa nikifanya hizo shughuli zingine (kufua, usafi wa nyumba nk) achemshe basi hata hiyo chai!