Hotuba ya Warioba Bungeni Dodoma: Jumanne, Tarehe 18 Machi 2014 na Hoja ya Muungano wa Serikali Tatu

Ila chadema hili la review ya taratibu za uchaguzi hasa la kuandikisha na kuboresha daftari hawataki kulifanyia kazi..watu tumelisema sana..sana ..

Dr. unafikiri Chadema ifanye nini? Maana wenye wajibu wa kufanya hivyo ni selikali chini ya tume ya uchaguzi.
 
Wadau, naamini mmeamka salama na akili zimetulia baada ya yale yaliyotokea jana.

Kwa mujibu wa maelezo ya Mwenyekiti wa Bunge Maalum ambayo ameyatoa jana usiku, ni kwamba Bunge litaendelea na kikao chake leo saa tatu kamili asubuhi. Kwamba, baada ya dua, wabunge ambao walikuwa hawajaapa watakula kiapo. Baada ya kiapo hicho ndipo Mwenyekiti wa Tume ya Katiba, Jaji Joseph Sinde Warioba atakapowasilisha Rasimu ya Katiba. Na kwa mujibu wa makubaliano waliyofikia, ni kwamba Warioba ataongea hadi atakapomaliza hotuba yake.

Nami kama kawaida kwa kushirikiana na wadau wenzangu akinina Skype, MaishaPesa, Simiyu Yetu, Deo Corleone, kbm, Mkuu ya Kaya na wengine tutaendelea kuwaletea yatakayojiri. Hadi wakati huo, Stay Connceted.

-================================================================
UPDATES
Mwenyekiti anaeleza kilichotokea jana. Kwamba baada ya kutokea kile kilichotokea, ni kwamba waliitisha kamati ya mashauriano. Katika kikao hicho wamekubaliana mambo yafuatayo.
*Kwamba baada ya kiapo watampokea Mwenyekiti na Makamu mwenyekiti
*kwamba Warioba atahutubia kuanzia saa tatu na nusu hadi atakapomaliza
*semina zilizokuwa na utata zimefutwa badala yake semina ya kanuni itafanyika leo jioni na kesho
*Siku ya Alhamisi kutakuwa na semina itakayoongozwa na Wakenya.
*Semina juu ya historia ya Tanzania Bara, Zanzibar na Muungano imefutwa kwa vile kwa kadri utakavyoteua watakaoendesha semina hiyo, hawataonekana kama wamesimama kati kati
*Siku ya Ijumaa asubuhi, Mwenyekiti atatangaza Kamati 12 za Bunge Maalum
*Siku ya Ijumaa saa 10 jioni, Rais atakuja kulizindua Bunge

sina shaka na upuuz unaoendelea bungen,kilichobadilika kwa sitta ni cheo,toka spika kuwa mwenyekiti,toka waziri kuwa mwenyekiti,watu wana ushabiki ila Sitta kama watawala wengine,hana jipya,
 
sina shaka na upuuz unaoendelea bungen,kilichobadilika kwa sitta ni cheo,toka spika kuwa mwenyekiti,toka waziri kuwa mwenyekiti,watu wana ushabiki ila Sitta kama watawala wengine,hana jipya,
Mkuu, punguza jazba kidogo kwa madhumuni ya mjadala huu
 
Leo tena wagome,kwanini wanasigina kanuni,kwani Shein si yupo kwanini azindui bunge
 
Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba wameingia Bungeni na muda wowote baada ya kutambulishwa Makamishna wa tume wataitwa kutimiza wajibu wao
 
Back
Top Bottom