Hotuba ya Warioba Bungeni Dodoma: Jumanne, Tarehe 18 Machi 2014 na Hoja ya Muungano wa Serikali Tatu

Chabruma

JF-Expert Member
Sep 19, 2013
5,660
1,777
Wadau, naamini mmeamka salama na akili zimetulia baada ya yale yaliyotokea jana.

Kwa mujibu wa maelezo ya Mwenyekiti wa Bunge Maalum ambayo ameyatoa jana usiku, ni kwamba Bunge litaendelea na kikao chake leo saa tatu kamili asubuhi. Kwamba, baada ya dua, wabunge ambao walikuwa hawajaapa watakula kiapo. Baada ya kiapo hicho ndipo Mwenyekiti wa Tume ya Katiba, Jaji Joseph Sinde Warioba atakapowasilisha Rasimu ya Katiba. Na kwa mujibu wa makubaliano waliyofikia, ni kwamba Warioba ataongea hadi atakapomaliza hotuba yake.


========================================
UPDATES:

DOWNLOAD HOTUBA NZIMA HAPA =>Hotuba ya Jaji Warioba, Bungeni - Machi 18, 2014

Mwenyekiti anaeleza kilichotokea jana. Kwamba baada ya kutokea kile kilichotokea, ni kwamba waliitisha kamati ya mashauriano. Katika kikao hicho wamekubaliana mambo yafuatayo.
*Kwamba baada ya kiapo watampokea Mwenyekiti na Makamu mwenyekiti
*kwamba Warioba atahutubia kuanzia saa tatu na nusu hadi atakapomaliza
*semina zilizokuwa na utata zimefutwa badala yake semina ya kanuni itafanyika leo jioni na kesho
*Siku ya Alhamisi kutakuwa na semina itakayoongozwa na Wakenya.
*Semina juu ya historia ya Tanzania Bara, Zanzibar na Muungano imefutwa kwa vile kwa kadri utakavyoteua watakaoendesha semina hiyo, hawataonekana kama wamesimama kati kati
*Siku ya Ijumaa asubuhi, Mwenyekiti atatangaza Kamati 12 za Bunge Maalum
*Siku ya Ijumaa saa 10 jioni, Rais atakuja kulizindua Bunge

==================
More UPDATES
Jaji Joseph Sinde warioba ameanza kuhutubia bunge mnamo saa tatu na nusu. Katika hotuba yake amepitia sehemu zote za Rasimu ya Katiba. Masuala muhimu aliyoeleza ni kama ifuatavyo
  • Mihimili ya dola itaendelea kuwa serikali, mahakama na Bunge
  • kuhusu Serikali, Rasimu inapendekeza kuwa matokeo ya Rais yanaweza kupingwa mahakamani na mgombea urais na si mwingine.
  • madaraka ya Rais yamepunguzwa hasa kwenye suala la uteuzi
  • Mawaziri hawatatokana na wabunge
  • Rais hatakuwa sehemu ya Bunge
  • Kuhusu Bunge, ukomo wa wabunge ni awamu tatu ya miaka 5
  • Spika na naibu Spika hatatokana na Wabunge
  • Warioba pia kazungumza juu ya Uraia na amesema kuwa uraia ni wa aina mbili nao ni wa kuzaliwa na wa kujiandikisha. Pia imeelezwa kuwa hakuna uraia wa nchi mbili
Baada ya hayo na mengine, akiwa amewasilisha hotuba yake kwa dakika 85, Jaji Warioba alipumzika kwa dakika tatu. Na baada ya hapo anazungumzia muundo wa Muungano. Kwamba muundo uliopendekezwa ni wa Serikali tatu. Warioba anasema kuwa wamefanya utafiti juu ya muungano wetu na utafiti huo umeibua malalamiko kadhaa kwa pande zote za muungano. Ni kutokana na malalamiko hayo ndipo walipofikia uamuzi wa kupendekeza muundo wa serikali tatu.


Baadhi ya Malalamiko ya Zanzibar;

4.Kutokuwa na Uwazi wa Mapato na Matumizi wa Fedha za Jamhuri ya Muungano,

5. Kutokuwa na Akaunti ya Pamoja.

6. Uwepo wa Mkanganyiko wa Mapato jinsi ya kuchangia gharama uendeshaji wa Serikali zote mbili.

7. Kuwepo kwa Tume mbili zinazoshindana katika Nchi moja.

8. Zanzibar kutoshirikishwa kikamilifu na Serikali ya Jamhuri ya Muungano katika mchakato wa kupata misaada kutoka kwa Nchi za nje.

9. Malalamiko kuwa Viongozi Wakuu wa Zanzibar wanachaguliwa Dodoma na sio Zanzibar

10. Zanzibar kulalamika kuwa kuna baadi ya mambo yamefanywa kuwa ya Muungano kupitia kutungwa kwa Sheria ya Bunge la Jamhuri ya Muungano na baada ya hapo mambo hayo huwa katika utatanishi.

Kwa Upande wa Tanzania Bara baadhi ya malalamiko ilikuwa kama ifuatavyo;

1. Zanzibar imekuwa nchi huru, inabendera yake, inawimbo wa Taifa,Serikali yake na imebadili Katiba yake kutambuliwa kama Nchi.

2. Zanzibar imebadili masharti ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano ambayo inasema Sheria za Muungano zinazotungwa na Bunge hilo,zitumike sehemu zote, badala yake Katiba ya Zanzibar inaelekeza kuwa ili Sheria
itumike Zanzibar Sharti ipelekwe kwenye Baraza la Muungano.

3. Zanzibar imetunga Sheria kuhusu Fedha, ambalo ni suala lililopo kwenye Katiba ya Muungano.

4. Zanzibar imetunga Katiba ambayo imechukua Madaraka ya Rais yaliyopo kwenye Jamhuri ya Muungano,inaeleza kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano anamadaraka ya kugawa Nchi katika maeneo ya Kiutawala, mabadiliko ya kumi ya Katiba ya Zanzibar ya 1984 yametambua kuwa Zanzibar ni Nchi na yamempatia Rais wa Zanzibar mamlaka ya Kuigawa Nchi katika meneo ya Muungano.

5. Katiba ya Zanzibar inaeleza Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Nchi mbili lakini Katiba ya Jamhuri inaeleza kuwa Tanzania ni Nchi moja.

6. Masharti ya Katiba yaliyowekwa kwenye Katiba ya Zanzibar kuhusu Mchango wa Zanzibar katika mambo ya Muungano yamepingana na masharti ya Muungano.

7. Muundo wa Muungano uliopo umepoteza kutambulisho Kihistoria Tanganyika kuhusu watu wa Tanganyika kupitia maslahi yao.

8. Wananchi wa Tanzania Bara, kutokuwa na haki ya kumiliki Ardhi,wakati wenzano wa upande wa Zanzibar wanahaki ya kumiliki Ardhi Tanzania Bara.

9. Wabunge wa Zanzibar huchangia mijadala ya Muungano na ambayo kwa uhakika wake ni mambo ya Tanganyika na kwamba Wabunge wa Tanganyika hawana nafasi ya kuchangia katika Baraza la Wawakilishi.

10. Kwa mujibu wa Sheria ya Mzanzibari ya mwaka 1985 Watanzania ambao ni Watanzania wa Bara kutakiwa kutimiza masharti Maalum ili kupata haki ya kiraia wakati Mzanzibari hutakiwi kupata haki hiyo bila masharti
yeyote,haki hiyo ni pamoja na kugombea Uongozi.

Tume iliamua kufanya uchambuzi wa kina kuhusu malalamiko haya na endapo malalamiko ya Zanzibar yakipatiwa ufumbuzi na ya bara yatakuwa yamepatiwa Ufumbuzi.

JAJI WARIOBA AKIWA NJE YA UKUMBI WA BUNGE

 

Attachments

  • image.jpg
    image.jpg
    396.9 KB · Views: 1,713
Wadau, naamini mmeamka salama na akili zimetulia baada ya yale yaliyotokea jana.

Kwa mujibu wa maelezo ya Mwenyekiti wa Bunge Maalum ambayo ameyatoa jana usiku, ni kwamba Bunge litaendelea na kikao chake leo saa tatu kamili asubuhi. Kwamba, baada ya dua, wabunge ambao walikuwa hawajaapa watakula kiapo. Baada ya kiapo hicho ndipo Mwenyekiti wa Tume ya Katiba, Jaji Joseph Sinde Warioba atakapowasilisha Rasimu ya Katiba. Na kwa mujibu wa makubaliano waliyofikia, ni kwamba Warioba ataongea hadi atakapomaliza hotuba yake.

Nami kama kawaida kwa kushirikiana na wadau wenzangu akinina Skype, MaishaPesa, Simiyu Yetu, Deo Corleone, kbm, Mkuu ya Kaya na wengine tutaendelea kuwaletea yatakayojiri. Hadi wakati huo, Stay Connceted.
mzee wa viwango alikuwa anapima kina cha maji?
 
Sitta ni kigeugeu...................na kwajinsi alivyoongea leo ni wazi kuwa anatumika kutoa maamuzi.
 
Mwenyekiti anaeleza kilichotokea jana. Kwamba baada ya kutokea kile kilichotokea, ni kwamba waliitisha kamati ya mashauriano. Katika kikao hicho wamekubaliana mambo yafuatayo.
  1. Kwamba baada ya kiapo watampokea Mwenyekiti na Makamu mwenyekiti
  2. kwamba Warioba atahutubia kuanzia saa tatu na nusu hadi atakapomaliza
  3. semina zilizokuwa na utata zimefutwa badala yake semina ya kanuni itafanyika leo jioni na kesho
  4. Siku ya Alhamisi kutakuwa na semina itakayoongozwa na Wakenya.
  5. Semina juu ya historia ya Tanzania Bara, Zanzibar na Muungano imefutwa kwa vile kwa kadri utakavyoteua watakaoendesha semina hiyo, hawataonekana kama wamesimama kati kati
  6. Siku ya Ijumaa asubuhi, Mwenyekiti atatangaza Kamati 12 za Bunge Maalum
  7. Siku ya Ijumaa asubuhi, Rais atakuja kulizindua Bunge
 
"Simplicity is genius" hili ndilo nalo weza sema kwa sasa ila na fikiri wabunge wengi kwenye hili bunge la katiba ni wanyonyaji na walafi kwenye pesa za watanzani siku taraji kuona watu wanagoma kuwakilisha rasimu jana kisha leo wanakubali hii si sawa au wamgoje rais mpaka atakapo pata muda ijumaa kweli kuna watu hawana huruma na hii nchi kabisa
 
Back
Top Bottom