Hotuba ya Uwasilishaji wa Bajeti Kuu ya Serikali, 2014 / 2015

muamba ngoma huvutia upande wake ! watunga sheria huvutia kwenye maslahi yao kwanza , taifa baadae
 
KESI YA EPA: Maranda, Farijala wafungwa miaka 5 [Kada wa CCM Rajabu Maranda (kulia) na binamu yake Farijala Hussein, wakitoka katika Mahakama ya Hakimu ...

Escrow, hakuna wizi hapo, mambo yako kwenye uchunguzi. Siwezi kuhukumu kwa sasa, lakini kila nikisoma habari zake naona hakuna wizi, kuna kuzidiana maarifa ya kibiashara tu.​
mnashitaki dagaa,wakina rostam mnawaogopa!
 
Kwa washauri wa uchumi waliopo serikalini ni bora wasitozwe kodi maana ukiwatoza kodi watajiongezea mishara .siunaona badala ya kutangaza ufisadi unakuwa wao wanasema uchumi unakua. Kwahiyo itakuwa tunajikaanga wenyewe kwa kujiongezea kodi na gharama za kuendesha serekali
Salaam wana jamvi,imekua ni kawaida kwa serikali yetu kuongeza kodi kwenye bia,soda sigara na mvinyo nyingine ili kuongeza pato kwenye bajeti yake kila mwaka.je hakuna vyanzo vingine vinavyoweza kuongeza pato la taifa kwenye bajeti?kwa mfano tuna dhahabu ,madini ya tanzanite nk.na ni kwanini rais,mawaziri na wabunge wasikatwe kodi kwenye miashahara yao?au kodi inatakiwa kutozwa kwa watumishi wa ngazi za chini tu?hamuoni kama kwa kufanya hivyo tunaongeza ugumu wa kupambana na umasikini.mimi naona umefika wakati sasa wa rais,mawaziri na wabunge kulipa kodi ya mapato kila mwezi maana huko ndio kujenga taifa kazi yakujenga taifa ni yakila mtanzania bila kujali yeye ni nani katika jamii.bila kufanya hivyo tusitegemee taifa kusonga mbele kiuchumi tutabaki na uchumi wa kwenye vikaratasi nasio kwenye maisha halisi ya mtanzania.nawasilisha.
 
Watumishi wa serikali mtaongezewa asilimia 1% ya mshahara na kupunguziwa kodi kwa asilimia 1% hadi mkome kuisifiasifia CCM ikiwa inabomoa nchi
 
Kwa wale wasiojua kiswahili, bajeti yao ni hii.
 
Attachments

  • Government Budget 2014-15.pdf
    827.1 KB · Views: 52
Hakika huyu mama yupo fit sana. Nadhani atatumia muda mfupi kuwasilisha bajeti yake tofauti na mawaziri wa fedha waliomtangulia. Yupo fluent zaidi kwenye kuwasilisha

Hiyo ndiyo, bajeti ya ccm,itapunguza umaskini,wakati hakuna uainisho wa vyanzo vya mapato.unaposema kuwa bado tunaweza kukopesheka ni aibu.
Tuna vyanzo vingi vya mapato lakini ccm imevikalia.kama ccm ilishindwa kuleta maendeleo toka ihuru,hasa umeme na maji iwre leo?
Kama maji,umeme vijijini umeshindikana BRELA iwe leo!
Ahadi za meli,ndege,viwanja havikujengwa!, sembuse bajeti hii.wafanyakazi wanamadai yaliyoshindikana kulipwa leo iwe kutatua kero zao.umeme vijiji umesemwa utakamilika 2016 bajeti ya ccm ni usanii,kila mpango wa maendeleo utakamilika baada ya uchaguzi.kwa tunaojua ccm inawadanganya wananchi kuwa iendelewe kuchaguliwa kwani baada ya uchaguzi,ndio umeme utafika!! ,changa la machi ahadi juu ya ahadi
 
Kwa hili la PAYE ni usanii mkubwa wengi hawajaelewa fumbo hapa:
Ni hivi
kama mshahara wako hauzidi 170,000 hukatwi kodi kwa maana hiyo hakuna punguzo ukilinganisha na mwaka Jana !

Mshahara wa chini unaokatwa kodi ni Tsh 190,000/ inayongezeka juu ya 170,000 ili kufikia 360,000/ Huhu ndio umepata nafuu ya kodi ya Sh 1,900/ tu yaani awali 190,000/ ilikuwa inakatwa 13Pct na sasa itakatwa 12pct

Stage inayofuata ni 180,000/ juu ya 360,000 ili kufika 540,000/ katika hizi kodi imebaki pale pale ni 20pct

Stage inayofuata ni 180,000 juu ya 540,000
na kufikia 720,000/
Hii kodi yake inabaki pale pale ni 25Pct

Stage ya mwisho ni chochote kilicho zaidi ya 720,000/ ambayo hukatwa 30 pct hii kodi yake inabaki pale pale

Kwa maana hiyo ili kumpunguzia mwananchi makali serikali sikivu ya CCM imempunguzia kila mfanyakazi anayepata zaidi ya sh 360,000/ kodi kiasi cha sh 1900

narudia tena kiasi cha sh 1900

Serikali ya kisanii wananchi wasanii basi ni fullu sanaaaaaa
 
Mods iunganisheni/ipandisheni hii kwenye ile mada ya jana ya uwasilishaji hotuba ya bajeti ili kuwe na mtiririko mzuri.
 
Kwa hili la PAYE ni usanii mkubwa wengi hawajaelewa fumbo hapa:
Ni hivi
kama mshahara wako hauzidi 170,000 hukatwi kodi kwa maana hiyo hakuna punguzo ukilinganisha na mwaka Jana !

Mshahara wa chini unaokatwa kodi ni Tsh 190,000/ inayongezeka juu ya 170,000 ili kufikia 360,000/ Huhu ndio umepata nafuu ya kodi ya Sh 1,900/ tu yaani awali 190,000/ ilikuwa inakatwa 13Pct na sasa itakatwa 12pct

Stage inayofuata ni 180,000/ juu ya 360,000 ili kufika 540,000/ katika hizi kodi imebaki pale pale ni 20pct

Stage inayofuata ni 180,000 juu ya 540,000
na kufikia 720,000/
Hii kodi yake inabaki pale pale ni 25Pct

Stage ya mwisho ni chochote kilicho zaidi ya 720,000/ ambayo hukatwa 30 pct hii kodi yake inabaki pale pale

Kwa maana hiyo ili kumpunguzia mwananchi makali serikali sikivu ya CCM imempunguzia kila mfanyakazi anayepata zaidi ya sh 360,000/ kodi kiasi cha sh 1900

narudia tena kiasi cha sh 1900
Asante sana mkuu, kumbe nilikuwa sijui lolote kuhusu mfumo wa kodi, umenifungua macho. Kweli tunafanyiwa usanii.
 
Kupitia bajeti ya serikali ya 2014/2015 ambayo imesomwa jana na Waziri husika, kuna kipengele kinaelekeza ule magari yatakayoingizwa yakiwa na zaidi ya miaka 8 (awali ilikuwa 10) toka yametengenezwa yatatakiwa kulipia uchakavu. Nimefanya utafiti kidogo kujua gharama utakayotakiwa kulipa kama unataka kuagiza Nissan X-trail ya mwaka 2007 na ile ya 2003 kama ifuatavyo. Hesabu hizi ni kwa hisani ya mtandao wa Beforward na kikokotozi cha TRA. Fuatana nami:

1) Ya mwaka 2007 Bei Ndogo Kabisa CIF= USD 8361 na Ushuru ni kama USD 2583 Jumla ni kama USD 10,944

2) Ya Mwaka 2001, 2003 Bei ndogo kabisa ni CIF=3197 na ushuru ni USD 3083 Jumla ni USD 6,280

Unapata tofauti ni Kama USD 4664. Kwa tofauti hii waagizaji wengi wa kima cha kawaida wataamua kununua magari chakavu.

Tatizo ni kukurupuka tu kutoa maamuzi. Ajali ni zao la mafunzo hafifu, ulevi, uchovu, miundombinu mibovu nk madereva wenzangu mtakuwa mashahidi.

Karibu tuelimishane zaidi.
 
Kabla sijachangia hebu nipe longterm ya CIF ili nikitoa yangu nijue nasema nini mdau najua wewe ni clearing & forwarding agent.
 
Wapendwa,

The problem ni kuwa Serikali ya CCM inajali kupata fedha kwa ajili ya kufadhili na kuendesha mipango yote halali na haramu. Ni wazi kuwa serikali hii imeshafanya mengi yasiyo halali ikiwemo kuwanyang'anya wananchi haki zao kama za kumiliki maeneo ili tu mwekezaji apishwe (mpaka kwa gharama ya wengine kupoteza maisha). Tumeshaona hata upande wa biashara jinsi wafanyabiashara wakubwa wanavyoongoza kukwepa kodi na kupewa misamaha ya kodi.

Kwa kifupi kinachofanyika siyo kutafuta maendeleo, ni kusaka fedha. kwa hiyo yeyote anayekuja na sababu ya kukusanya fedha, hiyo itapitishwa bila hata utafiti wala ushauri wa kitaalamu. Na kwa hilo tutegemee kila aina ya mazingaombwe na maigizo ya mfano huo mpaka aidha CCm itolewe madarakani, au nchi hii iwe imejaa skrepa kila kona.
 
Back
Top Bottom