Hotuba ya Tundu Lissu bungeni Julai 04, 2012 na hatma ya Muungano

lazima niwe mkweli..mimi nina uwezo wa kutafakari lakini LISU amenipita kidogo
 
Duh....! kilikuwa kitu kweli...

Mh. Lissu, au yeyote anayeweza kuwa na Hotuba hii katika PDF naomba aniwekee tafadhali.

Josam
 
Eti wanasema huu ni upepo tu uatapita, lakini kwa kasi gani, usije ukatunyanyua.
 
"Aidha, Muungano ulidumu mauaji ya viongozi waandamizi na wajumbe wa Baraza la Mapinduzi la kwanza la Jamhuri ya Watu wa Zanzibar kama Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar Abdallah Kassim Hanga"

sidhani kama muungano ulihusika na kifo cha Hanga kama sio kama masuala yaliyokuwa yakiendelea Zanzibar baada ya mapinduzi - mapinduzi si lele mama.
 
Angekuwa mkweli zaidi mh Tundu kama angesema kwamba Muungano uliepusha na kupunguza uhasama miongoni mwa watu wa Zanzibar. Muungano ulifanyika miezi micahache baada ya Mapinduzi wakati ambapo joto kati ya wanaunga mkono mapinduzi na wanayoyapinga lilikuwa bado juu.
 
Ni muhimu haya mambo ya muungano yanayoleta misuguano yakapatiwa ufumbuzi wa kudumu kuliko hii ya kuficha ficha na kufunika matatizo kwani mficha maradhi, kifo humuumbua.
 
Mungu anajua 'muungano ulikuwa mzuri kwa pande zote, tatizo wenzetu waliota ndoto ya mchana wamepata mafuta ktk ardhi yao kabla hawajaanza kuchimba wakaanza kujadili muungano!! Mh atazungumza kwa hoja za maana

.. Hili ndio tatizo la kusoma hitoria kwenye vitabu vya Nyerere nani alikwambia Muungano ulikuwa mzuri, day one Karume kasema Muungano kama koti likikubana unalivua alijua kuna matatizo katika muungano huu, matatizo yote yameletwa na uroho wa madaraka wa Nyerere alijua kuunda serikali tatu kama ilivyotakiwa iwe kwenye mkataba wa Muungano ni gamble kwake naama akiwa rais ya Muungano bila Tanganyika, Rashidi atakuwa na nguvu kuliko yeye na akiwa rais wa Tanganyika na mwengine akawa Rais wa Muungano yeye atakuwa chini, aakumua kuwaingia wowote katika Muungano bila ridhaa ya Zanzibar, maana sisi tulikubali mambi ya ulinzi ili comrade wasituzidi nguvu, mambo ya ndani kwa ajili hiyo hiyo na mambo ya nje kwa kuwa nchi nyingi zililaani mapinduzi yetu, tulifanya hivyo by purpose, nyine Tanganyika mkajifanya smart mkatupa turufu zenu zote chini mkijua sisi hatuna tujichobakiza sasa mnalia.

Mnamlilia nani kwa ujinga wenu, wajinga ndio waliwao, kuipata tanganyika yenu mapaka sisi zanzibar tukubali, vinginevyo hizo ni hekalu za alinacha. mtasema mpaka mtapasuka, hauitowi tanganyika ila mukubali kubeba madeni yote ya Tanzania maana nyinyi ndio muliokopo sio sisi, kama mtalikubali hilo leteni MoU tuone. Vinginevyo pigeni kelele hazitushituwi na hatutoshidwa kulala zanzibar kwetu maana hamna akili watanganyika mna utajiri mmeukalia, na hamtozinduka mpaka mtakapoacha kuaabudu mwenge huko ndiko alikowaroga Nyerere na kuwatoa msukule mkatoka akili nyie, hamtuwezi sisi, angali sisi milioni moja tunawachezesha ngoja mijitu millioni 40 kama ni ukalulu ni nini, mmesoma hamkujua sasa itabidi mjifunze mujuwe.
 
Mimi sioni sababu ya kutumia lugha kali kama hiyo katika kujenga hoja. Naamini walioanzisha Muungano walianzisha kwa dhamira njema tu. Nao kama binaadamu wana mapungufu yao. Wasindeweza kuona vikwazo vyote ambavyo vingeweza kutokea miakaa kadhaa baada ya Muungano. Isitoshe dunia siku zote inabadilika. Yawezekana wakati unaanzishwa muundo wake ulikuwa unafaa kwa wakati huo na kutokana na mabadiliko mbalimbali ya kiuchumi, kisiasa na kijamii unaelekea kuwa nyuma ya mabadiliko. Mhimu hapa ni kila mtu kutoa hoja yake kwa lugha inayomezeka juu ya matatizo ya muungano na kutoa mapendekezo. Hamna hata mmoja kati yetu anaestahili kulaumiwa kwa mapungufu ya Muungano. Wengi kati yetu tumekuta Muungano upo na mazuri na mapungufu yake. Ndio maana wana JF tunajadili na kuweka hadharani mapungufu ili yaonekane katika Mchakato unaoendelea wa kuandika Katiba mpya.

Ni bora kila hoja ikaheshimiwa maana kila zuri lina ubaya wake na kila baya lina uzuri wake
 
Back
Top Bottom