HOTUBA ya Seif Sharrif na Majibu yake kuhusu Maridhiano Zanzibar!

jamanii huyu mtu mbona haeleweki.uchizi unamnyemelea au anaweweseka? alianza kusema hamtambui bwana karume.baadae akabadiri msimamo.sasa kaja na mpya anataka haasimu wa ke aongezewe muda wa kutawala kweli hii inaingia akilini bila kuitilia mashaka akili yake?
 
jamanii huyu mtu mbona haeleweki.uchizi unamnyemelea au anaweweseka? alianza kusema hamtambui bwana karume.baadae akabadiri msimamo.sasa kaja na mpya anataka haasimu wa ke aongezewe muda wa kutawala kweli hii inaingia akilini bila kuitilia mashaka akili yake?​

Wewe ndiyo unaweweseka maana hujui unachoongea au ndiyo wamekutuma uje na gea hiyo kwanza uwe unapiga hodi ka post kwa kwanza tu ndo unakuja na mkwala hivyo.

Jumakidogo
Junior Member
red_left.png
red.png
red_right.png
green_left.png
green.png
green_right.png
Join Date: Thu Jul 2009
Posts: 1
Thanks: 0
Thanked 0 Times in 0 Posts
 
Wewe ndiyo unaweweseka maana hujui unachoongea au ndiyo wamekutuma uje na gea hiyo kwanza uwe unapiga hodi ka post kwa kwanza tu ndo unakuja na mkwala hivyo.

Jumakidogo
Junior Member
red_left.png
red.png
red_right.png
green_left.png
green.png
green_right.png
Join Date: Thu Jul 2009
Posts: 1
Thanks: 0
Thanked 0 Times in 0 Posts
Huo ni usanii wa Kisiasa! na kuna jambo linakuja watu watashangaa! Haiingii akili hata kidogo mwaka jana Karume amelia kama mtoto mdogo Dodoma hataki serikali ya Mseto, leo hii amekaribia kuondoka anaanza uswahiba na huyu nae ambaye amebaki mpinzani kwa jina tu! CUF sujui hawaoni! Huo ni unafiki na ubunafsi wa hali ya juu! Kama ulitaka mwafaka bila shaka hilo lingekuwa agenda no 1 from Day 1 ulipopata madaraka. Kwa sababu za kinafiki na kutaka kujiosha kwa macho ya Watanzania all over the sudden unazaliwa uswahiba ambao hata misingi yake haijulikani imetoka wapi for years they have been talking, bila mafanikio. Halafu haya majaribio ya kutaka kurudi madarakani kwa kutumia agenda ya kutafuta mwafaka, sijui amefanya kazi nzuri tumeyashtukia na tunajua mnachotaka. Dont even think about it! You are another failure! wewe ondoka tu!
 
hali zenu, wajukuu wangu...

kwa takribani muda mrefu sana, nimekuwa natumia nafasi na muda wangu kujibu hoja au kuandika kama sio kutia nguvu katika hoja ambazo mie binafsi nahisi zinanigusa.

kwa takribani muda wa mwezi mmoja sasa, suala la mgongano wa kimawazo juu ya KARUME NA HATIMA YA ZANZIBAR, imekuwa inapamba vichwa vya habari vya huku bara hata visiwani.lakini kwangu mimi hili ni jambo ambalo silijui kwa undani sana.

leo naingia barazani hapa hili kupatiwa maelezo ya kina juu ya nini kinaendelea huko zanzibar......

Miaka mitanu iliyopita kama sio tisa, katika nchi ya zanzibar palitokea mgongano mkubwa sana waa kisiasa. mgogoro ambao , hata bila ya uwoga viongozi walipanda majukwaani wakisema wameporwa matokeo na hata wakati fulani watu walikufa. jambo ambalo lilipelekea jumuiya za kimataifa kushusha wachunguzi wa mambo haya pale zanzibar.

migogoro hii haikuishia hapo tu, iliendelea hata huko pemba ambapo unaambiwa kuna kipindi kama sio hadi sasa, watu ndugu walikuwa hawazikani. hii yote sababu ya CUF na CCM.

leo hii ikiwa imebaki siku chache huyu bwana karume aondoke madarakani, Seif na CUF wanapaza sauti wakiomba huyu bwana mkubwa aongezewe muda wa madaraka.

maswali yangu , mimi
........ni yale maji ya kunywa ya chupa tu aliyokunywa bwana seif sharrif pale ikulu au lipo jambo zaidi la ziada
.......je ni nini hasa ambacho Karume kawafanyia hawa CUF hadi wamshabikie hivi
.......hatua hii ina mahusiano yoyote na kutojiandikisha kwa wana CUF kule pemba
.......kuna mpango wowote mzuri ambao Karume kaahidiwa na Seif, punde akishika madaraka.
.......je ni kweli Karume si mwanachama wa CCM
.......je ni kweli kuwa mama yake Karume anayajua haya?
.......kuna nini kitamu pale ikulu zanzibar hadi kila mtu atake kuongeza muda
.......kuna mtu anaitwa Mansoour Himid, huyu mtu ni nani?
.......kuongezewa muda kuna mahusiano yeyote na mikataba binafsi ya uchimbaji mafuta.
.......kama kuna hilo la mafuta, nn nafasi ya Seif na CUF katika hili?
.......nn hatima ya Muungano wetu?

wajukuu zangu, nahisi kama ninaweza kufa mapema maana maswali haya na muungano wetu, naona kama yanapishana.

HAWA CUF WAMEONA NINI KWA KARUME?

TUJIULIZE,..........Naomba jibu.
 
leo hii ikiwa imebaki siku chache huyu bwana karume aondoke madarakani, Seif na CUF wanapaza sauti wakiomba huyu bwana mkubwa aongezewe muda wa madaraka.
Hii statement inapotosha tuu, hoja ya msingi umejaribu kuiikimbia.Hapa kinachozungumzwa sio kumuongeza muda Karume bali ni kuongeza support kikatiba juu ya serekali ya kitaifa Zanzibar itakayoshirikisha vyama vyote huko visiwani kwa kufuata uwiano wa kura.

Sasa kutokana na kuwa Msekwa na Makamba na puppets wao walikuwa wakizorotesha jitihada zote za miafaka iliyopita.Finally Seif na Karume wameona wapige panga na kupita shortcut kuokoa maisha yetu huko visiwani.Kwetu sisi hawa mabwana wawili kufanya hivyo ni ushujaa mkubwa katika kunusuru na kipigo cha JWTZ kila unapokaribia uchaguzi.

Nafikiria ni ngumu kwa mtu ambae si mzanzibari kufahamu hii situation....

.......kuongezewa muda kuna mahusiano yeyote na mikataba binafsi ya uchimbaji mafuta.

Hichi ndio munacho lilia na kupiga makelele katiba iheshimiwe ili mupate kuja kuiba mafuta yetu. :D
.......nn hatima ya Muungano wetu?
Huo ni woga tuu...lakini hakuna uhusiano wowote baina ya maridhiano na muungano.Lakini tunalikaribisha kwa mikono miwili hili agizo la Butiama lenye kututetea sisi wazanzibari na kutaka kutupa nafasi ya kuamua mambo mazito ya kikatiba...kama alivyosema Chilingati.

Sisi huku Zanzibar tutafurahi sana kama na hili agizo la Butiama, maana halitokuwa tuu ni kuhusiana na GNU bali pia itabidi maswala mazito yote tuletewe wenyewe wananchi tutie baraka zetu.

Mambo hayo mazito aliyokusudia Chilingati ni kutuuliza wazanzibari kama tunataka muungano au hatutaki...na tukisema tunataka basi Butiama itaendelea kutuuliza mfumo gani wa serekali tunaopendelea.

Halafu mwishowe ndio agizo la Butiama litatoa nafasi ya kuuliza GNU :D

Hili agizo la Butiama naona inabidi lienziwe kweli kweli....
 
Sasa kutokana na kuwa Msekwa na Makamba na puppets wao walikuwa wakizorotesha jitihada zote za miafaka iliyopita.Finally Seif na Karume wameona wapige panga na kupita shortcut kuokoa maisha yetu huko visiwani.Kwetu sisi hawa mabwana wawili kufanya hivyo ni ushujaa mkubwa .



Huo ni woga tuu...lakini hakuna uhusiano wowote baina ya maridhiano na muungano.

Sisi huku Zanzibar tutafurahi sana kama na hili agizo la Butiama, maana halitokuwa tuu ni kuhusiana na GNU bali pia itabidi maswala mazito yote tuletewe wenyewe wananchi tutie baraka zetu.

Mambo hayo mazito aliyokusudia Chilingati ni kutuuliza wazanzibari kama tunataka muungano au hatutaki...na tukisema tunataka basi Butiama itaendelea kutuuliza mfumo gani wa serekali tunaopendelea.


Point acknowledged.
 
Labda wazanzibari wamegundua kuna technique ya divide and rule huko visiwani ndo mana wameamua kushikana na pia ni akili ya wazanzibari kwamba hali mbaya waliyonayo imesababishwa na bara,bendera na wimbo wao wameshapata wapeni na mafuta yao, wapeni serikali yao ya umoja wa kitaifa, mbona hizi dhahabu za buzwagi na gesi ya songosongo hamgawani nao?
Shida na seif anaiogopa kuna vidume vinapasha vikikamata hakuna cha muafaka wala maridhiano ni bakora tu na kwa CCm yetu ndivyo itakavyokua
 
Hey Great Thinkers!!!
Nimekua nikisikia kila siku kwenye vyombo vya habari kuwa ''CUF wataka Rais wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Aongezewe muda so Tarehe ya uchaguzi isogezwe mbele.
Could any one just tell me what is the motive behind all this!! hawa CUF watafaidikaje na hili?
 
Hizi sanamu zipo Zenji. Tena unajua zipo wapi???? Zipo ndani ya kanisa la Mkunazini. Ndani ya Misikiti hukuti vituko kama hivi. Sijui kulikuwa na ajenda gani baina ya Maaskofu/Wachungaji na Waengereza?
 
Labda wazanzibari wamegundua kuna technique ya divide and rule huko visiwani ndo mana wameamua kushikana na pia ni akili ya wazanzibari kwamba hali mbaya waliyonayo imesababishwa na bara,bendera na wimbo wao wameshapata wapeni na mafuta yao, wapeni serikali yao ya umoja wa kitaifa, mbona hizi dhahabu za buzwagi na gesi ya songosongo hamgawani nao?
Shida na seif anaiogopa kuna vidume vinapasha vikikamata hakuna cha muafaka wala maridhiano ni bakora tu na kwa CCm yetu ndivyo itakavyokua


Waswahili wanasema fumbo mfumbie mjinga mwerevu hung'amua sumu ya maendeleo zanzibar inasababishwa na Tanganyika na ni kutokana na wivu tangu na kabla ya uhuru.

Tuje katika swala la utumwa mimi nimebahatika kusoma shule ya msingi kote zanzibar na visiwani. Niliwahi kumuuliza mwalimu wangu darasani kuwa kwanini wakati wa biashara ya utumwa waingereza wasiulizwe wameshirikije katika utumwa maana walikuwa wakifanya biashara hiyo pia zanzibar. Pili nikauliza mbona makaburi ya watumwa hayaonekani bali tunaona makaburi ya mauaji ya halaiki (a.k.a Mapinduzi). Tatu mbona maduka (au maeneo ya watumwa) yamo kanisani tu ukitazama pale kanisa la mkunazini, kanisa la anglikan shangani na shule ya tumekuja ambayo waingereza walijenga but sio katika majumba ya hao waarabu waliokuwa wakidaiwa kuwa na biashara ya utumwa. Nilipouliza maswali haya mwalimu wangu (alikuwa jamaa yangu) akanambia nihamie shule niende dar kwasababu naweza kupata matatizo. Kiufupi hii historia ya utumwa zanzibar ni fabricated, untruly, na ina alot queries ndani yake.

Lakini kwanini inakuzwa jibu simple ili kujenga fitna na choko choko zanzibar kwasababu tanganyika walijua kuwa siri ya kuitawala zanzibar ni dividing rule basi watawatawala vizuri. Likewise, historia mbaya huwa haziadisiwi kwasababu zinaweza kuleta matatizo na chuki kwa nchi. Western countries huziita the dark side of the history ndio maana Uingereza na Marekani wana Black month, martin luther king etc ili kupunguza makali ya machungu ya yaliyotokea but katika historia you never hear them (kama hamfahamu tizameni discover channels, history channels etc mtaona). Lakini kwakuwa Tanganyika walifahamu kuwa zanzibar ina mchanganyiko wa watu wengi toka zamani wakaona waipandikize chuki among them ili ivunjike ile trust between them ili iwe rais kuwaongoza.

Niliwahi kusema zamani znz inajiandaa na kiufupi wamejiandaa kikweli labda itumike sasa jeshi kutawala znz yangu macho!!!!
 
MUWAZA (MUSTAKBAL WA ZANZIBAR) UNATOA PONGEZI ZA DHATI KWA:

Rais Amaan Abeid Karume na Maalim Seif Sharif Hamad kwa ujasiri na ushujaa wao uliojitokeza katika kuleta kuungana kwa wazanzibari, kuondosha uhasama, chuki, mifarakano isiokwisha na uadui usio na maana.

Tunawapongeza kwa kutuletea Zanzibar ishara njema inayoleta matumaini ya salama na amani na kuleta matarajio ya siasa za kidemokrasia na kujenga misingi ya maendeleo.

Tunampongeza makamo wa rais wa muungano mh. Ali muhammed shein na Mh. Mohammed Gharib Bilal kwa kuchukua jukumu la kuwahamasisha wana ccm katika kikao maaluum cha NEC Zanzibar.

Tunampongeza kiongozi wa upinzani Mh. Abubakar Khamis Bakari kwa mapendekezo ya kheri aliyoyawakilisha katika baraza la wawakilishi
vile vile tunalipongeza baraza la wawalikilishi zima kwa dhamana, hamasa na hisia za kizanzibari kwa upeo wao wa kuyakubali na kuyashindikiza mabadiliko ya kihistoria yanayolinda mustalbal wa Zanzibar.

Tunawapongeza wazanzibari wote waliojitokeza hadharani na wasiojitokeza ulimwenguni kote kwa kuwa na imani na viongozi wao pamoja na kuwaomba waonyeshe uzanzibari wao wa dhati kwa kusaidia viongozi wao na nchi yao ya zanzibar kwa kuchukua majukumu ya kila aina ndani na nje ya Zanzibar kuleta maendeleo ya kudumu Zanzibar.

Tunawaomba viongozi wakiwemo Rais Amani Abeid Karume, Maalim seif Shariff Hamad, wawakilishi, wabunge wa kizanzibari na wazanzibari wote kwa jumla wasimame kidete na imara kulinda mustakbal wa Zanzibar na kujilinda na fitina na mafatana wanaotaka kuiangamiza Zanzibar.

Zanzibar imeweka historia ya kuigwa afrika na ulimwenguni kote na kuweka mfano wa vipi mizozano ya kisiasa inaweza kutatuliwa kwa salama na amani – haya ni ya kuigwa ulimwenguni kote.

Ya Rabbi Mola wabariki milelele viongozi wema wa Zanzibar, wazanzibari na nchi ya Zanzibar.

KWA NIABA YA MUWAZA
Dr. Yussuf S. Salim
Copenhagen
 
MARIDHIANO NA MUSTAKBALI WA ZANZIBAR

Na Seif Sharif Hamad

UTANGULIZI

Zanzibar inapita katika mojawapo ya vipindi muhimu sana vya historia yake ya kisiasa. Nuru mpya ya matumaini imechomoza kupitia Maridhiano ya Wazanzibari. Hatua hii imekuja kufuatia mkutano na mazungumzo ya kihistoria kati ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dk. Amani Karume, na mimi nikiwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF) huko Ikulu ya Zanzibar , Novemba 5, 2009 yaliyokuwa na lengo la kujenga mustakbali mpya wa siasa Zanzibar .

Mazungumzo hayo yalifuatiwa na hatua ya kijasiri ya CUF ya Novemba 7, 2009 ya kwenda hadharani kutangaza kumtambua Rais Karume na Serikali anayoiongoza na kukubali kushirikiana na kufanya naye kazi pamoja kwa maslahi ya Zanzibar na watu wake.

Pamoja na hatua hiyo kuonekana kuwachanganya wana-CUF pale ilipotangazwa kwao kwa mara ya kwanza, lakini viongozi wa CUF tukiongozwa na Mwenyekiti wa Taifa, Prof. Ibrahim Lipumba, hatukuyumba wala kurudi nyuma na tukaamua kufanya kazi kubwa ya kuwaelimisha wanachama kupitia mikutano ya hadhara na vikao vya ndani hadi kufikia hatua ya sasa ambapo wana-CUF takriban wote sasa wanakubaliana na hatua zinazochukuliwa. Ushiriki mkubwa na wa aina yake wa wana-CUF katika kilele cha sherehe za miaka 46 ya Mapinduzi ya Januari 12, 1964 zilizofanyika kisiwani Pemba ni ushahidi tosha wa hali hiyo ninayoieleza. Nataka nitumie fursa hii kuwashukurukwa dhati wana-CUF wote kwa kutuelewa na kutuunga mkono katika hatua zetu hizi tunazozichukua.

Kwa upande wake, Rais Amani Karume naye amehutubia mkutano wa hadhara wa CCM Novemba 22, 2009 na kutoa hotuba iliyotoa mwelekeo mpya wa mahusiano ya kisiasa hapa Zanzibar . Pamoja na mambo mengine, alitangaza kwamba milango iko wazi kuweza kuzungumza jambo lolote lenye maslahi na Zanzibar na watu wake. Hotuba zake za hivi karibuni alipokuwa katika ziara rasmi kisiwani Pemba na baadaye katika matukio mbali mbali ya Sherehe za Mapinduzi zimeendelea kusisitiza azma yake ya kujenga Zanzibar mpya yenye umoja, maelewano, mshikamano, amani, utulivu na maendeleo kwa watu wake wote.

Nafurahi kuona hotuba zetu, mimi na Rais Karume, tukiwa ndiyo viongozi wakuu wa kisiasa hapa Zanzibar zimesaidia kuyazamisha maridhiano haya katika nyoyo za wafuasi wa vyama vya CCM na CUF na pia katika nyoyo za Wazanzibari wote. Zanzibar inashuhudia hali ya matumaini ambayo haijapata kuonekana kwa miaka mingi.

Kiwango cha kuaminiana kimekuwa cha juu kabisa na hatua ya karibuni ya Rais Amani Karume kutangaza kuwateua viongozi wawili waandamizi wa CUF, Mhe. Juma Duni Haji na Mhe. Nassor Ahmed Mazrui, kuwa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi imepokelewa kwa furaha kubwa kuwa ni hatua sahihi katika kuimarisha maridhiano yaliyofikiwa.

Umuhimu wa hatua tunazochukua umeonekana kutokana na kauli mbali mbali za viongozi wa ndani na hata nje ya nchi, taasisi zisizo za kiserikali na jumuiya mbali mbali za kiraia, wasomi, viongozi wa dini na wengine wengi za kupongeza hatua hizo. Nachukua fursa hii kuwashukuru wote hao kwa kutuunga mkono katika hili. Lakini na mimi pia naungana na Rais Karume katika kumpa shukrani nyingi na za pekee Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, kwa salamu zake za pongezi kwetu ambazo siyo tu zilibeba ujumbe mzito kwa wale wote wanaobeza hatua tuliyochukua lakini pia zilikuwa zimeambatana na ahadi yake kwamba anatuunga mkono kwa hatua tunazochukua na kwamba tutegemee kila msaada tunaouhitajia kufanikisha yale tuliyoyakusudia. Binafsi nimefarijika sana na ahadi yake hiyo kwani hapana shaka yoyote kwamba msaada wake unahitajika sana .

Ukiacha salamu hizo za pongezi, Wazanzibari wengi wameifurahia hatua tuliyochukua na wana matumaini makubwa kuwa itafungua milango mikubwa zaidi ya mashirikiano. Bila shaka wapo pia vidudu mtu wachache ambao wanafanya kila juhudi kutaka kuturudisha kule kule tulikotoka kwa sababu tu ya kujali maslahi yao . Natoa wito kwa wananchi wote kwamba wawapuuze na nawahakikishia kwamba mimi na Rais Karume tumekubaliana kuwa hakuna kurudi nyuma katika hatua tuliyoianzisha. Ni nia yetu kuona kuwa tunaitumia fursa hii kuirudisha Zanzibar katika nafasi yake iliyokuwa nayo huko nyuma ambayo ilipotea kutokana na kuendekeza kwetu tofauti zetu badala ya yale yanayotuunganisha. Time has come to make Zanzibar great and proud of herself again.

ZANZIBAR ILIKOTOKA
“Ipigwapo zumari Zanzibar , hucheza walioko katika Maziwa Makuu.” Huu ni usemi wa kihistoria unaoeleza nafasi kubwa viliyokuwa nayo visiwa vyetu katika kusarifu na kushawishi mwenendo wa mambo katika eneo la Afrika Mashariki na Kati. Hizo zilikuwa zama za Zanzibar kuvuma kutokea upande huu wa magharibi ya Bahari ya Hindi kuelekea ndani ya Bara la Afrika hadi mashariki ya Congo na pia kuelekea sehemu za kaskazini kwenda Bara Arabu, Bara Hindi na Mashariki ya Mbali na pia kupenya hadi Ulaya na Marekani.

Udogo wa visiwa vya Zanzibar haulingani na umuhimu wake katika historia ya Afrika Mashariki, Bahari ya Hindi, Arabuni hadi Mashariki ya Mbali. Umuhimu huo ulitokana na maendeleo makubwa yaliyokuwa yamepigwa Zanzibar katika nyanja mbali mbali za maisha. Na hali hiyo haikuja kwa bahati mbaya bali ilitokana na ustaarabu uliojengeka karne nyingi sana zilizopita. Inatambulika, kwa mfano, kwamba Zanzibar , au Dola ya Zinj, ndiyo dola kongwe kuliko zote katika eneo lote la Afrika kusini ya jangwa la Sahara .

Watu wa visiwa vya Zanzibar walitoka sehemu mbali mbali: Afrika ya Mashariki na Kati , Iran , Arabuni, Bara Hindi, Ngazija, Mashariki ya Mbali, Ulaya n.k.

Zanzibar inaelezwa kutajwa kwa majina tofauti tangu miaka 500 kabla ya kuzaliwa Nabii Issa (a..s.). Uvumbuzi wa karibuni wa mapango ya watu wa kale katika ukanda wa Mashariki Kusini wa kisiwa cha Unguja unaonesha kuwepo kwa makaazi ya watu tokea zama za mawe ziitwazo kama ‘Stone Age’. Katika kitabu maarufu chenye kumbukumbu za wasafiri wa kale wa Ugiriki waliotembelea mwambao wa Afrika Mashariki kiitwacho Periplus of the Erythrean Sea kilichoandikwa mwaka 100 A.D. (kabla ya Nabii Issa), Zanzibar imetajwa kwa jina la ‘Menouthias’ ikiwa tayari ni nchi yenye watu mchanganyiko tena walio na ustaarabu wakiwa wanavaa nguo za hariri. Huko Oxford, imeonekana ramani ya wasafiri wa Kiarabu iliyotayarishwa Karne ya 11 ambayo inaonesha visiwa vya Zanzibar na mji mkuu wake ukiwa Unguja Ukuu.

Kwa muda mrefu, Zanzibar ilikuwa imegawanyika katika falme mbali mbali, mpaka ilipofika mwaka 1500 ulipoanzishwa utawala wa Mwinyi Mkuu akiwa ndiyo alama ya utawala wa kienyeji Visiwani. Mwinyi Mkuu wa mwisho, Ahmed bin Muhammed bin Hassan el-Alawy alifariki 1873. Mwaka 1503 Wareno waliivamia Zanzibar kupitia Unguja Ukuu na wakaitawala kwa muda mrefu wakifanya vitimbi vya kila aina. Waomani kwa maombi ya wenyeji walikuja katika Dola ya Zinj na kupambana na Wareno na hatimaye wakafanikiwa kuwatimua. Sayyid Said bin Sultan alifika Zanzibar mwaka 1828, na kutokana na kuvutiwa na mandhari yake mwaka 1832 akaifanya Zanzibar kuwa makao makuu ya utawala wake badala ya Muscat .

Katika kipindi hiki Zanzibar iliweza kujitambulisha na kutambuliwa kama Dola huru katika ulimwengu. Zanzibar ikawa kituo muhimu cha kisiasa, kiuchumi na kibiashara katika Afrika Mashariki na Bahari ya Hindi.. Kutokana na umuhimu wake, Madola makubwa yalifungua Ofisi za Kibalozi mjini Zanzibar : Marekani (1837), Uingereza (1841), Ufaransa (1844), na baada ya hapo Ureno, Utaliana, Ubelgiji na Ujarumani zikafuata.

Madola ya Ulaya yalipoanza njama za kinyang’anyiro cha Afrika kwa lengo la kuigawanya kuwa katika makoloni yao , Zanzibar iligombaniwa baina ya Waingereza na Wajarumani. Baada ya vuta nikuvute, mwaka 1890 iliwekwa chini ya Himaya ya Kiingereza (Protectorate) katika Mkataba uliotiwa saini kati ya Mfalme wa Kiingereza na Sayyid Ali bin Said na kwa kutambua hadhi tofauti ya Zanzibar , masuala yake yalikuwa yakiendeshwa kupitia Wizara ya Mambo ya Nje (Foreign Office) ya Uingereza. Mwaka 1913, masuala ya utawala wa Zanzibar yalihamishwa kutoka Ofisi ya Mambo ya Nje (Foreign Office) na kupelekwa rasmi Ofisi ya Makoloni (Colonial Office).

Kidogo kidogo, harakati za kuanzisha mfumo wa Utawala wa sura ya kikoloni zikaanza pale ilipotungwa Sheria (Order-in-Council) ya 1926 iliyoanzisha Baraza la Kutunga Sheria (LegCo) na Baraza la Utawala (ExCo). Ni katika kipindi hicho ambapo mfumo wa uwakilishi wa kikabila ulianzishwa ukiwaweka kando Waafrika na Washirazi na hivyo kupanda fitina za mifarakano chini ya sera ya Waingereza ya ‘wagawe uwatawale’ (divide and rule). Ilichukua miaka 20, hadi mwaka 1946, ambapo Mshirazi wa kwanza, Sheikh Ameir Tajo, aliteuliwa kuingia katika Baraza la Kutunga Sheria akifuatiwa na mwenzake, Sheikh Ali Shariff Mussa, aliyeteuliwa mwaka 1948.

Miaka ya 50 ilishuhudia harakati za kudai uhuru kwa kuundwa vyama vya ukombozi: Zanzibar Nationalist Party (ZNP) kilichoasisiwa 1955 na Afro Shirazi Party (ASP) kilichoundwa 1957. Katika kipindi cha miaka saba ya mchuano mkali wa nani anafaa kukabidhiwa Uhuru wa Zanzibar, kulifanyika chaguzi nne ambazo ni Julai 1957, Januari 1961, Juni 1961 na Julai 1963. Chaguzi hizo zilishindwa kuwaweka pamoja Wazanzibari na badala yake zikawa chachu ya kugawika kwa jamii kati ya mapande mawili yenye nguvu takriban sawa sawa. Hali ikazidi kukorogeka pale vyama hivyo vikuu navyo vilipopasuka ambapo Afro Shirazi Party ilimeguka na kupelekea kuanzishwa Zanzibar and Pemba Peoples Party (ZPPP) mwaka 1959 na Zanzibar Nationalist Party nayo ikapasuka na kupelekea kuanzishwa Umma Party mwaka 1963. Zanzibar ikawa inaelekea katika Uhuru ikiwa ni jamii iliyogawanyika.

Uingereza ilikabidhi Uhuru kwa Zanzibar tarehe 10 Desemba 1963 chini ya Sultani na Serikali ya ZNP/ZPPP. ASP hawakuubali Uhuru huo na tarehe 12 Januari, 1964 ilifanya Mapinduzi na Zanzibar ikatangazwa kuwa Jamhuri.

Haya niliyoyaeleza ni mukhtasari tu wa historia ya Zanzibar unaoonesha vipindi mbali mbali ambavyo nchi ilipitia katika ujenzi wa Taifa.

Lakini pamoja na misukosuko ya kisiasa tuliyokumbana nayo, ni vyema ikaeleweka na hususan kwa vijana wa leo kwamba Zanzibar hii imeweka rekodi mbali mbali za kujivunia na kutoa mchango mkubwa katika maendeleo ya binadamu na ustaarabu. Ni vijana wangapi leo hii wanaojua kwamba mji wa Zanzibar ulikuwa wa mwanzo kuwasha taa za umeme za barabarani na mitaani (zikiitwa taa za stimu) kabla ya miji ya London na New York ? Balozi wa Marekani aliyemaliza muda wake mwaka jana, Bwana Mark Green, wakati akitoa hotuba yake ya kuaga, alisema meli za Marekani zilikuwa zikitia nanga katika bandari ya Zanzibar kuja kununua mafuta ya nyangumi kwa ajili ya kwenda kuwashia taa zao za barabarani wakati Zanzibar ikiwa inatumia umeme. Sayyid Said bin Sultan alipeleka Balozi wa kwanza wa Zanzibar nchini Marekani, Ahmed bin Nu’man mwaka 1840.

Zanzibar ilikuwa nchi ya kwanza kuwa na sarafu yake katika Afrika kusini ya Sahara zilizoanzishwa wakati wa Tawala za Kishirazi ambazo zilichimbuliwa katika maeneo ya Unguja Ukuu, Mkumbuu na Mtambwe Mkuu katika miaka ya tisini. Baadaye katika mwaka 1908, ikawa tena nchi ya kwanza katika eneo hili kuanzisha sarafu za noti zake wenyewe (rupia za Zanzibar ) ambazo ziliendelea kutumika hadi 1936 ilipoanzishwa sarafu ya shilingi ya Afrika Mashariki chini ya Bodi ya Sarafu ya Afrika Mashariki.

Zanzibar ilikuwa nchi ya kwanza katika eneo hili kufunga mikataba ya kibiashara na nchi za Marekani, Uingereza, Ufaransa na Jiji la Hamburg (kabla ya kuanzishwa kwa Shirikisho la Ujarumani). Zama hizo, nchi yetu pia ilikuwa na mahusiano ya kibiashara na nchi za Arabuni , India , China , Malaysia na visiwa vya Java na Sumatra (ambavyo sasa ni Indonesia ) na kupitia mahusiano hayo, iliweza kujenga utamaduni na ustaarabu wa kipekee.

Wakati Zanzibar inapata uhuru wake, ilikuwa nchi ya pili katika Afrika kwa ukubwa wa wastani wa pato la wananchi wake, na ya tatu kwa kiwango cha elimu na pia ikiwa na taasisi 17 za fedha zikiwemo benki na kampuni za bima.

Haya yalikuwa katika kipindi cha kabla ya Mapinduzi ya 1964 lakini hata baada ya Mapinduzi, nafasi ya Zanzibar katika Afrika haikupotea. Ilikuwa nchi ya kwanza katika Afrika kusini ya Jangwa la Sahara kuanzisha televisheni ya rangi na pia ikitoa huduma zote muhimu za jamii bure kwa wananchi wake. Ilifikia wakati ambapo Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar , Marehemu Mzee Abeid Amani Karume, alitangaza hadharani kwamba hakukuwa na nchi yoyote iliyokuwa ikiidai Zanzibar bali Zanzibar ndiyo iliyokuwa ikizidai baadhi ya nchi malimbikizo ya madeni yanayotokana na uuzaji wa karafuu zake.

Nimeamua kuchukua muda mrefu kidogo kuyadondoa haya ili tujue wapi nchi yetu ilikotoka na kwa vipi migogoro ya kisiasa iliyokuja kuvigubika visiwa vyetu na wananchi wake ilikuja kutuathiri vibaya na kuyapoteza mengi kati ya haya.


CHAGUZI: SUMU YA UMOJA WA WAZANZIBARI

Sina haja ya kurejea historia ya chaguzi mbali mbali zilizofanyika hapa Zanzibar kabla na baada ya Mapinduzi ili kuthibitisha hoja yangu kwamba chaguzi zimekuwa ndiyo sumu ya umoja wa Wazanzibari.

Ni bahati mbaya sana kwamba maendeleo ya kisiasa ya harakati za kudai uhuru wa Zanzibar yaliyoshika kasi kuanzia uchaguzi mkuu wa mwanzo visiwani wa 1957 yaliibua hisia kali zinazotokana na matukio ya vipindi mbali mbali vya historia ambavyo viliambatana na mapambano ya kitabaka na hivyo kupelekea siasa za wakati huo kugubikwa na wimbi la chuki, hasama na kutoaminiana lililokuwa limejikita kwa miongo kadhaa. Vyama vya siasa vilipokuja kuundwa havikuweza kukwepa athari hii na matokeo yake yakawa ni mapambano ya vuta nikuvute ambayo yalipelekea vurugu na fujo zilizoambatana na roho za watu kupotea. Kila kitu katika maisha ya Mzanzibari kikawa ni siasa. Shughuli zote za maisha ya kila siku zikawa zinafanywa kwa misingi ya vyama vya siasa. Jamii ya Zanzibar ikawa imegawanyika kati kati.

Bila shaka mbali na matukio hayo ya kihistoria, pia kulikuwa na athari mbaya za baadhi ya nchi jirani na za mbali ambazo zilikuwa na khofu kubwa na umaarufu wa Zanzibar , nchi ambazo ziliamua kujipenyeza katika siasa zetu na kuchochea na hata kuikoleza mifarakano iliyokuwepo.

Kabla ya Mapinduzi, chaguzi zikitegemea wingi wa viti ili kupata mshindi wa kuunda serikali. Wingi wa kura haukuwa kigezo cha ushindi. Pamoja na kwamba utaratibu huu ulilalamikiwa na ASP kwa kule kupata kwake viti vichache wakati ikiwa na kura nyingi, wingi huo bado ulionesha kwa wastani mgawanyiko wa takriban nusu kwa nusu ya ushindi wa vyama vya wakati huo.

Katika mtiririko wa historia ya kisiasa ya Zanzibar , kielelezo kikubwa cha ukosefu wa kuaminiana kinaonekana katika uendeshaji wa uchaguzi na matokeo yake. Kama nilivyoeleza kabla, Zanzibar ilifanya chaguzi nne kabla ya Mapinduzi ya 1964 ambazo ni zile za Julai 1957, Januari 1961, Juni 1961 na Julai 1963 na imeshafanya chaguzi tatu tokea mfumo wa vyama vingi uliporudishwa yaani 1995, 2000 na 2005.

Katika chaguzi hizo zote zilizowahi kufanyika Zanzibar , ukiacha uchaguzi wa mwanzo wa 1957, hakujawahi kutokea uchaguzi wowote ambao washiriki wake waliridhika kikamilifu na uendeshaji wake na wakayapokea kwa moyo mkunjufu matokeo yake. ASP ililalamikia uendeshaji na matokeo ya chaguzi za Januari 1961, Juni 1961 na Julai 1963 na katika kipindi hiki cha kurejeshwa kwa mfumo wa vyama vingi tokea mwaka 1992, CUF imelalamikia uendeshaji na matokeo ya chaguzi za 1995, 2000 na 2005. Kikubwa kinachokosekana ni imani kwa taasisi zinazoendesha na kusimamia chaguzi.

Ikiwa tunakubaliana na ukweli huu, ni wazi kwamba bila ya kushughulikia kiini hiki cha migogoro isiyokwisha katika siasa zetu basi ufumbuzi wa dhati na wa kudumu wa migogoro ya kisiasa hautapatikana.

Naamini kwa dhati kabisa njia mojawapo ya kujengeana imani kati ya kambi mbili kuu za kisiasa visiwani Zanzibar ni kuzifanya kambi hizo zifanye kazi kwa pamoja katika uendeshaji wa nchi.

Tafakuri ya kina ya hali ya mambo inavyokuwa wakati wa uchaguzi na pia dalili za kheri zilizooneshwa na Rais Amani Abeid Karume za kutaka kujenga mustakbali mpya wa kisiasa Zanzibar zilitufanya tuone haja ya kushirikiana naye ili kuwaunganisha Wazanzibari wawe kitu kimoja huku tukiamini kwamba katika umoja, tutaweza kuyafikia yale makubwa ambayo tumeshindwa kuyafikia kwa kule kufarikiana kwetu.


MARIDHIANO: FURSA ZILIZOKO MBELE YETU

Mmojawapo wa Marais wa Marekani anayeheshimika sana katika nchi yake na duniani kwa jumla, Abraham Lincoln, aliwahi kusema kuwa ‘A house divided against itself cannot stand’ yaani ‘Nyumba iliyogawanyika haiwezi kusimama’. Haya ni maneno yenye hekima kubwa sana . Ni wazi kwamba Zanzibar imepiga hatua kubwa za maendeleo katika sekta mbali mbali lakini ni jambo lisiloweza kupingika kwamba kama tutaendeleza umoja na mshikamano tunaouonesha hivi sasa na kufikia hatua ya kufanya kazi pamoja basi kuna faida na fursa nyingi na kubwa sana zinazoweza kutumiwa vyema kwa ajili ya kuiendeleza mbele zaidi nchi yetu na watu wake. Miongoni mwa faida za wazi za Maridhiano ni pamoja na:

1. Kisiasa: Kuondosha siasa za utengano, chuki, ubaguzi, uhasama, ugomvi na visasi miongoni mwa wananchi wetu na kuleta siasa za umoja, maelewano na mashirikiano.

2. Kiusalama: Kuondoa khofu na wasiwasi kwa kufuta viashiria vinavyoweza kuwa chanzo cha fujo na ghasia na ambavyo vingeweza kutumiwa hata na maadui wa Tanzania kuhatarisha usalama wetu na badala yake kuleta hali ya amani na usalama ambayo inavifanya hata vyombo vyetu vya ulinzi na usalama kufanya kazi zao katika hali ya utulivu na ushirikiano na wananchi wote.

3. Kiuchumi: Kuondoa hali iliyokuwepo ya sehemu ya wananchi kujiona hawashirikishwi au hawapaswi kushiriki katika harakati za ujenzi wa nchi na kuwaleta pamoja wananchi wote ili kwa pamoja tushiriki katika ujenzi wa Zanzibar mpya.

4. Kijamii: Kuondoa hali ya utengano na kutoaminiana miongoni mwa wafuasi wa vyama tofauti vya siasa na kuwafanya wapendane na washirikiane katika shughuli zote za kijamii wakijua kuwa wote ni wananchi wa nchi moja.

Tukizitumia vyema faida hizo zilizoletwa na maridhiano, tutaweza pia kuzitumia vizuri fursa zilizopo mbele yetu ili kuyabadili maisha ya watu wetu. Binafsi naamini kuwa sasa ile ndoto yetu ya muda mrefu ya kuifanya Zanzibar kuwa ni Hong Kong ya Afrika Mashariki itaweza kutimia ndani ya muda mfupi kabisa. Naamini Wazanzibari wote sasa watakunjua nyoyo zao na kila mmoja atapigana kikumbo na mwenzake katika kuona anatoa mchango mkubwa zaidi wa kuikwamua Zanzibar katika umasikini ambao hauna sababu ya kuwepo. Ubunifu na ari ya kutenda ni sehemu muhimu ya utamaduni wa Mzanzibari.

Zanzibar ina utajiri mkubwa wa watu wake wenye vipaji na nafasi kubwa kubwa katika kila pembe ya dunia. Hawa tukiwatumia vyema na kuwapa fursa wanaweza kutoa mchango mkubwa kwa kushirikiana na Wazanzibari wenzao walio ndani kuijenga upya Zanzibar .

Tukijituma na kujitutumua itakiwavyo, Zanzibar inaweza kurudia nafasi yake ya kuwa kituo kikuu cha biashara na harakati za uchumi katika Afrika Mashariki na Bahari ya Hindi. Zanzibar ina nafasi ya kuwa kituo kikuu cha huduma katika eneo hili. Tunataka kuona Uwanja wa Ndege na Bandari ya Zanzibar zinakuwa tena mlango wa kuingilia na kutokea Afrika Mashariki. Tunataka na tunapaswa kuona ndege za mashirika ya kimataifa zikitua na kuruka kutokea Zanzibar na pia meli zikitia nanga na kung’oa kupitia Zanzibar . Tunaweza kuvutia wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kuja kuwekeza Zanzibar kwa kuanzisha viwanda ambavyo vitatoa ajira kwa vijana wetu na pia kusaidia kuifanya Zanzibar izalishe na kuuza nje bidhaa. Tukizitumia vyema fursa zilizopo Zanzibar itakuwa johari na siyo tena jeraha katika Afrika. Vijana wetu wasio na ajira watapata ajira zenye kipato cha kuwatosha wao na familia zao. Mababu zetu waliweza huko nyuma na sisi tunaweza tena ikiwa tutaikumbatia fursa ya maridhiano tuliyo nayo. Tusiruhusu kidudu mtu yeyote akaingia kati kuturudisha kule tulikotoka.


MARIDHIANO NA CHANGAMOTO ZAKE

Wakati tukizungumzia faida na fursa hizo, tuna pia changamoto kadhaa zinazoyakabili maridhiano haya. Miongoni mwa changamoto hizo ni pamoja na:

1. Matumaini makubwa yaliyojengwa na Wazanzibari bila ya kujali vyama vyao wakiamini kwamba hatua ya viongozi wawili wakuu wa kisiasa kukutana na kukubaliana kuzika tofauti zao itapelekea mabadiliko makubwa katika maisha yao na ujenzi wa mustakbali mpya wa nchi yao .

2. Viongozi wabinafsi kutoka pande zote mbili wanaojali maslahi yao zaidi kuliko maslahi ya nchi na watu wake ambao wameanza kufanya fitina zenye lengo la kuyavuruga mafanikio yaliyopatikana.

3. Muda mfupi uliopo kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu ujao ambapo Maridhiano yanapaswa yawe yamejengewa msingi wa kuhakikisha kuwa yanaimarika na kuendelezwa..

Binafsi nimekuwa nikitafakari sana changamoto hizi na naamini tunapaswa kuzitafakari na kuzijadili kwa lengo la kuona tunazikabili vipi. Ni maoni yangu kuwa tukifanya haraka ya kukimbilia uchaguzi ambao nilishaeleza hapo awali kwamba umekuwa ndiyo chanzo cha kuvurugika kwa umoja wetu, kuna hatari ya kuyapoteza yote niliyoyaeleza.. Hatuwezi kukwepa uchaguzi maana ndiyo njia ya kidemokrasia ya kuwapata viongozi wetu lakini tumeshafanya chaguzi saba za vyama vingi Zanzibar , nne kabla ya Mapinduzi na tatu tokea 1992, na zote zimeshindwa kutupa umoja. Kwa Zanzibar na katika kipindi hiki, maridhiano ni muhimu zaidi kuliko uchaguzi. Tutapaswa kwenda katika uchaguzi lakini naamini tutakuwa na uchaguzi mzuri zaidi baada ya kufanikiwa kujenga msingi madhubuti wa maridhiano.

Hatuwezi kukwepa ukweli kwamba wapo watu wanaokodolea macho fursa ya kutaka kuchukua madaraka ya juu ya Zanzibar , yaani nafasi ya Urais na ambao hawayapendi maridhiano. Miongoni mwao wako wanaotumia vyombo vya habari kukuza habari za kuleta chokochoko na kuzibana taarifa zenye mtazamo wa umoja. Wako pia waliotuma ujumbe kwenda Tanzania Bara kueneza uzushi kwamba lengo la maridhiano haya ni kuvunja Muungano. Watu wa aina hii hawawezi kuisaidia Zanzibar na kwa hakika ni maadui wa umoja wa Wazanzibari.

Kwa msingi huo basi, na baada ya kutafakari, mimi binafsi naungana na wale wanaotoa wito wa kuchukuliwa hatua ya kusogeza mbele kidogo uchaguzi mkuu wa Zanzibar wa mwaka huu kwa kipindi cha kati ya mwaka mmoja au miaka miwili ili kutoa nafasi kwa Rais Amani Karume kuchukua hatua zaidi za kukamilisha kazi njema aliyoianza. Naelewa mwenyewe juzi katika hotuba yake ya kilele cha sherehe za Mapinduzi amesema kwamba anakamilisha kipindi chake na Katiba ya Zanzibar hairuhusu kipindi cha tatu. Nakubaliana naye na sipendekezi kuondolewa kwa ukomo wa vipindi viwili kwa mtu anayeshikilia madaraka ya Urais wa Zanzibar . Ila namuomba sana akubaliane na matakwa ya Wazanzibari walio wengi kama yalivyokwisha oneshwa kupitia taarifa na kauli mbali mbali kwamba kipindi chake cha pili tukiongeze muda kidogo ili tusiipoteze fursa ya kihistoria ambayo ameianzisha yeye.

Natoa wito kwa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wa pande zote mbili, Serikali na Upinzani, kulitafakari hili na kutupa Wazanzibari kile tunachokitaka. Kwa upande mwengine, nawaomba Wazanzibari tuungane pamoja kumtaka Rais Amani Karume aweke upande dhamira yake ambayo najua anaiamini sana ya kuondoka madarakani mwaka huu na badala yake akubaliane nasi juu ya haja ya kuendelea kuubeba mzigo huu tunaotaka kumtwisha na atuvushe pale ambapo waliomtangulia walishindwa kutuvusha.

Ahsanteni sana.


_______________________________
Mada hii iliwasilishwa katika Kongamano la Kitaifa kujadili Maridhiano na Mustakbali wa Zanzibar tarehe 14 Januari, 2010 katika Ukumbi wa Salama wa Hoteli ya Bwawani, Zanzibar na Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF).



Updates: # 1

MAJIBU KWA HOTUBA YA MAALIM SEIF SHARRIF
Gazeti la Raia Mwema na Lula Wa Nzela

LIMEFANYIKA jaribio dhaifu la hadaa ya kisiasa; jaribio ambalo maelfu ya Wazanzibari wameliamini na kulikubali na bila ya kujali itikadi zao na mirengo yao ya kisiasa, wamelikumbatia kama ukweli na kuandamana kuliunga mkono.

Jaribio hilo ni lile la kupotosha historia ya Zanzibar ili kujipa alama bora za kisiasa. Jaribio hilo limefanywa na Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Seif Sharrif Hamad katika hotuba yake ya kuelezea juu ya “maridhiano na mustakabali wa Zanzibar”.

hamad_1.jpg


Seif Sharrif Hamad

Kwa mtu yeyote aliyesoma hotuba hiyo ya Maalim Seif, ukweli mmoja unajionyesha wazi kama mwili wa mbuni aliyejificha kichwa chake mchangani, na kama mwangaza wa radi, hotuba hiyo imefunua ulaghai wa kisiasa ambao mtu makini anaweza kuuona toka mbali na kuukwepa.
Nasikitika wananchi wa Zanzibar katika kile kinachodhaniwa kuwa ni umoja wao, wamekumbatia historia hii mpya ya Zanzibar; historia ambayo kiukweli ni mpya!

Historia isiyo na doa ya Zanzibar

Kitu cha kwanza ambacho tunakiona katika historia hii mpya ya Zanzibar kwa mujibu wa Maalim Seif, ni historia isiyo na “doa” ya Zanzibar. Katika historia yake, Maalim Seif anaielezea Zanzibar katika mwanga wa uzuri wa paradiso. Anadai kuwa Zanzibar, licha ya udogo wake kama kisiwa, ilikuwa na umuhimu mkubwa katika eneo la Afrika ya Mashariki, Uarabuni, Bahari ya Hindi na Mashariki ya Mbali. Anadai kuwa umuhimu huo “ulitokana na maendeleo makubwa yaliyokuwa yamepigwa Zanzibar katika nyanja mbali mbali za maisha.”

Katika ‘maendeleo haya’ utumwa hautajwi wala kuhusishwa! (nitaliangalia hili mbele zaidi kwa wakati huu yatosha kuliweka mawazoni kama utumwa ni sehemu ya maendeleo ambayo Maalim Seif anaisifia Zanzibar!).

Mojawapo ya vitu vingine vya kihistoria ambavyo Maalim Seif amevionyesha katika kutangaza utukufu wa Zanzibar ni madai kuwa “Zanzibar inaelezwa kutajwa kwa majina tofauti tangu miaka 500 kabla ya kuzaliwa Nabii Issa (Yesu Kristo). Uvumbuzi wa karibuni wa mapango ya watu wa kale katika ukanda wa Mashariki Kusini mwa kisiwa cha Unguja unaonyesha kuwepo kwa makazi ya watu tokea zama za mawe ziitwazo ‘Stone Age’.

Katika kitabu maarufu chenye kumbukumbu za wasafiri wa kale wa Ugiriki waliotembelea mwambao wa Afrika Mashariki kiitwacho Periplus of the Erythrean Sea, kilichoandikwa mwaka 100 A.D. (kabla ya Nabii Issa), Zanzibar imetajwa kwa jina la ‘Menouthias’ ikiwa tayari ni nchi yenye watu mchanganyiko tena walio na ustaarabu wakiwa wanavaa nguo za hariri.”

Sasa alivyozungumza kwa uhakika ni kana kwamba wasomi wote duniani wanatambua kuwa “menouthias” ndiyo Zanzibar! Bila ya shaka Wazanzibari waliomsikia na kumsoma hivyo walifurahia mioyoni mwao kuwa kweli Zanzibar inatajwa katika maandishi ya kale.

Sitoshangaa kama watu wa Bara ambao hawajui historia yao waliinamisha vichwa vyao kwa sababu hawajui kama eneo lao linatajwa mahali popote au historia yao ndiyo imeanza mwaka 1884 au wanafikiria Bagamoyo ndiyo sehemu ya kale zaidi!

Kama Maalim Seif angependa kuwaambia ukweli wa Zanzibar juu ya miji ya kale na jamii za kale zilizowahi kutajwa kwenye maandishi ya kale, angewaambia watu wake juu ya mji wa kale wa Rhapta! Najua wengine mnajiuliza “ze what?”!

Katika kitabu hicho hicho cha maelezo ya safari za majini za kale katika bahari ya Hindi, kunatajwa vile vile mji wa Rhapta ambao tunaambiwa ulikuwa ni mji pwani ya Azania umbali wa usafiri wa kama siku mbili toka visiwa vya Menouthias.

Mmoja wa wataalamu wetu wa mambo ya kale Prof. Felix Chami anaweza kulielezea hili kwa kina kuwa siyo Zanzibar peke yake ambayo ina historia ya kale na kuwa watu wake walikuwa wakiishi katika jamii na kufanya biashara vizuri tu.

Ujio wa utawala wa Sultani

Katika historia yake hii mpya ya Zanzibar, Maalim Seif anadai kuwa “Mwaka 1503 Wareno waliivamia Zanzibar kupitia Unguja Ukuu na wakaitawala kwa muda mrefu wakifanya vitimbi vya kila aina. Waomani, kwa maombi ya wenyeji, walikuja katika Dola ya Zinj na kupambana na Wareno na hatimaye wakafanikiwa kuwatimua.” Katika hili tunaona mambo mawili yanayotajwa kwanza ni uvamizi wa Wareno (ambao kwa yeyote aneyejua historia haukukoma kwa visiwa hivyo tu) na pili “maombi ya wenyeji kwa Waoman”.

Kwamba Wareno walikuwa na vitimbi ni maneno machache; kwani historia yao inajulikana hadi Mombasa na Lamu. Tunapoambiwa kuwa wenyeji waliomba Oman ije kuwasaidia kuwaondoa Wareno, hatuambiwi ni wenyeji gani hao? Lakini wakati huo huo ni lazima tukumbuke kuwa utumwa ulikuwepo!

Yawezekana wenyeji waliotaka Oman kuja kuwaondoa Wareno walikuwa ni watumwa? Je watumwa walifaidika vipi na ujio wa Wa-Oman?

Balozi za kigeni huko Zanzibar

Maalim Seif anatuelezea katika hii historia mpya ya Zanzibar kuwa “Katika kipindi hiki Zanzibar iliweza kujitambulisha na kutambuliwa kama Dola huru katika ulimwengu. Zanzibar ikawa kituo muhimu cha kisiasa, kiuchumi na kibiashara katika Afrika Mashariki na Bahari ya Hindi.. Kutokana na umuhimu wake, madola makubwa yalifungua Ofisi za Kibalozi mjini Zanzibar : Marekani (1837), Uingereza (1841), Ufaransa (1844), na baada ya hapo Ureno, Utaliana, Ubelgiji na Ujarumani zikafuata.”

Mzanzibar ambaye hajui historia ya Zanzibar na mtu wa bara ambaye anayasoma maneno haya anaamini kabisa kuwa balozi hizo zilifunguliwa kwa sababu ya Zanzibar “kujitambulisha na kutambuliwa kama dola huru katika ulimwengu”.

Bahati mbaya ni kuwa kuna historia ambayo Maalim Seif hakutaka kuikiri hadharani inayohusiana na kufunguliwa kwa balozi hizo Zanzibar na siyo sehemu nyingine katika eneo letu hili. Naomba ruhusa nimkumbushe sehemu hii ya historia yetu.

Mwaka 1822 Sultan wa Oman, Sayyid Said Bin Sultan aliingia mkataba ujulikanao kama Mkataba wa Moresby. Mkataba huu, pamoja na mambo mengine, ulipiga marufuku uuzaji wa watumwa kwa nchi za Kikristu kutoka katika himaya yote ya Sultani huyo. Ni kutokana na mkataba huo na mingine iliyofuatia ndio nchi za Marekani, Uingereza , Ufaransa n.k zilipoamua kuanzisha ofisi zao za ubalozi huko ili kuhakikisha mojawapo ya mambo mengi kuwa Sultani wa Zanzibar anaheshimu makubaliano ya Moresby, Hamilton n.k

Ukiangalia tarehe ya kuanza kwa balozi hizo kama Maalim alivyoonyesha (1837) unaweza ukafikiria ni kwa bahati nzuri tu kuwa ndani ya miaka kama saba nchi mbalimbali za Kimagharibi zimefungua balozi zao huko?

Ikumbukwe kuwa mwaka 1832 (wanahistoria wengine wanaweka tarehe ya mbele kidogo) Sultani wa Oman alihamishia maskani yake kutoka Omani na kuwa Zanzibar makao makuu. Kutokana na ukaribu wake na nchi hizo za Magharibi Zanzibar hatimaye ilifanikiwa pole pole kukomesha utumwa na utumishi wa kulazimisha (servitude).

Omani, hata hivyo, ambayo tunaambiwa ndio walikuwa watu wema kwetu, waliendelea na hali hiyo kwa namna moja au nyingine hadi mwaka 1870 kufuatia mapinduzi yaliyomuingiza Sultan Qabus na Saudi Arabia yenyewe chini ya Mfalme Faysal ilifanya hivyo mwaka 1869!

Hii ni muhimu kuelewa kwa sababu ni sehemu ya Historia ya Zanzibar, na ni historia yetu vile vile. Hatuwezi kuikana, kujificha kwa haya au hata kuitaja kwa jina.

‘Uhuru’ wa Zanzibar ni uhuru?

Jambo jingine ambalo Maalim analielezea ni kuwa “Uingereza ilikabidhi uhuru kwa Zanzibar tarehe 10 Desemba 1963 chini ya Sultani na Serikali ya ZNP/ZPPP. ASP hawakuukubali uhuru huo na tarehe 12 Januari, 1964 ilifanya Mapinduzi na Zanzibar ikatangazwa kuwa Jamhuri.”

Wapo watu wanaoamini kabisa kuwa huu kweli ulikuwa ni “uhuru wa Zanzibar”. Ndio hawa ambao bado wanapata shida kuyatambua Mapinduzi ya Zanzibar na ulazima wa kwanini yalitokea. Unaweza kuliona hilo katika hotuba hiyo ya Maalim Seif.

Utaona mambo makubwa matatu ambayo ni sehemu ya historia ya Zanzibar hayatajwi kabisa na kama hilo hapo juu yanatajwa kama kwa kupita.

Kwanza ni suala la utumwa na pili ni utawala wa Sultani wa Zanzibar na kama wananchi waliokuwa watumwa au watu weusi walinufaika na utawala huo.

Ndugu zangu, tunapotaka kujenga Zanzibar mpya na Tanzania mpya tuipendayo, hatuna budi kuwa wakweli kwa historia yetu. Tusiikane au kuona ni vibaya kuikiri. Wamarekani walikuwa na utumwa, Wamarekani walipigana wenyewe kwa wenyewe na zaidi ya nusu milioni walikufa.

Wamarekani walikuwa na ubaguzi wa rangi licha ya Katiba yao kutangaza usawa wa binadamu wote na haki zao. Leo hii Wamarekani wameweza kumchagua mtu mweusi kuwa Rais wao miaka chini ya hamsini tu tangu vurumai za mwamko wa haki za watu weusi nchini humo!

Bila ya kura za watu weupe Obama asingeweza kuwa Rais wa Marekani! Watu weusi wa Marekani ni kama asilimia 12 tu ya Wamarekani wote! Kwa maneno mengine, watu weupe ambao wamekuwa wakiangaliwa vibaya na kubebeshwa lawama za utumwa na ubaguzi na watu weusi walikubali historia yao na kuikumbatia na kujitokeza kumchagua mtu mweusi.

Hii ni historia yetu!

Hii ina maana kwetu leo hii. Waarabu, Wahindi, Washirazi na watu weusi wa Zanzibar na Tanzania Bara, ni lazima watambue kuwa hata tukimbie vipi, hata tujifiche vipi na hata tukwepe vipi, historia yetu imefungamana milele. Hata kina Maalim wasipotaja utumwa wasidhanie kuwa basi utafutika katika historia!

Na pia ni lazima tutambue kuwa kama taifa hatuwezi kuwabebesha Waarabu na Waoman wa leo mzigo wa dhambi ya utumwa na kuwaona kuwa ni waonevu juu yetu.

Kama vile Marekani, natambua wapo watu ambao bado hawamuoni mtu mweusi kuwa ana haki sawa na kumheshimu. Wapo watu weupe Marekani ambao hadi leo hii hawamtambui Obama kama Rais wao! Sitoshangaa wapo kati yetu uzao wa Wa-Oman na Waarabu wengine ambao wanaona watu weusi bado ni duni!

Na katika upotofu Fulani, wapo watu weusi ambao wanaamini kabisa kuwa bila ya wao kukubaliwa na Waarabu hao au na Washirazi, basi siyo binadamu hasa. Na wengine wamefikia hata kujiita “Waarabu” ili waonekane kukubalika. Huu ni upumbavu.

Waarabu wa Tanzania ni wananchi wenzetu na wana haki zote kama Watanzania wengine. Hawana haki au utu zaidi kwa sababu ya Uarabu wao.

Watu wenye asili ya Omani ambao vizazi vyao vimegawanyika Zanzibar na Oman wasijione kuwa wao ndiyo Waarabu hasa kulinganisha na Waarabu waliochangia damu na Wamanyema na Wanyamwezi wa Bara!

Wahindi ambao hawajachangia damu yoyote na watu weusi na wana vizazi Tanzania na India wasijifikirie kuwa wao ni watu bora zaidi na kuwa watu weusi bado ni maboi wao!

Nayasema haya ili ijulikane kwamba Tanzania tunayoitaka ni Tanzania yetu sote - historia ya Zanzibar ni historia ya Tanzania. Huu upuuzi wa kutaka kufanya watu wa Bara ni duni kwa sababu hawana historia ya taa za barabarani na televisheni za rangi, ni lazima ukome hata ukitolewa na wanasiasa tunaowapenda.

Huu mtindo wa “Zanzibar ilikuwa pepo na mapinduzi yakaharibu”, ni mtindo tunaopaswa kuukataa kwa nguvu zetu zote!

Ndiyo maana ni muhimu kujua kama kina Maalim Seif wanatambua ulazima wa mapinduzi yale na kuyakubali si kwa ajili ya kupata pointi za kisiasa bali kifalsafa na kimaadili. Ni lazima tujue kama kina Seif wanaweza kusema kuwa waliona matatizo yoyote ya utawala wa Sultani huko Zanzibar au wao bado wanaamini kuwa Sultani alionewa tu.

Na ndiyo maana katika haya pia mimi ninaamini kabisa kuwa mojawapo ya mambo ya kupatana Zanzibar ni lazima suala la Sultani lizungumzwe siku moja na kuhitimishwa, kwa sababu tunajua hadi leo hii Sultani wa Zanzibar hajakikana kiti chake cha Usultani wa Zanzibar na watoto wao bado wanaendelea kujitambua kuwa ni wana wa Sultan (Prince na Princesses).

Wote hawa ndugu zangu ni sehemu ya historia yetu na wakati umefika tuache kujitenga kwa mambo ya kijinga tukifirikia kuwa tunachofanya ni hekima na busara na ni uzalendo. Zanzibar haiwezi kukaa katika kivuli cha Sultani anayesubiri siku moja arudi na kukalia kiti chake!

Wananchi wa Zanzibar wasikubali hadaa ya maneno ya kisiasa, wasikubali kuimbiwa zumari za uongo na wao wakacheza.

Zanzibar ina historia yake na historia hiyo ina mazuri na mabaya yake kama vile ilivyo historia ya Uingereza, Japani, na China!

Historia hiyo ya Zanzibar ni historia ya Azania! Ni historia ya Tanzania yetu leo hii. Katika hili hatuna sababu ya kuomba radhi na Wazanzibari wasifikirie kuwa tutawaonea wivu. Wao ni sehemu yetu, sehemu ya damu yetu; kwani hatuwezi kamwe kuandika historia ya Tanganyika au Mwambao wa Afrika ya Mashariki bila kuandika historia ya Zanzibar.

Wana CCM Zanzibar wameliabisha taifa

Kitendo cha uongozi wa CCM Zanzibar kukubali na kukumbatia uongo kwa kisingizio cha “Zanzibar moja” ni cha hatari kwa muafaka wa taifa; kwani kinalenga kudhoofisha muungano na Rais Kikwete na Watanzania wasipoangalia ni ujumbe mkubwa wa kisiasa ambao matokeo yake hata kichaa anaweza kuyatabiri.

Wana CCM wa Zanzibar na Watanzania wa Zanzibar watambue kuwa wao ni sehemu ya jamhuri yetu, historia yetu ni historia yao na historia yao ni yetu. Tofauti za kisiasa na kimtizamo ni tofauti zinazozungumzika (hata leo hii majimbo ya Marekani na hata Uingereza wanazungumzia tofauti zao za kisiasa na kiutawala)

Katika kutafuta sifa za kisiasa, Rais wa Zanzibar asilipeleke taifa kwenye uchaguzi mbaya kwa kukumbatia uongo.

Vinginevyo, Dk. Karume atajikuta anafifisha na kudunisha na kudharau damu ya wale waliokufa katika mapinduzi na kufanya mapinduzi yale kuwa hayana maana yoyote! Historia itamhukumu vibaya sana akiendelea na maamuzi anayofanya sasa.

Kina Maalim wasitugawe sasa kwa historia wakifikiri wanatutendea hisani. Na nimeudhika kuona wana CCM wameingia katika mtego huu huko Zanzibar kiasi cha kupepea uongo kwa kanga zao za kijani na njano!

Ninaona fahari kuwa Zanzibar ni sehemu ya Tanzania. Ninaona fahari ya kujua historia yetu kama taifa.

Naomba niishie hapa. Nitajibu hoja zake za kisiasa alizozitoa wiki ijayo, inshallah.



Sijaelewa natija ya kuandika haya majibu kwa taarifa aliyoitoa Seif Sharif Hamad. Lula na wanaomsupport kiufupi ni hivi jamaa ametoa reference wapi amepata artifacts zake na nyie toeni taarifa zenu wapi mmetoa taarifa zenu.

Haikataliwi kuwa utumwa ni historia mbaya kwa jamii na si kitu cha kujivunia but Seif hakuizungumzia kwa maksudi sio kwamba ameikataa bali si kitu cha kupendeza kuna watu walioua watu weusi kama waingereza tizame historia mtaona. lakini hili halizungumziwi kwasababu linaleta chuki na uhasama kwa jamii. Kwakuwa lengo ni kuleta umoja katika jamii waingereza wanakuwa wanalizungumzia kwa kifupi sana ili kudumisha umoja wao.

Sasa mie nataka nikuulize Lula na wenzio je ni faida gani ya kuitukuza historia ya utumwa???? Tunapata faida gani au faida gani tuliyoipata isipokuwa dividing rules. Na who is to benefit from that isipokuwa watu wa nje ambao wanawatawala kwa urahisi. India waingereza waliligundua hili wakalitumia sana kuwatawala india hadi Gandhi alipokuja akaona ni bora aliondoe ili watu wawe wamoja.

Karume hakukosea kabisa kuwa pamoja na CUF msimlaumu kwasababu zanzibar imekuwa inadhalilika sana. Sie ambao tumekaa dar na znz tunasikitishwa na hali ya zanzibar kwani ni aibu tupu. Umaskini umetapakaa, viwanda vimekufa, watu hawana mwelekeo kisa eti mapinduzi. Kuna faida ya mapinduzi wakati watu hawana chakula. Acheni zenu kina lula zanzibar haiko kama ile ya miaka ya 1960 sasa hivi wengi tunawasaidia kwasababu hali ya huko zanzibar hamuioni nyie mko mnang'ang'ania na utumwa wakati Tanzania bara mtu wa chini graduate analipwa 300,000 , zanzibar analipwa 70,000-50,000 eti mapinduzi!!!!.

Kiufupi kama walivyo wamarekani walipobreak ili glass ceiling kuwakubali watu weusi na hispanic. Tanzania has to accept zanzibar as it is. Watu weusi hawakuwezi kukubalika isipokuwa walipokubali kuunganika kuwa pamoja against watu weupe (tizama historia ya watu weusi, million man marching etc). Hispanics, Blacks, Jews, wajapan, wahindi waliungana against watu weupe ndio tukaipata tuijuayo marekani now. Sasa na zanzibar lazima wawe kitu kimoja ili wapate wanachokitaka.

Ile dividing rule ya kudai eti utumwa na nini sasa inafifia wakubwa no one is interest in that load piece of crap ikiwa hana kitu tumboni!!!!
 
Inashangaza katika historia nzima "fupi" ya Zanzibar.. neno utumwa hata halikuingia mawazoni kwa maalim; anaamini kabisa watu weusi wote walioko Zanzibar walikuja kwa ajili ya kutafuta maisha ya kheri visiwani humo na kuwa watu wote walioishi Zanzibar waliishi kama watu sawa na huru! This in history is known as revisionism!

In the compacted political history of hon Seif, slavery never happened and there is no evidence of its existence in the beautiful islands of Zanzibar!
jamani,Zanzibar lilikuwa ni soko la watumwa na ilikuwa ni transit station kwa watumwa wanaotoka bara(Kuanzia kongo burundi,rwanda,africa ya kati nk) wakiwa njiani kupelekwa huko wanapopelekwa. kwa nini mnaelekea kuibebesha mzigo zanzibar na biashara ya watumwa kuliko kuwabebesha lawama akina BABA WA BABU ZAKE LULA NDALI MWANANZELA kwa kuwauza ndugu zao?? ndio zetu kulaumu tunapoangukia na sio tulipojikwaa.machifu wa kibantu ndio wa kulaumiwa kwa kiwango kikubwa kwa kuendekeza tamaa.Afterall what about the EUROPEANS?(The promonent market for the slaves) au biashara ni kwa muuzaji tu,ila mnunuzi hahusiki na biashara hiyo???,....
Jiulizeni,,,, kwa nini hakuna muhehe toka Iringa aliyewahi kuchukuliwa utumwani LOL
 
Sijaelewa natija ya kuandika haya majibu kwa taarifa aliyoitoa Seif Sharif Hamad. Lula na wanaomsupport kiufupi ni hivi jamaa ametoa reference wapi amepata artifacts zake na nyie toeni taarifa zenu wapi mmetoa taarifa zenu.

Haikataliwi kuwa utumwa ni historia mbaya kwa jamii na si kitu cha kujivunia but Seif hakuizungumzia kwa maksudi sio kwamba ameikataa bali si kitu cha kupendeza kuna watu walioua watu weusi kama waingereza tizame historia mtaona. lakini hili halizungumziwi kwasababu linaleta chuki na uhasama kwa jamii. Kwakuwa lengo ni kuleta umoja katika jamii waingereza wanakuwa wanalizungumzia kwa kifupi sana ili kudumisha umoja wao.

Sasa mie nataka nikuulize Lula na wenzio je ni faida gani ya kuitukuza historia ya utumwa???? Tunapata faida gani au faida gani tuliyoipata isipokuwa dividing rules. Na who is to benefit from that isipokuwa watu wa nje ambao wanawatawala kwa urahisi. India waingereza waliligundua hili wakalitumia sana kuwatawala india hadi Gandhi alipokuja akaona ni bora aliondoe ili watu wawe wamoja.

Karume hakukosea kabisa kuwa pamoja na CUF msimlaumu kwasababu zanzibar imekuwa inadhalilika sana. Sie ambao tumekaa dar na znz tunasikitishwa na hali ya zanzibar kwani ni aibu tupu. Umaskini umetapakaa, viwanda vimekufa, watu hawana mwelekeo kisa eti mapinduzi. Kuna faida ya mapinduzi wakati watu hawana chakula. Acheni zenu kina lula zanzibar haiko kama ile ya miaka ya 1960 sasa hivi wengi tunawasaidia kwasababu hali ya huko zanzibar hamuioni nyie mko mnang'ang'ania na utumwa wakati Tanzania bara mtu wa chini graduate analipwa 300,000 , zanzibar analipwa 70,000-50,000 eti mapinduzi!!!!.

Kiufupi kama walivyo wamarekani walipobreak ili glass ceiling kuwakubali watu weusi na hispanic. Tanzania has to accept zanzibar as it is. Watu weusi hawakuwezi kukubalika isipokuwa walipokubali kuunganika kuwa pamoja against watu weupe (tizama historia ya watu weusi, million man marching etc). Hispanics, Blacks, Jews, wajapan, wahindi waliungana against watu weupe ndio tukaipata tuijuayo marekani now. Sasa na zanzibar lazima wawe kitu kimoja ili wapate wanachokitaka.

Ile dividing rule ya kudai eti utumwa na nini sasa inafifia wakubwa no one is interest in that load piece of crap ikiwa hana kitu tumboni!!!!

Unatia aibu na kusikitisha. Haswa kama una damu ya mtu mweusi.

Uingereza na marekani wanazungumzia sana historia ya utumwa tofauti na unavyotaka kutuambia. Marais wa marekani wakitembelea Afrika hutembelea Afrika Magharibi kwanza ili kutembelea sehemu ambako watumwa walichukuliwa kupelekwa Marekani. Aprili 2, 1998 Rais Bill Clinton alitoa hotuba akizungumzia biashara ya utumwa alipotembelea kisiwa cha Goree, Senegal. Julai 8, Rais George W. Bush alizungumzia utumwa alipotembelea kisiwa cha Goree. Tarehe 11, Julai 2009, Rais Barck Obama na familia yake walitembelea kasri ya Cape Coast ambako watumwa wengi walisafirishiwa kwenda Marekani alipotembelea Ghana. Waziri Mkuu Tony Blair aliandika kuhusu kusikitishwa kwake kuhusu biashara ya utumwa tarehe 27 Novemba 2006. Mwaka 2007 ulikuwa mwaka wa 200 toka biashara ya utumwa ipigwe marufuku katika himaya ya uingereza na palikuwa na matukio mengi kuwakumbusha wananchi wa uingereza kuhusu biashara hiyo haramu na mchango wa uingereza. Mjini Liverpool kuna makumbusho ya utumwa. Mwezi wa Februari nchini Marekani ni mwezi wa historia ya watu weusi ambapo mchango wa utumwa ni nguzo moja inayozingatiwa. Ukienda Poland, utaweza kutembelea Auschwitz ambako wayahudi na watu wengine waliuawa na wajerumani. Kambi hiyo inatunzwa kama ilivyo na ni mara nyingi tu viongozi kutoka ujerumani wanaitembelea. Mjini Berlin kuna Makumbusho ya wayahudi ambamo vitendo vilivyofanywa na ma-nazi dhidi ya wayahudi viko wazi. Hapo apo Berlin kuna Holocaust museum. Mifano iko mingi. Wenzetu wanafanya hivi ili kuwakumbusa wenzao maovu yaliyofanywa na waliowatangulia. Wanafanya hivi, si tu kuwaomba radhi waliowafanyia maovu ayo bali kuhakikisa kuwa watakaowafuata hawatakuja sahau na kutenda tena maovu hayo. Wanawaambia wenzao kuwa hayo maendeleo wanayojivunia yalicangiwa na uovu na wasisahau hicho wanapojisifia!

Sasa niambie lini kiongozi kutoka nchi ya kiarabu alitembelea Bagamoyo na kuzungumzia biashara ya utumwa? Ni wapi Zanziba ambapo historia ya utumwa imewekwa wazi ukiacha kanisa la kianglikana ambalo lilijengwa juu ya soko kuu la watumwa?

Hapana, inatulazimu kuzungumzia utumwa kila wakati ili tusijesahau siku moja na kuruhusu biashara hiyo irudi tena. Ndiyo maana tumesikitishwa kwa kitendo cha mtu ambaye anahesabika mmoja wa viongozi wakuu katika nchi ya Zanziba anaweza kuzungumzia hitoria ya nchi yake na kuwaenzi walioendesha biashara hiyo bila kuzungumzia madhara iliyoleta katika nchi yake. Ni kama vile kuwasifia wajerumani ma-nazi kwa kuwa na ndege ya kivita ya kwanza duniani inayotumia jet-engine ( Me 262) bila kuzungumzia siasa yao ya Final Solution.

Maalim alifanya kosa kutozungumzia utumwa. Hata mseme vipi.

Zanzibar kushindwa kumlipa vizuri mfanyakazi wake kunahusiana nini na Muungano?

Haujui historia ya marekani. Wajapani, wahindi na wahispania walishirikiana lini na watu weusi wakati wa Civil Rights Movement? Watu walioungana na watu weusi katika mapambano hayo walikuwa watu weupe na wayahudi wa mlengo wa kushoto. Sehemu kubwa ya wasio weusi walipinga au walikaa kwenye uzio na kuangalia. Ilichukuwa miaka 400 ya machozi, damu, vifo, vilio, kubakwa ili limbukeni kama wewe uweze kuamka na kuita slave trade kuwa ni piece of crap! Load of crap ni huu utetezi wako wa uovu waliotendewa babu zako.

Amandla......
 
Zanzibar kushindwa kumlipa vizuri mfanyakazi wake kunahusiana nini na Muungano?

Hivi hili suala unataka majibu kweli kutoka wazanzibari au unafanya jokes?
Mimi naona majibu yako mbele yako na jaribu kutizama ni mamlaka gani Zanzibar ilikuwa nayo kabla ya muungano, na sasa mamlaka yale yamekwenda wapi?

Kama utakubali sasa hivi mamlaka yapatayo 50 ya Zanzibar yameondoshwa na kuwekwa chini ya Muungano...naona hili jibu linatosha, ukinihitaji nikufanyie orodha nijuilishe tuu.

Lakini naona jibu hilo linatosha muungano kubeba lawama zote za Zanzibar.
 
Unatia aibu na kusikitisha. Haswa kama una damu ya mtu mweusi..
Amandla......

Hata wakati nchi zote za dunia zilipokubaliana kuupiga vita Utumwa, Zanzibar chini ya Sultani wa Oman, iliendeleza biashara ya Utumwa. Hiyo ni kwa sababu kwanza waarabu walifaidika sana na hiyo biashara na pili, hawakuwathamini kabisa watu weusi. Ilibidi nguvu za ziada zitumike kukomesha kiburi chao, tamaa yao na vitendo vyao viovu kama ile ya kuwabaka wanawake baada ya waume zao kuhasiwa.

Maalimu Seif kwa makusudi kabisa hakuweza kuongelea historia ya vitendo kama hivi kwani ni moja kati ya sababu zilizochochea sana mapinduzi ya mwaka 1964. Katika kitabu chake Field Marshall John Okelo, anaelezea jinsi jinsi uchungu wa kumwona mtu mweusi akifanyiwa unyama na Mwarabu tangu akiwa kijana kule Mombasa, ulimhamasisha kuhamia Zanzibar na kuongoza vita dhidi ya Usultani - jamani tusichezee historia.
 
Hata wakati nchi zote za dunia zilipokubaliana kuupiga vita Utumwa, Zanzibar chini ya Sultani wa Oman, iliendeleza biashara ya Utumwa. Hiyo ni kwa sababu kwanza waarabu walifaidika sana na hiyo biashara na pili, hawakuwathamini kabisa watu weusi. Ilibidi nguvu za ziada zitumike kukomesha kiburi chao, tamaa yao na vitendo vyao viovu kama ile ya kuwabaka wanawake baada ya waume zao kuhasiwa.

Maalimu Seif kwa makusudi kabisa hakuweza kuongelea historia ya vitendo kama hivi kwani ni moja kati ya sababu zilizochochea sana mapinduzi ya mwaka 1964. Katika kitabu chake Field Marshall John Okelo, anaelezea jinsi jinsi uchungu wa kumwona mtu mweusi akifanyiwa unyama na Mwarabu tangu akiwa kijana kule Mombasa, ulimhamasisha kuhamia Zanzibar na kuongoza vita dhidi ya Usultani - jamani tusichezee historia.

Sasa mkuu Seif ingelimsaidia nini kama angezungumzia utumwa na maovu yake kwa muda wa masaa 3?

Nini maudhui ya hilo kongamano?Kujadili utumwa?...naona kama ule ubaguzi wa watu weupe, sasa umehamia ndani ya mioyo ya watu weusi kuwabagua waarabu....Huu bado utaitwa ubaguzi, si kama mtu mweusi kubagua watu wengine ni sawa!
 
Sasa mkuu Seif ingelimsaidia nini kama angezungumzia utumwa na maovu yake kwa muda wa masaa 3?

Nini maudhui ya hilo kongamano?Kujadili utumwa?...naona kama ule ubaguzi wa watu weupe, sasa umehamia ndani ya mioyo ya watu weusi kuwabagua waarabu....Huu bado utaitwa ubaguzi, si kama mtu mweusi kubagua watu wengine ni sawa!

Kwa hiyo muarabu kumbagua mtu mweusi ni sawa? Ubaguzi wa aina yeyote unatakiwa ulaaniwe bila kujali nani anambagua nani. Mtu mweusi kumbagua mtu asiye mweusi ni sawa kabisa na yeye kubaguliwa na asiye mweusi! Muunguja kumbagua mpemba na mpemba kumbagua mmuunguja. Vitendo vyote inabidi vilaaniwe. Lakini pamoja na kuvilaani inatubidi tukumbuke historia na madhara ya aina yote ya ubaguzi. Hili ni fundisho kwa mtu mweusi pia kuwa kama nae atageuka na kufanya uovu aliofanyiwa iko siku jamii itamsuta na kumlaani vile vie.Kwa sabau nyinyi waarabu hamjawahi kukiri au kulaani uovu mliomtendea mtu mweusi ni rahisi sana mtakapopata nafasi kuweza kuvirudia. Kwenu nyinyi mtu mweusi atabaki kuwa mtwana. Hiki ndicho wengine tunachopinga.

Amandla......
 
Kwa hiyo muarabu kumbagua mtu mweusi ni sawa? Ubaguzi wa aina yeyote unatakiwa ulaaniwe bila kujali nani anambagua nani. Mtu mweusi kumbagua mtu asiye mweusi ni sawa kabisa na yeye kubaguliwa na asiye mweusi! Muunguja kumbagua mpemba na mpemba kumbagua mmuunguja. Vitendo vyote inabidi vilaaniwe. Lakini pamoja na kuvilaani inatubidi tukumbuke historia na madhara ya aina yote ya ubaguzi. Hili ni fundisho kwa mtu mweusi pia kuwa kama nae atageuka na kufanya uovu aliofanyiwa iko siku jamii itamsuta na kumlaani vile vie.Kwa sabau nyinyi waarabu hamjawahi kukiri au kulaani uovu mliomtendea mtu mweusi ni rahisi sana mtakapopata nafasi kuweza kuvirudia. Kwenu nyinyi mtu mweusi atabaki kuwa mtwana. Hiki ndicho wengine tunachopinga.

Amandla......

Naona tuko kwenye boti moja, kuwa ubaguzi upingwe kwa nguvu zote.
Kwa kumalizia mimi sijiweki kwenye category ya mwarabu wala sifikirii Zanzibar kama kuna waarabu....

Waarabu hawaishi Zanzibar, wanaishi nchi za kiarabu na kuzungumza kiarabu....kukurekebisha Zanzibar ni sehemu yenye watu wa mchanganyiko, wakiwemo baadhi yao wenye asili tuu za kiafrika-kibantu,kiarabu, kihindi, kizungu...etc

Hili huwezi kulikimbia sehemu yenye mchanganyiko kama Zanzibar...sasa kuniita mie muarabu au mzanzibari mwengine muarabu, si ndio unaendeleza ubaguzi...wakati huo huo ukionesha kuwa upigwe vita?

Naona ndugu zangu hususan wa watanganyiko munapata taabu sana kukubali kama kuna watu ambao ni wazanzibari...aidha munapenda mufanye chuki za kuwaletea ubaguzi....na hamuwezi kujificha lazima mutamtia label ya kibaguzi.

Ubaguzi wa kipemba na kiunguja upo, na tunaukubali sana kuwa upo huku visiwani....lakini jee Tanganyika hakuna ubaguzi wa kikabila?Au kuna sehemu gani ambayo hakuna?Kenya si ni majuzi tuu watu wamepigana mapanga?...

Sasa tupunguze kuchochea ubaguzi....sisi ni wazanzibari na tutaendelea kuwa na maridhiano yetu na kujaribu kufix matatizo yetu kama taifa jengine lolote....

Nyinyi kama mutaendelea jitihada zenu za kutaka kutugombanisha kwa sababu za kihostoria...fanyeni hivyo, lakini naona kama mmechelewa jamvini... :D
 
Naona tuko kwenye boti moja, kuwa ubaguzi upingwe kwa nguvu zote.
Kwa kumalizia mimi sijiweki kwenye category ya mwarabu wala sifikirii Zanzibar kama kuna waarabu....

Waarabu hawaishi Zanzibar, wanaishi nchi za kiarabu na kuzungumza kiarabu....kukurekebisha Zanzibar ni sehemu yenye watu wa mchanganyiko, wakiwemo baadhi yao wenye asili tuu za kiafrika-kibantu,kiarabu, kihindi, kizungu...etc

Hili huwezi kulikimbia sehemu yenye mchanganyiko kama Zanzibar...sasa kuniita mie muarabu au mzanzibari mwengine muarabu, si ndio unaendeleza ubaguzi...wakati huo huo ukionesha kuwa upigwe vita?

Naona ndugu zangu hususan wa watanganyiko munapata taabu sana kukubali kama kuna watu ambao ni wazanzibari...aidha munapenda mufanye chuki za kuwaletea ubaguzi....na hamuwezi kujificha lazima mutamtia label ya kibaguzi.

Ubaguzi wa kipemba na kiunguja upo, na tunaukubali sana kuwa upo huku visiwani....lakini jee Tanganyika hakuna ubaguzi wa kikabila?Au kuna sehemu gani ambayo hakuna?Kenya si ni majuzi tuu watu wamepigana mapanga?...

Sasa tupunguze kuchochea ubaguzi....sisi ni wazanzibari na tutaendelea kuwa na maridhiano yetu na kujaribu kufix matatizo yetu kama taifa jengine lolote....

Nyinyi kama mutaendelea jitihada zenu za kutaka kutugombanisha kwa sababu za kihostoria...fanyeni hivyo, lakini naona kama mmechelewa jamvini... :D

Hebu kuwa mkweli. Huko Zanziba hakuna watu wanajiita waarabu safi? Hakuna watu wanaitwa wangazija? Hivi ni kwa sababu gani kuna ubaguzi kati ya mu-unguja na m-pemba? Yote haya unataka kusema yameletwa na machogo? Kuweko na makabila na watu wenye asili tofauti si dalili ya ubaguzi. Ubaguzi ni pale unapotumia uasili wako kujiona bora na mwenye haki kuliko wengine. Wewe kuwa Mzanzibari muarabu si tatizo. Tatizo ni pale unapoona uarabu wako unakufanya bora kuliko wazanzibari wengine watumbatu, wanyasa, wanyamwezi, wangazija ,n.k. Mbona bara kuna watanzania wanaotambuliwa kama waarabu na wahindi? Tatizo si kuwatambua hivyo. Tatizo ni pale tunapowaona hawana haki sawa kama sisi wenye ngozi nyeusi. Huo ni ubaguzi na unastahili kupingwa. Kama vile tunavyopinga yule mwenye anayejihesabu muarabu au mhindi anapoona mtu mweusi nafasi yake ni kuwa mtwana wake.

Amandla......
 
Back
Top Bottom